Kuna siri kubwa hapo, Let's assume walitumia Jina la Richmond through Gire but deal ni ya mafisadi wetu wa hapa hapa kwetu, think about that!!!!
Vipi kama kweli Richmond hawajalipwa na tulichofanyiwa ni mazingaombwe na Richmond fake wakati hela zimeingia mifukoni mwa watu? Maana kukanusha kama hivyo si kitu kidogo, especially kama serikali ya Tanzania inatakiwa kuwa na paper trail ya monies.
Sasa inabidi serikali ya Tanzania ijibu tuhuma, Richmond wanasema hawajalipwa, zile $140,000 per day zilikuwa zinaenda wapi?
Vipi kama kweli Richmond hawajalipwa na tulichofanyiwa ni mazingaombwe na Richmond fake wakati hela zimeingia mifukoni mwa watu? Maana kukanusha kama hivyo si kitu kidogo, especially kama serikali ya Tanzania inatakiwa kuwa na paper trail ya monies.
Sasa inabidi serikali ya Tanzania ijibu tuhuma, Richmond wanasema hawajalipwa, zile $140,000 per day zilikuwa zinaenda wapi?
The fax from Richmond did not say why the contract had not been canceled if the company had not received payment, nor who else might have received it. But it emphasized the company which says it has projects on four continents "has no prior record of wrongdoing" and was not implicated in investigations by the U.S. Department of Commerce or previous committees in Tanzania investigating the project.
The report said the company with which the contract had been signed did not exist in the United States. It said the government was paying the company US$140,000 a day, and asked who was collecting that money.
Now controversial Richmond company resurfaces
THISDAY REPORTER
Dar es Salaam
THE controversial Richmond Development Company (RDEVCO) resurfaced yesterday, claiming to have no links with former prime minister Edward Lowassa who resigned last week after being implicated in a major corruption scandal involving the US-based company.
No RDEVCO executive team member, nor any RDEVCO employee, has ever had a relationship of any kind with (Prime Minister) Lowassa, says part of a press release faxed to THISDAY by the company.
The unsigned press statement, dated February 8 this year, says neither the president of Richmond, Dr Mohammed Huque, the companys manager, Mohamed Gire, nor any employee of RDEVCO has ever even met the prime minister (Lowassa).
The statement, which was supposedly issued on Friday - a day after Lowassas resignation - arrived in our newsroom yesterday by fax from Houston, Texas.
Richmond also said the total value of the contract negotiated with the Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) was just $83m (approx. 98bn/-), and not $172m as reported in local media reports.
The government of Tanzania has not made a single payment to RDEVCO for the emergency power plant project, says the statement issued by one Ms Claudine Lllg on behalf of the Richmond company.
The company stated that it had not paid out bribes to any Tanzanian government official to facilitate the deal.
RDEVCO has not drawn down even one penny from a government issued Letter of Credit. Neither RDEVCO nor any of its employees have received a single penny from, or paid a penny to, the government of Tanzania or any of its officials, said the statement.
Richmond, which was uncovered by a parliamentary investigation as a mailbox or briefcase company with no registration either in Tanzania or the US, defended itself as a reputable US company in good standing and has no prior record of wrongdoing.
The statement said the companys two principal officers, Huque and Gire, were interviewed by an unnamed official from the US Department of Commerce in January 2007.
The interview and site visit satisfied US authorities of RDEVCOs efficacy, said the statement, without revealing the identity of the US official who made the site visit, nor disclosing the companys registration number and status.
The Richmond statement further claimed that the Tanzanian government formed numerous special committees to investigate the project between October 2006 and November 2007 but could not find evidence of any illegal or unethical business being conducted by RDEVCO.
The RDEVCO team has worked on successful projects on four different continents, said the statement, again not mentioning any specific countries and projects where the suspected briefcase company has worked.
The press release issued by Richmond was purportedly faxed from the companys headquarters on 5825 Schumacher Lane, Houston, Texas 77057. Its other listed contacts are phone (713) 952-3472 and fax (713) 952-0932.
Gire is quoted as saying in the statement that he has not personally seen the parliamentary report on the Richmond scandal.
First, I want to say that I have not seen the committee report mentioned in conjunction with prime minister Lowassas resignation. I and members of my staff have been working diligently to obtain a copy of the report from the Tanzanian parliament, Gire was quoted as saying.
He said RDEVCO would issue a complete and thorough response once it has received and reviewed the report.
On the companys website, Gire is described as a prominent businessman and active private investor in emerging high-tech companies and offshore real estate and infrastructure sectors.
He reportedly also serves on numerous boards and commissions, including Houstons Mayoral Advisory Board for International Affairs and Development.
Dr Huque is said to have over 25 years experience in the energy infrastructure sector, and for the last seven years has been a successful developer of infrastructure projects totalling $500m.
In its final report, a parliamentary committee formed to investigate the Richmond deal said there was sufficient evidence suggesting that Lowassa and Igunga legislator Rostam Aziz had personal business interests in the Richmond contract.
It was uncovered that the postal and e-mail addresses of a company owned by Rostam, Caspian Construction Company Ltd, was being used by Dowans Holdings S.A, a little-known company from the United Arab Emirates that inherited the Richmond contract.
Naamini hata mjadala huu pia ni muhimu sana kwa taifa kwasababu unagusa maisha ya mtanzania moja kwa moja
Mjadala wa Richmond kwenye hatihati
Na John Daniel, Dodoma
Source: Majira
WAKATI Watanzania wana shauku ya kuendelea kwa mjadala mkali bungeni kuhusu taarifa ya uchunguzi wa mchalato wa zabuni ya Richmond Development Limited na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuna taarifa kwamba 'mchezo' unapangwa kuzima mjadala huo.
Taarifa hiyo iliyowasilishwa bungeni wiki iliyopita na kusababisha Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Nazir Karamagi na Dkt. Ibrahim Msabaha wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki kujiuzulu, tayari imejadiliwa na wabunge wachache huku orodha ya waliojiandikisha kuchangia ikiwa bado ndefu.
Inadaiwa, kwamba Serikali inataka kuzima mjadala huo kutokana na sababu kuu mbili; kwanza mawaziri waliotajwa tayari wamechukua hatua ya kujiuzulu hivyo ni nafasi kwa Serikali sasa kuifanyia kazi na kuchukua hatua zinazostahili kwa mujibu wa sheria.
Sababu ya pili iliyotajwa ni kutoa nafasi kwa wabunge kujadiliana na kupitisha Muswada wa Sheria ya Fedha, unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni wiki hii na kuelezwa kuwa una umuhimu wa kipekee katika maendeleo ya Taifa kwa sasa.
Ilidaiwa kwamba tayari Serikali imefanya mawasiliano na Spika wa Bunge Bw. Samwel Sitta, juu ya suala hilo na kwamba kuna mawasiliano pia kati ya Ofisi ya Spika na wabunge waliojiorodhesha kuchangia ripoti hiyo wiki hii.
Kwa kawaida hata kama mpango huo wa Serikali utakuwa wa kweli na kufanikiwa, bado nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati Teule iliyoundwa kuchunguza Richmond, Mbunge wa Kyela, Dkt. Harrison Mwakyembe, kuhitimisha hoja yake na kutoa mapendekezo iko palepale.
Akizungumza na Majira kwa njia ya simu juzi, Spika Sitta hakuwa tayari kuweka wazi iwapo amepokea taarifa hiyo kutoka serikalini na badala yake alisisitiza kuwa kwa mujibu wa kanuni za Bunge, wabunge waliokwishajiorodhesha kujadili ripoti hiyo wataendelea kufanya hivyo.
Kwa kawaida hoja ikitolewa inajadiliwa kisha mtoa hoja hupata nafasi ya kuhitimisha, Mwenyekiti wa Kamati Teule atapata nafasi hiyo kama kawaida, alisema Bw. Sitta bila kutoa maelezo kama amepokea taarifa hiyo kutoka upande wa Serikali au la.
Alipoulizwa kama amepokea taarifa hiyo alisema: Wapo wabunge waliojiorodhesha kujadili ripoti hiyo na watapewa nafasi, labda kama wao wenyewe waheshimiwa wabunge wakijitoa, basi nitatoa nafasi kwa mtoa hoja kuhitimisha, ila mimi najua wataendelea na mjadala, alisema.
Taarifa zinadai kwamba upande wa Serikali umejipanga kuzima mjadala huo kwa hofu, kwamba ukiendelea, utazua mambo mengi zaidi ambayo yanaweza kuleta upepo mbaya kwa CCM na Serikali yake huku baadhi wakiielezea kauli ya Mbunge wa Same Mashariki, Bibi Anne Kilango, kuwa ilikuwa kali zaidi kwa maslahi ya CCM.
Waziri Mkuu kama kiongozi mkuu wa shughuli za serikali bungeni anatarajiwa kuwasilisha ombi hilo kutoka serikalini na atatoa ahadi kwamba serikali itaifanyia kazi taarifa hiyo bila kupindisha wala kuangalia sura ya mtu, ila hii inategemea jibu kutoka kwa Spika wa Bunge, kilisema chanzo chetu.
Habari hizo zilidai kuwa kutokana na wazo hilo la serikali, tayari Bw. Sitta ameitisha Kikao cha Kamati ya Uongozi kukutana kujadili kwanza wazo hilo mapema pamoja na ile ya Balozi Fulgence Kazaura kumwandikia Bw. Sitta akilalamikia Kamati Teule ya Richmond.
Akiahirisha Kikao cha Bunge hadi Alhamisi wiki hii, Bw. Sitta alisema anaona orodha ya wabunge waliojiandikisha kuchangia taarifa hiyo ni wengi kuliko muda wa siku mbili zilizopangwa.