nzalendo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 12,106
- 12,916
watu wengi wanaosambaa sana nchi zingine na hata mikoa mingine huwa population yao inakuwa kubwa mno na kunakuwa na tatizo kubwa linalowafanya wasambae hivyo.mfano wachaga wana tatizo kubwa la ukosefu wa ardhi kule kilimanjaro hivyo utakuta ndio wanaongoza tanzania kusambaa mikoa yote.
Ukienda kenya,ghana,nigeria na china zina idadi kubwa ya watu na matatizo makubwa ya ukosefu wa ardhi, ajira na makazi na hivyo kuwafanya wawe kazi yao kuzunguka kutafuta maisha nchi zingine.nchi ikiwa na uhakika wa maisha hata wa kiwango kidogo kwa mahitaji yale makubwa matatu ya chakula,malazi na mavazi utakuta watu si wahamaji sana kuzurura nchi za watu sababu walipo japo wanapata kidogo lakini wanaona chatosha kuendelea na maisha.nchi nyingi tu zina watu wachache sana nje na watu wake wako vizuri kwa viwango vyao sababu satisfaction is subjective kwa kila mtu. Si kila mtu unachoona wewe kizuri wakihitaji mtu mwingine naye aona akihitaji. Waweza ona kwenda nje ya nchi ni kuukata mwingine anaona ujinga tu wala hawazi na hana mpango wa kwenda nje ya nchi hata umpe tiketi ya bure na umlipie kila kitu.ameridhika alipo apatacho na aishivyo.
Kusambaa sana nchi za watu hakumaanishi kuwa mtu atokako kuko vizuri au asiyesambaa basi hana akili na hajui kutafuta fursa nchi zingine.wahenga wanasema ukitukana mke wa mtu haifanyi mkeo awe mzuri kama ni mbaya.
thats bravo roger