Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Hii kuchanganyana; ukiona hivi ujue wameshazidiana akili wenyewe kwa wenyewe. Lengo kubwa lilikuwa kuwachanganya wananchi ili wao waweze kuendelea kula kamisheni ya tenda taratibu. Sasa ukiona watu wanaanza kuropoka ovyo inaonyesha ni jinsi gani mradi mzima unavyoendeshwa kihuni.
 
IA
Hapo umenena. Rais wetu ambaye alihusika katika kashfa ya IPTL anahusika kabisa katika sakata hili. Alipokuwa New York alidiriki hata kuwapa Richmond an clean bill of health akisema ingawa kumekuwa na maneno maneno lakini kampuni hiyo ni safi. He said things would be okay by the end of October and here we are going into Christmas and New Year and nothing seems okay.
 
Kwa kasi hii itakapofika 2010, tutakuwa na hali mbaya sana. Ni aibu kubwa kwa mwaka wa kwanza kufanya madudu ya aina hii, hususani kwa mtu alietajwa kama mkombozi na wengine kukufuru kwamba Chaguo la mungu(Masihi, yule alienenwa na manabii).

Pamoja na kushindwa kuonyesha muelekeo wa nchi awamu ya nne. Mwaka wa kwanza umekuwa na matokeo hasi. Angalia hasara hizi:
1. Mkatataba unaonuka ulafi na rushwa wa Richmond
2. Mgao wa umeme ambao umechangiwa sana na uzembe, uzalishaji kupungua
3. Safari nyingi za Jk na EL za kuuza sura
4. Gharama kubwa mno wa kulighramia baraza kubwa kabisa la mawaziri katika historia ya Tanzania
5. Mikutano isio na kichwa wala miguu ya Ngurdutudo(Mawaziri kisha Ma RC na Madc)
6.Sherehe kubwa za Uhuru(Japo walichangishwa wafanyabiashara, bado wangeweza kuhamasihwa kuchangia madawati na dawa mahospitalini badala ya yale maonyesho)
7. Ubalozi wa Denmark Kupunguza misaada kwa kushindwa kuwasilisha muswada jii ya rushwa na kukimbila muswada wa Tawala za mikoa za kuongeza madiwani katika halmashauri(gharama ya ziada kwa halmashauri)

Kwa hasara kama hizi kwa mwaka wa kwanza, na shaka hali tutakayokuwa nao 2010. Uongozi wa awamu ya NNE una dali zote za kuwa janga la kitaifa. Tunapita katika kipindi kigumu kabisa na kibaya katika historia ya Nchi. Ole wake Tanzania.
 
Wadanganyika woote wamelala, hata madudu yafanyike kiasi gani hawawezi kuamka!!!!

FD
 
Wakishaanza Denmark wewe subiri usikie wengine watakavyofanya kuwaunga mkono. Hii eti ni kwa faida yetu; ili kuongeza vita dhidi ya rushwa na kupeleka muswada bungeni. Mwinyi alishindwa kukusanya kodi wafadhili hawakumkawiza, JK anashindwa kuwahi kupeleka muswada wa rushwa bungeni, Denmark imemkumbusha kwa kukata 20% ya misaada. Watakaoumia ni wale wale walala hoi. Tuzidi kumuomba Mungu, maana hapa tulipo na huko mbele ni kiza kinene.
 
Waziri wa Nishati na Madini Bw. Nazir Mustafa Karamagi amezungumza nami mapema leo kuhusu suala la nishati, mikataba mibovu ya madini na mipango ya baadaye ya kuhakikisha kuwa Taifa letu linapata suluhisho la kudumu la nishati. Nilipomuuliza nini kitatokea kama RDC hawatatimiza mkataba, Waziri Karamagi alisema "wataadhibiwa"!

Sikiliza mahojiano yangu na Waziri Karamagi, Siku ya Jumatatu kwenye KLH News http://mwanakijiji.podomatic.com
 
Ingawa sijasikilza mahojiano yako. Nina dukuduku kujua alikuwa na maana gani kusema "wataadhibiwa". Je watachapwa viboko au watatupwa jela au vipi: nina dukuduku sana
 
subiri Jumatatu... katika mahojiano hayo pia anasema kuwa hakuna tatizo kwenye mikataba kwani imeingiwa kisheria!
 
Nanukuu: "..katika mahojiano hayo pia anasema kuwa hakuna tatizo kwenye mikataba kwani imeingiwa kisheria!"

I have never heard a more illogical statement in my life (and I have been around for a while). Tuna matatizo na mikataba mingi iliyoingiwa kisheria. Mikataba ya kiwizi kama ile ya madini, hata kama imeingiwa kisheria, ina matatizo. Kwani kuwa na matatizo kwenye mikataba maana yake ni nini? Na mkataba usioingiwa kisheria ni wa namna gani?

Augustine Moshi
 
Akijibu swali la "Je anataka kuwahakikishia vipi Watanzania kuwa Taifa letu chini ya uongozi wake katika wizara hiyo halitaingizwa kwenye mikataba mibovu" Waziri Karamagi aliahidi jambo moja tu na ni kuwa "maslahi ya wananchi yatalindwa"..!

Agustine, hisia yangu ni kuwaalimaanisha kuwa hata kama mkataba mbaya ulioingiwa kisheria hauna budi kuheshimiwa!
 
Kwani huo mkataba unapaswa kuwa umetekelezwa hadi kufikia lini?Iweje hayo maslahi ya Taifa yatakayozingatiwe pindi Richmond wataposhindwa kutekeleza mkataba badala ya kuzingatiwa wakati wa zoezi zima la utafutaji wa kampuni yenye uwezo wa kutatua tatizo la umeme nchini?
Japo napongeza jitihada zako Mwanakijiji kufanya mahojiano na Karamagi lakini nadhani unapaswa kwenda mbali zaidi ya kumkariri wanasiasa huyo mwanamtandao na m-babaishaji flani ambaye alishaahidi kuwa umeme ungepatikana by December 1 na leo ni th 15/12 wala hakuna dalili ya umeme huo.
Service delayed is service denied.
 
Mzee wa Kijiji,

You are absolutely wrong. Kama kiongozi anaingiza nchi kwenye mkataba kisheria, na mkataba huo unadhulumu maslahi ya wananchi, basi sisi wananchi hatubidiki kuuheshimu.

Carl Peters aliingia mikataba na viongozi wa wakati ule na pale ilipobidi, wananchi walitwaa silaha kufukuza wakoloni waliokuwepo kwa kutumia hiyo mikataba.

Evil deeds, even if legal, are morally objectionable and we must reject them.

Asitokee mtu akaingia mkataba wa kuuza nchi kisha atuambie ni wa kisheria, tuuheshimu. Ni sheria za haki tu ndio zinastahili kuheshimiwa.

Augustine Moshi
 
Kama kweli Mheshimiwa alikwa na maana hiyo, mimi napata picha tofauti kabisa.

Kwa vile kila mikataba ya serikali inaingiwa kisheria kwa hiyo ina maana kuwa hakuna mkataba wa serikali ambao una matatizo; je wakati Kikwete akiahidi watu kuwa mikataba yote yenye matatizo itapitiwa upwa alikuwa hajui kuwa miktaba hiyo imeingiwa kisheria? Au Mzee JK alikuwa akidanganya wananchi kwa vile Mbowe alilizungumzia hilo kwenye kampeini zake na lilikuwa linachoma sana kisiasa?
 
Moshi anamkumbuka Carl Peters na mikataba yake; alikuwa amevaa miwani ya kiajabuajabu. Ama kweli tuna asili ya kuwa ni viongozi wanaoingia mikataba ya kuuza nchi hii; hatukuanza leo, lipo kwenye damu yetu! Itabidi tupigane tena kukomboa nchi yetu na labda kuwakabidhi viongozi wengine wataoiuza tena kwa mikataba mingine: Vicious circle
 
Hata ununuzi wa rada na ndege ya rais na uuzaji wa nyumba za serikali tuliambiwa kuwa niwa kwa kulinda 'maslahi ya wananchi' hivyo hakuna jipya hapo .
 
Kwa maoni yake (jinsi nilivyomuelewa) hadi hivi sasa mkataba huo hauna matatizo hata malumbano ya hivi karibuni kati ya RDC na Tanesco si ishara ya tatizo la mkataba. Amesema waliokuwa wanalumbana ni viongozi wa ngazi za chini wa makampuni hayo!
 
Yaani anasema mkataba hauna matatizo kwa maana ya kuwa "hauna vifungu visivyoeleweka." Naona hapa ni swala la lugha tu, sidhani kama hayo ndiyo matatizo tunayoongelea. Tunajua kuwa walioundika ni wanasheria kwa hiyo kila kifungu kitakuwa kinaeleweka.

Sisi tunasema mktaba ule una matatizo kwa kuwa umetolewa kwa kampuni isiyokuwa na uzoefu na shughuli hizo wakiwa hawana hata mhandisi mmja wa mambo ya nishati, huku ukiwa umelipiwa gharama kubwa mara nne ya bei ya generator MPYA kabisa kutoka GE.
 
Fikiraduni,
Sasa tufanye nini? Tutaendelea kuliwa mpaka lini?
 
Mzee Mwanakijiji kwani mkataba wa RDC na serikali unasemaje, kama upande mmojawapo ukishindwa kutimiza vipengele walivyokubaliana?

Kusema wataadhibiwa hii ni lugha ya kisiasa mnooo.
 
Back
Top Bottom