TANZIA Said Ngamba alias 'Mzee Small wa Ngamba' afariki dunia

daaaaah,jamaa anasikitisha sana,yaani issue ya kumtuma mwakilishi anataka kwenda kuhudhuria yeye,shilingi inazidi kushuka thamani yeye bado anafikiria kuuza sura tena hata misibani,hivi huyu dingi kweli hana washauri?

JK mtu wa watu...rais wetu ana utu sana...hiyo thamani ya shilingi inayoshuka nenda kaipandishe wewe..au mwambie mumeo akkaipandishe,,nyambafu zako
 
ila rais hanakosa hawa ndo waanzilishi na wakongwe wa filamu na maigizo si mbaya
 
chadema hawana utu kabisa,,hawahudhurii misiba,,wanahudhuria harusi tu wakanywe pombe na kitimoto
 
J.K. mtu wa maana sana.

yes mwepesi wa kukimbia ofisi....na ikitokea msiba wa mtu anayemfahamu haraka haraka anafunga ofisi na kwenda msibani. Akitoka hapo si ajabu ukasikia anasafiri kwenda Rio kuangalia viwanja vya mpira
 
[h=3]MAMIA WAMZIKA MSANII MKONGWE WA MAIGIZO NCHINI MZEE SMALL[/h]


Msafara wa magari na waendesha Bodaboda wakiwa katika barabara ya Segerea Kinyerezi wakati wakielekea Makaburi ya Segerea kwaajili ya Kumpumzisha Kwa Amani Mkongwe wa Sanaa ya Vichekesho Nchini Said Ngamba almaarufu Mzee Small

Gari lililobeba Mwili wa Marehemu Said Ngamba aka Mzee Small (la kwanza) likiwa limesimama kwaajili ya Vijana kuubeba Mwili wake hadi kwenye Makaburi ya Segerea jioni Hii

Vijana wakishusha jeneza lenye mwili wa Marehemu Mzee Small kwaajili ya kuelekea kwenye Makaburi ya Segerea




Vijana wakiwa wamepanga mstari kuanzia Barabara ya Segerea Kinyerezi hadi makaburini kwaajili ya kupokea jeneza lenye Mwili wa Marehemu Mzee Small

Vijana wakiwa wamebeba jeneza lenye Mwili wa Marehemu Mzee Small wakielekea kwenye Makaburi ya Segerea Jioni Hii.

Watu mbalimbali wakisubiri Mwili wa Marehemu kuwasili katika makaburi ya Segerea

Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifamba akiwasilika katika eneo la Makaburi ya Segerea jioni hii kwaajili ya kumzika Mzee Small


Mwili wa Marehemu Mzee Small ukitolewa kwenye jeneza tayari kupumzishwa katika Nyumba yake ya Milele katika makaburi ya Segerea.

Watu mbalimbali wakiwasili kwenye makaburi ya Segerea kwaajili ya kumzika Mzee Small. Picha Zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

Umati wa watu wakielekea Kupokea Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mzee Small wakati ulipowasili kwenye eneo la Makaburi ya Segerea.




Wanahabari wakitafuta taswira katika mazishi ya Mzee Small katika Makaburi ya Segerea















Picha Zote na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

Chanzo
:matukio.blogspot
 
Ushiriki wa Bongo Movie ulikua vipi? maana wanaangalia ni mtu gani amefariki
 
Sikusikia,alale kwa amani mahala pema peponi huyo gwiji wa tasnia ya bongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…