Saida Karoli: Meneja wangu amemtapeli Diamond mamilioni, mi nilimpa wimbo bure

Saida Karoli: Meneja wangu amemtapeli Diamond mamilioni, mi nilimpa wimbo bure

Ni kweli umemuinua kijana maana alikuwa kaanza kupotea!
 
Amesahau kwamba hana chake saida. Haki zote za kazi zake ni za mzee meneja lakini asikate tamaa njia bado ipo na taste ya mziki wake ni ya kipekee..asi base sana kwenye kilugha awe na fusion ya kilugha na bongo fleva ...Haoni watora mari cjui ni matusi ila watu wanapagawa nao
 
Mhhhhhh bila shaka umekula tani kadhaa za chumvi,kama hadi leo unamuona Saida msichana.....
PRINCESS NIFAA. WAHAYA HAWAZEEKAGI. WANARUTUBA YA UGALI WA MUHOGO.

WATU WA MJINI WANAZEEKA SABABU YA CHIPS ZEGE MY PRINCESS
 
Muimbaji huyo amedai hizo asilimia 25 za mapato za wimbo ‘Salome’ ambazo zilielezwa na viongozi wa WCB hazijui kwa kuwa hakuhusishwa kwenye hilo.

“Tatizo limekuja kwa meneja wangu aliyempatia Diamond kazi, mimi nimempatia bure Diamond hiyo kazi aitumie,” alisema Saida katika runinga ya KUTV ya nchini Kenya. “Lakini kwenye kusikia masikioni kwangu na kwenye vyombo vya habari kwamba Diamond amempatia pesa milioni 25 meneja wangu wakawa wametengeneza mkataba kwamba huu wimbo utatumika hivi na hivi ila mimi kama mimi huo mkataba siujui na wala sikuuona na wala hawakunionyesha. Mimi ninachojua nimempatia kazi Diamond bure ili aitumie tuinuane wasanii wa Tanzania,”

Pia muimbaji huyo amedai yeye alishiriki kiasi fulani katika kuandaa kiitikio cha wimbo huo kwa kuingiza sauti yake.


Ameshindwa hata kujua kuwa wimbo unabaki kuwa mali ya muandaaji (Producer) ndiyo maana akaombwa consent yake tu and that was it. Elimu Elimu Elimu.
 
53d9e6ec9f303dee1dad65a466a4ce5a.jpg
 
Sallam kama kawaida yake kampiga Saida Chenga ya mwili.

Diamond alitamba siku ile kuwa kuna hela wamempa Saida alafu Saida kaja kutoa siri kumbe aliwapa wimbo bure wao wakaenda kumpa hela meneja.

Kama kawaida yao kuongeza sifuri wapate kiki bado meneja kutoa siri kuwa nae akupewa chochote ulikuwa ujanja ujanja tu
 
Labda atuambie mkataba wake na meneja ukoje! kwenye huo mkataba yeye anafaidika vipi na manager anafaidika vipi, kama anadhulumiwa kwa nini haendi mahakamani? Tunahitaji kujua mkataba kwanza.
 
hivi muta bado anapiga hizi deal za huyu mama dah awe na huruma aisee.
ila ule wanja aiseee.....
 
Wahaya wana tamaa sana, huyo meneja anatia aibu kazi ya umeneja wa wasanii.

Ni wakati wa meneja kuulizwa maswali sasa. Na Saida kama ni meneja wake, lazima angekuwa na majibu kutoka kwa tapeli wake.
 
Hivi hakuna Wahaya wanasheria wamsaidie huyu Dada Kweli? Au wanachojua ni kujisifia na kutoa orodha dhefu ya wasomi walioko UN basi.
 
Back
Top Bottom