Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts


Thats what we want to hear..............tunajua Mkuu MP kuw akuna mengine yanahitaji utashi wa JK mwenyewe............kinachotia moyo ni kuwa hata yeye JK keshasema anasubiri mapendekezo na majumuisho ya Bunge ili a-implement...........!!! safi sana Mkuu Pinda
 


Mkuu MP.....tena pa kuanzia ni hapo nilipo-mark in red.........pambana kisawa sawa Mkuu......kila la kheri
 

UUGH..OOGH.... KICHEFU CHEFU.....
 
Ya Richmond yamekwisha. Tusubiri rasha rasha za EPA ya BOT; halafu mambo waaaaa. Tunaendelea kula kuku kwa mrija mpaka mengine yatakapoibuliwa na akina Zitto na mwenzie Slaa.

Tume ya Buzwagi na mikataba ya madini itakapotoka hapo hakuna mshindo, kwani tutaridhishwa kuwa wachawi wakuu wamekwishakalishwa pembeni.

Jamani, tumefanya kazi kubwa hii, tupeni tuendelee kuimarisha haya yote hadi 2015. Makofiiiii Paa...paaa....Paaa...
 
Jambo limezua jambo sasa ni majambo.

Mmezoea kuiba mali ya umma sasa umma mwenyewe kaamka anawakaba koo mtakoma kulinga na mali ya wizi.

Jiwe lisibakie juu ya jiwe katika hilo mpaka kieleweke.

Lowassa na timu yako ni lazima mlipwe sawa sawa na matendo yenu na Mungu awape amani katika hilo.

Sasa MH Lowassa ile seat yako maalum pale Azania Lutheran church bado unaendelea kuikalia au weneywe wameiotesha mbigiri kwii kwii kwii kwii!

Mvi nyingine bwana zimejaa ujinga mtupu.


Heshima ni lazima irudishwe tena Irudishwe pale pale ilipokuwa.
 
Kikubwa hapa ni inflated price ya yale ma Get set, in the process tunaletewa habari ndefu za vifungu hivi sijui kifungu gani ilhali tatizo liko spotlessly clear bei imekuwa inflated more than double..
 
Hiyo ndo SISIEM tuliyonayo, na ndio tumewapa dhamana ya kuongoza nchi....

Ukitazama kwa ukaribu utaona wasomi walio ndani ya CCM wanaogopwa na kutengwa sana tu, wanabebwa watu wasio na elimu walio hodari wa kunyenyekea na kupigia wanaowabeba matarumbeta ya sifa.

Muungwana ana cheti cha economy, lakini hii inajidhirisha kwamba ni cheti tu na hakuna chochote kichwani cha kumwonyesha yeye ni economist. Tatizo after school watu wameingia kwenye siasa za kubebana, na ndo maana hata wanaposhika hatamu wanaanza kulipa madeni ya watu waliowabeba na kuwaweka kwenye limelight tokea mwanzo wa maisha yao ya kisiasa.

Elimu sio lazima kwenda shule, lakini hawa jamaa they dont take time to advance themselves by even reading journals, books etc. In short hawajui kinachoendelea duniani isipokuwa juu juu tu kwa kusikia story zinapigwa wakati wapo kwenye vigenge vya kunywa pombe.

Tunategemeaje hawa viongozi wetu waweze kugundua kwamba ndani ya mkataba anaoletewa na subordinates wake una matatizo??? wao wamebaki tu kusoma vichwa vya habari na kutia saini zao.
 
Haya ndiyo matatizo ya kuwaachia watuhumiwa waendelee kuwa huru, wanapata kiburi cha hali ya juu na kufikia kutoa vitisho. Pia si ajabu wameshahakikishiwa kwamba hakuna lolote litakalowafika kutokana na kuhusika kwao na kashfa ya Richmonduli.

Richmond probe team under threat: Seek advice from the Speaker

Committee chairman Dr Harrison Mwakyembe
THISDAY REPORTER
Dodoma

LEGISLATORS who investigated the Richmond corruption scandal complained in parliament yesterday that they have been subjected to death threats over their roles in the probe, whose findings led to the resignation of Prime Minister Edward Lowassa last week.

''Please pray for us...This was a very difficult job. We have even suffered death threats,'' one of the parliamentary probe committee members, Lucas Selelii (Nzega-CCM), declared in the National Assembly yesterday.

He continued: ''We have received several threatening phone text messages, which we shall submit to the Speaker (Samwel Sitta) so that he may act accordingly if anything happens to us.''

Selelii did not go into detail about what the text messages actually said, or where they originated from.

Another member of the committee that investigated the 172.9bn/- Richmond power generation scandal, Ms Stella Manyanya (Special Seats-CCM), also told parliament yesterday that members of the probe team had put their lives at risk in investigating the dubious deal.

''I dedicate this (Richmond) report, or even my own life for that matter, to all Tanzanians out there who have been suffering from paying hiked power tariffs because of dubious deals like the Richmond contract,'' she said.

Contributing to the parliamentary debate on the probe team's final report findings on Thursday, the Kilindi MP, Ms Beatrice Shellukindo (CCM), also declared in parliament that MPs have been receiving threats over the Richmond affair.

The lawmaker's husband, William Shellukindo (Bumbuli-CCM), is the chairman of the parliamentary investments and trade committee which initially recommended the formation of the parliamentary probe team to investigate the Richmond deal.

Contacted for comment, the Deputy Speaker of the National Assembly, Ms Anna Makinda, told THISDAY that parliament as an institution can do little about such death threats against MPs, and it is the responsibility of the police to take up the matter.

''The legislators have done their part in bringing the matter to the attention of parliament and society at large. Law enforcement agencies must have seen and heard what the MPs said, and therefore are responsible for providing them with sufficient protection like other citizens,'' she said.

The Director of Criminal Investigation (DCI), Commissioner of Police Robert Manumba, said his office has not received any formal complaints from the MPs about any death threats they may have received over the Richmond affair.

''We only heard about these reports from the media, but the matter has not been formally brought to our attention,'' Manumba told THISDAY.

Contacted by phone after the adjournment of parliament in Dodoma yesterday afternoon, Selelii himself said none of the committee members had officially reported the death threats to the police yet.

''We are still gathering more evidence and consulting with the Speaker to see the best procedure to follow,'' he said.

Selelii named other committee members who have been subjected to death threats as committee chairman Dr Harrison Mwakyembe (Kyela-CCM) and Ms Manyanya, who was the committee vice-chairperson.

The remaining members of the five-strong Bunge team that investigated the Richmond power generation contract are Herbert Mntangi (Muheza-CCM) and Mohamed Mnyaa (Mkanyageni-CUF).
 
Nafikiri sasa hivi Sisiemu ina kikundi kinacho-act kama MAFIA; kwa maana nyingine wamekula kiapo cha kuwa "MAFIOSO" ambao kujitoa ndani ya kundi maana yake ni Kifo. Hivyo hata Muungwana huenda ameshatiwa kitanzi cha "COSA NOSTRA" kiapo cha mafioso nachokilinganisha na cha mafisadi waliojaa sisiemu.Muungwana atandelea kuwaweka huru EL na wenzake ili wafanye clearance na kuzuia moto unaowaka kuelekea Mahali Patakatifu"IKULU". Hawa wanaotishia wajue siku yao yaja.
 
Haya ni matatizo makubwa leo Tanzania, hao washauri wa rahisi wako wapi? Na kazi zao ni nini? Kama cheti chenyewe ni feki, hata hapo alipofika leo ni kwa utapeli tu! Hawa ndio majizi wakubwa, watatumia kila njia kujipatia vyeo kwa manufaa yao binafsi na sio wananchi. Naomba wenye habari za huyu mtu (Mkulo)wajitokeze ili tumuangalie kwa makini..Wizara hii ni nyeti
 
Yaani uzushi wa mtu mmoja ndio unapelekea watu kufikia hatua ya kutokuwa na imani na JK kiasi hicho? Mtoa hoja anaweza kutuongoza kidogo ili tuweze kuchangia vizuri? Ni ukweli gani unaomuhusisha JK ktk sakata la Richmond?

Uzushi? What are you talking about, hii ishu lazima watu waishikie bango isife ki hivi hivi, manake attention yote iko kwa ziara ya kichaka, kuna mambo mengi yanaendelea nyuma ya pazia ambayo kwa mtu wa kawaida si rahisi kuyajua kwa sababu mafisadi wameweza kununua asilimia nyingi ya media, but thanx to jf for all the effort za kufichua hayo mambo so keep it up, mie sijawahi kuona Rais mswahili kama JK, badala ya kuongelea mambo yanayoweza ku unify taifa katika kipindi hiki kigumu cha miskendo kedekede anaanza kutafuta sifa za chama, oh silly me, sijui nilitegemea nini kwa mtu type ya Kikwete, the bottom line ni kuwa tumekwishawang'amua!
 
Posted Date::2/23/2008
Waandishi wanaotetea watuhumiwa wa Richmond ni majasiri wa kifisadi
Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

GEORGE Walker Bush katika siku nne za ziara yake kuanzia Februari 16, mwaka huu pamoja na mambo mengine aliweza kufunika mjadala kuhusu Richmond.

Siku nne za Bush Tanzania, pamoja na kuonekana kuitangaza nchi hii katika anga za kimataifa bado ziara yake imeweza kuwa gumzo kutokana na mambo mbalimbali ikiwemo kufungwa kwa barabra za miji aliyotembelea, kuingiliwa kwa mawasiliano ya simu na ulinzi mkali ambao hatukuwahi kuuona kwa viongozi wetu.

Binafsi, ni mmoja wa Watanzania kwa upande wa waandishi ambaye nilionja ugumu wa ziara hiyo lakini ikinifunza mengi makubwa, hasa jinsi ya kufanya kazi katika mazingira yenye ulinzi wa hali ya juu sawa na mazingira ya kivita.

Bush sasa ameondoka, ametuachia Sh 850 bilioni za MCC, vyandarua milioni tano na tumepata ahueni kuwa sasa Tanzania haitakuwa kituo kijeshi cha Marekani. Ni wakati sasa wa kuangalia gumzo letu la Richmond lililokuwa limeahirishwa kwa muda lichukue nafasi yake na kuendelea kuitikisa mitaa yetu.

Wiki hii nilitaka nisiandike mada ya Richmond kwani nimeshaandika mara mbili, nilianza na Kauli ya Nyerere kwa Lowassa nikaongeza Mvua ya Thailand. Leo nimeona nilijadili kwa mara ya tatu baada ya kujitokeza mambo mapya.

Uamuzi huo unatokana na mwenendo wa suala hilo ambao sasa unatanua wigo kwa kugusa eneo nyeti la vyombo vya habari, likituhusisha sisi waandishi wa habari.

Kubwa ambalo limejitokeza, ni kwamba kuna timu ya waandishi katika vyombo mbalimbali inajaribu kucheza mchezo ambao ni wa hatari, unafiki na aibu wa kutaka kuonyesha kwamba waliotiwa hatiani na Kamati Teule ya Bunge walionewa, kudhulumiwa na kutolewa kafara.

Bila kuuma maneno, moja kwa moja nasema kwamba waandishi wa aina hii hawawezi kukwepa kuingia katika kundi la �majasiri wa kifisadi katika nchi yetu.

Ujasiri wa kifisadi kwa baadhi ya waandishi umejitokeza bila aibu wala kificho, baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na wenzake akina Naziri Karamagi na Dk Ibrahim Msabaha kujiuzulu nyadhifa zao.

Waandishi hawa wamekuwa wakitumia kigezo cha uhuru wa kutoa maoni kujaribu kujenga hoja nyepesi za kifisadi kujaribu kuwapaka mafuta waliojiuzulu kwa kashfa ya Richmond.

Uhuru wa kutoa maoni sasa unaonekana kuwa mhuri wa kutetea watu ambao wenyewe wamejipima wakaona hawawezi kuwa watumishi wa umma, wakaamua kujiuzulu wakijua kwamba walishindwa kuwajibika katika nafasi zao.

Ile dhima ya vyombo vya habari kuwa taswira ya jamii na zile sifa tele zilizotolewa na Kamati ya Bunge, Wabunge na wananchi kuhusiana na suala hili inaweza kupotea kama waandishi wa aina hii wataendeleza nia yao na kujifanya viziwi wakati wana masikio na vipofu wakati wa macho.

Upofu na ukiziwi unaojitokeza sasa unasikitisha na kutia aibu baadhi yetu, ambao maandishi yetu ya siku za nyuma yanatusuta na kuweza hata kuwa kitanzi kwetu cha msimamo wetu wa leo.

Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu maoni na mitazamo ya kichambuzi, kabla na hata baada ya Bunge kuamua kuunda Kamati Teule kuchunguza mchakato wa zabuni ya Richmond.

Kubwa ambalo nimegundua ni kuwepo mchezo mchafu, wa kinafiki, aibu na wa kusikitisha na unaokatisha tamaa kuhusu mustakabali wa nchi hii hasa baada ya kuona baadhi ya waandishi hadi wale wanaoitwa waandamizi wameangukia katika ujasiri wa kifisadi.

Nimegundua, baadhi ya waandishi wakati gumzo kuhusu Richmond likiwa limepamba moto baada ya kusainiwa mkataba huo na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Juni mwaka 2006, kwa namna moja au nyingine waliandika na kumhusisha aliyekuwa waziri mkuu.

Walitumia kalamu zao kuandika kwa mapana na mtiririko maalumu kuhusu sakata hilo huku wakisisitiza kwa kujaribu kuashiria si kutaja moja kwa moja jinsi Waziri Mkuu alivyokuwa akihusika kusimamia mchakato.

Lakini kwa mshutuko mkubwa, naona aibu na fedheha kubwa, baadhi yetu waandishi tumegeuka 'vinyonga' tunabadilika rangi katika aina ya mazingira tunayoingia.

Hili ndilo nimebaini baada ya kujiuzulu kwa mawaziri hao na Rais Jakaya Kikwete kuvunja baraza na kuliunda upya.

Ni dhahiri sasa baada ya matokeo hayo vita hii inahamishiwa kwenye vyombo vya habari, baadhi ya waandishi miongoni mwetu sijui kwa ushawishi gani, tunanaonekana kupofuka macho na kuziba masikio kuwa viziwi na kuyapa kisogo maslahi ya taifa.

Ni ajabu kuona miongoni mwa Watanzania maskini wanaolilia kupanda kwa gharama za umeme, ugumu wa maisha na nchi kuhujumiwa kwa mkataba mbovu wa Richmond, wanaibuka baadhi ya waandishi bila woga wala aibu wanajaribu kujenga hoja za kitapeli kutetea maslahi ya watu wachache.

Sawa, waliowajibika kwa kujiuzulu ni Watanzania wenzetu na ndugu zetu, lakini lazima tukubaliane katika msingi wa uwajibikaji kwamba hakukuwa na njia ya mkato zaidi ya kujiuzulu vinginevyo bunge lingewang'oa.

Nimejaribu kusoma, wengine wanajenga hoja kwamba ndani ya chama kuna watu wana chuki na Lowassa, wengine wanasema utendaji kazi wake na azma ya kugombea urais 2015, ni mambo ambayo yamemfikisha hapo.

Wengine wanahoji uwajibikaji wa pamoja (Collective Responsibility) ambao ni utamaduni wa kiutendaji katika serikali za CCM, pasipo kubainisha uwajibikaji wa pamoja katika jambo lipi.

Hili la uwajibikaji wa pamoja linaonekana ni jambo kubwa ambalo baadhi yetu waandishi tunalijengea hoja ya kitapeli, lakini hatuangalii upande wa pili vipi maamuzi ya baraza la mawaziri nayo yalipindishwa katika mchakato huu?

Watu wamekaa katika baraza la mawaziri chini ya uenyekiti wa Rais, halafu wengine kutoka hapo wanapindisha maamuzi hayo na kufanya ya kwao, je hapo uwajibikaji wa pamoja uko wapi?

Dhana ya uwajibikaji wa pamoja inakuja pale tu watu wanapokaa pamoja wakapitisha jambo fulani lakini baadaye likaleta matatizo. Lakini hapa unaweza kujiuliza, kama wanaotetewa wanajua uwajibikaji wa pamoja, vipi walipindisha maamuzi ya baraza la mawaziri?

Hapo utaongeza, kama watu walikaa ndani ya baraza la mawaziri wakaamua maamuzi fulani halafu, wengine wakaamua hivi kwa maslahi yao binafsi bila kuangalia maslahi ya taifa na yaliyopitishwa na vikao halali, nani wa kuwajibika?

Isitoshe ni aibu kusema Lowassa katolewa kafara na kamati ya bunge na kutoa taarifa za uzushi, kuchochea na zilizokuwa na nia mbaya naye. Hii si kweli, kamati ilitamka bayana watu wote waliopaswa kuwajibishwa na kuchukuliwa hatua za kinidhamu, lakini haikusema Lowassa ajiuzulu bali kwa nafasi yake apime uzito wa suala la lenyewe kisha achukue uamuzi.

Lowassa alipima uzito wa sakata hilo la Richmond na nafasi yake ya Uwaziri Mkuu jinsi ilivyotumika vibaya katika utoaji wa zabuni hiyo, akaamua kufungua mlango na kujiuzulu akifuatiwa na Karamagi na Dk Msabaha.

Amesema tatizo ni Uwaziri Mkuu ni kweli, tatizo si Lowassa bali ni madaraka ya umma yametumika vibaya katika mkataba wa Richmond, hivyo alipaswa kuyaachia.

Bahati mbaya aibu iliyoje, baadhi ya watu wanaacha ukweli uliozunguka suala lenyewe na maamuzi ya wazi aliyoyachukua Lowassa kuanza kujenga hoja zisizo na kichwa wala miguu.

Huu ni mtandao mpana, upo unajengwa ndani ya vyombo mbalimbali vya habari kwa lengo la kuwasafisha waliojiuzulu na kuwapaka matope waliounga mkono maamuzi ya kamati na wale wajumbe wa kamati husika.

Waandishi hao 'vipofu na viziwi' wengine wanajaribu kumchonganisha Lowassa na Rais Kikwete, kwamba kamtosa mwenzake, wanasahau kwamba inapofika wakati wa kuwajibika 'umwenzake' unawekwa kando, maslahi ya nchi yanachukua nafasi yake.

Lakini wakati baadhi ya waandishi wameamua kufanya ujasiri wa kifisadi, wenzao wenye fikra za kimapinduzi wanazidi kula kiapo cha kupigania maslahi ya taifa, hawaogopi mafisadi na majambazi wa kisiasa.

Fikra za kimapinduzi zinazidi kusambaa, watu wamechoka kuona nchi yao ikigeuzwa kapu la mjinga kila mtu anatia mkono, kazi ni moja kulinda na kutetea maslahi ya nchi.

Vita itapiganwa, waandishi wanaotetea maslahi ya taifa watashinda na wale wanaotetea maovu kwa kigezo cha uhuru wa kutoa maoni mbadala huku wakijaribu kujifanya mabingwa wa kupanga hoja za kifisadi, watashindwa na umma utawabaini na kuwahukumu.

Fedheha kubwa, haiwezekani baadhi ya waandishi watumie kigezo cha uhuru wa kutoa maoni kujenga hoja sawa na baadhi ya mawakili mahakamani, ambao kwa ujanja wa vifungu vya kisheria huweza kusaidia watuhumiwa hata wa mauaji kuweza kukosa adhabu ya kunyongwa na kuachiwa huru.

Kibaya zaidi, utakuta baadhi ya waandishi hawa watetezi wa watuhumiwa wa ufisadi nyumbani kwao ndugu zao hawana maji safi ya kunywa, hakuna huduma za afya, lakini wao wako Dar es Salaam wanapewa fedha kidogo wanasahau kabisa matatizo hayo, hawa ni majasiri wakubwa wa ufisadi katika nchi.

Ramadhan Semtawa ni mwandishi wa mwananchi;0782 528229 semtawa@yahoo.co.uk
 
Hiyo ndio Demokrasia, hata ingekuwa ni mahakamani basi kungekuwa na mawakili wa kuwatetea.
 
Mkurugenzi wa TIC Ole Naiko Leo amenukuliwa akisema kuwa amehusishwa na Richmond kwa kuwa anatoka Monduli na kuwa kamati Ya Bunge kuhusu Richmond ilikuwa na agenda ya siri na watu wa Monduli.

Habari hii si tu kwamba ina harufu ya ukabila kabila, umajimbo na kulenga kumsafisha mtu mmoja kwa kutaka kuugeuza mjadala wa wizi wa Richmond kuwa ni suala la chuki dhidi ya kundi fulani katika nchi yetu bali pia ni kauli ya hatari sana ambayo haiwezi kuachwa ipite bila kukemewa na wapenda amani na utengamano wa nchi yetu.

Watu wengi wamehusishwa na suala la Richmond, wamo Vinara kama Lowasa, Rostam, Karamangi, Msabaha, Mwanyika, Hosea na wengine wengi. Ina maana hawa wote wanatoka Monduli? Ni kwa nini basi suala la Lowasa na Naiko liwahusishe pia watu wote wa Monduli na suala la Karamangi Kuwahusisha watu wote wa Bukoba Vijijini? Kuna namna iko hapa na hizi ni mbinu chafu na kufilisika kisiasa kunakojaribu kutumiwa na wanasiasa waliofilisika. Ukabila! Monduli! haiwezekani Richmond kuihusishanisha na wakazi wa Monduli ambao wanateseka kutokana na ufisadi wa Richmond.

Tunataka Naiko utueleze ni kwa Vipi TIC unayoingoza wewe ikahusishwa na Richmond, Kama huna maelezo ondoka hapo usianze kutuletea tatizo lingine la ukabila hapa.

Monduli ina historia kubwa sana kwa nchi yetu kwani kuna Marehemu Sokoine ambaye ni mtu muhimu sana na ni alama ya nchi. alifanya mambo makubwa ambayo hakuna mtu anyeweza kuyakwepa. Kwa nini Sokoine asifiwe na si Lowasa?

Sala ya Kuiombea Tanzania
E mola, Mungu wa rehema, Ibariki Tanzania na watu wake, tuepushe na mafisadi ambao sasa wanataka kutupandia mbegu za Kibaguzi. Ukawa laani na kuwahukumu sawasawa na hukumu yako na kipimo wanachostahili, Tuepushe na upepo huu mchafu wa mafisadi na ukambariki rais wetu, makamu wake na waziri mkuu, Bunge letu, spika na Tume ya Richmond na wajumbe wake ukwape maisha marefu. Tujengee ujasiri waTanzania wakukataa ufisadi na tuzidi kushimana hasa hapa JF ambayo ni kioo cha Jamii. Amen [/B
]
 
ANALYSIS: Tanzania: The open society and its enemies, after Richmond

THISDAY CORRESPONDENT
Dar es Salaam

A SPECTRE is haunting Tanzania, the spectre of a leadership code; from the head of state to village leaders, varsity dons to street hawkers, parliamentarians and born again priests - all cry for the setting up of a code of conduct for anyone wishing for leadership, those running for elective office or serving in the public sector. All are basically agreed that it is this code which will guarantee the good leadership that the country requires for development; it is the missing link in the country’s battle against poverty. Donors are startled; many are inclined to agree.

If a leadership code is what the country needs for development, one may ask, precisely what brought it into devastating poverty in the first place, if not that same ’leadership code’? How could Tanzania develop when its head of state banned enterprise for anyone who wasn’t Arab or Indian - thus not looking for any sort of public office or employment in the public sector - for all but five years of his 24 years in office? Is there anything as surprising as the fact that learned people don’t realize that a leadership code is the last thing that development needs?

Listening to breakdown elements of how such a code would be conducted or what it entails, there is just shock and amazement at how careless so many Tanzanian intellectuals seem to be about enterprise, jobs, economic growth and incomes. A don says there is little chance that most bars operating in residential areas would be licensed, but they are properties of leaders so they are licensed; that it is leaders who build kiosks all over the place - they weren’t demolished because they belong to leaders, etc. All the old operations will now start again, as the more are caught the better.

The picture one gets is one of total paralysis and mental dependence on government or public sector activity, which ignores the fact that it is only when everyone tries to uplift their own lot, that the net effect of this is that economies generally get uplifted. The dons and ’members of civil society’ are crying out that all but Arabs and Indians should have no role in conducting trade, or a few Africans now operating as traders. The others should work in public offices, or serving as political leaders.

Checking figures of where Tanzania stands in development as a whole, despite efforts to give the most glowing picture possible, the real image is astonishing. Tanzania compares with Afghanistan in the level of girls in secondary school as all eligible girls, at five per cent, and quite simply the lowest in the world. There is no doubt that traditions of strict licensing of schools, stopping hiring of teachers from across the border, tied to lack of ownership of land privately or ability to purchase land (rather than obtain right of occupancy), constant intervention in relation to use of plots of land by public authorities and third parties without the least commercial interest in a plot of land, etc have all done their bit to take us there. And with a leadership code it gets even worse.

Instead of pursuing a policy where all possible enterprise is nurtured, the way President Benjamin Mkapa sought to foster, and remove crying anomalies like protecting sugar factories and selling sugar at 1,000/- while it still was available at half that price if the doors were open, we do the opposite. And while we are yet to realize the benefits of opening the doors and obtain cheap commodities from outside, commodities are beginning to become more expensive, shutting out this door of lessening the cost of living. Now we shall have to get investments to be located right here so as to cheapen commodities; that means plenty of trouble.

The noise made about the Richmond affair was for instance not worth all this outpouring of sentiment and ink, for it easily was consequential upon a faulty policy line upon the start of the fourth phase government. The report read out by Dr Harrison Mwakyembe seemed to suggest that rising costs of electricity arise from faulty contracts - which seems to include all there is in the Tanesco investment line up, namely Richmond, IPTL, Songas, Kiwira etc. The wisdom in the legislature is to investigate these deals and hold all those responsible - but how many ministers are there to dismiss? Was it not more intelligent to say Tanesco ought to have been privatized so as to eliminate the temptation to act as middleman?

And the benefits of Tanesco privatization aren’t just in eliminating the ’Richard of Monduli’ phenomenon from appearing, albeit with an email address labelled Houston, Texas but obtaining the necessary capital to revamp infrastructure without excessive rise in costs, or relying on loans. This sort of wisdom is elementary all over the world, and the plentiful availability of capital constitutes globalization - such that the United States enters into problems for making plentiful use of the capital that flows there - and we could have taken a portion of that, as a supposedly communist China does, so massively. But our less clever communists here hate capital like the plague, and we equal Afghanistan in girls’ education.

Were it that the University of Dar es Salaam taught something serious about capital and not the parroting on ’people, land, good policies and good leadership’ it is likely someone would have understood why we need major investors to purchase Tanesco, the railway corporation, the airline etc. But we hate capital and our mental outlook on globalization, as the late Seithy Chachage used to emphasize, should never betray the hero, Kinjeketile Ngware and his closest medicinemen associates. With that kind of outlook it is hard to see how Tanzania breaks into modernization.

Close to 14 years after the death of ex-premier Edward Moringe Sokoine a sort of spirit of the ’poor people’s hero’ is taking over the reins of state, as current rulers know the popularity one gets when he descends heavily on the rich and powerful. But the fact that Mwalimu Nyerere intervened and stopped the ’anti-sabotage campaign’ is more or less lost - or that from that time Mwalimu allowed economic reform to start, and with his vacating the presidency in 1985, it was intensified. Meanwhile the University of Dar es Salaam, stuck with Kinjeketile Ngware, the need to use Kiswahili and other backward outlooks, has never understood that a policy combating trade and investment is sure recipe for disaster.

Thus, with the establishment’s incapacity to explain the BoT saga, and especially given the juicy precedent of Richmond probe and results, so many appetites have been whetted to take ’the revolution’ farther into everyday life. Suddenly a million sources of enterprising activities, that is, those serving in the public sector or involved in politics, should be closed out. The state, via taxes and foreign aid, shall make up for this loss in individual effort, risk taking, loan cultivation and management...!
 
kwanza watu wengi hawajui lowassa baba yake ni mmeru na mama yake massai na amekulia monduli lakini lowassa si jina la kimassai kwasababu baba yake alikuwa mmeru. Wameru wanaasili ya kichaga lakini waliamia milimai arusha.
 
Richmond yawatia nyongo Tanesco
Mwandishi Wetu
Daily News; Friday,February 29, 2008 @06:11

*Wataka viongozi waliosaini mkataba washitakiwe haraka
*Wadai wanachangia kuiua kwa mikataba mibovu, gharama

Na Shadrack Sagati

WAFANYAKAZI wa Shirika la Umeme (Tanesco) wamecharuka na kutaka viongozi na watendaji wengine serikalini walioliingiza shirika hilo katika hasara kwa kusaini mkataba na kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond, washitakiwe haraka.

Katika mkutano wao uliofanyika mapema leo makao makuu, wafanyakazi hao walisema baadhi ya viongozi ndani ya serikali wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Tanesco inakufa, ndiyo maana wanaliingiza kwenye mikataba waliyoiita ya kinyonyaji.

"Yaani Tanesco imegeuzwa mwarobaini, kila mtu analeta mkataba wake ili anyonye na kuondoka," alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano ya Tanesco, Abdul Mukama.

Alisema mkataba wa Richmond ambao ulipigiwa kelele na wafanyakazi wa shirika hilo, unadhihirisha namna viongozi wa siasa walivyodhamiria kuhakikisha shirika hilo linakufa kutokana na fedha zinazolipwa na shirika hilo kwenda kwenye kampuni binafsi.

Mukama alisema wafanyakazi kwa muda mrefu wamekuwa wanajituma kuhakikisha shirika hilo linainuka, lakini tangu serikali iingie mkataba na kampuni ya IPTL, Songas, Aggreko na sasa Richmond, zimekuwa zinalipwa fedha nyingi na shirika hilo.

"Mimi sioni kama hawa walistahili kujiuzulu, hawa wanatakiwa kukamatwa na kushitakiwa haraka," alisema Mukama wakati akifungua mkutano huo ambao ulikuwa unajadili suala hilo la mkataba wa Richmond.

Mukama alisema mtu wa kwanza ambaye alitaka kuiua Tanesco ni Rais mstaafu Benjamin Mkapa, ambaye aliingiza menejimenti ya Afrika Kusini kwa nguvu ambayo pia haikuleta ufanisi wowote zaidi ya kuuza mali za shirika hilo na kuliacha likiwa hoi kifedha.

Alisema Rais Mkapa aliipeleka Tanesco kwa dalali ambaye ni Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC) kwa miaka 10. Alisema katika kipindi hicho shirika hilo halikuruhusiwa kuingia katika mkataba wa aina yoyote ile mkubwa, hali iliyosababisha miundombinu yake kuchakaa.

Baadhi ya wafanyakazi wengine ambao walipata fursa ya kuchangia kwenye mkutano huo, walisema viongozi wa siasa wakiwamo wale ambao wameingia mkataba wa Richmond, wameshiriki kuidhoofisha Tanesco.

"Rais Kikwete ameelemewa na ufisadi wa watangulizi wake. Haya yanayofanyika ndani ya Tanesco yameanza siku nyingi, anashindwa afanye nini kama anataka kusafisha uozo, ni vyema pia amshitaki Rais mstaafu," alisema Thomas Njumayo.

Walisema kitendo cha kampuni ya Richmond na sasa Dowans kulipwa Sh bilioni 4.7 kwa mwezi na Tanesco inaonyesha namna ambavyo viongozi wa siasa wasivyokuwa na uchungu na shirika hilo.

Mfanyakazi mwingine alisema ni vyema serikali iilipe fidia Tanesco kwa vile katika miaka minane shirika hilo limeathirika kwa kiasi kikubwa, ikiwamo kupoteza chuo chake cha Morogoro kilichokuwa kinatoa wataalamu wa hali ya juu.

Alisema pia Tanesco inatakiwa kulipwa faida, kwa vile menejimenti ya Netgroup iliuza baadhi ya majengo katika hali ya kutatanisha, huku wakiliacha shirika likiwa katika hali mbaya ya fedha.

Mfanyakazi mwingine aliyejitaja kwa jina la Mwakugile alitaka wafanyakazi hao waazimie kama fedha hizo zinalipwa kutoka hapo Tanesco wazizuie, ziweze kuongeza ufanisi wa shirika hilo.

Suala la Richmond lilitokana na ripoti ya Kamati teule ya Bunge iliyokuwa inaongozwa na Dk Harisson Mwakyembe ambayo ilibaini namna ambavyo baadhi ya viongozi, akiwamo aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha kujiuzulu.

Wafanyakazi wa Tanesco walisema jana kwamba viongozi hao wameshiriki katika kulidhoofisha shirika hilo, hivyo wanastahili kushitakiwa na siyo kujiuzulu tu.
 
Actually nimeipenda hiyo ticket,
kwamba mapambano dhidi ys ufisadi hadi kwa 'washinda hoi'

Bado kidogo tutafika kule ambako raia wataipigania malia sili ya nchi yao.
Tukaze buti. tusonge mbele,
 
Hii nayo ni kali kwa kweli .Haya wacha nivute gazeti za dail news kwanza na Uhuru nione unazi wa hawa jamaa .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…