Invincible,
Wizara wanaposema mkataba uliingiwa sheria na hakuna matatizo!...
Ndugu yangu afadhali wangekuwa na maana hiyo, lakini sii kweli bali hii ni siasa za kutumia Utaaalam.
Waziri mwenyewe alitusisitizia kuwa - "kuna habari za uvumi zinatembea kuwa serikali yetu imetapeliwa na sijui magendo n.k. Sio Kweli kabisa" alisisitiza. Hawa jamaa Richmond pamoja na kampuni nyingine tatu walijitokeza na wala sii kweli Richmond pekee walipewa Tender nzima.
Ktk maelezo yake zaidi akasema mashirika mengine (mbali na Richmond) wameisha funga mitambo yao na inafanya kazi tatizo ni kuwa walipewa kiasi kidogo kulinganisha na Richmond.
Ungekuwepo ktk mkutano huo ungeweza kuona sura zilivyowashuka mshikaji wangu alipoliangusha swali. Na huyu waziri Karamagi alituhakikishia mambo yote safi kabisa hakuna ubabaishaji uliotumika.
Siku za nyuma kabla ya huo mkutano tulikuwa ktk bar ya hotel moja kubwa walipofikia. Na kwa bahati swala hili likazuka ktk mazungumzo. Waziri fulani ambaye sintapenda kulitaja jina lake alianza kubwata ovyo...alikandya kishenzi serikali na mkataba huo! Unajua tena chupa zikianza kufanya kazi. Mara kuna mtu akamshitua na kumuomba aende akalale kesho yake wana safari ndefu.... bra... bra... bra na mzee akajikokota huku bado akibwata. Richmond!... Mkataba - wizi mtupu wezi hawa. Watu kimyaaaa, mzeee kalaleee!
Hiyo ndiyo picha kamili na Karamagi hana jinsi zaidi ya kuendelea kutetea kama wakili wa serikali.
Kama alivyoeleza Mzee Moshi huko nyuma, swala letu wananchi sio ufuatiliaji wa sheria za hao Richmond kupata hiyo Tender. Richmond wanaweza kabisa kuwa walifuata sheria zote na lotto (bahati nasibu) ikawaangukia wao. Swala letu ni kwa nini tender ya umeme iuzwe kwa bahati nasibu ambayo haitazami uwezo wa hawa jamaa. Hata hiyo Website yao wameijenga hivi majuzi tu na wanatumia sana makampuni wanayoshirikiana nayo kujitangaza.
Invincible,
Ikiwa leo hii serikali inipe mimi - Mkandara, Tender ya kuwauzia UDA mabus toka General Motors -GM, nikashindwa kutimiza on time kisha wananchi wadai kwa nini serikali (UDA) hawakununua mabus moja kwa moja toka GM. Waziri asimame na kusema eti kuwa GM hawakujitokeza ktk Tender!...
Jamani hii lugha kweli inaeleweka akilini? Yaani kweli kiongozi anafikiria GM wanaweza kuja kuomba ku-supply na kuchukua majukumu ya ukarabati nchini TZ hali.
Invincible, hii ndio nasema ni elimu na siasa bila kufahamu jinsi nchi hizi zinavyofanya biashara!
Hiki ndicho kinachotuchosha, waziri kudai GE hawakujitokeza ktk mnada wetu hali wao ni watengenezaji sio walanguzi inachosha. na huwezi kuwaambia kitu.
Mara utaambiwa serikali haina Mtaji -Umaskini ndio unaotukwamisha!..trust me, Invincible kuna rafiki yangu ameshindwa kabisa kuelewa uwezo wa sisi kutanua kiasi hiki hali tunasema nchi yetu maskini. majumba, magari, hotel tunazokaa n.k ingekuwa nchi hizi za magharibi hiyo tosha kabisa kwa serikali kuanguka...
Mtaji imekuwa umaskini wetu hali tunaishi kama Wazaire ambao wapo radhi kulala chini bila Umeme lakini wakitoka nje wamevaa Armani na G Franco Ferre.
Serikali yetu ina jina zuri sana (credit) kama wanavyozidi kudai pia then swala la credit haliwezi kuwa taabu - mabenki kibao yangeweza kutupa huo mkopo huo. Unless, kweli sisi ni ma drug addicts na mabenki yanafahamu hivyo!