Sakata la DP World: Kamati ya Bunge Yaahirisha Kupokea Maoni ya Marekebisho ya Sheria za Maliasili ikitaka Ufafanuzi wa Serikali

Umeaongea points sn, ubovu unaanza hapa kwanza
Angalia hawa wastaafu kupitia TISS watu wanaotuwekea kuongoza, hivi mtu km Bashungwa, Ndumbaro, Kijaji, Pinda mdogo, hata spika, MaDC wengi tu hawana uwezo na sifa hata kuwa VEO... kwa kutizama tu..unaona sifa yoyote ya kiuongozi kwenye sura za watu hao??? mtu mwenye sifa ya kuwa kiongozi hata kwa sura yake tu utaona kipo kitu anacho cha kiuongozi, TISS wanataka watu wa aina hii ili wao ndio wafanye maamuzi, huyo waliyemuweka ni km picha tu..hawataki watu wako na sharp mind na wenye independent brain wapewe nafasi kwenye uongozi sababu si rahisi kumdrive mtu wa aina hiyo..! wao ndio wametufikisha hapa..watanzania tudeal na chanzo cha tatizo..mambo ya DPW ni matokeo ya tatizo kubwa tunaliruka hata kulitaja! tunakalia kubishana na faiza foxy au mwashamba..
 
Hakuna vetting yoyote inayofanyika zaidi ya maigizo
 
Vipi serikali ya UAE / Emirati ya Dubai inaweza kubadilisha sheria ili Tanzania, tuwekeze UAE/ Dubai?
 
Mkuu tatizo ni nini? Lipi? Tunalitatuaje?
 
Maelezo mengi ya nini badisheni uo mkataba au la muachane nao
Hata kusingekuwepo hayo makubaliano ya DPW, hizo sheria ilibidi zibadilishwe haziendani na stabilisation clauses za mikataba ya kimataifa. Clauses ambazo hakuna mwekezaji ataingia mkataba wa muda mrefu bila ya kuziweka.

Shida ni hizo sheria zenyewe katika ulinzi wa asset na rights za mwekezaji, lakini si IGA.
 
Yaani huyu Mwarabu amekuja kutubadilishia sheria zetu kwa faida yake.
Kwa faida ya Tanzania, mtegemee mabadiliko makubwa kila sehemu, msiishi kimazowea, ieleweni kwanza falsafa yake ya RRRR.

mkiielewa Hamtopata shida na kustuka kwa sheria zitazokuja kubadilishwa, ni nyingi sana, mpaka Katiba itabadilishwa:

 

Shida serikali zetu haziko makini kwenye mikataba.

Ndio maana Magufuli akiweka hiyo sheria kulinda rasilimali za Taifa.

Hatujawahi kushinda kesi yoyote muhimu, IPTL, Escrow, Gesi, Madini, mengine zote.

Tulitumia ubabe tu kuishinda Acacia., Barrick Gold. Ndio maana Magu akaona aachane na huo ujinga na upumbavu wa kupigwa mabilioni kwa kuweka sheria na kulinda rasilimali zetu. Ukitaka mkataba fuata sheria zetu za ndani.
 
Hamna kitu hapo, zitapitishwa tu. Hapo labda wamerudisha tu huenda kuna mahali kuna nukta ama kama imekosekana...
 
Hiyo siyo ",approach" sahihi kwa utawala.

Kiutawa ulio bora , ni lazima uwe Resilience, ielewe R hiyo ya falsafa ya mama Samia utanielewa namaanisha nini.
 
Hakuna anaekataa nia njema ya hizo sheria, lakini haziendani na clauses za mwekezaji na yeye kwenye kulinda uwekezaji wake wa miaka mingi.

Njia pekee ya kupambana ni kutengeneza wanasheria wetu na negotiators wetu watusaidie kufunga hiyo mikataba na wenye uwezo wa kuitetea hiyo mikataba panapo migogoro.

Lakini tupeleweke wenyewe wanasheria kwenye tribunals. Wanapokuwa huko kwenye ‘cross examination’ waseme hawakulala vizuri jana yake, au unabeba sister duh ndani ya safari hata kama uwezo wake mdogo kwa sababu unazozijua mwenyewe team leader. Unapeleka mtaalamu wa sijui wa maswala gani ya sheria kujadili commercial contracts.

Halafu ukitoka hapo ulaumu mkataba mmbovu baadae na ukivunja kiholela baada kuona unapunjwa ukienda mahakamani ukashindwa kesi useme umeonewa mahakamani.

Unaweza kuona najiona mjuaji ila ukweli ni hivi kama wanasheria wengi wameshindwa kuilewa hiyo IGA ambayo ni framework tu, basi Tanzania ina nafasi ndogo sana ya kushinda kesi za uwekezaji nje ya nchi ambazo ni fully ‘commercial contracts’ huo ndio ukweli wenyewe.
 
Flamework ni msingi muhimu , ni flame, nguzo zinazoibeba nyumba, jengo, familia, Taifa, mikataba yote inayokuja.

Makubaliano ya msingi ndio hayo IGA. Kutatua matatizo, haki, wajibu migogoro, tofauti. Ingawa kwenye HGA kunakuwa na specifics.

Wanasheria wetu huwa wako upande wa wawekezaji huku wakifanya kazi serikalini. Wanapiga huku na Kule kwa kukosa uzalendo. Serikali yetu mara nyingi ipo upande kwa maslahi ya wageni tunahiwaji w wawekezaji sahihi. Mara nyingi ni wapigaji wakishirikiana na serikali yetu.

Mkabata wa Gesi, IPTL, Sakata la Escrow, Issue za Loliondo, Ngorongoro zinalisaidiaje hili Taifa?
 
Upo sahihi 100% frameworks ndio nguzo ya msingi na baadhi ya clauses hapo kwenye IGA ni sehemu ya aspects za mikataba ya mbele.

Lakini hakuna kilichopo hapo ambapo hutakikuta katika BIT ya nchi nyingine yoyote; hizo ni standard clauses katika mikataba ya biashara za kimataifa kwenye kulinda investments.

Bila ya hayo mambo mwekezaji anakuwa anachukuwa risk kubwa sana katika usalama wa uwekezaji wake na hawa wenzetu wana experience tosha ya kugeukwa mbeleni ndio maana wanataka hayo mambo yawepo katika mkataba au sheria ya nchi kwanza.

Solution ni moja tu kama tunataka kufanya biashara na dunia, ni kuwajengea uwezo watanzania wa kuweza kujadiliana consideration ya hiyo mikataba (na hayo mambo huwa ni siri hatuoni n’go) vinginevyo tutaendelea kuibiwa tu na kushindwa kesi kwa sababu atujifunzi hayo majadiliano ni tenchical.

Tutalaumu miaka nenda miaka rudi wakati mchawi wetu sisi wenyewe.
 
Hiyo siyo ",approach" sahihi kwa utawala.

Kiutawa ulio bora , ni lazima uwe Resilience, ielewe R hiyo ya falsafa ya mama Samia utanielewa namaanisha nini.
Yeye aliyeianzisha aielewe na kuiweka kwenye vitendo..resilience anatakiwa kuwa nayo yeye na watu wake sio sisi, wanaharibu na kutufanyia maigizo kisa wana excuse ya sijui rrrr..we believe in action fullstop, muda wa kupindua pindua misemo mara kkk mara rrr ulishapita kitambo..we need ACTION, wakiharibu sisi hatuna muda wa kuchambua nani ndio nani, ni kuwamwaga wote, wakaulizane huko watakakokuwa wenyewe kwa wenyewe.
 
Uzalendo unatokana Sana na uongozi, kiongozi, utamaduni, uwazi, uwajibikaji na kuwajibishwa, katiba nzuri.

Wataalmu wote, wanasheria, wachumi hawatafanikiwa wakiwa na Viongozi wabovu.
 
Kuna nchi kama Saudi, UAE, Singapore, Hong Kong, Malaysia, South Korea, Oman, Namibia, Botswana hata Magufuli asingekubali mikataba kama hii.

Wanafuata katiba zao, Sheria zao zinafuatwa na wananchi ni wazalendo. Sio kama Wana akili kuliko Watanzania ni systems, structures zinawafanya wawe hivyo.
 
So as to fulfil Malicious Agendas, and nothing else !!
 
Hawa wenzetu wakishika nchi wanakuwa bize kukwapua kuliko kuangalia wengine
 
Wabunge akili zimeanza kuwarudia.
Kupiga plaste ukuta uliobomoka kazi kwer kwer!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…