Mzee,
sina details za hilo tamko la mgao kwisha.. maana hiyo news nimetumiwa kwa text message tu. Tusubiri magazeti ya 'kesho'.
Ni jana tu nimesoma ripoti yako ya suggestions za kumaliza rushwa ndogo ndogo. Nakubaliana nawe weekly or biweekly payments will solve the problem a lot more, na kuongezwa mishahara. Lakini hili la kuhakikishiwa kulipwa on the dot naliona ni hatua!
Mgao wa umeme sasa wamalizika
2006-12-28 10:22:04
Na Usu-Emma Sindila
Mgao wa umeme uliodumu kwa takriban mwaka mmoja, hatimaye sasa umefikia kikomo, baada ya vina vya maji katika baadhi ya mabwawa ya kuzalisha nishati hiyo, kuongezeka.
Kina hicho kimeongezeka, kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini.
Kujaa kwa baadhi ya mabwawa hayo ya kuzalisha umeme, kumezifanya baadhi ya mashine na mitambo mingine ya kuzalisha nishati hiyo, kutotumika mara kwa mara isipokuwa wakati wa matumizi makubwa tu.
Hata hivyo, licha ya kina cha maji kuongezeka katika baadhi ya mabwawa, bwawa la Mtera bado limefungwa ili kuruhusu maji kujaa na kuweza kutumika kwa muda mrefu zaidi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Arthur Mwakapugi, aliiambia Nipashe Jijini Dar es Salaam jana kuwa, hivi sasa umeme unaotumika zaidi ni ule wa maji kwa kuwa ni wa nafuu zaidi.
Bw. Mwakapugi alisema hadi kufikia jana, bwawa la Kidatu lilikuwa linazalisha megawati za umeme 193, wakati uwezo wake ni megawati 204, Kihansi lilikuwa linazalisha megawati 185.20, ambazo ni zaidi ya kiwango chake cha kawaida cha megawati 180.
Bwawa la New Pangani Falls lenye uwezo wa kuzalisha megawati 68, lilikuwa linazalisha megawati 66, Nyumba ya Mungu linazalisha megawati 3.50 wakati uwezo wake ni megawati nane na Bwawa la Hale ni megawati 10 wakati uwezo wake ni megawati 21, alisema Bw. Mwakapugi.
Alisema uwezo wa kuzalisha umeme kwa bwawa la Kihansi, umezidi hadi kufikia kuruhusu maji yamwagike ili kulinusuru lisibomoke.
Kuhusu mitambo mingine ya kuzalisha umeme ikiwemo ya Songas, IPTL, Richmond, Aggreko na Ubungo Power Supply (UPS), alisema kwa sasa haituimiki sana.
Alisema kwamba umeme wake umekuwa ukichukuliwa pindi mahitaji yanapohitajika zaidi.
Alisema kwa siku ya jana, mitambo ya Songas iliweza kutoa megawati 35.60 za umeme na ule wa Aggreco megawati 40.70, wakati ile mingine haikutumika kufua nishati hiyo.
Alisema uwezo wa mabwawa yote ya maji nchini kuzalisha umeme ni megawati 561.
Alisema kwamba uzalishaji wa sasa ni megawati 457.1, ambayo ni sawa na asilimia 81.48 ya umeme wote unaozalishwa kutokana na nguvu za maji.
Mgao wa umeme ulianza rasmi nchini Februari 16, mwaka huu na uliathiri kwa kiasi kikubwa uzalishaji na huduma zingine za kijamii.
SOURCE: Nipashe
Ndugu zangu; ukarimu huu wa mwenyezi Mungu kuleta mvua usitufanye tuache kujadili issue za msingi- jinsi Rich-monduli ilivyotumia vyema nafasi ya ukame kutuhadaa na kutukejeli. watanzania. Nadhani ndicho mzee Rich-monduli anasubiri; kwamba sasa maadam mgao hakuna basi atapata usingizi. Tutakuwa tumejikosea haki tusipo-pursue hii issue mpaka kieleweke!