Sakata la Jezi za Taifa Stars: Nani Aliruhusu Nini kati ya Makonda, Mwana FA, TFF na Sandaland?

Sakata la Jezi za Taifa Stars: Nani Aliruhusu Nini kati ya Makonda, Mwana FA, TFF na Sandaland?

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Hapa kuna maswali kadhaa ambayo naamini TFF na Wizara wanapaswa kuyajibu waziwazi.

Jezi hizi zilifikaje hatua ya kuzinduliwa, kupromotiwa na kuanza kutangazwa rasmi kama jezi za Taifa Stars kama kweli Wizara haikuwa na taarifa wala haikutambua mchakato huo?

Naibu Waziri alionekana akiwa amevaa jezi hizo na hata kuzitumia kwenye promotion. Hii ina maana gani? Je, Naibu Waziri hakujua kwamba Wizara haikuwa imeidhinisha jezi hizo, au kulikuwa na mawasiliano ndani ya Wizara ambayo hayakuwa wazi?

Pili, kama Sandaland ina mkataba halali na TFF na tayari imetumia gharama kubwa kutengeneza, kusambaza na kutangaza jezi, nani atawajibika endapo itathibitika kuwa mchakato ulikuwa na kasoro?

Cha kushangaza zaidi, kwanza tunaambiwa “hii sio jezi ya Taifa Stars”, kampuni inasema imeharibiwa brand yake na inataka kuchukua hatua za kisheria, halafu baada ya siku mbili tunasikia mkataba wa mzabuni unataka kuchunguzwa na kuangaliwa upya.

Sasa swali la msingi ni hili: tatizo lilikuwa kwenye jezi, kwenye ubora, kwenye mkataba, au kwenye mchakato wa kuzipitisha?

Kama jezi hazina kiwango, kiwango hicho kilipimwa na nani kabla hazijazinduliwa?
Kama mkataba una matatizo, uliingiaje?

Kama Wizara haikushirikishwa, kwa nini hatua hazikuchukuliwa kabla ya jezi kuzinduliwa na kutumika?
Na kama mkataba ni halali, kwa nini suala limeibuka baada ya kampuni tayari kutumia fedha na kuanza biashara?

Soma Pia: Mzabuni wa Jezi Taifa Stars Sandaland kumpeleka Makonda Mahakamani

TFF yenyewe sasa inasema suala liko kwa mamlaka za juu. Basi Watanzania tunataka tuone mnyororo mzima wa maamuzi, siyo tu mwisho wa story.

Maana hapa kuna kampuni imeingia gharama, kuna TFF, kuna Wizara, kuna Naibu Waziri aliyepiga promotion, na kuna Taifa Stars inayotakiwa kuwakilisha taifa.

Nani aliruhusu nini, kwa tarehe gani, na kwa mujibu wa mkataba gani?

Hilo ndilo jibu ambalo umma unahitaji sasa. 🇹🇿
 
Kuhusu jezi nitapingana waziwazi na BASHITE. Zile jezi ni nzuri sana tu! Na pia zina sifa zote za kuitwa jezi za timu ya Taifa. (Ifahamike wazi sina maslahi binafsi na huyo Sandaland).

Ila kwa sababu hawa wote ni maccm, kwa kweli ninafurahia wakiparuana.
Je nani ana makosa hapo?
 
Nahisi pia kuna shida kati ya FA na Makonda
Katika portfolio zao nahisi Mawaziri na Manaibu Mawaziri hawapewi miongozo ya utendaji kazi na mipaka ya majukumu yao

Huu mwenendo wa kuadhirishana hadharani kwa viongozi hasa wa kisiasa umeasisiwa katika utawaka wa marehemu JPM na haujaachwa sababu haujawahi kukemewa

Nakumbuka enzi za utawala wa Mkapa Waziri wa kazi ajira na Vijana Sebastian Kinyondo alikua hakubaliani na Naibu wake Wiliam Lukuvi.

katika awamu ya JK aliyekua Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamis Sued Kagasheki alikua anafanya kila kitu yeye mwenyewe bila kumshirikisha naibu wake Bwana Lazaro Nyalandu na chochote atakachofanya Naibu alikutana na vikwazo kutoka kwa bosi wake

Lakini sasa Kinyondo na Lukuvi na Kagasheki na Nyalandu tofauti zao hazikuwahi kujionyesha hadhani isipokua walio karibu yao ndio walifahamu. After all wote ni wateule wa Rais
 
WAFANYA BIASHARA bongo hupitia kipindi kigumu sana, mfano Fred vunja bei alipo kua simba, aliagiza JEZI mzigo mkubwa kinoma Kwa AJILI ya maandalizi ya msimu mpya, baada ya JEZI kufika, zikagomewa eti mdhamini kabadilishwa sio sportpesa ni betway🤣🤣🤣, alafu simba day hii hapa, yani wao hawakuona ile hasara Fred atapata kutengeneza mzigo mara mbili, nadhani Kuna lack of communication pia selfishness, kutokua integrity
 
Katika portfolio zao nahisi Mawaziri na Manaibu Mawaziri hawapewi miongozo ya utendaji kazi na mipaka ya majukumu yao

Huu mwenendo wa kuadhirishana hadharani kwa viongozi hasa wa kisiasa umeasisiwa katika utawaka wa marehemu JPM na haujaachwa sababu haujawahi kukemewa

Nakumbuka enzi za utawala wa Mkapa Waziri wa kazi ajira na Vijana Sebastian Kinyondo alikua hakubaliani na Naibu wake Wiliam Lukuvi.

katika awamu ya JK aliyekua Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamis Sued Kagasheki alikua anafanya kila kitu yeye mwenyewe bila kumshirikisha naibu wake Bwana Lazaro Nyalandu na chochote atakachofanya Naibu alikutana na vikwazo kutoka kwa bosi wake

Lakini sasa Kinyondo na Lukuvi na Kagasheki na Nyalandu tofauti zao hazikuwahi kujionyesha hadhani isipokua walio karibu yao ndio walifahamu. After all wote ni wateule wa Rais
Mkuu umeongea point na umenikumbusha mbali, hasa mzee wa mtemba Sebastian Lukiza Kinyondo.
Kuhusu suala la Jezi nadhani kama ulivyosemai wanasiasa wanatumia uwanda wa michezo kushughulikiana.
Hili halitakuwa na faida kwenye mchezo wa soka na hasa timu ya taifa
 
Back
Top Bottom