Saikolojia: Jinsi ya kuondokana na mawazo yanayoumiza au kuhuzunisha

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285

Msongo wa mawazo unaweza kukufanya ushindwe kufanya shughuli zako za kila siku kwa ufanisi. Jambo la kufurahisha ni kuwa msongo wa mawazi unaepukika, leo nimechambua baadhi ya mambo ambayo yanaweza kukuwezesha kuepuka kupata msongo wa mawazo.

1. Usiweke Malengo ambayo Hayafikiki
Kila mtu ana uwezo na vipawa vyake tofauti na mtu mwingine, unapoweka malengo yako hakikisha unazingatia uwezo, vipawa na muda ulionao ili kuweza kuyafanikisha. Usiweke malengo sababu watu wengine wameweka hayo,au ukaweka muda kiasi fulani sababu watu wote wameweka hivyo, daima zingatia uwezo wako ili malengo yako yaweze kufanikiwa na kuepuka kupata stress'.

2. Jifunze Kukubali Changamoto
Katika maisha huwa tunakutana na mambo ambayo hatukutaka kukutana nayo na pia tunashindwa kupata yale tuliyoyataka, karibu kila mtu huwa anapitia hali hii kwa namna moja au nyingine. Jifunze kukabili changamoto na sio kusikitika kwa nini mambo hayajawa kama ulivyotaka na kubaki ukisononeka. Jaribu kukubali mambo kwa busara zaidi, na utulivu huku ukitafakari nini cha kufanya ili kulipata lile ulilo kusudia. Changamoto iwe ni chachu ya wewe kuzidi kukazana na kujaribu zaidi.

3. Fanya Maamuzi Pale Unapopaswa
Kutokufanya maamuzi katika muda sahihi hyleta wasiwasi hofu na msongo wa mawazo. Uwe na ujasiri wa kuamua mara baada ya kutafakari pande zote kwa makini na kuona faida na hasara za kila upande. Usihofu sana juu ya kuweza kufanya makosa hadi ukaishia kupata msongo wa mawazo, mara nyingine watu hujifunza kutokana na makosa.

4. Kuwa na Mipango
Hili nimeshaliongelea sana, angalia hapa . Kutokuwa na mipango ni sababu moja kubwa sana inayoweza kukuletea msongo wa mawazo.

5. Usiweke Jambo Linalokusumbua Moyoni
Pale unapokutana na jambo ambalo umeshindwa kulitatua ni vyema ukamshirikisha mzazi wako au mlezi, rafiki wa karibu, mume au hata mshauri. Jifunze kutokuweka mambo yanayokuumiza moyoni maana katika hali hiyo ni rahisi sana kupata msongo wa mawazo. Uwe na tabia ya kupeleka wasiwasi na hofu zako zote mbele za Mungu kwa maombi na pia kuongea na mtu ambaye unajua atakuwa msaada kwako.

6. Jali Mwili Wako
mara nyingi tunakuwa na shughuli nyingi kiasi cha kuusahau mwili na kuuchukulia tu kwa juu juu. Ni muhimu sana mwili wako uwe katika hali nzuri na afya bora ili uweze kufanya kazi zako vizuri na kwa wepesi. Hakikisha unakula chakula chenye virutubisho bora na pia unakunywa maji ya kutosha. Fanya mazoezi ya viungo mara kwa mara na pata muda wa kutosha wa kupumzika kila siku.





PIA UNASHAURIWA KUSOMA HAPA:
- Athari za msongo wa mawazo (Stress) mwilini
- Jinsi ya kudhibiti msongo wa mawazo katika biashara yako
- Saikolojia: Jinsi ya kuondokana na mawazo yanayoumiza au kuhuzunisha
- Kufanya ngono kunapunguza msongo wa mawazo
- Yathibitika: Mbegu za kiume huwaondolea wanawake sononi au msongo wa mawazo.!



BAADHI YA USHAURI NA MAWAZO YA WADAU KUHUSU NAMNA YA KUONDOKANA NA MSONGO WA MAWAZO
---
---
---
---

Common sources of work stress​

Certain factors tend to go hand-in-hand with work-related stress. Some common workplace stressors are:
  • Low salaries
  • Excessive workloads
  • Few opportunities for growth or advancement
  • Work that isn’t engaging or challenging
  • Lack of social support
  • Not having enough control over job-related decisions
  • Conflicting demands or unclear performance expectations
================

Watafiti wa magonjwa wanadai kuwa msongo mkali wa mawazo wakati wa ujauzito unaweza kusababisha hitilafu katika uumbaji wa mtoto na hatimaye mtoto kuzaliwa akiwa mlemavu.

Ripoti ya watafiti hao inazidi kuthibitisha matokeo ya tafiti zilizopita kuwa mama mwenye msongo wa mawazo wakati wa ujauzito kutokana na mambo kama kufukuzwa au kuachishwa kazi, kutengana na mwenza wake au kufiwa ana hatari ya kuzaa mtoto mwenye ulemavu kama vile midomo sungura (cleft lip na cleft palate) au matatizo kwenye uti wa mgongo (spina bifida).

Jopo la watafiti wa kidenmark likiongozwa na Dr Dorthe Hansen walifanya uchunguzi ili kuthibiitisha ukweli na uhakika wa dhana hii.

Wakitumia rikodi za taarifa za kitabibu za kipindi cha miaka 12 kutoka 1980 mpaka 1992 kutoka masjala ya Taifa ya kitabibu, watafiti hao waliweza kuwatambua wajawazito wote waliokumbwa na matatizo makubwa ya kimaisha wakati wa ujauzito na hata miezi 16 kabla ya kupata ujauzito. Matatizo makubwa ya kimaisha yaliyochunguzwa yalikuwa kukumbwa na msiba wa ndugu au jamaa wa karibu, ndugu au jamaa wa karibu kulazwa hospitali kwa mara ya kwanza baada ya kugundulika kuwa na kansa ya aina yeyote au ndugu au jamaa wa karibu kupatwa na ugonjwa wa mshtuko wa moyo. Mambo haya yalichunguzwa kwa kigezo kuwa, mjamzito yeyote aliyewahi kukumbana nayo ana hatari kubwa ya kuwa katika msongo wa mawazo bila kujali tabia yake, kama ana watu wa kumfariji au uwezo wake wa kukabiliana nayo.

Jopo hilo lilichunguza maendeleo ya mimba kwa wajawazito 3,560 ambao walikumbana na matukio hayo kwa kulinganisha na wajawazito wengine 20,299 ambao hawakukumbana na hali yeyote ambayo ingewasababishia kupata msongo wa mawazo wakati waujauzito.

Matokeo ya uchunguzi wao yalionesha kuwa ulemavu na hitilafu za viungo kwa watoto waliozaliwa ulikuwa mara mbili miongoni mwa kundi la wajawazito waliokumbwa na msongo mkali wa mawazo ikilinganishwa na kundi la kinamama ambao hawakuwa na hali hiyo.

Kadhalika ilionekana kuwa wanawake waliowahi kukumbwa na hali kama hiyo katika ujauzito mbili mfululizo za nyuma walikuwa katika hatari kubwa zaidi ya kuzaa watoto wenye ulemavu wa viungo tofauti na wale waliowahi kupatwa na hali hiyo mara moja tu au wale ambao hawakupatwa kabisa.

Ilionekana pia kuwa tukio lililoongeza uwezekano wa mtoto kuzaliwa akiwa na ulemavu wa viungo ilikuwa ni iwapo mjamzito atafiwa na mtoto wake mwingine mkubwa wakati akiwa katika miezi mitatu ya mwanzo wa ujauzito wake huu wa sasa. Hatari ya kuzaa mtoto mlemavu iliongezeka iwapo kifo cha mtoto huyo mkubwa kingetokea bila kutarajiwa kwa mfano kwa ajali.

Watafiti wanasema kwamba, msongo mkali wa mawazo huchangia kuathiri uumbaji wa mtoto aliye tumboni kwa kusisimua uzalishaji wa homoni ya cortisone. Homoni hii husababisha ongezeko la kiwango cha sukari katika damu na upungufu wa usambazaji wa hewa safi ya oksijeni kwa mtoto, mambo ambayo husababisha kutokea kwa hitilafu katika uumbaji wa viungo vya mtoto hatimaye kusababisha ulemavu wa viungo vya mtoto.

Uwezekano mwingine ni kuwa msongo mkali wa mawazo humchochea mama mjamzito kutumia zaidi vileo vyenye alcohol na pia kula lishe duni hali ambayo huongeza madhara zaidi kwa kiumbe kilicho tumboni. Hata hivyo Professor Peter Hepper wa Chuo Kikuu cha Queen's cha Belfast, anasema hakushangazwa na mtokeo ya utafiti huo.

Anasema kuwa, "tunafahamu msongo wa mawazo husababisha mabadiliko ya kifiziolojia katika mfumo wa mwili wa mjamzito, na hivyo hakuna sababu kwanini mabadiliko hayo yasimfikie pia mtoto aliye tumboni kupitia kondo la nyuma na kumuathiri. Matokeo haya yanazidi kuthibitisha kile tulichokuwa tukikifahamu tangu awali kuwa msongo wa mawazo wa muda mrefu kwa mwanamke una madhara makubwa kwa mendeleo ya uumbaji wa mtoto aliye tumboni na hivyo basi hakuna budi kufanyike kila njia kuwasaidia wajawazito walio katika hali hii ili waweze kujifungua watoto walio na afya njema na salama."

Matokeo ya utafiti huu pia yalichapishwa kwenye Jarida la kitafiti la The Lancet medical journal.
 
Kujirusha kwa raha zako pia husaidia sana katika kuondoa stress, ukiingia club na kujirusha kwa masaa kadhaa kwa raha zako ukitoka hapo roho kwatuuuuu. Namshukuru Mungu sana hii kitu mie naisikia tu namuomba iendelee kuwa hivi.








 
Last edited by a moderator:
Count your blessings. Stress inaletwa na tamaa. Gari zuri walitaka wewe, pesa nyingi, watoto wazuri, nyumba nzuri, kazi nzuri! Kuna mtu anatafuta afya tu haipati! Angalia jinsi ambavyo umejaaliwa mambo ambayo hata wengine hawajajaaliwa.

Ofcoz hanging out (courtesy of BAK) nayo lazma Ikutoe stress.

A massage and nice coffee nayo ni dawa murua
 
Last edited by a moderator:
High life siyo!? haya banaaaa....hapo kwenye blue ni ukweli usiopingika hata kidogo.




 
Last edited by a moderator:
NJIA ZINGINE ZA KUKABILIANA NA MSONGO WA MAWAZO (STRESS) HIZI HAPA


Msongo wa mawazo ama stress kwa kiingereza, ni tatizo ambalo kwa bahati mbaya sana limeendelea kuwa kitu cha kawaida sana kwa wanaadamu katika zama tulizo nazo. Katika miaka hii tuliyo nayo, ni sahihi kabisa

kusema kuwa, takriban wanaadamu wote walio hai wamekuwa wakikabiliwa na tatizo hili.Kuna baadhi ya aina za msongo wa kimawazo, ambazo zinaepukika na nyingine ni ngumu kuziepuka ila unapaswa kujua jinsi ya

kukabiliana na shinikizo la msongo wa mawazo pale linapokukabili. Hapa ni baadhi tu ya njia zilizo rahisi ambazo unaweza kuzitumia kukabiliana na hali hii pindi unapojikuta umetumbukia ndani yake

1. Jifunze kusema hapana
Hii ni katika mambo yako binafsi au kazi yako, unaitumiaje hii hapana? Unajua maofisini kuna swala la kupeana vikazi visivyoeleweka hata vimetokea wapi, yaani hujamaliza hili unaletea jingine hata kama sio kazi yako sasa jifunze kukataa hizi kazi zisizo za kwako ili mradi tu mfurahishe tu. hivyo hivyo vitu vidogo vidogo ndivyo vinavyokuletea msongo wa mawazo.

2.Jiepushe na watu ambao mara nyingi wanakusababishia Stress,
Unajua ukikaa chini na kufikiria utagundua kuna mtu flani au kundi flani la watu ndo linalokuleta msongo wa mawazo, sasa kaa nao mbali kabisa.

3. Simamia mazingira yanayokuzunguka.
Mazingira yanakuzunguka yanaweza kuwa sababu ya stress zinazokukumba, mazingira yapo nayozungumzia mimi hapa? njia unayotumia kwenda kazini au kurudi nyumbani ina foleni sana? hiyo nayo inawea kuwa sababu ya stress ulizonazo, lakufanya epuka matumizi ya

barabara kwa wakati huo, mazingira ya soko wakati wakufanya manunuzi ya bidhaa mbali mbali yanakupa stress? nenda katika supermarket maana kwa kiasi flani kuna utulivu na hali ya hewa nzuri

4.Epuka Hasira za haraka, kuna ya mambo yanayohusu dini
Siasa au maisha yako binafsi huwa yanakupa msongo wa mawazo basi jitahidi kuepukana nayo katika mazungumzo yako ya kila siku kwasababu yatakupa

hasira na kukufanya ukasirike na hili hupelekea kuwa na msongo wa mawazo, ukiingia sehemu ukakuta watu wanaongelea swala hilo epuka nao ili usiweze kuchangia na kujikuta unaingia katika mgogoro wa nafsi

5.Tengeneza orodha ya vitu anavyotaka kufanya sikuhiyo asubuhi tu ukiamka,
Mara nyingi unapaswa kujua mambo ambayo ni ya lazima kuyafanya kwa siku ambayo unaianza ili ikifika jioni usiwe na viporo, katika orodha

yako tenganisha orodha hiyo kwa vitu vya lazima kufanya na vitu vya kawaida ambavyo hata usipovifanya hazitakuharibia ratiba yako. kujua kipi cha lazima ni moja ya njia kubwa ya kupunguza msongo wa

mawazo.Naomba niishie hapa kwa leo maana nimewaonjesha yale ninayoyajua na ambayo nimejifunza, swala la kuondoa msongo wa mawazo linapaswa kuangaliwa kiundani zaidi maana ni pana sana, hapa juu nimeongelea

kuepuka stress ambazo si za muhimu ila kuna swala la saikolojia ambalo kwa kadiri siku zinaendelea, tutaligusia.

ninawatakieni afya njema MziziMkavu.
 
Mkuu kweli umenena,kutamani mambo makubwa ni janga la dunia!
 
maisha ni mafunzo na hasa ukiishi na watu ambao kila siku wanakuacha kwa maendeleo... kwangu mimi nimejifunza kuishi mwenyewe, hasa kwamba kila kitu nakubaliana nacho aidha naweza ama siwezi.

Pia nimekubali kuishi maisha yangu mwenyewe na sio ya kuigiza, pia kuttokuwa na marafiki wengi ambao wanamahitaji makubwa kuliko uwezo wao...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…