1. upate mpenzi, hii huwa inasaidia sana kuwa na mtu wa kuongea nae, kujuliana hali, n.k na ukipata mtoto maisha yako yataongezeka kusudi la kuendelea kuishi.
2.Jichanganye na watu, hizi stori na kujuliana hali zinasaidia sana na hata unapopata tatizo kuna mtu wa kukufariji.
3.Tafuta kazi, hata kama wewe ni mhitimu wa chuo usijifungie ridhiki kwa kusubiria kazi ya taaluma uliyosomea, kazi siku hizi kupata ni ishu nzito maana wasomi wapo kibao wenye sifa za kupata kazi ila kazi chache, Unaweza kujiajiri kwenye upishi maana hii biashara uhakika wa kupata chochote ni mkubwa sana, ila pia waweza kujifunza na kufanya kazi nyingine kama ususi, ushonaji, ufugaji, kilimo, n.k. ukikaa hivi hivi utaboreka na kuanza kupata mawazo ya kuboreka na maisha.
4.Usijiongize kwenye vilevi kudhani kwamba ndio vitatatua hali yako, hapa utakuwa teja wa kilevi,
5.Fanya mazoezi, ikifika hata jioni we kimbia tu au kufanya mazoezi mengine, hii itakupunguzia sana mawazo na unaweza pata kampani mpya unavyotoka.