Kichuguu, naona umemiss sura ya 2 ibara 37 ya katiba kifungu cha 2 ambapo kinaelezea nini kifanyike endapo Rais hataweza kutekeleza wajibu wake kwa sababu ya kiafya. Kinasomeka hivi:
Endapo Baraza la Mawaziri litaona kuwa Rais hawezi
kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi ya mwili au ya akili,
laweza kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio la kumwomba Jaji
Mkuu athibitishe kwamba Rais, kwa sababu ya maradhi ya mwili
au ya akili hawezi kumudu kazi zake. Baada ya kupokea azimio
kama hilo, Jaji Mkuu atateua bodi ya utabibu ya watu
wasiopungua watatu atakaowateua kutoka miongoni mwa
mabingwa wanaotambuliwa na sheria ya matababu ya Tanzania,
na bodi hiyo itachunguza suala hilo na kumshauri Jaji Mkuu
ipasavyo, naye aweza, baada ya kutafakari ushahidi wa kitabibu
kuwasilisha kwa Spika hati ya kuthibitisha kwamba Rais
kutokana na maradhi ya mwili au ya akili, hamudu kazi zake; na
iwapo Jaji Mkuu hatabatilisha tamko hilo ndani ya siku saba
kutokana na Rais kupata nafuu na kurejea kazini, basi
itahesabiwa kwamba kiti cha Rais ki wazi, na masharti yaliyomo
katika ibara ndogo ya (3) yatatumika.