Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe ndo yule bintiMtanda huyu huyu alijaribu kuivuruga kesi ya ulawiti iayomkabili mmakonde mwenzake aliyekuwa RC Simiyu, hafai kukalia ofisi ya uuma.
Kwahiyo RC ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa?RAS ana kazi yake tofauti, katibu Mkuu kiongozi hawezi kufanya kazi za Rais za kisiasa
Naunga mkono hojaMkoa wa Mwanza ni mkoa "injini", kama ni timu, basi mwanza ni " Kiungo mchezeshaji".Kwa Kanda ya ziwa, Mwanza ikipiga chafya, mikoa jirani lazima nguo zipeperuke kutokana na upepo. Hakuna mtu aliyejipata wa Kanda ya ziwa asiyewekeza Mwanza. Mkoa unahitaji damu changa ya amsha amsha.
Mkoa una miradi mingi ya maendeleo ambayo inahitaji kuifuatilia mguu kwa mguu, kuisemea kwa wananchi. Damu changa maana yake akiamka hana haja ya kupima presha wala kisukari kabla ya kuvaa gambuti na kuvuka kwenda ukerewe na ukara kukaa na wavuvi wakijadili changamoto zao, na hata kuvuta kokoro kidogo, sengerema, misungwi, Magu, Kwimba.
Kuingia mashambani kupanda mpunga na wakulima, kupanda juu ya majengo kuangalia kazi ya makandarasi.
Naona kama Mtanda ana asili ya "umwinyi" na yuko katika mikoa ya wachapa kazi. Mikoa yenye asili ya umwinyi, saa nne asubuhi hata supu mitaani hakuna.
Mwanza ina visiwa ambavyo havijavamiwa, hatuoni mkoa ukitenga visiwa kwa ajili ya mahoteli makubwa kama ilivyo Zanzibar. Mkuu wa Mkoa hatumuoni sana saiti. Kulikuwa na tamasha la Balimi la waendesha mitumbwi, limekufa. Hatumuoni Kisesa kwenye kituo cha tamaduni za wasukuma. Hatumuoni akipigia debe barabara za mawe. Hapigii debe shule kama kirumba na kitangiri na pansiansi ziwe za ghorofa. Kule kishiri na Igoma panahitaji shule mpya na vituo vipya vya afya kwa kuwa sasa kuna watu wengi, huko hajawahi hata kufika.
Mpaka sasa Mwanza haina public beach kama ilivyo Coco Beach ya Dar es salaam. Hakuna promotion ya utalii wa ziwa, pale kamanga ferry vijana wanajiongeza wenyewe tu na mitumbwi ya matete, hawapi hata mchongo wa Songoro Marine au Kampuni ya Meli Tanzania (Marine) wawachongee viboti kama corporate social responsibility.
Mwanza kuna jengo ambapo tarehe 18/09/1958, ulifanyika mkutano wa PAFMECA pale karibu na Mwanza Hotel, nani anajua?
Kenani anajua sana ku-mingle na jamii anayoiongoza, tumeona juzi kakutana na upinzani, katatua mgogoro wa Lamadi kwa wajuaji na mambo mengi.
Nashauri kama Rais akiamua kuchekecha wawakilishi wake, basi Mwanza amlete Kenani Kihongosi.
Nasema tu, mimi sio mwana Simba
Unajua muda wake wa kukaa Mwanza?Me. Rais hayo ni majungu. Hakuna Mkuu wa Mkoa mstaarabu, muungwana, mshirikishaji watu, mpenda watu kama Mhe. Mtanda. Kwanza ana muda mfupi hapa Mwanza. Mwache amalize muda wake mpaka muda wa uchaguzi 2025.
Umeona eeehhMbona kama wewe unafaa?!...wallah ningekua mshauri wa Rais, ningemshauri akuteue wewe uende pale Mwanza ukatekeleze yote uliyoyataja kwenye bandiko lako...na ungefanikiwa kufanikisha kwa asilimia 75 tuu...Mwanza ingekuwa kama Capetown.
Huyo ni yeye anajipigia promo, sema kaileta kitaalamu asishtukiwe..Utakuwa unal....... Na kihongosi nini?Kwa Nini upendekeze kihongosi na siyo wewe?
Tafuta helaUpuuzi. Toka uanze kutafuta hujazipata!
Huyu ni kenani anajipigia promo.Mkoa wa Mwanza ni mkoa "injini", kama ni timu, basi mwanza ni " Kiungo mchezeshaji".Kwa Kanda ya ziwa, Mwanza ikipiga chafya, mikoa jirani lazima nguo zipeperuke kutokana na upepo. Hakuna mtu aliyejipata wa Kanda ya ziwa asiyewekeza Mwanza. Mkoa unahitaji damu changa ya amsha amsha.