Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Kuna siri kubwa hapo, Let's assume walitumia Jina la Richmond through Gire but deal ni ya mafisadi wetu wa hapa hapa kwetu, think about that!!!!

Hivi Rostam Aziz kachukuliwa hatua gani mpaka sasa? Je kajiuzulu ubunge kutokana na kutajwa katika ripoti ya kamati ya Mwakyembe?
 
Guys guys guys DON'T WORRY.........................this is typical MAFIA....if you guys now what i mean........JF at work......kaeni chonjo MAFISADI!!!

Nawapongeza sana wana JF waliochukua hatua ya kuwaanika hawa jamaa huko huko waliko na sasa wanataka kujisafisha kibiashara US..........kama wanaona wanachafuliwa waende mahakamani
 
Is their any evidence that Gire register Richmond development Limited in US? Because if so, then U.S federal agent can prosecute them by using International Anti-Bribery and Fair Competition Act of 1998.
The act makes it illegal for a citizen or corporation of the United States or a person or corporation acting within the United States to influence, bribe or seek an advantage from a public official of another country.

So, if there is any proof that Richmond use money to get a deal, then they can be in trouble through that act. However this is up to JK to pressurize Bush about that particular company.
 
Vipi kama kweli Richmond hawajalipwa na tulichofanyiwa ni mazingaombwe na Richmond fake wakati hela zimeingia mifukoni mwa watu? Maana kukanusha kama hivyo si kitu kidogo, especially kama serikali ya Tanzania inatakiwa kuwa na paper trail ya monies.

Sasa inabidi serikali ya Tanzania ijibu tuhuma, Richmond wanasema hawajalipwa, zile $140,000 per day zilikuwa zinaenda wapi?
 
Ni ukweli kinadharia kuwa Richmond hawajalipwa fedha zote. Hiyo capacity charge nk wamelipwa Dowans. Lakini ni ukweli pia kuwa Richmond wamelipwa kwa kuwa kiuhalisia Dowans waliwalipa Richmond. It is a simple mathematics. Wasitake kuzungusha maneno hapa! Huu mzunguko hata Dr Msabaha aliunza bungeni alipokanusha kuhusu 10,000 Usd walizopewa Richmond. Hapa ni kuungia kiundani uhusiano wa kibiashara baina ya Dowans na Richmond; kwa kuwa Dowans si wazabuni wapya kuna fungate la kimalipo hapa!

JJ
 
Vipi kama kweli Richmond hawajalipwa na tulichofanyiwa ni mazingaombwe na Richmond fake wakati hela zimeingia mifukoni mwa watu? Maana kukanusha kama hivyo si kitu kidogo, especially kama serikali ya Tanzania inatakiwa kuwa na paper trail ya monies.

Sasa inabidi serikali ya Tanzania ijibu tuhuma, Richmond wanasema hawajalipwa, zile $140,000 per day zilikuwa zinaenda wapi?

Majibu yako yapo hapa hapa.. inaonekana ujaipitia vizuri taarifa yao na kukimbilia kutoa hukumu.
Cheki maeleozo yao hapa chini

The fax from Richmond did not say why the contract had not been canceled if the company had not received payment, nor who else might have received it. But it emphasized the company — which says it has projects on four continents — "has no prior record of wrongdoing" and was not implicated in investigations by the U.S. Department of Commerce or previous committees in Tanzania investigating the project.
 
Richmond wanacheza mchezo wa "Seek and Hide". Ni ukweli usiofichika kuwa Jina La Kampuni yao ndilo lilishinda tenda hiyo. Kama kuna mtu alitumia jina lao si wangemshtaki? Kama waliwauzia mafisadi wa Tanzania jina kwa makubaliano ya wao kupata asilimia fulani ya mapato basi sasa mambo yameharibika. Kama kweli hawakulipwa si waishtaki Kamati Teule ya Bunge kwa kuchafuliwa jina? Naamini bado kuna mengi yamefichika licha ya report kutoka.
 
  1. Mkataba wa Richmond/Dowans na Tanesco(serikali ya Tanzania) ufutwe.
  2. Paper and money trail zifuatwe. Hata kama kina Gire hawakulipwa pesa, midhali waliingia mkataba laghai, iwe tosha kuwashitaki kwa kujifanya ni wataalamu wa nishati.
  3. Dowans washitakiwe kwa kushindwa kutoa umeme kwa Taifa.
  4. Lowassa na wenzake wafunguliwe mashitaka ya Uhujumu wa Uchumi kwa kutumia sheria za Uhujumu Uchumi na kudhoofisha Usalama na Maslahi ya Taifa.
 
The report said the company with which the contract had been signed did not exist in the United States. It said the government was paying the company US$140,000 a day, and asked who was collecting that money.

Eti kuna wanaosema kuwa kati ya waliohusika na huu wizi hawakupewa Due Process?
 
Ngoja tuweke mantiki hapa (logic)

a. Je mtu anaweza kuingia Mkataba na Kampuni ambayo haipo? (kwa mujibu wa Ripoti ya Mwakyembe).

b. Kama Kampuni haipo Tanesco iliingia mkataba na nani? Hivyo kama Kampuni haipo the contract fundamentaly does not exist (it becomes inexistent)

c. Kama Mkataba kati ya Tanesco na RDC haupo kwa vile kampuni yenyewe haipo hivyo Mkataba kati ya RDC na Dowans nao haupo.

d. Kama RDC haipo, na Dowans inaendelea kulipwa kutokana na mkataba ambao haupo, hizo fedha zinalipwa kutokana na mipango gani?

e. Kama Dowans inalipwa kutokana na kuingia mkataba wa geresha ambao haupo basi hicho kilichoandikwa hakiwezi kutufunga.

f. Mkataba unaingiwa in good faith na watu wenye uwezo wa kuingia mkataba huo. Kama Tanzania iliingizwa kwenye mkataba under "deception" kuwa Kampuni ipo wakati haipo serikali inaweza kujitoa na kuwaacha hao jamaa waende kwenye International Trade Tribunal wakatuamulie.

g. Kwa wakatoliki ingawa ndoa huwa haifutwi kuna kitu kinachoitwa "annulment" ambacho technically ni kuwa hata kama "ndoa" imefungwa kanisani lakini baadaye ikajulikana kuwa a, b, na c havikuwepo basi ndoa hiyo inakuwa "invalid" na inakuwa annulled kwa maana ya kwamba it never was.

Ingawa mkataba umeingiwa kwenye makaratasi lakini kama serikali inaweza kuthibitisha kuwa a, b, na c havikuwepo basi mkataba wenyewe nao haukuwepo, kwa sababu kuingia mkataba kunapresume certain conditions are met ya kwanza kabisa ni kuwa wanaoingia mkataba wana uwezo wa kufanya hivyo.
 
Jamaa wameruka sio! mimi nina mashaka sana na kale kamchezo ka kubadilisha jina la kampuni walishajua mbele ya safari kuna mlipuko! damn!
 
Bila shaka waziri mkuu mpya MH Pinda atatupa majibu ya kilichotokea kabla ya Richmond kuuza Deal na Nani analipwa hayo mamilioni kila mwezi.

Wale waliodhani hii kesi kuhusu RDC na Mzee Lowasa ndo imekwisha kwa MH Lowassa kujihudhuru inabidi wayarudishe maneno walo kwisha sema vichwani mwao wakayafikirie upya kisha wayaseme tena.

Huenda utetezi wa Richmond uka funua mauza uza mengine ya kutia kinyaa.
Ni kweli fedha hizo zinaishia kwenye mifuko ya kampuni za umeme au akina Lowassa na wajinga wenzie wengine wanazisunda?

Kweli Private Jet ya Lowassa inazidi kupaa,lakini ile ya kubebea wananchi bado iko juu ya vinu pale vingunguti.

Kesi ya RDC itanoga sana ikihamia hapa Marekani kwa sababu itatapakaa kila kona ya dunia.

Wenzetu mnao mliosoma sheria jaribu kutupa nondo zaidi.
 
Madela wa Madilu,

Hii kesi ikifika US ndo itakuwa poa- tusubirie!

Je kutakuwa na kesi?

Mbona ile ya rada UK iliishia hivi2!
 
Kila nikiwaza simuoni kabisa Lowasa akiwa kasimama kizimbani kujibu tuhuma za Richmond, I dont think this will ever happen. Kwa ulimwengu wa CCM, mtu akiresign ni punishment tosha kabisa na utamaduni wao wa kulindana naona utaendelea kwake. Ditoplie ana murder(is there anything worse than this?) lakini huyoooo anakata mitaa kama kawa, Mkapa alitakiwa awe ananyea ndoo saa hizi lakini JK anamuone haya!
 
Nimekasirika mpaka mikono inatetemeka? Kumbe hii nchi ilifikia hatua ya kujidhalilisha kiasi hiki? na hawa jamaa wangejua jinsi watakavyopandisha hasira za watu kwa utetezi wao huu wa kijinga ni bora wangekaa kimya tu.

Sasa nimeshafahamu kwa nini Downs waliingizwa haraka haraka kwenye hii dili. Ni kwamba RDC ilikuwa ni hewa, kwa hiyo EL na RA wakaichomeka Dowans chap chap baada ya kuona kelele zinazidi. Naona kina Dire waliambulia patupu kwenye hii dili baada ya kushindwa kazi.

Yaani bila aibu wanasema uchunguzi wa kwanza wa TKUKURU uliwa-vindicate hivyo wao sasa ni clean? Mambo yote jamani sasa yapelekwe mahakamani tu. Mwanakijiji hata mkataba ukivunjwa bado pesa tulizopoteza hatutazipata kwani kampuni tunayoidai ni hewa. It does not exist. Hivyo chenchi yetu imetoka jumla.. jamani?
 
Hapa naona wanajaribu kufanya "PR stunt" ingawa naona ita-backfire, bora wangesubiri vumbi litulie.

Now controversial Richmond company resurfaces
THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

THE controversial Richmond Development Company (RDEVCO) resurfaced yesterday, claiming to have no links with former prime minister Edward Lowassa who resigned last week after being implicated in a major corruption scandal involving the US-based company.

’’No RDEVCO executive team member, nor any RDEVCO employee, has ever had a relationship of any kind with (Prime Minister) Lowassa,’’ says part of a press release faxed to THISDAY by the company.

The unsigned press statement, dated February 8 this year, says neither the president of Richmond, Dr Mohammed Huque, the company’s manager, Mohamed Gire, nor any employee of RDEVCO ’’has ever even met the prime minister (Lowassa).

The statement, which was supposedly issued on Friday - a day after Lowassa’s resignation - arrived in our newsroom yesterday by fax from Houston, Texas.

Richmond also said the total value of the contract negotiated with the Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) was just $83m (approx. 98bn/-), and not $172m as reported in local media reports.

’’The government of Tanzania has not made a single payment to RDEVCO for the emergency power plant project,’’ says the statement issued by one Ms Claudine Lllg on behalf of the Richmond company.

The company stated that it had not paid out bribes to any Tanzanian government official to facilitate the deal.

’’RDEVCO has not drawn down even one penny from a government issued Letter of Credit. Neither RDEVCO nor any of its employees have received a single penny from, or paid a penny to, the government of Tanzania or any of its officials,’’ said the statement.

Richmond, which was uncovered by a parliamentary investigation as a mailbox or briefcase company with no registration either in Tanzania or the US, defended itself as a ’’reputable US company in good standing and has no prior record of wrongdoing.’’

The statement said the company’s two principal officers, Huque and Gire, were interviewed by an unnamed official from the US Department of Commerce in January 2007.

’’The interview and site visit satisfied US authorities of RDEVCO’s efficacy,’’ said the statement, without revealing the identity of the US official who made the site visit, nor disclosing the company’s registration number and status.

The Richmond statement further claimed that the Tanzanian government formed numerous special committees to investigate the project between October 2006 and November 2007 but could not find evidence of any illegal or unethical business being conducted by RDEVCO.

’’The RDEVCO team has worked on successful projects on four different continents,’’’ said the statement, again not mentioning any specific countries and projects where the suspected briefcase company has worked.

The press release issued by Richmond was purportedly faxed from the company’s headquarters on 5825 Schumacher Lane, Houston, Texas 77057. Its other listed contacts are phone (713) 952-3472 and fax (713) 952-0932.

Gire is quoted as saying in the statement that he has not personally seen the parliamentary report on the Richmond scandal.

’’First, I want to say that I have not seen the committee report mentioned in conjunction with prime minister Lowassa’s resignation. I and members of my staff have been working diligently to obtain a copy of the report from the Tanzanian parliament,’’ Gire was quoted as saying.

He said RDEVCO ’’would issue a complete and thorough response’’ once it has received and reviewed the report.

On the company’s website, Gire is described as a ’’prominent businessman and active private investor in emerging high-tech companies and offshore real estate and infrastructure sectors.’’

He reportedly also serves on numerous boards and commissions, including Houston’s Mayoral Advisory Board for International Affairs and Development.

Dr Huque is said to have ’’over 25 years experience in the energy infrastructure sector’’, and for the last seven years has been a ’’successful developer of infrastructure projects totalling $500m.’’

In its final report, a parliamentary committee formed to investigate the Richmond deal said there was sufficient evidence suggesting that Lowassa and Igunga legislator Rostam Aziz had personal business interests in the Richmond contract.

It was uncovered that the postal and e-mail addresses of a company owned by Rostam, Caspian Construction Company Ltd, was being used by Dowans Holdings S.A, a little-known company from the United Arab Emirates that inherited the Richmond contract.

THISDAY
 
Hii noma, naona JK (Ukimuangalia nyani usoni........)AIPE MAMLAKA SHERIA IFANYE KAZI YAKE. HII NI KESI YA MAHAKAMANI, MANENO YA KUTOA HUKU NA KULE YATATUCHANGANYA SANA WATZ.JAMBO LIKO HADHARANI KILA MTU ANASEMA SIYO YEYE..... JE NANI ANAHUSIKA?????? WAKASEMEE MAHAKAMANI WAKIWA NA USHAHIDI KUTETEA HOJA ZAO, PUMBAVU ZAO WAHUSIKA.
 
Naamini hata mjadala huu pia ni muhimu sana kwa taifa kwasababu unagusa maisha ya mtanzania moja kwa moja

Mjadala wa Richmond kwenye hatihati

Na John Daniel, Dodoma
Source: Majira
WAKATI Watanzania wana shauku ya kuendelea kwa mjadala mkali bungeni kuhusu taarifa ya uchunguzi wa mchalato wa zabuni ya Richmond Development Limited na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuna taarifa kwamba 'mchezo' unapangwa kuzima mjadala huo.

Taarifa hiyo iliyowasilishwa bungeni wiki iliyopita na kusababisha Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Nazir Karamagi na Dkt. Ibrahim Msabaha wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki kujiuzulu, tayari imejadiliwa na wabunge wachache huku orodha ya waliojiandikisha kuchangia ikiwa bado ndefu.

Inadaiwa, kwamba Serikali inataka kuzima mjadala huo kutokana na sababu kuu mbili; kwanza mawaziri waliotajwa tayari wamechukua hatua ya kujiuzulu hivyo ni nafasi kwa Serikali sasa kuifanyia kazi na kuchukua hatua zinazostahili kwa mujibu wa sheria.

Sababu ya pili iliyotajwa ni kutoa nafasi kwa wabunge kujadiliana na kupitisha Muswada wa Sheria ya Fedha, unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni wiki hii na kuelezwa kuwa una umuhimu wa kipekee katika maendeleo ya Taifa kwa sasa.

Ilidaiwa kwamba tayari Serikali imefanya mawasiliano na Spika wa Bunge Bw. Samwel Sitta, juu ya suala hilo na kwamba kuna mawasiliano pia kati ya Ofisi ya Spika na wabunge waliojiorodhesha kuchangia ripoti hiyo wiki hii.

Kwa kawaida hata kama mpango huo wa Serikali utakuwa wa kweli na kufanikiwa, bado nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati Teule iliyoundwa kuchunguza Richmond, Mbunge wa Kyela, Dkt. Harrison Mwakyembe, kuhitimisha hoja yake na kutoa mapendekezo iko palepale.

Akizungumza na Majira kwa njia ya simu juzi, Spika Sitta hakuwa tayari kuweka wazi iwapo amepokea taarifa hiyo kutoka serikalini na badala yake alisisitiza kuwa kwa mujibu wa kanuni za Bunge, wabunge waliokwishajiorodhesha kujadili ripoti hiyo wataendelea kufanya hivyo.

“Kwa kawaida hoja ikitolewa inajadiliwa kisha mtoa hoja hupata nafasi ya kuhitimisha, Mwenyekiti wa Kamati Teule atapata nafasi hiyo kama kawaida,” alisema Bw. Sitta bila kutoa maelezo kama amepokea taarifa hiyo kutoka upande wa Serikali au la.

Alipoulizwa kama amepokea taarifa hiyo alisema: “Wapo wabunge waliojiorodhesha kujadili ripoti hiyo na watapewa nafasi, labda kama wao wenyewe waheshimiwa wabunge wakijitoa, basi nitatoa nafasi kwa mtoa hoja kuhitimisha, ila mimi najua wataendelea na mjadala,” alisema.

Taarifa zinadai kwamba upande wa Serikali umejipanga kuzima mjadala huo kwa hofu, kwamba ukiendelea, utazua mambo mengi zaidi ambayo yanaweza kuleta upepo mbaya kwa CCM na Serikali yake huku baadhi wakiielezea kauli ya Mbunge wa Same Mashariki, Bibi Anne Kilango, kuwa ilikuwa kali zaidi kwa maslahi ya CCM.

“Waziri Mkuu kama kiongozi mkuu wa shughuli za serikali bungeni anatarajiwa kuwasilisha ombi hilo kutoka serikalini na atatoa ahadi kwamba serikali itaifanyia kazi taarifa hiyo bila kupindisha wala kuangalia sura ya mtu, ila hii inategemea jibu kutoka kwa Spika wa Bunge,” kilisema chanzo chetu.

Habari hizo zilidai kuwa kutokana na wazo hilo la serikali, tayari Bw. Sitta ameitisha Kikao cha Kamati ya Uongozi kukutana kujadili kwanza wazo hilo mapema pamoja na ile ya Balozi Fulgence Kazaura kumwandikia Bw. Sitta akilalamikia Kamati Teule ya Richmond.

Akiahirisha Kikao cha Bunge hadi Alhamisi wiki hii, Bw. Sitta alisema anaona orodha ya wabunge waliojiandikisha kuchangia taarifa hiyo ni wengi kuliko muda wa siku mbili zilizopangwa.
 
Kama hii ni kweli basi CCM na JK watakuwa hawajawa nania ya kupambana na mafisadi. Wanaogopa nini ?
 
Naye Lowassa akawaambia mawaziri wengine, kesheni mkiomba kwani hamjui siku wala saa atakayokuja Dr Mwakyembe.
Nami naenda mtaani kuwaandalia kijiwe ili nitakapokuwepo na ninyi muwepo.

Nanyi muonapo tume zaundwa basi mtambue muda wa mavuno ya MAFISADI umekaribia. Kisha akakwea tena Ikulu kuomba rais asimfilisi.

Lakini Kazaura akatokea na jeshi la Mwakyembe na kusema nitakayembusu huyo ndie....
 
Back
Top Bottom