Saidia Nchi Yako: NUNUA bidhaa MADE IN TANZANIA.

Saidia Nchi Yako: NUNUA bidhaa MADE IN TANZANIA.

Sikonge

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2008
Posts
11,584
Reaction score
6,136
Ndugu Watanzania,

Imekuwepo Kasumba ya watu kusujudu vitu vya nje kufikia hata kununua fanicha za nje kama meza, makabati, vitanda wakati vya hapa Tanzania ni vyema sana. Utaona mtu anaenda kunywa bia za Makopo na anaona sifa kubwa kwa sababu tu zimetoka nje na anaacha zilizotengenzwa Tanzania.

Utaona mtu anatumia vyakula vya kwenye makopo na hadi nyanya za kwenye makopo na kuanza nyanya safi kabisa kutoka sokoni ambazo akinunua hapo, huyo muuzaji ambaye ni jirani, kesho ataenda tena kwa mkulima kununua.

Vifaa vya ujenzi MADE IN TANZANIA navyo vinaanza kuwa vingi. Bila kujali ni kiwanda cha nani, tununue bidhaa zilizotengenezwa nchi kwetu kwanza na kama hakuna ndiyo tuhamie za majirani zetu, za Africa na mwisho ndiyo tunaweza kuchukua za mataifa mengine.

TAFADHALI: Mwambie mwenzio, mtumie ujumbe wa SMS, Email kuwa kama walivyosema wana Mtwara, basi hii kampeni iwe kwa TANZANIA nzima kuwa TANZANIA KWANZA. Utaifa kwanza, mengine baadaye. Tafadhali hii iwe ni kampeni ya UTAIFA na msiingize mambo ya VYAMA hapa. Mods, naomba atakayeingiza VYAMA au DINI au kitu kingine chochote cha kugawa Watanzania kwenye thread hii basi iondolewe. Hii ibaki kuwa TANZANIA KWANZA.

MADE IN TANZANIA KWANZA.

(2) kwa kawaida usipende kununua cementi zinazotoka nje ya nchi, bali zilizotengenezwa Tanzania. .....kwa sababu ya kusaidia uchumi wetu.........
 
sasa na nguo tuvae zipi.....? viwanda vimekufa, viatu tulikuwa na Bora.....wapi Bora...? usiniambie nivae Bata.....nitavaa Next...HM....River Island etc.....na kidogo nitatupia vya Primak mpaka pale Kiltex.....Sunflag et all watakapofufuka......
 
Made in Tanzania:

MAMA_AKIANGALIA_GARI_LINALOTUMIA_SOLA.jpg

thumb_COLOURBOX2566982.jpg
made_in_tanzania_hat-re1977499adec4ee4ab9401be94fe90e0_v9wfy_8byvr_216.jpg
africafecoffee.jpg

NYUMBU-TRUCK.jpg
SO-97-19-RoadThruMikumiSM.jpg
 
Ukitaka kutangaza bidhaa zako, sehemu yenye watu wengi jamani ni JAMIIFORUMS.

Njoo tangaza bidhaa zako na uisaidie JF kuendelea kuwepo hapa Tanzania. Nayo ni MADE IN TANZANIA.

Jamii-Forums.png
 
Kuna promo kubwa inaendelea clouds ambapo commercial breaks wanaweka 'made in Tanzania'.
Wakulugo, je ndio hiyo-hiyo inayoendelea au umekuja na yakwako kivingine?
 
Preta, mbilo hilo nimeandika? Maana utauliza pia magari muendeshe yepi wakati hatuna viwanda.

Unajua kama huu mpango wa MAJIMBO utafanikiwa na kodi iwe inakatwa kwanza na Jimbo na mwisho ni ya Taifa, basi amini kuwa kutakuwa na upinzani hadi wa majimbo. Kama mie nipo hapa Sikonge, basi ntahakikisha sinunui Asali ya Iringa kwa sababu ntawatajirisha jimbo la Iringa. Kwa nini ninunue dagaa wa Mwanza wakati kodi itakwenda Mwanza? Ntanunua kwanza dagaa wa Kigoma kwa sababu ni wa Jimbo langu. Pamba au mafuta ya Pamba, ntanunua kwanza ya Nzega na Igunga na kama hakuna ndiyo ntatafuta ya Shinyanga, Singida au Mwanza nk.

Kama Nguo hakuna, basi hatuna ujanja ila tutanunua za nje. Ila unakuta watu wananunua Mafanicha mabayaaa (Angalia nyumba ya Mchungaji Rwakatare na fanicha za Indonesia sijui. Zile fanicha nyepesi mno halafu za ovyo. Kwa nini nisiende Arusha na kununua mbao za Loliondo ambazo ni nzito au Mninga na kupata fanicha zangu za uhakika?

Kuna bidhaa nyingi sana ambazo hatutakiwi kununua za nje. Kuna umuhimu gani kununua nyanya za Kopo kweli? Kwanza ni SUMU tupu humo ndani na haijulikani kama zimeshaisha ubora wake au bado nzima. Nafikiri unaelewa ninasema nini.

IMG_1191.JPG

sasa na nguo tuvae zipi.....? viwanda vimekufa, viatu tulikuwa na Bora.....wapi Bora...? usiniambie nivae Bata.....nitavaa Next...HM....River Island etc.....na kidogo nitatupia vya Primak mpaka pale Kiltex.....Sunflag et all watakapofufuka......
 
Mimi nazani ni Uzalendo hatuna, kwa sababu Uukijaribu kusoma Historia ya China au Korea Kusini mpaka kufikia Kujitegemea haikuwa rahisi,
 
Ndugu Watanzania,

Imekuwepo Kasumba ya watu kusujudu vitu vya nje kufikia hata kununua fanicha za nje kama meza, makabati, vitanda wakati vya hapa Tanzania ni vyema sana. Utaona mtu anaenda kunywa bia za Makopo na anaona sifa kubwa kwa sababu tu zimetoka nje na anaacha zilizotengenzwa Tanzania.

Utaona mtu anatumia vyakula vya kwenye makopo na hadi nyanya za kwenye makopo na kuanza nyanya safi kabisa kutoka sokoni ambazo akinunua hapo, huyo muuzaji ambaye ni jirani, kesho ataenda tena kwa mkulima kununua.

Vifaa vya ujenzi MADE IN TANZANIA navyo vinaanza kuwa vingi. Bila kujali ni kiwanda cha nani, tununue bidhaa zilizotengenezwa nchi kwetu kwanza na kama hakuna ndiyo tuhamie za majirani zetu, za Africa na mwisho ndiyo tunaweza kuchukua za mataifa mengine.

TAFADHALI: Mwambie mwenzio, mtumie ujumbe wa SMS, Email kuwa kama walivyosema wana Mtwara, basi hii kampeni iwe kwa TANZANIA nzima kuwa TANZANIA KWANZA. Utaifa kwanza, mengine baadaye. Tafadhali hii iwe ni kampeni ya UTAIFA na msiingize mambo ya VYAMA hapa. Mods, naomba atakayeingiza VYAMA au DINI au kitu kingine chochote cha kugawa Watanzania kwenye thread hii basi iondolewe. Hii ibaki kuwa TANZANIA KWANZA.

MADE IN TANZANIA KWANZA.

WAZO LAKI NI ZURI SANA NA KIKUBWA KUPITA ZOTE NI KUTOA AJIRA NYINGI KWA WATANZANIA. wewe fikiria jinsi mturuki alivyojipenyeza nchini mpaka kuanza kuleta suti za kwao na kuuza katika maduka yetu. Hii mimi imeniuma sana kwa sababu bila ya kujijua tumepeleka ajira ya watu kama 200 kule uturuki na wao wanfaidika sasa baada ya kupata soko la nguo zao hapa bongo.

Uturuki baada ya kupata soko tuu hapa nchini, wakafungua viwanda vyao vya kushona nguo na kuanza kuajiri watu wakati sisi tulikuwa na kiwanda cha Ubungo Garment ambacho sasa kimekufa . jamani hata mavazi baada ya kutengeneza wenyewe tunategemea kutengenezewa nje halafu tunalalamika kuwa hakuna ajira?
serikali inabidi ipunguze baadhi ya bidhaa zitokazo nje na ifanye juu chini bidhaa hizo zije kutengenezwa hapa nchini ili watu wapate ajira. hii ni kazi ya waziri wa kazi na ustawi wa jamii na si mwingine.
 
hicho kitanda cha mama Lwakatare hapana.........mweeee.....ni bora nitengeneze cha chuma coz mbao ni ghali.....nitakwenda Aim steel nitachagua black pipe na flat iron size ninayotaka.....nitatengeneza kitanda.....kodi itabaki Chugga.....yippeeeeee......
 
Wala sijaisia hiyo Promo bado maana nikiri kuwa ni mvivu sana kusikiliza Radio. Ila kama na wao wanafanya basi ni poa tu hakuna Ubaya maana wote lengo letu ni moja wa kukaya.

Nimeamua tu kuanzisha kampeni baada ya kusoma ujumbe wa @Pmwasokye hapo juu na kuupenda maneno yake. Nimekuwa mtangazaji sana wa bidhaa za Tanzania na hata Band yangu BORA ya Mziki kwa Tanzania ni JAGWA MUSIC.

https://www.youtube.com/watch?v=vnAPPXVCQQg

https://www.youtube.com/watch?v=LvoRrRSO67o , mambo ya LIWALO NA LIWE.
Kuna promo kubwa inaendelea clouds ambapo commercial breaks wanaweka 'made in Tanzania'.
Wakulugo, je ndio hiyo-hiyo inayoendelea au umekuja na yakwako kivingine?
 
Last edited by a moderator:
Unaona sasa tunaanza kuongea lugha moja? Kwanini kuwatajirisha wa Indonesia na fanicha zao za ovyo? Mambo mengine hapahapa Bongo na bei poa na cha zaidi, unaweza hata kwenda na mchoro wako.
hicho kitanda cha mama Lwakatare hapana.........mweeee.....ni bora nitengeneze cha chuma coz mbao ni ghali.....nitakwenda Aim steel nitachagua black pipe na flat iron size ninayotaka.....nitatengeneza kitanda.....kodi itabaki Chugga.....yippeeeeee......
 
sikonge hiyo ni hoja nzuri sana lakini sijuhi tulipokosea..vitu vya ndani vina bei kuliko ata vya nje...tembelea maofisi yetu ata pale mjengoni 'fenicha' zote za nje..nenda kwa fundi issa mwambie akuchongee kitanda ukimpa advance humwoni tena!!ukibahatika kumwona story nyiingiiii ohh nilifiwa au nilikuwa naumwa nk...fundi nguo hivyo hivyo !!!kuondoa usumbufu watu wanaamua kwenda dukani nunua fenicha mambo yanakwisha....hatuamini vya kwetu maana tunajialibia tunapopewa nafasi...njoo contractors sehemu ya kuweka mifuko kumi ya cement anaweka mitano mingine anajengea kwake magorofa yanaanguka!!!!tunajiharibia wenyewe bwana sikonge...ndio maana wanapenda kwenda kutibiwa nje sijuhi hawaamini ma doctors wetu au hospitali zetu !!!tunajiharibia wenyewe... juice zinatengenezwa nchini lakini bei ni sawa au juu kidogo ya zile zinazotoka nje!!!
 
Hivi yale masofa wanayokalia waheshimiwa bungeni yametengenezwa wapi?
 
Uzalendo ni kununua made in Tanzania???
Huku viwanda vyote mmewauzia WAHINDI!!!! Hapo ni made in Tanzania au made in INDIA?
Labda uzungumzie fanicha za JKT pale keko na zile za MAGEREZA ndo kweli made in Tanzania by Tanzanians!!!!
Vinginevyo ni promotions za wahindi kwa jina letu!!!
(Socialist is me) chinese socialist!!!
 
Mkuu hata China kuna wawekezaji wa nje. Ziko faida lukuki kununua bidhaa za ndani hata kama viwanda vinamilikiwa na wageni.
 
Ndugu Watanzania,

Imekuwepo Kasumba ya watu kusujudu vitu vya nje kufikia hata kununua fanicha za nje kama meza, makabati, vitanda wakati vya hapa Tanzania ni vyema sana. Utaona mtu anaenda kunywa bia za Makopo na anaona sifa kubwa kwa sababu tu zimetoka nje na anaacha zilizotengenzwa Tanzania.

Utaona mtu anatumia vyakula vya kwenye makopo na hadi nyanya za kwenye makopo na kuanza nyanya safi kabisa kutoka sokoni ambazo akinunua hapo, huyo muuzaji ambaye ni jirani, kesho ataenda tena kwa mkulima kununua.

Vifaa vya ujenzi MADE IN TANZANIA navyo vinaanza kuwa vingi. Bila kujali ni kiwanda cha nani, tununue bidhaa zilizotengenezwa nchi kwetu kwanza na kama hakuna ndiyo tuhamie za majirani zetu, za Africa na mwisho ndiyo tunaweza kuchukua za mataifa mengine.

TAFADHALI: Mwambie mwenzio, mtumie ujumbe wa SMS, Email kuwa kama walivyosema wana Mtwara, basi hii kampeni iwe kwa TANZANIA nzima kuwa TANZANIA KWANZA. Utaifa kwanza, mengine baadaye. Tafadhali hii iwe ni kampeni ya UTAIFA na msiingize mambo ya VYAMA hapa. Mods, naomba atakayeingiza VYAMA au DINI au kitu kingine chochote cha kugawa Watanzania kwenye thread hii basi iondolewe. Hii ibaki kuwa TANZANIA KWANZA.

MADE IN TANZANIA KWANZA.

condom za tanzania zinapasuka kama maputo kwanini nisitumie condom za nje

cement ya tanzania zinaangusha majengo we jengo kifusi kimekuwa mchanga mchanga kwanini nisinunue za nje

juice za bakhresa zina ma uchafu chafu kesi zake zimeletwa hapa mara nyingi nadhan tumeshuhudia kwanini nisinywe TANG

makochi na fanicha ziko pale keko barabarani zimepangwa vumbi lote la barabarani liaishia pale unanunua kochi jeupe lakini ukiliangalia ni jeusi kwanini nisiende kwa Mchina

suti unashonesha ila unapata suti baada ya kumweka fundi polisi ndio anamalizia nguo yako kwanini nisinunue Gucci

viatu vile vya mbeya design mbovu kiatu kimekaa kama mkate bwana na sio ngozi kwanini nisinunue viatu vya Italy

Sabuni zinazotengenezwa na wajasiliamali wetu hazikawii kuchubua mikono kwanini nisinunue Dettol

ARV mnawatengenezea feki

Bia Bingwa ulikuwa ukinywa lazima uharishe kwanini watu wasinywe heinekeen
 
Ata hizi bidhaa za nje zinazoingia zinachangia sana pato la taifa zikisimamiwa vizuri ndio maana tra wanasema wanakusanya 600ml kwa siku chache tu...huu ni ushuru wa bidhaa za nje,ukiingiza cement kwa mfano Tbs wanatakiwa kupima ubora na gharama ya kupima ni 350,000/tsh hachilia mbali ushuru wa tra na gharama za port...kama tax ikisimamiwa vizuri ni sawa tu bidhaa za nje zije watu wapate ajira na tra wakusanye mapato..nchi nyingi zinakua kwa kukusanya ushuru na kuutumia vizuri,tukitengeneza bidhaa nzuri zenye ushindani si lazima tutegemee soko la ndani twaweza ku export nje..india,pakistan,bangladesh,nepal ni nchi zinazoongoza kwa kunywa chai yaani hawa jamaa wanakuywa sana chai na Kenya wame monopolise soko lao la chai wanapenda sana chai ya kenya,tutengeneze bidhaa nzuri zitapata soko la ndani na nje...ukienda Geita mananasi yanaoza wakati tunakuywa juice za nchi zisizona mananasi..njombe nyanya zinaoza ndoo moja tsh 500 tungekuwa na kiwanda kizuri cha tomato ketchap zenye ubora mzuri tungeuza nje na ndani ya nchi...tulikuwa na kiwanda cha dabaga nakikumbuka sana pale iringa lakini hakuna mazingira mazuri kwa viwanda maana umeme ni wa kubahatisha sana...tutengeneze bidhaa bora soko la ndani na nje ni kubwa sana
 
Back
Top Bottom