Hivi yule Harmonise aliyekuwa hana uhakika wa kula na kulala hata angeambiwa aingie mkataba atapewa chumba cha kulala tu na atahudumiwa chakula angeweza kukataa? Priorities za kwanza kwenye maisha huwa ni channels, kuji'brand na kutengeneza solid foundation, mtu mwenye uwezo wa kuweka masharti wakati wa kusainiwa ni yule ambaye label inamuhitaji kwa kujitangaza kuliko yeye anavyoihitaji label katika harakati zake za kutafuta mafanikio na kuya'maintain.
Hata wafanyakazi(waajiriwa) na makampuni kama Vodacom, Tanzania Breweries and the likes kiuhalisia wananyonywa sana kulingana na jinsi kampuni hizo zinavyoingiza mapato huku waajiriwa wakiwa ndiyo wanaovuja jasho kila siku.
Kujitegemea huwa ni jambo zuri sana lakini ni kamari(gamble) pia kwani unaweza kufanikiwa tena sana at times hali kadhalika unaweza ukaangukia pua ukajuta na kutamani kurudi kambi uliyoinyea.
It's a fifty fifty scenario.