Sakata la Kakoko wa TPA kudaiwa kuweka nyumbani begi lenye USD 1,625,800. Mkurugenzi wa TAKUKURU akanusha

Sakata la Kakoko wa TPA kudaiwa kuweka nyumbani begi lenye USD 1,625,800. Mkurugenzi wa TAKUKURU akanusha

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Nimesoma kuwa Takukuru wameingia nyumbani kwa Kakoko leo ghafla na kumkuta na begi lenye $1,625,800 cash baada ya kusimamishwa kazi jana!

Haijulikani hizo alizichota lini, lakini kama ni kweli inawezekana alikuwa akizichota pole pole kwa muda mrefu kidogo na huenda sasa hivi ana "vijisenti" vingi sana huko Jersey au Switzerland kama yule mzee.
===

Kanusho la Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU



Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo amethibitisha kumshikilia kwa mahojiano Mkurugenzi Mkuu wa Bandari Tanzania (TPA) Deusdedit Kakoko. Pia Brigedia Mbungo amekanusha picha na video zinazosambaa mitandao zikionyesha fedha ikidaiwa zimekutwa nyumbani kwa Injinia Kakoko.

Brigedia Mbungo amesema; "Hapana huo ni uongo taarifa za kukutwa na Pesa nyumbani kwake sio sahihi ni watu nadhani ni maadui zake wanajaribu kutengeza hoja ya kuonyesha alikuwa na hizo fedha.

Kakoko anashikiriwa na sisi(TAKUKURU) hilo halina ubishi na tunamshikiria kwa sababu za Kiuchunguzi kwahiyo tunaufanya uchunguzi lakini tunahitaji na yeye awepo, Unajua kwa mfano unapokwenda kumpekua mtu ni zoezi la uchunguzi, sasa huwezi kumpekua wakati yeye hayupo lazima awepo"
 
Bado tunasafari ndefu.

IMG_20210330_020334.jpg


Hiyo ni kama 3.7 Billion Tshs to be exact.

Halafu kuna watu wanasema ufisadi uliisha awamu ya tano. Haukumalizwa bali ni watu wachache walijimilikisha mianya ya pesa kwa kukingiwa kifua na ikulu.

Siku ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma utakapopigwa vita kwa vitendo na kwa nguvu zote ndo nchi itasonga mbele.
 
Nimesoma kuwa Takukuru wameingia nyumbani kwa Kakoko leo ghafla na kumkuta na begi lenye $1,625,800 cash baada ya kusimamishwa kazi jana!

Haijulikani hizo alizichota lini, lakini kama ni kweli inawezekana alikuwa akizichota pole pole kwa muda mrefu kidogo na huenda sasa hivi ana "vijisenti" vingi sana hujo Jersey au Switzerland kama yule mzee.
Aaaah! Bandari ilikuwa yake! Takataka hii kwa kiasi hiki tu cha fedha aingie lupango kwa makofi ya nguvu. Mbona mitaani kibaka wa jogoo tu anaingia lupango huku ameshavunjwa mikono, sembuse hili jangili la nyala za serikali.

Jamani, na sisi pia tuna matumbo ya kulisha, mbona mnatufanya waTz wenzenu mafala hivi? Maisha kwetu magumu lakini kwa huyu chizi na familia yake ni tambarale akitumia nyala zetu za serikali.

Tupa jela akiwa na mguu mmoja tu hayawani huyu.
 
Back
Top Bottom