Izy_Name
JF-Expert Member
- Apr 9, 2020
- 772
- 1,733
Mkataba huo mpya utakuwa na maboresho makubwa kwenye mshahara wa staa huyo, kutoka kiwango anacholipwa kwa sasa cha Pauni 70,000 kwa wiki na kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi kwenye kikosi hicho kinachonolewa na Mikel Arteta, Pauni 300,000 kwa wiki sawa na pesa ya Kitanzania Sh858 milioni kwa wiki, Sh122,532,429 kwa siku, Sh5,105,518 kwa saa.
Atampiku Gabriel Jesus kwa mshahara mkubwa huko Emirates, ambapo Mbrazili huyo analipwa Pauni 250,000 kwa wiki, wakati aliposajiliwa kutoka Manchester City kwa ada ya Pauni 45 milioni majira ya kiangazi ya mwaka jana.
Kocha Arteta na mkurugenzi wa michezo Edu wanataka kumpa Saka kiwango anachostahili kulipwa kutokana na ubora wake ndani ya uwanja huku jambo hilo likimfanya kuwa mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi kwenye kikosi hicho.
Kwenye rekodi za Arsenal, mchezaji ambaye aliweka historia ya kulipwa mshahara mkubwa zaidi ni Mjerumani, Mesut Ozil, aliyekuwa akilipwa Pauni 350,000 kwa wiki. Mkataba wa Saka utakwisha 2028 na hilo litafuta minong’ono yote ya kuhusu mchezaji huyo kuwindwa na timu nyingine wakiwamo vigogo wa Ligi Kuu England, Man City na Liverpool.
Gabriel Martinelli alishasaini mkataba mpya hadi 2027 na kumekuwa na mazungumzo juu ya dili la beki William Saliba.
Saka amefunga mabao 12 na kuasisti mara 10 kwenye Ligi Kuu England msimu huu akitisha pia na timu ya taifa.