Katika hali ya kushangaza kanisa lililotikisa mkoani Tabora kwa karibu miaka miwili , kupiga muziki kwa sauti kubwa sana , mahubiri ya kashfa kwa dini zingine kuhubiri mahubiri ya ndoa hadharani limebainika kutokuwa na kibali wala usajili wa kuendesha ibada mkoani Tabora . Licha ya malalamiko ya muda mrefu sana ya majirani na wananchi wa mtaa wa Kariakoo eti viongozi wa halmashaurina wilaya ndio wanabaini kanisa hilo kutokuwa na kibali ? Wala usajili ? Kanisa limesajiliwa Kahama linakuja kufanya shughuli zake mkoani Tabora bill kibali cha mamlaka za mkoa na wilaya ? Miaka miwili ? Kama sio rushwa Ni nini ? Tarehe 22 mwezi huu kanisa hilo limepewa notisi ya kuondoa kanisa na kuacha shughuli zake katika mtaa wa Kariakoo, Mchungaji aliyetamba kuwaweka mfukoni viongozi wa Tabora ameenda kumhonga kigogo mmoja wa ofisi ya mkuu wa wilaya Tabora mjini , sasa hivi kigogo huyo anahangaika kweli kutafuta mbinu ya kulifungulia kanisa hilo huku akijua halina kibali , halina usajili , kibali cha ujenzi , kibali cha muda cha kuendesha ibada katika mkoa wa Tabora . Tunaomba mamlaka zake za juu zifuatilie uvunjifu huu wa sheria huku wananchi wa mtaa husika tukiteseka kwa kelele na sauti kubwa sana za muziki na mahubiri ya watu wasio na vibali , usajili na miongozo mingine inayotakiwa , Serikali ya Tabora inalea genge la wahuni ? Hata rushwa zenyewe hebu muogopeni mwenyezi Mungu . Mnaruhusu watu wanajenga mpaka barabarani ?