VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Kuanzia Mawaziri, Wakurugenzi na hata Wabunge wa chama chetu (CCM) na viongozi wa kichama na kiserikali wameshindwa kuiona, kuipata na kuijibu hoja ya wananchi kuhusu mkataba wa uwekezaji kwenye Bandari zetu. Ni mkataba kati ya Tanzania na Emirati kupitia kampuni ya DP World.
Hoja kuu ya wananchi ( wale wanaoitwa wapinzani; viongozi wa kidini; wananchi wa kawaida na wananchi wasio wa kawaida) ni kuhusu vipengele vya mkataba. Mkataba huzungumza kupitia masharti yake yaliyomo kwenye mkataba husika. Masharti huwekwa kama vipengele viitwavyo ibara au vifungu au aya na kadhalika.
Wananchi, kila wanaposoma vipengele vya Hati ya Makubaliano na Mkataba, wanatishika. Wanaisikia sauti ya kuogofya kutokana na vipengele hivyo kuzungumza. Sauti hiyo ya kuogofya ya vipengele vya mikataba hiyo ndizo zinazotakiwa kutolewa majibu na Serikali.
Serikali na wadau wake niliowagusia wao wanang'ang'ania kuelewesha na kutaka kueleweka juu ya manufaa na faida za mikataba hiyo, yaani uwekezaji/ubinafsishaji/ukodishwaji wa bandari yetu. Wao wanasisitiza kuhusu manufaa ya kibiashara na kiuchumi tutakayoyapata. Hawazungumzii na kueleweka kuhusu vipengele vyenye kelele vya mikataba husika.
Kwenye mkataba wowote wa kitaifa au kimataifa (kama ulivyo wa Bandari), vipengele kama pande husika za mkataba; majukumu ya kila pande; haki za kila pande; muda wa mkataba; sheria zitumikazo; utatuzi wa migogoro; uhuishaji wa mkataba; taarifa za kimkataba; kuvunja mkataba;usiri na haki miliki ni zaidi ya mambo muhimu. Yote haya yana ukakasi uletao wasiwasi na yamekosa majibu.
Sasa, Serikali inaposhindwa kutoa majibu/ufafanuzi juu ya mikataba hii ya Bandari, sisi wananchi tuchukue hatua gani?
Kosa lolote kuhusu Bandari ni hatari!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Chato, Geita)