Saida Karoli: Najihisi kuzaliwa upya

Saida Karoli: Najihisi kuzaliwa upya

Freelancer Wakala

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2016
Posts
1,193
Reaction score
828
Msanii wa nyimbo za asili Saifa Karoli aliyevuma kitambo amefunguka na kusema kuwa kitendo cha msanii Diamond Platnumz kurudia moja ya kazi yake anajihisi kuzaliwa upya.
1474453601548.jpg

Saida Karoli
Saida Karoli ambaye aliwahi kufanya vizuri na nyimbo kama"Mapenzi kizunguzungu,Kaisiki,Maria Salome na nyingine kibao na alifanikiwa kilele soko la Afrika Mashariki kwa nyimbo hizo na kujipatia umaarufu mkubwa mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Said a Kalori amesikika kwenye clip ambayo ameipost Diamond Platnumz kwenye mitandao yake ya kijamii na kusema kuwa mwanzoni waandishi wa habari walisha msahau walikuwa hawanfuatilii tena,laki I hata baadhi ya watu pamoja na ndugu zake walikua waliambiwa kuwa amekufa lakini baada ya kazi ya Diamond Platnumz kutoka imemrejesha watu kwenye himaya take kwani wameanza kumtafuta na Kumpigia simu sana.
"Mimi nimejisikia vizuri hii kazi tunayofanya ni kwa ajili ya mashabiki,mashabiki ndiyo wadau wetu wanaotufanya sisi,tuwe juu kwa hiyo si kazi ya kwangu Mimi peke yangu,ila Mimi kama Mimi,nimejisikia vizuri kusikiliza kwa sababu hata vyombo vya habari vilinisahau Leo hii vinanitafuta,haya ndugu zangu baadhi na wengine wanajua hata siko duniani wanajua nilishakufa lakini Leo hii naona watu mbalimbali wananitafuta kweli nimefunguka najihisi kuzaliwa upya" alisikika Saida Kalori.

Chanzo:East Africa Television (EATV)
 
Mapromota wezi walimmaliza dada huyu, Diamond Mungu ambariki angalau dada wa watu aache kuishi kishetani
mbona nasikia hela kapewa meneja wake yeye hajapata hata 100
 
Daimond akifanikiwa kumuibua huyu mama alieshia kutumbuiza vilabuni nitamheshimu sana. Watu walitumia kipaji chache halafu wakamtupa kama takataka.
Kuna kutumiana flani kwenye soko, lakini wajibu wa kujitunza na kufanya kazi kwa bidii na kutafuta chaka lingine bado unabaki kwa msanii mwenyewe!
Mbona wakati wanatamba maisha huwa bam bam, hawawekezi? Tunawaonea mapromota wakati mwingine...
 
Naona mazaa amerudi tena na kibao chake cha TETEMEKO LA ARDHI kipo vizuri sana na ujumbe mzuri..

Maza alitakiwa awe bilionea uyu alijaza uwanja wa taifa siku anazindua Chambua kama Karanga...
 
Rwegasira alimkamua sana Saida,eti kwa kuwa amemuibua kutoka kijijini.
Hao mapromota waliwahi kumtelekeza nje ya nchi.
 
  • Thanks
Reactions: ovi
Sio sir huyu mama alitisha enzi zake ila nilikuja kumuona mwanza maeneo ya nyakato anatumbuiza na bendi yake kwenye pub duuh kweli mziki bila usimamiz mzuri ni hovyoo kabisa
 
Back
Top Bottom