BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Leo kuna jambo nimelisikia kutoka kwa Mtaalamu mmoja wa Saikolojia aliyehojiwa na Clouds FM akisema matukio ya Ukatili yamekuwa yakiendelea kutokea kwasababu Watoto wanaoishi katika mazingira hayo wanaharibiwa kisaikolojia na hali hiyo inawafanya kuja kutenda Ukatili pale wanapokuwa wakubwa.
Mtaalam huyo amesema ndio maana Watoto wengi wanaoishia Mazingira yanayowaonesha Vitendo vya Ngono katika umri mdogo wanakuja kuwa tabia chafu zikiwemo kupenda ngono kupita kiasi au kupenda ngono na Watoto wadogo au Watu waliowazidi umri.
Pia, Mtoto mwenye umri huo akishuhudia wazazi, ndugu au jamaa wa karibu wakitamka maneno makali, vipigo ubakaji wengi wao wanakuja kuwa watendaji wa mambo hayo.
Sasa ndugu yangu, mwanao anakuwa katika mazingira gani? Anaona na kusikia vitu gani kila wakati?
Tafakari