Sakata la Fei Toto, Yanga inachekesha na kusikitisha

Sakata la Fei Toto, Yanga inachekesha na kusikitisha

Habari wakuu,

Ni dhahiri kwa hali ilipofikia inaonyesha fika kuwa Yanga wameamua kutia aibu brand ya klabu na mashabiki wao kuijumla.

Hii ni kuhusiana na sakata la Feitoto
Kila dalili zinaonyesha kuwa Fei haitaki Yanga lakini Yanga wanaonyesha ung'ang'anizi wa hali ya juu kwa mchezaji huyo, jambo linalotafsiriwa kama ni aibu kwa klabu upande wa wadau mbalimbali wa soka.

Tayari taswira inaonyesha kuwa Fei ni mkubwa kuliko Yanga kwa vitendo vinavyoonyeshwa na Yanga. Kutokana na hili hata Mama Fei mwenyewe anashangaa kwa nini Yanga wamekuwa Sikio la kufa kwa mteja wake!.

THIS IS INSANE FOR THE CLUB!
Tukumbuke nyuma kidogo Simba SC ilivyoonyesha hadhi yake mbele ya wachezaji wake mahiri kama Singano Messi na Emmanuel Okwi kudhihilisha ukubwa wa klabu mbele yao.
THIS IS HOW MUST BE!

Okay tuachane na hayo tuje kwenye ukweli sasa, Kama Yanga wanatambua mchango wa Fei kwenye klabu yao, kwa nini wasitimize au kumpatia stahiki zake ikiwemo na vigezo vyake anavyohitaji!?

Karibu Tanzania nzima inafahamu ni jinsi gani Feisal Maestro alivyoipenda sana Yanga, kiasi cha dhahiri kudhihilisha kuwa Yanga ndio waliomkosea kijana wao kwani si rahisi Feisal kuibadilika Yanga kufikia hatua hiyo.

Ikumbukwe mchezo huu mchafu haujaanza leo kwa klabu ya Yanga kutaka kudhulumu stahiki za wachezaji wake, na mara kadhaa kesi hizi zimepelekwa TFF na ngazi zingine za juu, endapo ukiangazia sakata la Kakolanya na Morrison.

Itoshe kusema dharau kwa wachezaji wa ndani zikome kwani kinachoangaliwa ni kiwango na si utaifa. Pili, Yanga ijitathmini maana kuhonga kwenye ngazi za Uongozi haiwezi tosha mbele ya haki ya mtu!.

Naomba wachezaji mjifunze kwa hili ambalo YANGA wanafanya kwa wachezaji wa ndani. Kwa kweli inasikitisha sana.

View attachment 2535389
Subiri tarehe 6 mkuu kihere here Cha nini
Screenshot_20230303-134418_1.jpg
 
Wewe hukuona mtoa mada alichokiandika kuwa kinashusha hadhi? Tena hadhi ya taasisi kubwa kama Yanga, nanukuu

"Ni dhahiri kwa hali ilipofikia inaonyesha fika kuwa Yanga wameamua kutia aibu brand ya klabu na mashabiki wao kuijumla."

Na kisha hakuishia hapo kaja kukazia kwa kimalkia tena, nanukuu

"THIS IS INSANE FOR THE CLUB!"

Mwambie kwanza mleta uzi aanze kwa kuheshimu taasisi za watu aache lugha za kejeli wakati hata sheria yenyewe haijui.
Akikurudishia tusi au dharau kitakachojibu ni wewe si yanga.Mtatukanana kwa umoja wenu uzoefu unanionesha hivyo.maumivu ya kichwa huanza pole pole.
 
Ukiona mtu amekomalia swala la Fei basi jua kabisa ni tahira na mpuuzi, hivi umewahi sikia habari ya Mane na liver?, Vipi kipindi kile Theo na Asernal?. Ujinga na ungubali umetuja watanzania kisa kutaka haki isiyotambulika kisheria?.
 
Akikurudishia tusi au dharau kitakachojibu ni wewe si yanga.Mtatukanana kwa umoja wenu uzoefu unanionesha hivyo.maumivu ya kichwa huanza pole pole.
Nimemwambia kuwa ana upeo mdogo, kisha nikawasilisha hoja zangu kwanini nimemwambia ana upeo mdogo. Hivyo ilikuwa ni yeye kuonesha kuwa ana upeo mkubwa wa mambo kwa kujibu hoja zangu. Pole sana maana ishu ya Feisal kwenu ni zaidi ya ubingwa wa NBC premier league. Endeleeni kupambana mkuu msichoke na huko CAS mpelekeni hadi ashinde kesi.
 
Nimemwambia kuwa na upeo mdogo, kisha nikawasilisha hoja zangu kwanini nimemwambia ana upeo mdogo. Hivyo ilikuwa ni yeye kuonesha kuwa ana upeo mkubwa wa mambo kwa kujibu hoja zangu. Pole sana maana ishu ya Feisal kwenu ni zaidi ya ubingwa wa NBC premier league. Endeleeni kupambana mkuu msichoke na huko CAS mpelekeni hadi ashinde kesi.
Umeniunganisha kuwa mwanachama wa simba bila kunilipia kadi, wakati mimi nilisimama kwenye utu tu.Feisal hata akilipwa milioni mia mbili hanigawii japo.Mungu awajalie mumpate tena mkuu.
 
Una upeo mdogo sana wa kufikiria.
Mshahara wa milioni nne, Feisal alisainiwa na nani kwenye mkataba? Alikuwa amelewa alivyokuwa anasaini? Alishikiwa bunduki wakati wa kusaini? Hakuona ni ndogo wakati anasaini? Je aligoma kusaini mpaka aongezewe au alilidhika nayo?

Unataka Yanga iachane na Feisali sawa je waachane kienyeji au kisheria? Kama kisheria unajua ni taratibu zipi za kufuata timu inayomuhitaji Feisal?
Feisali ni mkubwa kuliko Yanga.
 
Kwanini swala hili TFF imeamua kulifanya siri haitaki kutoa mchanganuo wa kanuni zilizotumika kuhukumu pamoja na sheria aliyovunja Feisal kila mtu aone

Hiyo ndio hoja yangu mimi
Kwani shauli ni kati ya nani na nani?
 
Kwa nini TFF wafanye unavyotaka wewe wafanye, na wasipofanya kwamba kuna ukakasi? Wanabanwa na sheria ipi kufanya hivyo?
Sio wafanye navyotaka mimi, bali wafanye fair kiuwazi kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwenye mashtaka yaliyopita wakitoa fursa kwa watu kuhoji

Ukakasi unakuja kutokana na mwenendo wa shitaka lilivyo wailishwa na namna lilivyokuja kuamuliwa

Shtaka lilidai Feisal amevunja mkataba, maamuzi yanakuja kuwa Feisal ni mchezaji halali wa Yanga (two different things)

Pamoja na hivyo kumkuta mchezaji akiwa na hatia bado hajawajibishwa (maana yake hakuvunja sheria)

Hii controversial ndio iliyopaswa kuwekwa bayana kila mtu ajue ni sheria ya kifungu gani ambayo imeamua, waweke ufafanuzi kama ambavyo walifanya kwenye kesi ya Morrison
 
Kwamba hajawajibishwa inamaana hajavunja sio hoja sawia, Yanga hoja yao iliyowafanya kwenda TFF ni kwamba Feisal ana mkataba nao, anaetoa adhabu ni mwajiri (Yanga ataamua anamuwajibisha vipi kulingana na mkataba) na unaweza isishangaze baadae huko akamfungulia tena madai ya kutotumikia kimkataba (hiyo itakua issue yao nyingine)

Ni kesi ngapi hazijaitiwa press conference na hijawahi kua issue? kwa mfano kwenye kesi ya Morrison TFF waliamua against Yanga na wakafanya press, Yanga wakaenda CAS na still CAS wakaamua agaist but hakukua na press walifanya CAS, je ni sahihi Yanga kudoubt hukumu ya CAS kwa kua hawakufanya press?
 
Kwahiyo wewe ulitaka waamuaje ili ionekane imefanya fair?

Umesema shtaka linadai kuwa Feisal amevunja mkataba, je hapo kwanza unatambua mchezaji akivunja mkataba maanake lengo lake ni kutokuwa mchezaji wa sehemu husika?

Maamuzi ya kusema Feisal ni mchezaji halali wa Yanga maanake taratibu za uvunjani wa mkataba uliotumika na muhusika haukuwa sahihi hivyo bado yumo ndani ya mkataba wa Yanga.
 
Kwamba hajawajibishwa inamaana hajavunja sio hoja sawia, Yanga hoja yao iliyowafanya kwenda TFF ni kwamba Feisal ana mkataba nao, anaetoa adhabu ni mwajiri (Yanga ataamua anamuwajibisha vipi kulingana na mkataba) na unaweza isishangaze baadae huko akamfungulia tena madai ya kutotumikia kimkataba (hiyo itakua issue yao nyingine)

Ni kesi ngapi hazijaitiwa press conference na hijawahi kua issue? kwa mfano kwenye kesi ya Morrison TFF waliamua against Yanga na wakafanya press, Yanga wakaenda CAS na still CAS wakaamua agaist but hakukua na press walifanya CAS, je ni sahihi Yanga kudoubt hukumu ya CAS kwa kua hawakufanya press?
Mkuu makolo watakukausha koo tu,hawana wajualo hao mbu3
 
Kwanini swala hili TFF imeamua kulifanya siri haitaki kutoa mchanganuo wa kanuni zilizotumika kuhukumu pamoja na sheria aliyovunja Feisal kila mtu aone

Hiyo ndio hoja yangu mimi
Je ni sahihi kusema CAS waliamua kufanya siri na kutaka kuficha mambo (walikua na ajenda ya siri kuinyima haki Yanga) kwa hukumu yao dhidi ya Young Africans Vs Morrison?
 
Kwamba hajawajibishwa inamaana hajavunja sio hoja sawia, Yanga hoja yao iliyowafanya kwenda TFF ni kwamba Feisal ana mkataba nao, anaetoa adhabu ni mwajiri (Yanga ataamua anamuwajibisha vipi kulingana na mkataba) na unaweza isishangaze baadae huko akamfungulia tena madai ya kutotumikia kimkataba (hiyo itakua issue yao nyingine)

Ni kesi ngapi hazijaitiwa press conference na hijawahi kua issue? kwa mfano kwenye kesi ya Morrison TFF waliamua against Yanga na wakafanya press, Yanga wakaenda CAS na still CAS wakaamua agaist but hakukua na press walifanya CAS, je ni sahihi Yanga kudoubt hukumu ya CAS kwa kua hawakufanya press?
Hapo ndio mnazidi kunichanganya

Yani Yanga imepeleka kesi mahakamani ili itolewe hukumu

Mahakama imetoa hukumu halafu nayo Yanga tena inakuja kutoa adhabu kupitia hukumu

Umeiona paradox hiyo?

***************************
No sio kila kesi inawekwa hadharani, kuna kesi ambazo hazina pressure au hazina attention kubwa ni kesi fulani ndogo ndogo ambazo watu hawazifatilii na wala hawazijui.

Na ndio maana ilikpokuja kwenye ishu ya Manara kulingana na Title yake na jinsi anavyofahamika na jamii wakaona ni vyema kuijulisha jamii.

Kesi ya Morrison ilikuwa wazi, vifungu vya sheria viliainishwa na sababu ziliwekwa. Na TFF walikuwa wanafanya hivyo kuweka wazi ili kuondoa shaka kwa watu ambao walikuwa wanaweza kufikiria kinyume.

Yale maswali yaliyoulizwa pale na waandishi wa habari ndio maswali ambayo watu wengi walikuwa wanataka wapewe ufafanuzi, waandishi wa habari walituwakilisha wapenda soka na watatiliaji wa lile sakata.

Hata majibu ya CAS yalikuwa open, ilitolewa barua ambayo ilielezea kila kitu ikiwemo sheria iliyovunjwa na faini, pamoja na utetezi wa Yanga ambao ulikuwa disputed kulingana na kutafsiri vibaya vifungu vya sheria.
 
Je ni sahihi kusema CAS waliamua kufanya siri na kutaka kuficha mambo (walikua na ajenda ya siri kuinyima haki Yanga) kwa hukumu yao dhidi ya Young Africans Vs Morrison?
CAS haina utaratibu wa kufanya press, ila TFF upo, CAS ikihukumu kesi, majibu yanatumwa TFF na TFF ndio ina share kwa umma hayo majibu.

Swala la Morrison lilianzia TFF ambapo huko kila kitu kilikuwa bayana watu tuliweza kupima hoja regarding sheria za mahakama zinavyo sema

So point yangu haikuwa tu kuitaka TFF ifanye press conference, bali kuweka mchanganuo wa hukumu ilivyofanyika kupitia hata press release tu.
 
Back
Top Bottom