Said Bakhressa ana mchango wowote katika kuendeleza elimu?

Said Bakhressa ana mchango wowote katika kuendeleza elimu?

unajua mm binafsi naamini kuwa jf ni forum inayounganisha wasomi wenye uwezo wa kufikiria mambo mbalmbal kwa upambanuz na uyakinifu kwa kutumia busara stahiki.
Leo hii mtu anatoa mada ambayo kama ikijadiliwa vizuri mimi,ww na hata yy anaweza kunufaika kwa namna moja ama nyngne.
Badala yake watu wametawaliwa na ubinafsi, kebehi,ufedhuli na dharau.
Mtoa mada kauliza swali ambalo kama kuna ushahidi unaweza kuutoa.
Sijaona ktk post yake kama kuna sehemu katumia lugha ya kulalama.
Wallahi huu ni msiba (inna lillahi wa inna illahi raaj'un).
Tunatakiwa tutumie busara jamani ktk mambo ya msingi na yenye mashiko.
Una comments "changia", hauna basi we "pita" waache wachangiaji.
Kama mtoa mada kakosea basi we fanya kama una"PM" kumsahihisha sio kukebehi publicily.
Binafsi naipenda thread hii maana najua huyu SS B. kwa uwezo wake anaweza fanya mengi sana, kujenga shule,vyuo,kugharamia miundombinu mashuleni, n.k. ili jamii izidi kumtambua, kumkumbuka na kumuenzi.
Lakin km alishawah kufanya bac tunaomba evidence.

Evidence tayari imeshatolewa kwa kuwasaidia SUZA
 
nchi hii watu wengi huwa wanatoa misaada kwa ajili ya sekta mbali mbali sema si kila mmoja anapenda kupiga tarumbeta akishasaidia! Tunafahamu mtu kama baba wawili hata siku akipikia pilau walemavu basi hiyo ndo itakuwa habari kwenye media zake... Wengine tabia hiyo hawana... Wanatoa kimya kimya! Mfano mzuri ni hiyo post # 10 inayoonesha dr. Shein akitoa tuzo kwa ssb kama ishara ya kuthamini mchango wake ndani ya suza! Si ajabu kama si hiyo sherehe, wengi wasingefahamu kwamba ssb anaisaidia suza.

na sifa kuu ya muungwana .. Anasaidia na kukaa kimya....sio kutangazia
 
Kwa taarifa za ndani ni kwamba ni vigumu sana kujua SSB kasaidia nini kwa sababu hana tabia ya kupiga tarumbeta anapotoa msaada. Inasemekana hii huenda inatokana na mafunzo ya dini yake yanayomtaka muumini anapotoa asijitangaze wala kutaka sifa. Hizi ni speculations tu na taarifa za watu mbalimbali walio karibu na duru za huyu bwana.

yap ni kweli kidini hairuhusiwi kutoa kitu kwa dhamira ya "kujionesha" hii inaitwa "ria" ambayo ni unafikhi, bimaana kwamba tunatakiwa kutoa kwa moyo kwa mafundisho swahih ya mtume (s.a.w).

Hata hivyo kupeana taarifa kuwa fulani kafanya hivi ktk dini inajuzu, japo hata si kwa picha, ama video. Nia ni kwamba tuweze kujifunza bimaana hii ni ilimu yakini.
 
Gmali, hapa umepiga fyongo, kati ya watu waliopewa tuzo kwa kulipa kodi tena bila usumbufu ni huyu Azam. Kuchangia elimu ni maamuzi yake lakini kumbuka matajiri bado wana jukumu la kusaida jamii maskini ili ziweze kuinuka kimaisha, comments zako zinaashiria ubinafsi uliokithiri ambao kwa dunia ya sasa ya wapenda maendeleo hauna nafasi. Acha fikra za ubinafsi

Fungwe! suala la msaada haliangaliwi kwa kipato cha mtu, jiulize mwenyewe umejitoa kwa kiasi gani japo kwa kidogo ulichonacho ili uwe mfano kwa wengine humu jamvini.

Suala la msaada kwa kampuni kubwa ni la kujipanga si kukurupuka ukaamka asubuhi na kugawa pesa.Kwa taarifa tu, Tanzania haihitaji msaada zaidi ya ulionao, juu ya elimu ni suala la mpango mkakati.

AZAM ni kampuni ya kuigwa kwa Afrika Mashariki
 
WanaJF,

Hakuna ubishi kwamba Billionia wetu mpendwa SAID BAKHRESSA a.k.a AZAM anamchango mkubwa katika uchumi wa nchi yetu na kwamba anangoza kulipa kodi, kwa hili anastahili pongezi.

Lakini nimejaribu kuchunguza katika Nyanja adimu na muhimu ya elimu, kwa upande wangu sikuona chochote kutoka kwa Bwana huyu, kama kuna mwenye taarifa kuhusu mchango wa Bw. Bakhresa kweye elimu dunia atujuze iwe bara au visiwani

Kwa uwezo wake wa kifedha tulitarajia natuone kwa mfano, AZAM UNIVERSITY OF TECHNOLOGY au AGRICULTURE n.k. Nimejaribu kuuliza wenyeji na majirani zake pale AZAM COMPLEX kama angalao amejenga hata shule ya msingi lakini majibu ya wenyeji ni kwamba ameweza kujenga Misikiti na ofisi ya Serikali ya Mtaa pale Chamazi Mwembe Bamia.

Jamani wenye ushahidi bandikeni hapa tusijekuwa tunamhukumu bure.

blaza tuache ujinga...mtu na pesa zake usimlimit ..hujui kazipataje then wewe unajikuta unamlazmsha akuchangie.

aje mtu baki akusaidie wakati viongoz wako wanaweka heshma ulaya. unamlaumu bure huyu jamaa...kutoa ni moyo co utajir...kama hamjui matumiz ya michango ipasavyo hata mpew nn hamna kitu
#twendeni hivihivi
 
WanaJF,

Hakuna ubishi kwamba Billionia wetu mpendwa SAID BAKHRESSA a.k.a AZAM anamchango mkubwa katika uchumi wa nchi yetu na kwamba anangoza kulipa kodi, kwa hili anastahili pongezi.

Lakini nimejaribu kuchunguza katika Nyanja adimu na muhimu ya elimu, kwa upande wangu sikuona chochote kutoka kwa Bwana huyu, kama kuna mwenye taarifa kuhusu mchango wa Bw. Bakhresa kweye elimu dunia atujuze iwe bara au visiwani

Kwa uwezo wake wa kifedha tulitarajia natuone kwa mfano, AZAM UNIVERSITY OF TECHNOLOGY au AGRICULTURE n.k. Nimejaribu kuuliza wenyeji na majirani zake pale AZAM COMPLEX kama angalao amejenga hata shule ya msingi lakini majibu ya wenyeji ni kwamba ameweza kujenga Misikiti na ofisi ya Serikali ya Mtaa pale Chamazi Mwembe Bamia.

Jamani wenye ushahidi bandikeni hapa tusijekuwa tunamhukumu bure.

sio lazima
 
hahahahahaaaaaaaa.....duuuuhhh....wabongo noma....eti kabsaaaaa.....unang'ang'ania mali ya mwanaume mwenzio....tafuta yako nawe utoe...usilalie mlango waz cha mwenzio...ndomana hamwendelei kwa kupenda misaada....na msaada sio lazma kijana...nyie mmemwona azam tu...wengine hamuaoni

umeona eeeh...
 
WanaJF,

Hakuna ubishi kwamba Billionia wetu mpendwa SAID BAKHRESSA a.k.a AZAM anamchango mkubwa katika uchumi wa nchi yetu na kwamba anangoza kulipa kodi, kwa hili anastahili pongezi.

Lakini nimejaribu kuchunguza katika Nyanja adimu na muhimu ya elimu, kwa upande wangu sikuona chochote kutoka kwa Bwana huyu, kama kuna mwenye taarifa kuhusu mchango wa Bw. Bakhresa kweye elimu dunia atujuze iwe bara au visiwani

Kwa uwezo wake wa kifedha tulitarajia natuone kwa mfano, AZAM UNIVERSITY OF TECHNOLOGY au AGRICULTURE n.k. Nimejaribu kuuliza wenyeji na majirani zake pale AZAM COMPLEX kama angalao amejenga hata shule ya msingi lakini majibu ya wenyeji ni kwamba ameweza kujenga Misikiti na ofisi ya Serikali ya Mtaa pale Chamazi Mwembe Bamia.

Jamani wenye ushahidi bandikeni hapa tusijekuwa tunamhukumu bure.

kujenga shule na kuuza lambalamba vyote ni ujasiliamali.

Ikiwa bwana SSB ataona kunahaja ya kujenga shule, ili azidishe uchumi wake, basi atajenga. Ni wajasiliamali wangapi ulimwenguni waliojenga shule?

Tumpe uhuru achague cha kufanya ktk kusongesha mbele maisha yake.
Mi naona mchango wake katika elimu kama mjasiliamali mwenye huruma, ni kutoa misaada ktk shule na vyuo vyetu kama alivyofanya kwenye chuo cha suza na kungineko ambako hakutaka kupigiwa tarumbeta, pamoja na kuajiri wasomi!
 
Back
Top Bottom