Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Vipi alisemaje? Bila shaka atasema ni hujuma za wapinzani hizi...hatuna uwezo wa kufikiri zaidi ya hapo.
 
Yote yanawezekana,

Fikiraduni, Jasusi na wengineo... Hakuna marefu yasiyo na ncha. Kuna mwisho wa uvumilivu. Haya yatokeayo sasa yana mwisho wake. Najua wazi kuwa huenda wengi wasiamini pale watakapoona mambo yanabadilika ghafla.

Hakuna kitu kibaya kama pale mtumwa anapoamua kudai uhuru wake kwa njia mbadala (anayodhania ni sahihi) ambayo kwa namna moja ama nyingine inaweza kumwathiri kwa kiwango kikubwa mwajiri wake.

Kadiri ya maneno niyasikiayo mitaani, wengi hawaridhishwi na utendaji wa baadhi ya watanzania wenzetu walio katika nafasi flani.

Ieleweke wazi pia kuwa malipo yapo, wengine kama Ditopile hawakutarajia kuwa wafungwa. Hilo mbona dogo? Kuna bomu baya sana linaweza kulipuka kabla ya 2007 kuisha. Maneno haya yatakumbukwa, kuna watakaoshangaa, lakini wale wanaojua hali halisi watajua kuwa mabomu haya yalipandikizwa siku nyingi.

Ninachoomba kwa Mungu ni kimoja, hata yakitokea mabadiliko yasije kwa KASI kubwa sana, yaje taratibu na wanaoshughulikiwa washughulikiwe taratibu bila kasi ambayo inaweza kupelekea maamuzi mabovu na ya kujutia.

Mungu hajalala!
 
Mzee Mwanakijiji kwani mkataba wa RDC na serikali unasemaje, kama upande mmojawapo ukishindwa kutimiza vipengele walivyokubaliana?

Kusema wataadhibiwa hii ni lugha ya kisiasa mnooo.


Alles, nimemuuliza yeye kama waziri ameuona mkataba huo kati ya RDC na Tanesco?
 
Waziri Nazir Mustafa Karamagi anaposema 'wataadhibiwa' kama watashindwa kutekeleza kama mikataba inavyotaka ana maana gani (au naye yumo)? So far RDC hasn't delivered yet, MBONA HAWAADHIBU??

Uwaziri kwake ni tonge kubwa ambalo hatoweza kumung'unya na kumeza bora aende kwenye biashara yake ya microfinance - anayoijua zaidi.

WHY CAN'T DRAFRTS OF THESE CONTRACTS BE AVAILABLE KWA WANANCHI WATOE MAONI YAO BEFORE EXECUTION?

Kaiba Wambandwa
 
Obviously the president himself is involved in corruption. It is a power crisis, and power is a backbone of our economy, kwa nini Rais asifanye partnership na world reknowned players in power/energy sector kama CAT, GE ambao wana all incentives in long term working with governments worldwide? Huyu president alijua wazi kuwa hawezi kupata commissions kutoka CAT au GE kwa sababu ya transparency akaingia kimgongo mgongo na hawa watu kama Richmond. Hata hizo za songas similar deals ila tu haziku-fault.

Power crisis na kuipa richmond deal kama hii, inatupa nafasi hata bunge kuunda probe team ku-question what happened lakini state ya bunge letu ndiyo hivyo. This is enough to question the ability of the sitting president, and all the cabinet; the parliament included..


IT'S US WHO WENT TO THE BALLOT TO.......
IT'S US WHO CAN MAKE CHANGES sawa si sawa?
 
Mwanakijiji.

WAMBANDWA kauliza HAPO JUU, WHY CAN'T DRAFRTS OF THESE CONTRACTS BE AVAILABLE KWA WANANCHI WATOE MAONI YAO BEFORE EXECUTION? Je Karamagi alijibu nini?

Mwanakijiji, vipi Mzee mbona hivi sasa hukutuuliza/kutuambia kuwa utamhoji karamagi wanabodi wakachangia kukupa maswali??

Au ni mimi ndio nimepitwa na wakati!!
 
Hivi sasa twaambiwa maji yameanza kutiririka ktk mabwawa. Je lile tope waliliondoa? walio na inf. zaidi watumegee
 
Wambandwa,
Katiba yetu haina kipengele cha "Recall" au "Vote of no Confidence" kwa President. Wala haina kipengele cha kuiondoa serikali madarakani inapoonekana kushidwa kazi. Kuongeza rigidity ya katiba yetu, endapo Rais akipata matatizo kama yaliyomkuta Ariel Shalon, bado ataendelea kuwapo madarakani hadi baada ya miaka mitano. Katiba inaruhusu makamu wa Raisi kushika madaraka tu baada ya Rais kufariki au kujiuzulu.
 
Ogah, niliwauliza wachache hapa kwenye PM zao na walikuwa na masaa mawili kunijibu kwani Bw. Karamagi alizungumza nami akiwa anamsubiri Rais...so si maswali yote niliyotaka kuuliza niliweza kuuliza. Sikutaka kuweka public hapa maana kuna watu mbalimbali wanasoma na wangemtonya maswali yangu. So, next time I'll include you katika PM....
 
Mwanakijiji.

WAMBANDWA kauliza HAPO JUU, WHY CAN'T DRAFRTS OF THESE CONTRACTS BE AVAILABLE KWA WANANCHI WATOE MAONI YAO BEFORE EXECUTION? Je Karamagi alijibu nini?

Mwanakijiji, vipi Mzee mbona hivi sasa hukutuuliza/kutuambia kuwa utamhoji karamagi wanabodi wakachangia kukupa maswali??

Au ni mimi ndio nimepitwa na wakati!!

Ogah
hata mimi wakati napitia michango mingi hapa nilikuwa najiuliza swali hilo hilo, maana M/Kijiji anaweza kusahau mambo mengine na kuishia kumnukuu tu huyu msanii mwingine. Mfano Kichuguu kauliza kitu cha msingi kabisa, vile sijasikia hayo mahojiano pengine M/kijiji alikumbuka, utasemaje hauna matatizo wakati uzoefu wa hao Richmond ni wa kutilia shaka na gharama zenyewe ndio hivyo tena? Ukiona wote wanao watetea namna hiyo ujue bahasha zimesha watembelea.
 
Kichuguu, naona umemiss sura ya 2 ibara 37 ya katiba kifungu cha 2 ambapo kinaelezea nini kifanyike endapo Rais hataweza kutekeleza wajibu wake kwa sababu ya kiafya. Kinasomeka hivi:

Endapo Baraza la Mawaziri litaona kuwa Rais hawezi
kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi ya mwili au ya akili,
laweza kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio la kumwomba Jaji
Mkuu athibitishe kwamba Rais, kwa sababu ya maradhi ya mwili
au ya akili hawezi kumudu kazi zake. Baada ya kupokea azimio
kama hilo, Jaji Mkuu atateua bodi ya utabibu ya watu
wasiopungua watatu atakaowateua kutoka miongoni mwa
mabingwa wanaotambuliwa na sheria ya matababu ya Tanzania,
na bodi hiyo itachunguza suala hilo na kumshauri Jaji Mkuu
ipasavyo, naye aweza, baada ya kutafakari ushahidi wa kitabibu
kuwasilisha kwa Spika hati ya kuthibitisha kwamba Rais
kutokana na maradhi ya mwili au ya akili, hamudu kazi zake; na
iwapo Jaji Mkuu hatabatilisha tamko hilo ndani ya siku saba
kutokana na Rais kupata nafuu na kurejea kazini, basi
itahesabiwa kwamba kiti cha Rais ki wazi, na masharti yaliyomo
katika ibara ndogo ya (3) yatatumika.
 
Tabasamu, ukitaka kuwekwa kwenye "cycle" ya watu ambao naweza kutaka maoni yao ni lazima uwe na uhakika wa kuweza kunijibu angalau siku hiyo hiyo, maana wakati mwingine wanakubali kufanya mahojiano ndani ya saa moja..! Kwa mfano hili la Karamagi nimepata go ahead jana.. hivyo nikawatumia watu kama wanne na wote walinibu kabla ya asubuhi leo...
 
Invincible, sitauliza hadharani maswali ninayotaka kumuuliza kiongozi itakuwa ni sawa na kumtumia mtu maswali ili ajiandae kujibu. Viongozi wetu lazima wajifunze kuelewa nini kinaendelea katika idara zao kwani maswali tunayouliza sisi siyo ya wabunge. Kiongozi anayefuatilia nini kinaendelea basi anakuwa tayari wakati wote na habari sahihi na zinazoeleweka. Narudia tena, kama kuna mtu anayetaka nimtonye ninapoandaa mahojiano na kiongozi au mtu fulani basi lazima awe ni mtu anayepitia hapa mara kwa mara!!
 
Kichuguu, naona umemiss sura ya 2 ibara 37 ya katiba kifungu cha 2 ambapo kinaelezea nini kifanyike endapo Rais hataweza kutekeleza wajibu wake kwa sababu ya kiafya. Kinasomeka hivi:

Endapo Baraza la Mawaziri litaona kuwa Rais hawezi
kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi ya mwili au ya akili,
laweza kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio la kumwomba Jaji
Mkuu athibitishe kwamba Rais, kwa sababu ya maradhi ya mwili
au ya akili hawezi kumudu kazi zake. Baada ya kupokea azimio
kama hilo, Jaji Mkuu atateua bodi ya utabibu ya watu
wasiopungua watatu atakaowateua kutoka miongoni mwa
mabingwa wanaotambuliwa na sheria ya matababu ya Tanzania,
na bodi hiyo itachunguza suala hilo na kumshauri Jaji Mkuu
ipasavyo, naye aweza, baada ya kutafakari ushahidi wa kitabibu
kuwasilisha kwa Spika hati ya kuthibitisha kwamba Rais
kutokana na maradhi ya mwili au ya akili, hamudu kazi zake; na
iwapo Jaji Mkuu hatabatilisha tamko hilo ndani ya siku saba
kutokana na Rais kupata nafuu na kurejea kazini, basi
itahesabiwa kwamba kiti cha Rais ki wazi, na masharti yaliyomo
katika ibara ndogo ya (3) yatatumika.


M/kijiji asante sana kwa kunifahamisha hilo, nilikuwa silijui.

Hata hivyo angalia ilivyo vigumu kumwondoa madarakani hata kama atakuwa kichaa wa kuharibikiwa na ubongo. Kwanza kazi ya kupendekeza imepewa kwa Baraza la mawaziri ambao ni wateule wake; inawezekana ikawa vigumu kwao kufanya hivyo ili kulinda maslahi yao. Kazi hiyo ingefanywa na bunge ambalo ndilo linalowakilisha mawazo ya wananchi. Pili, kuna mzunguko mrefu kutoka baraza la mawaziri, jaji Mkuu, kundi la madaktari bingwa, Spika; yote hayo ya nini na tena ni mpaka liwe kundi la madakatari bingwa wasiopungua watatu.

Je kuna kipengele kinachoruhusu kum-impeach president akifanya makosa ya jinai? Hebu chukulia kuwa Ditopile angekuwa ni President halafu akafanya mambo yale, katiba inasemaje?
 
Mimi hii ndiyo home page yangu. lakini siwezi kuahidi kuwa naweza kujibu kila kitu kila wakati kwa sababu inategemea na siku yenyewe. Siku nyingine lazima nipalilie ugali kwa bidii sana, na siku nyingine kama ya leo naweza kunadika hata mara ishirini. Hata hivyo ungetafuta njia ya kukusanya mawazo kijanja bila ya kufahamisha watu kuwa una mpango wa kumwuliza kiongozi.
 
Kichuguu, hapa kuna wasomi bwana... naweza kumzuga mmoja lakini si wote. La maana ni kuwa nijue mtu yuko available kwani bado mwaka mpya ndo unakuja na nina uhakika tutakuwa na nafasi nyingi tu za kuzungumza na watu mbalimbali.
 
Mzee wa Kijiji,

Mzee on the serious note, huyo Waziri Karimagi, kama kiongozi wa taifa ni lazima ajibu masuala ya yeye kupora mke wa kiongozi mwenziwe, kwa kutumia pesa, huyo amempora mke wa Patric Mongella, DC huko Kigoma, kwa kutumia mapesa mengi ikiwa ni pamoja na kumpatia apartment ya kisasa hapa mjini,

sasa yeye kama kiongozi wa juu anafanya hivyo, vipi haoni kuwa ni mfano wenye matatizo kuigwa na vijana ambao ndio taifa letu la kesho? Je tutajenga taifa la wananchi wa aina gani ambao hawaheshimiani? Kama kiongozi mmoja wa ngazi yake hawezi kumheshimu mwenziwe je wananchi itakuwaje katika kuheshimiana? Na kama viongozi hawaheshimiani binafsi, je wataheshimiana kwenye shughuli za taifa? Je angechukuliwa mke wake na kiongozi mwenziwe atakubali yaishe?

Message yake kwa taifa ni nini? Kwamba tafuta mali kwa nguvu na bidii zote, halafu pora wake wa wananchi wenzio?

Ahsante Mzee Wangu!
 
Back
Top Bottom