Jamani Wanabodi,
haya maswala ya Umeme nchini yanashangaza sana.
Nimepitia home page ya hii site nimekuta kitu hiki! Sioni kabisa jina la JK wala bunge letu!
MRADI MKUBWA WA UMEME WAYEYUKA! Thursday, 21 December 2006
Mchoro wa bwawa la Mto Rufiji
WAKATI Rais Jakaya Kikwete akitimiza mwaka mmoja akiwa madarakani huku nchi ikilemewa na tatizo kubwa la ukosefu wa umeme, imebainika kwamba, maamuzi ya kitatanishi ya mamlaka moja ya umma yamelikosesha taifa mradi ambao ungezalisha nishati hiyo kwa kiwango cha mara tatu ya kile kinachopatikana hapa nchini.
Taarifa ambazo Tanzania Daima inazo zinaonyesha kwamba uamuzi wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la Mto Rufiji (RUBADA) kuvunja mkataba na taasisi moja ya Kitanzania iliyokuwa ikifadhiliwa na wawekezaji wa nchini umeliweka taifa katika hatari ya kuchelewa kuanza kupata megawati 2,100 za umeme ambazo zingeanza kuzalishwa wakati wowote.
Hivi sasa Gridi ya Taifa ina uwezo wa kuzalisha megawati zisizodi 600 na ambazo kupungua kwake kumekuwa kukiisababishia nchi mgawo wa umeme.
Mamlaka hiyo inalaumiwa kuvuruga mpango wa mradi mkubwa wa umeme, uliokuwa ukifanywa na Kampuni ya wazawa ya CP Limited & Associates, kupitia mradi uliojulikana kama Stiegler's Gorge Hydropower Plant.
Taarifa zinaonyesha kwamba wakati mamlaka hiyo ya umma ikitangaza kuuvunja mkataba, CP ilikuwa imeshapata kiasi cha dola za Marekani bilioni 10, kwa ajili ya kuendesha mradi huo ambao ungekamilika baada ya miaka sita kuanzia sasa na ungemaliza kabisa tatizo la umeme nchini.
Habari za ndani ambazo Tanzania Daima imezipata, zinaeleza kuwa, RUBADA, iliingia mkataba wa kuendesha mradi huo na Trade CP Limited & Associates Machi 30 mwaka huu.
Chini ya mkataba huo ambao Tanzania Daima imeiona nakala yake, Trade CP Limited & Associates ilitakiwa kusaka fedha kwa ajili ya mradi huo muhimu nchini.
Mkataba huo, ulisainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa RUBADA, Barnabas Kabuzya na Mkurugenzi Mtendaji wa Trade CP, George Fuko.
Baada ya kusainiwa mkataba huo, Trade C.P Limited ilianza kusaka fedha na Juni 5, 2006 mwaka huu iliandika barua kwa RUBADA kujulisha maendeleo ya utafutaji wa fedha hizo kwa ajili ya mradi wa Stieglers's Gorge ambao ndani yake una miradi mingine mikubwa 23 ambayo inakadiriwa ingetoa ajira kwa watu 4,500.
Barua hiyo iliwajulisha RUBADA kuwa, hadi wakati huo, tayari Trade CP ilishafanya mawasiliano na wadau mbalimbali wa kutoka Norway na China.
Wakati Trade CP ikihaha kupata fedha za kuendesha mradi huo mkubwa, RUBADA iliiandikia barua kampuni hiyo Oktoba 12, ikielezea nia yake ya kutaka kuvunja mkataba kwa madai kuwa kampuni hiyo imeshindwa kutafuta fedha za kuendesha mradi huo kwa zaidi ya miezi mitano.
Hata hivyo Trade CP Septemba mwaka huu, ilifanikiwa kupata dola za Marekani 10,000,000, sawa na sh bilioni 10 kutoka Saudi Arabia ambazo zingetumika kwa ajili ya mradi huo.
Vyanzo vya habari vimeieleza Tanzania Daima kwamba, hata baada ya kupata fedha hizo, Trade CP Company, iliijulisha serikali juu ya ujio wa fedha hizo kwa vile ni nyingi.
Katika hali ya kushangaza, hata baada ya kufanikiwa kupata fedha hizo, RUBADA imeamua kuvunja mkataba na kampuni ya Trade CP kwa madai kuwa kampuni hiyo imeingia makubaliano ya kupata fedha Saudi Arabia kupitia Kampuni ya M/s Al Muweisaat Establishment bila kutoa taarifa kwa RUBADA.
"Kutokana na sababu hiyo, tumeamua kuvunja mkataba tuliosaini na kampuni yako Machi mwaka huu," ilisema barua hiyo ya RUBADA ya Desemba 14 mwaka huu.
Hata hivyo habari zaidi ambazo Tanzania Daima imezipata, zinasema RUBADA imeamua kuingia mkataba wa mradi huo wa umeme na kampuni nyingine ya kutoka Afrika Kusini.
Tayari RUBADA na Kampuni hiyo ya IDF, yenye namba za usajili 99/09749/07 walitiliana saini mkataba huo Desemba 8 mwaka huu, na kuwaacha Trade CP wakishangaa wasijue la kufanya na fedha walizokwishapata.
Kutokana na hali hiyo, Trade CP inakusudia kulifikisha suala hilo mahakamani kupinga kuvunjiwa mkataba huo na pia kudai fidia kutokana na gharama, usumbufu na hata kuvunjiwa heshima kwa kampuni hiyo.
Mradi huo mbali ya kuzalisha umeme wa uhakika kwa nchi nzima, pia ungezalisha umeme wa bei nafuu kuliko gharama za sasa na pia ungeweza kutumika kuanzisha uchimbaji wa chuma Liganga na kiasi kingine cha umeme kingeuzwa katika nchi jirani.
Alipoulizwa na Tanzania Daima kuhusu suala hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa RUBADA, Barnabas Kabuzya, kwanza alikiri mamlaka yake kuingia mkataba na Trade CP, na akakiri kuingia mkataba na kampuni nyingine ya Afrika Kusini aliyoitaja kwa jina la UDF.
Hata hivyo alisema wameamua kuvunja mkataba na kampuni hiyo ya Trade CP baada ya kubaini kuwa haina uwezo wa kuendesha mradi huo, kwani hata ofisi hawana.
"Huo mradi kwa sasa unahitaji dola za Marekani bilioni mbili, Trade CP haina uwezo na ndiyo maana tumeamua kuingia mkataba na Kampuni ya IDF.
Halafu, kwa nini amekwenda mahakamani au kwenye vyombo vya habari? Kwani amesambaza taarifa zake kwa mawaziri, Rais, badala ya kuwasiliana na RUBADA, lakini kama kweli amepata fedha, bado ana nafasi, kwani nia ya serikali ni kuona mradi huo unaanza ili kuondoa tatizo la umeme," alisema.
Hata hivyo alisema hawezi kuzungumzia kwa undani suala hilo, kwa madai kuwa kwa sasa liko mahakamani.