denooJ
JF-Expert Member
- Mar 31, 2020
- 18,509
- 68,228
Salaam..!!
Kama tujuavyo lile sakata la Fei na Yanga kuhusu suala la mkataba namna lilivyoendeshwa kwa magumashi na TFF kwa kushirikiana na wanasiasa, na jinsi maamuzi ya kesi ile yalivyokuwa ya ajabu, baada ya TFF kudai Fei ni mchezaji wa Yanga Sc bila kusema amekiuka vipengele gani kwenye mkataba wake.
Sasa taarifa zilizopo rasmi ni kwamba, Fei Toto amesaini mkataba mpya na utopolo wenye thamani ya milioni 350 za kitanzaniaa ili kurejea jangwani, mpaka kufikia hapa, inaonesha wazi, Fei ndie alikuwa na haki kwenye lile sakata.
Kwasababu, huwezi kwa akili ya kawaida ukamuongezea mkataba mpya muajiriwa wako aliyevunja mkataba wa awali kinyume cha sheria, kitendo cha uto kumuongezea Fei mkataba kinaonesha mchezaji ndie alikuwa na haki, na bado ni tegemeo kwao, ndio maana Nabi kila siku alikuwa akihangaika kupiga simu za kubembeleza kwa mchezaji.
Mwisho nitoe wito kwa wanasheria wetu wa makaratasi hapa JF, haya mambo ya kisheria siku zote sio ya kukariri kama hesabu za darasani, eti kilichopo kwenye mkataba wako, lazima kiwepo kwenye mkataba wa mwenzio, huko ni kujidanganya, kisheria kila mkataba unaamuliwa na vipengele vilivyopo kwenye mkataba husika, sio nje ya hapo.