Said Mtanda amepwaya Mwanza, impendeze Rais atuletee Kenani Kihongosi ambaye sasa yuko Simiyu

Unamlaumu kwa kigezo Cha jana tu kuvurugana na Simba. Hii sio sawa.
 
Unamlaumu kwa kigezo Cha jana tu kuvurugana na Simba. Hii sio sawa.
Amevaa nguo nyeupe, na jana kaitupia tope ambalo linaonekana kuliko nguo yenyewe. Kufanya jema ni wajibu, hutarajii kusifiwa, Ila ukitenda baya litaonekana
 
Mbona kama wewe unafaa?!...wallah ningekua mshauri wa Rais, ningemshauri akuteue wewe uende pale Mwanza ukatekeleze yote uliyoyataja kwenye bandiko lako...na ungefanikiwa kufanikisha kwa asilimia 75 tuu...Mwanza ingekuwa kama Capetown.
 
Mambo ya ulinzi na usalama hayahitaji njia ambayo haijanyooka (chain of command). Nyie chadema mnataka Mwenyekiti wa Halmashauri awe ndio Mkuu wa Mkoa, au Mkuu wa Mkoa apigiwe kura, kama mikoa ikiwa na wakuu wa mikoa wa vyama tofauti, na jambo la ki usalama linagongana na maslahi yao ya kisiasa, nchi itachafuka.

Mkuu wa Mkoa ni extension ya kura alizopata Rais, uwepo wake mkoani, ni uwepo wa Rais
 
Mchukueni Makonda
 
Kenani Kihongos angepelekwa Arusha, Paul Makonda apelekwe Dar, Albert Chalamila apelekwe Mwanza...Kenani ALIWAHI kuwa Arusha na aliunganisha watu wale sana na ndo pekee atayeweza kuendekeza ya Makonda...Paul Makonda akae Dar MAANA Dar ndio Tanzania yenyewe...kwa maslahi ya Taifa Paul aende Dar...Albert Chalamila aende Mwanza..Mwanza ataiweza sana..Albert ataipaiza Mwanza kiuchumi na kimaendeleo haswa idara ya elimu na biashara
 
Mtanda huyu huyu alijaribu kuivuruga kesi ya ulawiti iayomkabili mmakonde mwenzake aliyekuwa RC Simiyu, hafai kukalia ofisi ya uuma.
 
Wakuu wa Mikoa & Wilaya wengi hawajui mipaka za kazi zao hata JD zao sidhani kama wanazielewa.

Miaka ya Mwalimu ukisikia Mkuu wa Mkoa aisee mtu wa heshima kubwa katika jamii, leo hii ni mtifuano.
 
Wewe si chawa sijui kupe wa Mama Samia mpigie simu tu umueleze hayo majungu yako juu ya Mtanda maana Samia anasikiliza sn chawa kuliko watu wengine.
Hamna majungu hapo
 
Acha majungu kwenye vyeo vya kuteuana. Kama humtaki, gombea Urais ili ukishinda umteue huyo Mkuu wa Mkoa umpendaye.
 
Una mawazo ya kijinga sn, hujui Mkoani kuna RAS naye kateuliwa na Rais
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…