Saidia Nchi Yako: NUNUA bidhaa MADE IN TANZANIA.


hahahaha nimewakubali lakini chumvichumvi si ya mda mfupi namna hiyo na haiwekwi kwenye kitu kama mchicha wa siku saba..sawa?
 


Bia Bingwa ulikuwa ukinywa lazima uharishe kwanini watu wasinywe heinekeen
kuna safari,serengeti,ndovu,eagle,balimi,kilimanjaro......Made in Tanzania ndo mpango mzima..mtaani kwetu kuna supermarket mbili tatu......Mimi huwa naenda moja tu kwa sababu wanauza vitu vinavotengezwa Tanzania kwa kwenda mbele......na hii nimeinakili kwa majirani zetu Wakenya ....akikuta bidhaa mbili dukani ya Kenya na nchi nyingine lazima achukue ya Kenya
 
Ni suala jema sana kuhamasisha matumizi ya bidhaa zinazozalishwa na Watanzania ili kuwaunga mkono na kukuza Uchumi wa nchi. Lakini ni suala jema zaidi kuhamasisha ubora wa bidhaa hizo ili ziweze kukidhi mahitaji ya walaji na Soko, kwani kwa kufanya hivyo zitaweza kushindana na bidhaa nyingine zinazotoka nje ya nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…