Ujamaa...
Naanza na hili la ''kujitapa.''
Kama nikitaka kujitapa sitaweka hayo kuwa mimi ni mwandishi.
Ningekueleza kama nataka kujitapa ni miradi mingapi ya wachapaji wakubwa wa vitabu nimeshirikishwa kuandika na vitabu nilivyoandika vimechapwa vipo sokoni na vinasomeshwa.
Kwani wewe uliposema umesoma vitabu vingi umetaka kujitapa?
Nataka kukufahamisha kuwa kati yetu na Nyerere au kati ya Nyerere na wengi aliowakuta katika kupigania uhuru wa Tanganyika ni suala la historia hii na mchango wa Waislam na nini kimepatikana kwao?
Mimi hapa hilo ndilo suala langu kubwa ninalosomesha hapa JF kiasi wamenipa ''Certificate of Appreciation.''
Naamini hili unalifahamu.
Mimi siko katika mjadala huo unaouleta hapa wa Vijiji vya Ujamaa nk.
Ikiwa unataka tujadili hayo mimi simo jadili na wengine.
Muafaka wa kitabu changu nimeupata miaka zaidi ya 20 iliyopita pale Prof. Haroub Othman alipomkabili Julius Nyerere na nakala ya kitabu changu na kumuomba na yeye aeleza historia yake kwani historia niliyoandika ya Abdulwahid Kleist Sykes imefuta mengi ambayo watu walikuwa wanayaamini kuhusu yeye.
Haya nimekupa kwa kifupi.
Nyerere akakubali kuwa kiandikwe kitabu cha maisha yake yeye wakati ule alikuwa mgonjwa anaumwa hawezi kuandika.
Nyerere na yeyote awaye yule hawawezi kumpuuza Abubakar Mwilima wala yeyote yule anaemfahamu yeye toka enzi za kudai uhuru.
Historia hii niliyoandika ipo katika Dictionary of African Biography (DAB) mradi wa Harvard na Oxford University Press, New York.
Haya hayajapata kuwa mambo ya kupuuzwa.
Hapa kulikuwa na njama ya kufuta historia ya kizazi cha jamii yangu, historia ya zaidi ya miaka 100.
Pale walipokuwa wameamini kuwa wamefanikiwa kuifuta historia hiyo ndipo niipokuja na kitabu cha Abdul Sykes mwaka wa 1998.
View attachment 2263220View attachment 2263231View attachment 2263233