Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,584
- 6,136
Ndugu Watanzania,
Imekuwepo Kasumba ya watu kusujudu vitu vya nje kufikia hata kununua fanicha za nje kama meza, makabati, vitanda wakati vya hapa Tanzania ni vyema sana. Utaona mtu anaenda kunywa bia za Makopo na anaona sifa kubwa kwa sababu tu zimetoka nje na anaacha zilizotengenzwa Tanzania.
Utaona mtu anatumia vyakula vya kwenye makopo na hadi nyanya za kwenye makopo na kuanza nyanya safi kabisa kutoka sokoni ambazo akinunua hapo, huyo muuzaji ambaye ni jirani, kesho ataenda tena kwa mkulima kununua.
Vifaa vya ujenzi MADE IN TANZANIA navyo vinaanza kuwa vingi. Bila kujali ni kiwanda cha nani, tununue bidhaa zilizotengenezwa nchi kwetu kwanza na kama hakuna ndiyo tuhamie za majirani zetu, za Africa na mwisho ndiyo tunaweza kuchukua za mataifa mengine.
TAFADHALI: Mwambie mwenzio, mtumie ujumbe wa SMS, Email kuwa kama walivyosema wana Mtwara, basi hii kampeni iwe kwa TANZANIA nzima kuwa TANZANIA KWANZA. Utaifa kwanza, mengine baadaye. Tafadhali hii iwe ni kampeni ya UTAIFA na msiingize mambo ya VYAMA hapa. Mods, naomba atakayeingiza VYAMA au DINI au kitu kingine chochote cha kugawa Watanzania kwenye thread hii basi iondolewe. Hii ibaki kuwa TANZANIA KWANZA.

MADE IN TANZANIA KWANZA.
(2) kwa kawaida usipende kununua cementi zinazotoka nje ya nchi, bali zilizotengenezwa Tanzania. .....kwa sababu ya kusaidia uchumi wetu.........