Madela Wa- Madilu
JF-Expert Member
- Mar 24, 2007
- 3,063
- 735
Ni Watanzania pekee ndiyowenye jukumu lakuikomboa Tanzania kutoka kwenye makucha ya wakoloni weusi wachache wanaoendelea kusimika mirija yao kila siku.
Kulia lia kwenye vyombo vya kimataifa kama IMF, Wrld Bank nk ni ujinga usio weza pimika. Vyombo hivi viliundwa na Mabepari wakubwa wa dunia kugandamiza wanyonge wote duniani. Vipi leo wanyonge wanadhani vyombo hivi viko upande wao?
Uzito wa matatizoyetu ndo unatufanya tuone sela za WB na IMF kuwa nzuri kuliko sera muflisi za Serikali ya SISIEMU. Kuvililia vyombo vya kimataifa ni kuonyesha wazi kwamba tunakubali sera zao pia tuna kiri kwamba sisi ni watu duni kamwe hatuwezikujikomboa bila mkombozi kutoka nchi za magharibi.
Mapambano ya kuwaondoa wale wote wanaochzea Uhuru wetu ni yetu wenyewe Watanzania.
Mapambano ya kuwang'oa Mafisadi na kuangamiza kabisa mazalia yao ni yetu Watanzania.
Mapmbano ya kubadiri fikra za watanzania na kujenga utaifa kwa kuhimiza elimu ya uraia, ili kuamsha uzalendo na utaifa wa kila mtanzania ni yetu Watanzania wenyewe.
Mapambano ya kurejesha njia kuu zote za uchumi mikononi mwa watanzania kwa kubadiri sheria za umiriki wa ardhi na makapuni ya kibiashara yako juu ya mabega yetu na ndani ya akili zetu.
Mapambano ya kuiondoa Tanzania katika kundi la nchi masikini zaidi duniani kwa kuanzisha na kukuza uwezo wa kuzarisha bidhaa za viwandani, chakula mashambani,uvuvi badharini na kupandisha hali za maisha ya watanzania ni majukumu yetu watanzania wenyewe.
Wakoloni weupe walishindwa kutuletea maendeleo ya kweli walipo tutawala moja kwa moja. Leo hii wakoloni wale wale wanatutawala kwa kutumia makampuniyao ya kimataifa kupitia maajenti wao weusi ambao ni viongozi wanao ongoza taifa letu, wana hila zile zile za kuchelewesha au kukwamisha kabisa maendeleo yetu.
Watanzania hatuwezi kuendelea kukaa kimya na kuiacha Tanzania yetu ikigawanywa vipande vipande na kuuzwa sokoni na viongozi wetu ambao ni wakala wa ukoloni mambo leo.
Tukisubiri wagawane na kuuza hadi washibe tutasubiri hadi siku ya kiama, viongozi makupe hawa hawatashiba kamwe.
Gharama ya kuiachia Tanzania iendelee kuongozwa na kundi la watu wenye njozi za kuuza hata mama zao wazazi ni kubwa isiyo weza bebwa na mtanzania yeyote wakiwemo viongozi wenyewe.
Kwa kuzingatia ukubwa wa gharama ya kuiacha Tanzania iendelee kudharirishwa na makampuni ya kimataifa na yale kutoka nchi masikini kama yetu (IPTL ya Malaysia), Watanzania ni lazima tujiandae kupambana katika pambano la Ama zao Ama zetu.
Mapmbano ya kuikomboa Tanzania ni mapambano ya kufa na kupona.
Tukiacha kupambana na Ufisadi tutakufa kwa kihoro na utapiamlo, tukipambana naufiusadi kuna wengine kati yetu tutakufa kwa kisasi cha fisadi.
Ni bora kufa ukipambana kutetea haki yako kuliko kufa ukisononeka kwa kufanywa mtumwa katika nchi yako.
SAA YA UKOMBOZI NI SASA NA WAKOMBOZI NI MIMI NA WEWE