mugah di matheo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2018
- 6,307
- 12,410
Saido na Ambudo wametimuliwa kambini baada ya kutoroka mazoezini na kwenda disco baada ya mchezo wa Biashara dhid ya Yanga ulioisha 1-1.
Hivyo hao wachezaji hawatakuwa sehemu ya kikosi jumamosi
===
SIKU mbili kabla ya mchezo wa nusu fainali Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kati ya Simba na Yanga, kocha mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amewatimua Saido Ntibazonkiza na Dickson Ambundo kambini mjini Shinyanga.
Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti imezipata ni kwamba, sababu za kutimuliwa kwao inatajwa kuwa ni kutoroka kambini na kwenda mtaani kinyume na utaratibu.
Simba na Yanga watakwaana Jumamosi Mei 28 katika mchezo ambao utaamua nani atacheza hatua ya fainali na timu hizo zinakutana zikiwa na kumbukumbu ya kugawana pointi kwenye michezo miwili ya ligi msimu huu.