Sakata la Feisal Salum linahusiana vipi na siasa za ndani ya CCM?

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Ngoja leo niwape za ndani ndaniii kabisa.

Kuna mwanasiasa mmoja ambaye kwa miaka ya hivi karibuni amejipenyeza katika mambo ya mpira ili kutafuta ushawishi wa kisiasa.

Wote tunajua kuwa toka Mwendazake aondoke, kumekuwa na mtifuano wa chini chini ndani ya chama kati ya wale waliokuwa wamewekwa pembeni na wale aliokuwa amewaweka karibu. Sasa huyu mwanasiasa alikuwa anaingia ndani ya circle ya karibu ya Mwendazake na kutoka katika hali inayoonyesha kuwa pande zote mbili hazimuamini 100% ingawa zimekuwa zinamtumia maana anaonyesha ana personal ambition kali za kisiasa kwa hiyo wanacheza naye kwa step.

Hili sakata la Feisal limewekwa mtego kwake kumkumbusha kuwa hana nguvu au ushawishi kama ule aliokuwa anajiaminisha kuwa anao. Amehusishwa katika jitihada za kuokoa jahazi bila kujua yupo katika mchezo asioujua na akitumia madaraka yake vibaya ili kujitutumia kuonyesha hashindwi kitu, atajitengenezea maadui ndani ya chama bila kutarajia na hilo litakuwa anguko lake la kisiasa.

Siyo pesa wala vitisho vimemtikisa kijana mdogo.
 
Wahi hapo Lumumba kabla ofisi hawajafunga ukachukua buku7 yako ili kesho ukafungulie mwaka
 
Taarifa yko haina macho
 
Ndiyo umeandika nini mkurugenzi! Mbona hueleweki?
 
Mimi ni Simba ila siyo vyema kumtaja Mwigulu kimafumbo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…