Nominee
JF-Expert Member
- Sep 5, 2017
- 464
- 1,260
Ni haki na wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha rasilimali za nchi yake hazichezewi hovyo.Nawapongeza nyote munaotoa maoni yenu ya kuukosoa huu mkataba ila chonde chonde, tujitahidi kuongeza umakini tunapokosoa.
Kikawaida,imani ina nguvu sana kwenye suala la ushawishi. Unaweza kushangaa mtu tangu abalehe hajawahi kukanyaga msikitini wala kanisani lakini ukikashifu dini yake anabadilika kuwa mbogo.Hiyo ndo nguvu ya imani.
Hili suala la bandari lijadiliwe bila kuweka mitizamo ya kidini. Nimeona baadhi ya watu wanasema "Mama anataka kuhonga bandari kwa waislamu wenzake wa uarabuni". Hii sio kauli yenye afya. Huyu ni Rais wetu sote,sio Rais wa waislamu tu.
Je, na waislamu nao wakiamua kufukua mikataba ya hovyo iliyofanyika kipindi cha Marais wakristo,patakalika kweli?.Tunashindwa nini kujadili maswala ya kitaifa bila kuingiza udini?
Kulikuwa na ulazima gani wa kupeleka waraka makanisani ama misikitini?.Munafahamu madhara ya hiki munachokifanya?.
Sisi sote ni WaTanzania bila kujali dini zetu wala makabila yetu.Tusimame kutetea na kukosoa mikataba kwa sababu ni Watanzania na sio kwasababu aliyeingia mkataba ni Mkristo ama Muislamu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI AFRIKA.