Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Mzee ES,
Nafikiri ni mke wa John aliyeporwa, kwani Patrick ni mkubwa kwa John yupo hapo Dar kama Director of operations wa shirika moja nadhani ni PPF au NSSF, kama sijakosea.
Lakini yote tisa kumi kama ulivyouliza, ni message gani anatuma kwa walalahoi wa Tanganyika akiwa kama kiongozi wa kitaifa?
 
Mzee Machifula,
Ni kweli mke alikuwa wa John kabla hajawa DC. Na kaka mtu yuko PSRC.
 
Guys, hapo juuu nimewasikia lakini hapa nina-deal na big picture nayo ni Karimagi Waziri hao mnaowang'ang'ania niliishi nao US, na ninajua mpaka walivyorudishwa kwa kukimbia madeni ya Credit Cards ambayo mpaka leo hawajalipa, wala mama yao hajalipa, please do not get me started......!

Mzee wa Kijiji,

Utakapoongea naye tena Waziri Karimagi, ikiwezekana mpatie the message!
 
Mzee Mwanakijiji,
Huyu waziri alipita mitaa hii akiwa na waziri mkuu na tulikutana naye.
tatizo langu napokutana na watu hawa huwa msikilizaji zaidi ya kuuliza kwa sababu nashindwa kabisa kuelewa sababu zinazochanganywa kisiasa na utaalam. Yaani huwezi kumsikia kiongozi akikubali kuwa makosa yamefanyika kiutaalam kutokana na hizo siasa zao.
Alidai hivyo hivyo kuwa mkataba huu wa Richmond ulikwenda kisheria na hakuna upendeleo zaidi ya kwamba Richmond walitupa bei nafuu ya umeme wao wa mita kuliko wengine wote...Alikwepa swali kama hawa Richmondo kulifanyiwa uchunguzi (kwa sababu hawakufanya) pia pendekezo la kuwa kwa nini serikali wasiagize genereta moja kwa moja toka GE!...
madai yake kampuni kama GE hazikujitokeza ktk tender, hivyo hawawezi kuvuta kampuni ambazo hazikujitokeza.
mtu mwingine aliuliza kwa nini tanzania zisiweze kujiingiza na serikali za nchi za huku moja kwa moja ktk miradi mikubwa ya kitaifa badala yake wanapitia kwa mawakala ambao wengi wao ni wezi watupu.
Jibu lake, unajua nchi kama hizi miradi ikiwa haina faida huwa hawana interest, hapa bado yeye akitazama swali hili kwa mpango wa tender na sio serikali kwa serilaki kuingia mkataba wa contact kama tulivyokuwa tukifanya enzi za mchonga - Ujamaa.
kwa hiyo hawa viongozi wanakwepa maswali kiujanja ujanja na kupotosha maana ya swali la mtu. wao wana tafsiri zao ama upungufu wa upeo ktk maswala mengi mbali na hizo elimu zao. Kuna vitu hawavifahamu kabisa zaidi ya kitabuni walivyosoma na siasa zao.
Jamani wanabodi ebu nambieni, labda mimi nakosea hizi sheria na mipango ya kitaifa inavyokwenda. Hivi kweli mradi mkubwa kama wa umeme (commanding height) unauweza ktk tender? tena basi kibaya zaidi hawa Richmond ni watu wa katikati sio supplier. Hii ina maana mali ghafi inatoka Songo (mradi ulishikwa na wageni) hawa wanawapa Richmond (mradi mwingine wa wageni) kisha Richmond anamuuzia supplier wetu -Tanesco (mali yetu). Ina maana toka songo wanaweka faida yao kisha Richmond kwa Tanesco na mwisho mlalahoi ndio anapata umeme uliopitia mikono mitatu.
Mbali na hapo navyojua mimi mlolongo huu huanzia kama Gas ni mali ya serikali (mali yetu) Kisha kwenye magenerator (mali yetu) na mwisho ktk supplier ndipo utakuta kampuni za nje.
sababu kubwa ni kwamba serikali inaweza ku-control uzalishaji wa umeme kwa bei nafuu kuliko umeme uzalishwe na mtu binafsi kisha eti serikali kazi yake ni kusambaza. Huyu mgeni tunampa nguvu na uwezo wa kusaliti uchumi wa nchi na pia nafasi kubwa ya kutu - blackmail.
Sasa tumeanza kuyaona ya Richomd akiweka madai kuwa gas yetu ni chafu! well, kama Karamagi amedai mkataba ulikwenda kisheria imekuwaje hili swala liwe geni kwa Serikali?...
Navyofahamu mimi mkataba ni lazima ueleze kinaga ubaga hiyo gas ipo ktk hali gani?! na wala sio kazi yetu sisi (serikali kuhakikisha Richomond anapata gas iliyokuwa imesafishwa. Richmond kama mfanya biashara ndiye alitakiwa kufanya utafiti wake na kufahamu gharama zitakazo wakuta kabla hawajaweza kuuza umeme kwa Tanesco!
Itakuwa ajabu kubwa kama walitegemea kupewa gas safi na wao kazi yao kubwa ni kuwasha generator tu!...
Jamani hata sijui niseme kitu gani zaidi.
Mwisho, karamagi mwenyewe alituhakikishia kuwa mkataba na Richomnd ulipewa deadline ya April mwaka 2007!.. jamani kweli huu ni mkataba wa dharura? yaani kuna uwezekano tusiwe na umeme hadi April 2007 hali viongozi hawa hawa wanazidi kufunga masafari kuitangaza nchi!

Binafsi nimechoka na wanasiasa hasa hawa wasomi!..Hili swala la Umeme lingekuwa muhimu kwao lisingewekwa ktk tender kabisa. Hili ni swala la rais au waziri mkuu kulifanyia kazi ktk hiyo misafara yao badala ya kuomba fedha eti kujenga zahanati. Huu sii ulevi jamani?
Ombeni utaalam na sio fedha!... vijiwe (drug addicts) ndio huomba fedha sio ajira ama Utaalam.
 
Mkandara,'
We are all drug addicts. Nilishangaa pale New York mwezi Oktoba mheshimiwa rais alifvyoifagilia Richmond na kusema by end of October matatizo ya umeme yatakuwa historia. Now we know differently. Hivi kwa nini tunalazimika kununua gesi ya Songosongo ambapo Songosongo ilipaswa kuwa mali yetu na sisi ndio tulipasswa kuuza Songosongo. Kama huo si addiction ni nini tena? You mark my words, come April 2007 kuna tatizo jingine litakuwa limeshajitokeza na hawa Richmond because the guys are just walanguzi and they do not have the expertise in these umeme things.
 
Mwanasheria mkuu wa awamu ya tatu hivi karibuni alisema,kwa jinsi walivyowazoefu na sheria za mikataba, hata kama angeamshwa usingizini angejua kama mkataba ni mbovu au mzuri. Nadhani alisahau kuwa mikataba mingi aliyoishughulikia wakati huo ilikuwa ni mibovu!

Tunaweza kusema, labda hawa wasomi wetu wanaotuingiza katika mikataba mibovu hawaoni huo ubovu wakati wakiishughulikia. husoma hiyo mikataba wakiwa wamevaa mawani ya jua.
 
Mzee wa Kijiji,

Mzee on the serious note, huyo Waziri Karimagi, kama kiongozi wa taifa ni lazima ajibu masuala ya yeye kupora mke wa kiongozi mwenziwe, kwa kutumia pesa, huyo amempora mke wa Patric Mongella, DC huko Kigoma, kwa kutumia mapesa mengi ikiwa ni pamoja na kumpatia apartment ya kisasa hapa mjini,

sasa yeye kama kiongozi wa juu anafanya hivyo, vipi haoni kuwa ni mfano wenye matatizo kuigwa na vijana ambao ndio taifa letu la kesho? Je tutajenga taifa la wananchi wa aina gani ambao hawaheshimiani? Kama kiongozi mmoja wa ngazi yake hawezi kumheshimu mwenziwe je wananchi itakuwaje katika kuheshimiana? Na kama viongozi hawaheshimiani binafsi, je wataheshimiana kwenye shughuli za taifa? Je angechukuliwa mke wake na kiongozi mwenziwe atakubali yaishe?

Message yake kwa taifa ni nini? Kwamba tafuta mali kwa nguvu na bidii zote, halafu pora wake wa wananchi wenzio?

Ahsante Mzee Wangu!

Huyu naye pia LOL; Nilikuwa najua wachache ikiwa ni pamoja na kiranja kumbe wapo wengi ambao kwenye chni hatoki mtu. Ningekuwa na mke waziri nadhani ningekuwa najiuliza sana kama yuko salama huko.
 
Hivi tunanvyojadili mauji mengine tena yametokea muda mfupi tu uliopita. Ni Nyerere road njia panda kwenda vingunguti, Karibu kabisa na kampuni ya Micronix.

Watu wa watatu wameuwawa papo hapo.Walikuwa kwenye pickup imebeba hela ikitokea Mohammed Enterprieses. Majambazi wanne wamemimina risasi isivyo kawaida, mithili ya watu kwenye filamu.

Polisi, na wafanyakazi wawili wamekufa hapo hapo. Nilikuwepo kwenye eneo la tukio, nimeshuhudia mtu akikat
a roho mikononi mwa walalahoi waliliokimbilia gari baada ya majambaizi kutoka na kuanza kuwasachi majeruhi na marehemu.

Siku hizi Mauji yanafanyika hadharani. Habari hizi zitatoka kwenye vyombo vya habari kesho naamini. Damu ni mbaya mno, hizi ni dalili mbaya, dali za giza, dali za kukata tamaa dalili za damu.

Haya yanatokea takribani wiki mbili tangu jeshi la polisi lifagiliwe kwa kudhiubiti ujambazi.

Wananchi wanaishi maisha ya hofu na umaskini. Viongozi wanaishi maisha salama na kwenye bahari ya utajiri. Utajiri ambao una gharimu umeme, elimu yetu, afya zetu, maisha yetu. Utajiri ambao unafuja dhahabu na almaisi zetu, utajiri haramu na unaonuka.

Ila hii ndio Tanzania sugu,wananchi husau haraka na huamini haraka mno viongozi wake,pengine hata kuwaabudu. Yumkini si swhari tena!
 
Ndugu Eric Ongara: poleni sana na matatizo hayo jamani!! Very disturbing indeed.
 
Nimekusikia mtumishi wa bwana! Ile huo utabiri wako ndugu yangu uuhuu, naomba usikamilike maanake duh!
 
Eric Ongara ,

Nimekusikia maneno yako na kweli inahuzunisha sana . Mimi siku zote huwa najiuliza hawa viongozi wetu wanajua matatizo ambayo wananchi wa kawaida wanayapata ? Ukiangalia kwa ndani sana utagundua ya kuwa khali ta watanzania inazidi kuwa mbaya jinsi siku zinavyozidi kwenda mbele .. .

Sasa jee sisi kama wananchi tutafanya nini kuwakumbusha hawa miungu watu viongozi wetu ? manake tumelalamika sana lakini hakuna hakuna jipya ..
 
Hivi serikali (kupitia waziri muhusika) inaposema mkataba wa Richmond uliingiwa kisheria na hauna matatizo, nyie mnapata picha gani?

It implies: hatuna uwezo wa kufanya chochote hata kama tunajua ukweli!

Kama alivyosema Mwanasiasa: tuna kazi kweli kweli.......katika nchi hii ya wadanganyika.
 
Hapana, sisi si wadanganyika... Wao ndo wanadhania hivyo, na ukijishusha sana nao wana-take advantage.

Hukumu ya wote waliohusika na mikataba hii feki kuna siku itatoka. Naombea Mzee ES (or the alike) awe rais walau miezi kama 7 tu. Iko siku tu, heri sisi tuanike uozo unaojitokeza na kama tunakuwa tumekosea, wakosoe na kuthibitisha.

Tatizo lao ukiwabana kutaka ukweli wa mambo wanapandisha jazba na kujibu kwa dharau kuwa ndio hivyo!

The salvation day will come, soon & very soon I tell you!
 
Invincible,
Wizara wanaposema mkataba uliingiwa sheria na hakuna matatizo!...
Ndugu yangu afadhali wangekuwa na maana hiyo, lakini sii kweli bali hii ni siasa za kutumia Utaaalam.

Waziri mwenyewe alitusisitizia kuwa - "kuna habari za uvumi zinatembea kuwa serikali yetu imetapeliwa na sijui magendo n.k. Sio Kweli kabisa" alisisitiza. Hawa jamaa Richmond pamoja na kampuni nyingine tatu walijitokeza na wala sii kweli Richmond pekee walipewa Tender nzima.
Ktk maelezo yake zaidi akasema mashirika mengine (mbali na Richmond) wameisha funga mitambo yao na inafanya kazi tatizo ni kuwa walipewa kiasi kidogo kulinganisha na Richmond.
Ungekuwepo ktk mkutano huo ungeweza kuona sura zilivyowashuka mshikaji wangu alipoliangusha swali. Na huyu waziri Karamagi alituhakikishia mambo yote safi kabisa hakuna ubabaishaji uliotumika.
Siku za nyuma kabla ya huo mkutano tulikuwa ktk bar ya hotel moja kubwa walipofikia. Na kwa bahati swala hili likazuka ktk mazungumzo. Waziri fulani ambaye sintapenda kulitaja jina lake alianza kubwata ovyo...alikandya kishenzi serikali na mkataba huo! Unajua tena chupa zikianza kufanya kazi. Mara kuna mtu akamshitua na kumuomba aende akalale kesho yake wana safari ndefu.... bra... bra... bra na mzee akajikokota huku bado akibwata. Richmond!... Mkataba - wizi mtupu wezi hawa. Watu kimyaaaa, mzeee kalaleee!
Hiyo ndiyo picha kamili na Karamagi hana jinsi zaidi ya kuendelea kutetea kama wakili wa serikali.
Kama alivyoeleza Mzee Moshi huko nyuma, swala letu wananchi sio ufuatiliaji wa sheria za hao Richmond kupata hiyo Tender. Richmond wanaweza kabisa kuwa walifuata sheria zote na lotto (bahati nasibu) ikawaangukia wao. Swala letu ni kwa nini tender ya umeme iuzwe kwa bahati nasibu ambayo haitazami uwezo wa hawa jamaa. Hata hiyo Website yao wameijenga hivi majuzi tu na wanatumia sana makampuni wanayoshirikiana nayo kujitangaza.
Invincible,
Ikiwa leo hii serikali inipe mimi - Mkandara, Tender ya kuwauzia UDA mabus toka General Motors -GM, nikashindwa kutimiza on time kisha wananchi wadai kwa nini serikali (UDA) hawakununua mabus moja kwa moja toka GM. Waziri asimame na kusema eti kuwa GM hawakujitokeza ktk Tender!...
Jamani hii lugha kweli inaeleweka akilini? Yaani kweli kiongozi anafikiria GM wanaweza kuja kuomba ku-supply na kuchukua majukumu ya ukarabati nchini TZ hali.
Invincible, hii ndio nasema ni elimu na siasa bila kufahamu jinsi nchi hizi zinavyofanya biashara!
Hiki ndicho kinachotuchosha, waziri kudai GE hawakujitokeza ktk mnada wetu hali wao ni watengenezaji sio walanguzi inachosha. na huwezi kuwaambia kitu.
Mara utaambiwa serikali haina Mtaji -Umaskini ndio unaotukwamisha!..trust me, Invincible kuna rafiki yangu ameshindwa kabisa kuelewa uwezo wa sisi kutanua kiasi hiki hali tunasema nchi yetu maskini. majumba, magari, hotel tunazokaa n.k ingekuwa nchi hizi za magharibi hiyo tosha kabisa kwa serikali kuanguka...
Mtaji imekuwa umaskini wetu hali tunaishi kama Wazaire ambao wapo radhi kulala chini bila Umeme lakini wakitoka nje wamevaa Armani na G Franco Ferre.
Serikali yetu ina jina zuri sana (credit) kama wanavyozidi kudai pia then swala la credit haliwezi kuwa taabu - mabenki kibao yangeweza kutupa huo mkopo huo. Unless, kweli sisi ni ma drug addicts na mabenki yanafahamu hivyo!
 
Katiba inasema -
Rais hawezi kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi ya mwili au ya akili.

Sasa hapa nambieni hiyo lini tuwe na nafasi kama hiyo?

Mnakumbuka wakati wa BM alipokuwa hospital?... alikataaa katakata kuachia uzi na hata hotuba yake fulani aliitoa kitandani. Tena alikuwa hoi na baada ya hapo hakuweza tena kuongoza vizuri hadi uchaguzi mpya. hata Castro mpenda madaraka kaweza kuachia, sisi Wabongo sii rahisi hivyo!...
CCM wataendelea kushinda kwa miaka 20 ijayo, hihli wazi kabisa hadi hapo tutakapo weza kubadilisha mawazo ya wananchi wengi wa vijijini.
Kumbukeni tu kwamba asilimia kubwa ya wateja wa CCM wapo vijijini na biashara hii inafanyika mjini kwa hiyo hata Mungu mwenyewe hataweza kupokea dua zenu.
tanzania imejaaliwa ktk ardhi na kilimo, leo kilimo ni wizara ambayo hatuijali kabisa kisha tunategemea Mungu alete mvua na chakula.. well, aliyafanya kwa Yesu peke yake na kwa sababu kubwa ya miujiza. Biblia na vitabu vya dini vyote vinasema wakati wa miujiza umekwisha! sasa hivi ni mazingaombwe tu. Mbengu za mafanikio haziwezi kuota juu ya jiwe...
Kama tunataka mabadiliko ni jukumu letu sisi kuangalia riziki zetu Mungu kaziweka wapi na tuzifanyie kazi. Wakati tukienda mbio kuzifikia ndio Mungu ataweza kutujaalia tukavuna tulichopanda...
 
Mzee Maxence,

Heshima juu bro, inshallah maana hata wana Israel kule Egypt nao walilia sana lakini baadaye Mungu akasikia, na bongo iko siku inakuja, wallahi tutamkoma nyani giladi, tena pale Sanamu Monument, kila siku mchana tutadondosha mmoja!
 
Eric Ongara,
kwa kweli hali inatisha na kusikitisha

Jamani eehh hala hala mnaoshuka na vidola vyenu pale DIA, vingunguti sio mbali, duuuhh.

Kitu cha ajabu ni kwamba hizi sehemu, Mbagala, Vingunguti, gongo la mboto, tabata ni sehemu ambazo kila wakati unasikia ujambazi tu, ni kama vile ile njia ya Moshi Arusha, kati ya KIA Junction na Boma ng'ombe (mivinjeni), Mlima wa Simba (between Muleba na Bihalamuro), Kitonga, hakuna asiyejua kuwa hizo ni sehemu za majambazi.................
 
Back
Top Bottom