Sakata Binti wa Yombo: Familia ya anayetajwa ‘afande’ kuwashtaki wanaomchafua kwenye mitandao ya kijamii

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Familia ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (SSP), Fatuma Kigondo imesema inafikiria kufungua mashtaka dhidi ya wote waliosambaza kwenye mitandao ya kijamii kuwa ndugu yao amehusika kutuma vijana kufanya ukatili kwa binti anayedaiwa kuwa mkazi wa Yombo Dovya, Dar es Salaam.

Akiandika katika ukurasa wake wa X (zamani Twitter), Mwanasheria wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Emmanuel Muga amesema familia hiyo inataka kuhakikisha haki inatendeka na ukweli wa jambo hilo unawekwa wazi.

Amesema familia hiyo imeeleza kuwa SSP Fatuma siyo afande anayezungumziwa kwenye video hiyo na kwamba ndugu yao ni Ofisa wa Polisi mwenye cheo cha SSP na si ASP kama inavyoelezwa katika mitandao ya kijamii.

“Familia imethibitisha kuwa SSP Fatuma ni mjane na hana mume ambaye angeweza kuporwa kama ilivosemwa,” ameeleza.

Aidha, amesema famili hiyo imefafanua kuwa washukiwa wa ubakaji wamebainika kuwa wanatoka kwenye vikosi vingine visivyo chini ya amri ya SSP Fatuma, hivyo inawapa maswali kuwa ofisa huyo angewezaje kutoa maagizo kwa washukiwa hao, iwe ni kisheria au isivyo kisheria.

Chanzo: Nipashe
 
nafikiria kufungua mashtaka
Kwanini wafikirie? Kwanini wasifungue kabisa waje na ushahidi kwamba watu wanamsingia na si yeye aliyewatuma...Then DPP akavute PIDIEFU TISIARAEI waone CONVO zao kisha ziwekwe hadharani...Ubaya Ubwela.
 
Lile lishangazi kuna jamaa analidinya mdinyo wa kulimwemwesa, wanawatu watu wazima ( mashangazi) ukiwamwemwesa vizuri Huwa wanakuwa Na wivu balaa, asione umesimama Na mwanamke ni kosa kubwa Na yuko tayari kufanya lolote ili kulinda penzi lake, naandika kitu ambacho kimewahi kunitokea Mimi..
 
Si anadinywa na mwamba kutoka my gresheni 😂😂😂

Kuhusu amri kwa wale madogo mbona ipo wazi kuwa hawa watu wanakuwa na mitandao mirefu sana. Ataonekana hana akili endapo angewatuma vijana waliopo chini yake
 
Familia ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (SSP), Fatuma Kigondo imesema inafikiria kufungua mashtaka dhidi ya wote waliosambaza kwenye mitandao ya kijamii kuwa ndugu yao amehusika kutuma vijana kufanya ukatili kwa binti anayedaiwa kuwa mkazi wa Yombo Dovya, Dar es Salaam.

Akiandika katika ukurasa wake wa X (zamani Twitter), Mwanasheria wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Emmanuel Muga amesema familia hiyo inataka kuhakikisha haki inatendeka na ukweli wa jambo hilo unawekwa wazi.

Amesema familia hiyo imeeleza kuwa SSP Fatuma siyo afande anayezungumziwa kwenye video hiyo na kwamba ndugu yao ni Ofisa wa Polisi mwenye cheo cha SSP na si ASP kama inavyoelezwa katika mitandao ya kijamii.

“Familia imethibitisha kuwa SSP Fatuma ni mjane na hana mume ambaye angeweza kuporwa kama ilivosemwa,” ameeleza.

Aidha, amesema famili hiyo imefafanua kuwa washukiwa wa ubakaji wamebainika kuwa wanatoka kwenye vikosi vingine visivyo chini ya amri ya SSP Fatuma, hivyo inawapa maswali kuwa ofisa huyo angewezaje kutoa maagizo kwa washukiwa hao, iwe ni kisheria au isivyo kisheria.

Chanzo: Nipashe
Hahaa atubu yaishe aache kupambana na watanzania hawatamwacha salama
 
Back
Top Bottom