Kwa kasi hii itakapofika 2010, tutakuwa na hali mbaya sana. Ni aibu kubwa kwa mwaka wa kwanza kufanya madudu ya aina hii, hususani kwa mtu alietajwa kama mkombozi na wengine kukufuru kwamba Chaguo la mungu(Masihi, yule alienenwa na manabii).
Pamoja na kushindwa kuonyesha muelekeo wa nchi awamu ya nne. Mwaka wa kwanza umekuwa na matokeo hasi. Angalia hasara hizi:
1. Mkatataba unaonuka ulafi na rushwa wa Richmond
2. Mgao wa umeme ambao umechangiwa sana na uzembe, uzalishaji kupungua
3. Safari nyingi za Jk na EL za kuuza sura
4. Gharama kubwa mno wa kulighramia baraza kubwa kabisa la mawaziri katika historia ya Tanzania
5. Mikutano isio na kichwa wala miguu ya Ngurdutudo(Mawaziri kisha Ma RC na Madc)
6.Sherehe kubwa za Uhuru(Japo walichangishwa wafanyabiashara, bado wangeweza kuhamasihwa kuchangia madawati na dawa mahospitalini badala ya yale maonyesho)
7. Ubalozi wa Denmark Kupunguza misaada kwa kushindwa kuwasilisha muswada jii ya rushwa na kukimbila muswada wa Tawala za mikoa za kuongeza madiwani katika halmashauri(gharama ya ziada kwa halmashauri)
Kwa hasara kama hizi kwa mwaka wa kwanza, na shaka hali tutakayokuwa nao 2010. Uongozi wa awamu ya NNE una dali zote za kuwa janga la kitaifa. Tunapita katika kipindi kigumu kabisa na kibaya katika historia ya Nchi. Ole wake Tanzania.