Sakata la Fei Toto

Sakata la Fei Toto

Aende sasa akakae na timu yake avunje mkataba. Siyo aendelee kujificha kama digidigi. Aachane pia na hao wapuuzi wake wanaompotezea muda na fedha zake.

Mambo ya kusema mimi ni wakili wa Drogba! Sijui nilisimamia mkataba wa Emmanuel Eboue, Simon Msuva, nk. Unaihusu nini klabu ya Yanga na mchezaji wake?
Faisal(Toto) acha Kuwa kama mtoto,jinasue kwenye hayo makucha ya🦁.Umepewa fursa ya kumalizana na mwanchi🤔
 
Namsikitikia sana huyu mtoto. Atasahaulika kama hajawahi kucheza mpira yote sababu ya ushauri mbovu aliopewa.
 
Mdogo wetu Feisal anaua kipaji yake
Kabisa. Katika dunia ya mpira kila siku aliyokuwa nje ya uwanja ni siku moja ya upungufu wa uwezo wake kimpira.

Kufanya mazoezi na kushiriki mechi ni vitu viwili tofauti. Asijidanganye kuwa anafanya mazoezi.
 
Mpira nidhamu, hayo anayofanya ni utovu wa nidhamu
Mwisho wa siku atakapokuja poteza relevance hata hao washauri wake watamkimbia.

Ni haki yake kupigania maslahi yake lakini angeyapigania huku akionyesha uwezo wake uwanjanj na kukuza kipaji chake.

Hata Yanga ingeona umuhimu wa kukaa nae chini. Lakini sasa hivi yanga ishajua inaweza kuendela bila Fei toto hivyo haina uhitaji nae tena.
Na huku ndio kuporomoka kwa thamani yake.
 
Mwisho wa siku atakapokuja poteza relevance hata hao washauri wake watamkimbia.

Ni haki yake kupigania maslahi yake lakini angeyapigania huku akionyesha na kukuza kipaji chake.
Angeoenesha kipaji zaidi na angepewa anachotaka… wanampotosha kumeishakuwa na wachezaji wazuri kuliko yeye walipo anza utovu wa nidhamu wakapotea mazima.. nidhamu muhimu sana mchezoni
 
Aende sasa akakae na timu yake avunje mkataba. Siyo aendelee kujificha kama digidigi. Aachane pia na hao wapuuzi wake wanaompotezea muda na fedha zake.

Mambo ya kusema mimi ni wakili wa Drogba! Sijui nilisimamia mkataba wa Emmanuel Eboue, Simon Msuva, nk. Unaihusu nini klabu ya Yanga na mchezaji wake?
Wa elewa ni wachache na ndio wako nyuma yake
 
Hivi kwa nini sheria zetu zimeandikwa kwa lugha ya hao wacheza eksi
 
Nataka kuelewa, nini kinamfanya Fei asiende Yanga mwenyewe kuvunja mkataba?
Anajua alichokifanya ni ujinga na aibu kwani alikuwa na fursa nzuri ya kukaa na viongozi wake wakaja dili mkataba wake ila njia ya kinafiki aliyopitishwa na washauli wake ndio imemfikisha hapo alilpo, anaona haibu kwa kuwa kapita njia ya usaliti...
 
Aisee!
Vijana bhana😀😀
 
Ukiondoa maagizo ya wanasiasa na mahaba ya utimu, Hii kesi ni nyepeai Fei anashinda mapema sana,

Nilikua napitia mkataba wa fei na yanga na vipengele vya kanuni na sheria, TFF inaenda kuaibishw kwa kushindw kusimamia na kulimaliza hili shauri.

ManTycon wa sheria za soka tumeamua kuingilia kati kumuokoa kijana dhidi ya manyangau yasiyojua thamani ya mchezaji hasa wazawa
 
Back
Top Bottom