Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Wakati Tanesco ikizidi kuliwa na mafisadi, serikali imeendelea kukopa ili kuisaidia Tanesco. mikopo hii si msaada bali italipwa kwa kutumia kodi za wananchi wa Taifa hili. Kwa maelezo zaidi

STATEMENT BY MR. GRAY S.MGONJA, PERMANENT
SECRETARY TO THE TREASURY, AT THE SIGNING CEREMONY
OF THE LOAN AND GRANT AGREEMENTS BETWEEN THE
GOVERNMENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AND
THE WORLD BANK, HELD AT THE MINISTRY OF FINANCE
CONFERENCE ROOM ON JANUARY 31, 2008 AT 11.00 AM.
Mr. John Murray McIntire,
World Bank Country Director for Tanzania and Uganda,
Members of the Press,
Distinguished Guests,
Ladies and Gentlemen:
1. On behalf of the Government of Tanzania I would like to express my appreciation for this opportunity of signing, two agreements, i.e. (i) concessional Loan Agreement between the Government of the United Republic of Tanzania and International Development Association (IDA); of US $ 105 Million and Global environment facility Grant at US $ 6.5 million which is managed by the International Bank for Reconstruction and Development (IBRD). This makes a total of US $ 111.5 million. 2. The concessional Loan and Grant is in support of Tanzania Energy
Development and Access Expansion Project aimed at improving the
quality and efficiency of provision of electricity, and establish a sustainable basis for energy supply, transmission and distribution in the country. The Project consists of three main components: Component A relates to investments designed to improve TANESCOs Transmission and Distribution Network capacities. This will be achieved through implementation of several sub-components; including:-
1. Supporting upgrade investments in electric power transmission
and distribution system;
2. Supporting ongrid access expansion investments;
3. Supporting implementation of a low loss High Voltage
Distribution System; and
4. Provision of technical advisory services to support commercial
and institutional capacity development to improve TANESCOs revenues and reduce system losses; The project also seeks to establish a framework for Off- Grid
investments for rural areas. This component will focus on institutional set-up of the Rural Energy Agency (REA) and developing, testing and demonstrating new electrification approaches through implementation of the rural electrification
demand-driven small power generation and distribution subprojects; sustainable solar market development in remote rural areas; and strengthening the institutional and human capacity of The Rural Energy Agency (REA), MEM and EWURA. The third component of the project seeks to strengthen capacity of the Government to develop enabling environment for public private partnership in power generation. The Government has already made progress in creating a legal framework in this endeavor. As you can see, the Banks assistance in this area has really come at material time. By improving the quality and efficiency of the provision of electricity and establish a sustainable basis for energy expansion, the Government envisages that, TANESCO will be placed in a better position to improve its financials, and implement its trategic plan. We all know that Energy is a necessary infrastructure for ealization of any economic development. This project and the WB support is therefore very crucial. The Government is committed to ensure effective implementation of this project.

Ladies and Gentlemen, with these few remarks let me conclude by
thanking John all once again for your kind attention.
The Treasury
January 31, 2008
.
 

Attachments

kama kuna ukweli hapo, basi inajibu swali kwanini ameshindwa kumfukuza Msabaha!!! Huwezi kukata tawi la mti uliokalia!!!

There's a natural mystic blowing through the air;
If you listen carefully now you will hear.
This could be the first trumpet, might as well be the last:
Many more will have to suffer,
Many more will have to die - don't ask me why.

Things are not the way they used to be,
I won't tell no lie;
One and all have to face reality now.
'Though I've tried to find the answer to all the questions they ask.
'Though I know it's impossible to go livin' through the past -
Don't tell no lie.

There's a natural mystic blowing through the air -
Can't keep them down -
If you listen carefully now you will hear.

There's a natural mystic blowing through the air.

This could be the first trumpet, might as well be the last:
Many more will have to suffer,
Many more will have to die - don't ask me why.

There's a natural mystic blowing through the air -
I won't tell no lie;
If you listen carefully now you will hear:
There's a natural mystic blowing through the air.
Such a natural mystic blowing through the air;
There's a natural mystic blowing through the air;
Such a natural mystic blowing through the air;
Such a natural mystic blowing through the air;
Such a natural mystic blowing through the air



MAAJABU YANAKUJA HAWA JAMAA HAWATAAMINI HAYA YANATOKEA KWA WALIOKUWA WAKIWADHULUMU NCHI YAO... HATUTAFAYA YA KENYA ILA TUTAANZA NAO WAO NA FAMILIA ZAO
 
Tuandamane,
Mimi sija kuelewa hapo mkuu unamaanisha nini kwa shairi hilo?

festog
 
Vyovyote iwavyo Lowassa kesha wajibika tunasubiri apelekwe mahakamani! Akataje huko kuwa anashirikiana na nani? Na wameiba ngapi! Kama Kikwete yupo tutajua
 
Naye Lowasa akawaambia mawaziri wengine, kesheni mkiomba kwani hamjui siku wala saa atakayokuja Dr Mwakyembe.
Nami naenda mtaani kuwaandalia kijiwe ili nitakapokuwepo na ninyi muwepo.
Nanyi muonapo tume zaundwa basi mtambue muda wa mavuno ya MAFISADI umekaribia. Kisha akakwea tena Ikulu kuomba rais asimfilisi.
Lakini Kazaura akatokea na jeshi la Mwakyembe na kusema nitakayembusu huyo ndie....


Tuwe macho, tuongeza mawe,zege na nondo juu ya kaburi asije akafufuka baada ya miaka 3, akapaa juu zaidi, akawa presida.
Mafisadi wana mbinu nyingi mno!
 
EDITORAL: No stone should be left unturned in the Richmond scandal
THIS DAY

TANZANIANS are eagerly waiting to see the conclusion of the debate on the Richmond saga as Parliament session resumes today after the swearing in of the new cabinet announced by President Jakaya Kikwete on Tuesday. Speaker Samwel Sitta was compelled to adjourn the National Assembly session following dissolution of the cabinet which was prompted by the resignation of Premier Edward Lowassa after being implicated in the Richmond corruption scandal.

Many would particularly like to see the panacea the Bunge will come out with, on what steps should be taken against all leaders involved in the Richmond mega-corruption scandal.

We want to emphasise at this juncture that time has come for the House to take its real place in society by playing its constitutional role of being a watchdog to the executive on matters of state and good governance.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) legislators, who form the majority in Parliament, should make self appraisal and identify the role they are supposed to play in the House. Playing party partisanship, bandwagon ridding and supporting motions hurriedly sent to Parliament without regard to their effect on national interests, have all pushed the popularity of both the party and government to a precipice!

We need not dwell on that issue for too long, for the REDET study which came out some few months ago, has much to tell to a sober mind.

Most CCM legislators had their trying moments in their constituents- were booed and heckled- in the wake of an opposition MP�s persecution and temporary ouster in the House by the majority CCM caucus in the wake of his revelations of some anomalies in the Buzwagi contract saga.

The august House need not be reminded that Tanzania is a potentially rich country. There are different types of minerals that are found everywhere not to mention other natural resources that are plundered by unscrupulous people, while the majority owners are living in abject poverty.

We urge the House to debate the parliamentary select committee report fully and come out with rules that will plug all loopholes used by politicians and so-called investors in the plundering of our resources.

The MPs should understand the gravity of the situation the country has been plunged into. People entrusted with authority, have betrayed the masses and have led the government into a blood-sucking contract with ’a briefcase company.’

We sincerely call on the House to pass a code of conduct for its members, and also to adopt an action to take on all leaders engulfed by corruption. Richmond scandal should only be the starting point.

The House must be pro-active and stress that the major preoccupation of every Tanzanian should be to get our country and people out of poverty, by ensuring that all our energies and resources are mobilised to realize that objective.

We believe, and will continue to believe that the poverty of our people has been exacerbated by corrupt leaders who have been led by greed to play sell outs.

The Bunge has now been presented with an unenviable opportunity to make history.
 
Mwanyika mbele ya Kamati ya Richmond

Mwandishi Wetu Februari 13, 2008
Raia Mwema

MWISHONI mwa mwaka jana, Spika Samuel Sitta, aliunda Kamati Teule ya Bunge kuchunguza zabuni iliyotolewa kwa Kampuni ya Richmond Development ya kuzalisha umeme wa dharura. Kamati hiyo iliongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk. Harisson Mwakyembe. Wajumbe wake walikuwa ni mbunge-CUF Habib Mnyaa na wabunge wa CCM: Stela Manyanya, Lucas Selelii na Herbert Mtangi. Raia Mwema wiki hii imefanikiwa kupata nakala ya mahojiano ya Kamati na mmoja wa mashahidi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika. Mahojiano na mashahidi wengine yatachapishwa kwa kadri yatakavyopatikana.

Dk. Harrison Mwakyembe: Mheshimiwa (Mwanasheria Mkuu) AG, baada ya Richmond kuelekea kushindwa kutekeleza majukumu yake, TANESCO ilitoa default notice kwa Richmond, tunayo barua hapa. Tulitaka kujua ni nani aliyei-convince TANESCO isiendelee na intention (nia) yake ya kuvunja huo mkataba na badala yake kazi hiyo ikawa assigned (ikapelekwa) kwa Dowans.

Johnson Mwanyika: Sijui

Dk. Harrison Mwakyembe: Ofisi yako haikushiriki katika mchakato huo?

Johnson Mwanyika: Sina habari hiyo.

Dk. Harrison Mwakyembe: Kifungu cha 15 (12) cha makataba ambao mlishiriki kuutengeneza kati ya Richmond na TANESCO, kinataka assignment yoyote ifanyike kwa mutual agreement kati ya TANESCO na Richmond; Je, ushiriki wenu katika hili ulikuwaje, maana ni suala la kisheria?

Johnson Mwanyika: Labda kwa sababu Ofisi yangu ni kubwa, mimi ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali lakini pia nina wakuu wa Idara. Kwenye sehemu kama hizo ambazo unazungumzia, kuna mkuu wa madai ambaye mara nyingi anashughulika na mambo kama hayo.

Inawezekana kabisa labda Wizara ya Nishati iliomba ushauri kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, inawezekana. Lakini mimi binafsi kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kama Mwanyika, halikunifikia hilo.

Dk. Harrison Mwakyembe: Sasa unaweza kutusaidia afisa ambaye anaweza kuwa ame-handle masuala kama hayo ili aweze kuisaidia Kamati?

Johnson Mwanyika: Afisa ambaye anashughulikia masuala kama haya ya nishati katika ofisi yangu ya Mwanasheria Mkuu ni Chidowu.

Dk. Harrison Mwakyembe: Ambaye pia amekuja kwenye Kamati na masuala mengi alikuwa anakusukumia wewe, akisema utayajibu.

Johnson Mwanyika: Kama lipi alinisukumia?

Dk. Harrison Mwakyembe: Tutamrudia tena kwa sababu tulimwambia tukimhitaji tutamwita tena, awe tu na, kwanza una imani naye kubwa.

Swali jingine ambalo pengine lilikufikia, ni masuala ya kisheria tu kwa sababu inaonekana mkataba huu umekuwa na maswali ambayo mengi yanatokana na udhaifu katika negotiation na vile vile katika drafting.

TANESCO imeingia mkataba na kampuni inayoitwa Richmond Development Company LLC ya Marekani lakini Marekani hakuna kampuni ya aina hiyo. Sasa washauri wako, walishindwaje ku-notice kitu hicho? Sisi tumeshindwa kabisa kuipata kampuni inayoitwa Richmond Development Company LLC Houston, hakuna kabisa!

Johnson Mwanyika: Kama unavyofahamu, sisi tunaingia kwenye mambo ya mikataba much later, mambo ya kutafuta mtu yeyote ambaye wanaingia naye mkataba, ni juu ya procurement entity na ni juu ya Accounting Officer. Wakishamaliza mazungumzo na huyu mtu, ndiyo wanatuletea sisi barua kutueleza kwamba, kuna mambo kama haya ambayo yametendeka. Kwa hiyo, wanatushauri sisi tuweze kuwatayarishia mkataba. Kwa hiyo, whether or not kulikuwa na huyu Richmond LLC, watu ambao wanaweza kujua ni Wizara ya Nishati na Madini.

Stella Manyanya: Mheshimiwa mwenyekiti, mimi naomba unisaidie kidogo. Kwa sababu ya uelewa wangu mdogo wa sheria, napatwa na tatizo juu ya mipaka ya shughuli zetu katika Serikali kuhusu huyu Accounting Officer, ambaye pengine kiutaalamu, anaweza kuwa ni mtu wa aina tofauti kabisa na sheria na juu ya Mwanasheria ambaye nilifikiria ndiye wa msaada au consultant wa masuala ya kisheria katika department kama hizo.

Sasa katika hili, unatuambia kwamba masuala yote yanayohusu utafiti wa kisheria, ambayo labda yangetumika kuweza kutambua kama hii kampuni iko kule au haiko, yalikuwa hayahusu kabisa kupata msaada kutoka kwa Mwanasheria wa Serikali?

Johnson Mwanyika: Mheshimiwa Mwenyekiti, jibu langu ndiyo hilo kwamba sisi kazi yetu ni kutayarisha mikataba kama tutaombwa na wizara zinazohusika. Mazungumzo ya namna ya kumpata huyo mtu wanayetaka kuingia naye mkataba ni wizara yenyewe, ndiyo inayohusika.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali kazi yake ni kushauri kisheria tu kama ataombwa na Wizara zinazohusika, lakini whether huyo mtu alikuwapo au hakuwapo ni juu ya hawa ambao walimtafuta wakampata, wao ndio wanaopaswa kujua kwamba yupo au hayupo, yupo wapi. Sisi wakati tukiangalia mkataba, tunaangalia capacity kutokana na maandishi yaliyoko pale.

Je, huyu mtu ana capacity ya kuingia mkataba? Kama tukiridhika kwamba ana capacity ya kuingia ndiyo tunaendelea. Je, kuna muhtasari wa bodi yao kuzungumzia juu ya huo mkataba ambao tunapaswa sisi tutayarishe? Tukiona upo ndiyo tunaendelea na shughuli ya kutayarisha mkataba huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala hili ambalo mnalizingumzia sasa hivi, nilipozungumza na mtaalamu wangu ambaye alikuja kutoa ushahidi mbele yenu, alinihakikishia kwamba, vitu vyote hivi vilikuwapo. Kulikuwa na resolution ya bodi ya Richmond kuhusiana na mkataba huu, vitu vyote hivi waliviona.

Dk. Harrison Mwakyembe: Bahati mbaya, mtaalam tulikuwa naye hapa, tulijaribu hata kumwuliza, maana katika maelezo yake, moja ya sababu kubwa iliyofanya Richmond kupewa mkataba ni ushiriki katika hii zabuni, pamoja na kampuni popular inayoitwa Pratt and Whitney. Sasa tukasema kwa sababu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ndiyo advisor mkuu wa mambo ya sheria, ndio tukamwuliza yeye alihakikishaje kwamba Pratt and Whitney na Richmond wana uhusiano wa kisheria?

Akatuonyesha mkataba fulani ambao ni ku-share information lakini wa kushirikiana katika ku-execute project yoyote, tukio ambalo ni weakness kubwa pengine hata katika ku-interpret huu mkataba wenyewe.

Johnson Mwanyika: Mheshimiwa Mwenyekiti labda kwa sababu record zilizoko kule ofisini zinaonyesha wazi kwamba huyu Richmond pamoja na huyo Pratt, kuna mtu wao alihusika kabisa katika negotiation juu ya mkataba huu, watu wa Nishati wanamtaja kwa jina.

Ukiangalia minutes za vikao vile ambavyo wamekaa kabla ya kuingia huu mkataba, zinaonyesha wazi kwamba kuna mtu wa hiyo kampuni ambaye alishiriki katika majadiliano.

Dk. Harrison Mwakyembe: Kwa nyaraka tulizonazo, huyu hakushiriki, kilichokuwapo ni business card feki tu.

Johnson Mwanyika: Wakati fulani wanasema kulikuwa na video conference kati ya hiyo Negotiation Team na huyo Pratt huko Marekani. Ndivyo walivyosema, kufuatana na minutes zilizoko kwenye mafaili ofisi zetu.

Stella Manyanya: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli kama ulivyosema kwamba, mengi uli-delegate kwa watu ambao wangefanya, kwa hiyo, tunachohitaji kwako hasa ni kutaka kufahamu zaidi.

Kwa mfano, nimeona mahali kuna abbreviation za RDEVCO ikiwa imesajiliwa kama kampuni na sehemu nyingine nikaona kuna kitu kinachoitwa Richmond Development Company LLC; je, ile abbreviation ni lazima iwe hiyo kama hakujawa na definition ambayo imeelezwa mahali popote pale?

Johnson Mwanyika: Mheshimiwa Mwenyekiti kama nilivyosema awali, katika negotiations kulikuwa na Kamati Maalum, ambayo iliteuliwa iliyoitwa Government Negotiation Team. Wao ndio walishiriki katika negotiations pamoja na huyo Richmond. Kwa hiyo, hao watu ndio wanaweza kujibu maswali yote haya ambayo mnaniuliza, lakini mimi as Mwanasheria Mkuu wa Serikali, mambo ya negotiation sikushiriki kabisa.

Herbert Mtangi: Mheshimiwa AG, tunakuomba utusaidie kwa sababu swali lililokuwa limeulizwa hapa ni la kutaka opinion yako wewe kama AG ili kuisaidia Kamati.

Kwa mfano, tunafahamu TANESCO kama TANESCO ikiandikwa vile TANESCO ni kifupi cha Tanzania Electric Supply Company, lakini bila kupewa tafsiri ya shirt form hii, nikikuta mahali pameandikwa TANESCO na mahali pengine pameandikwa Tanzania Electrical Supply Company Limited, hivi kutakuwa na dosari nikisema hizi ni entities mbili tofauti?

Johnson Mwanyika: Mheshimiwa Mwenyekiti, inategemea vitu vingi, inawezekana mtu ana makosa ya kuandika hivyo, lakini ambao wanaweza kujibu swali hilo vizuri ni watu wa Wizara ya Nishati na Madini, ambao ndio walihusika tangu mwanzo katika kushughulikia suala hili la kutafuta mwekezaji wa kutupatia jenereta kwa ajili ya kuzalisha umeme wakati ule wa dharura.

Herbert Mtangi: Ni kweli tunaweza tukajibiwa hilo na watu wa Wizara ya Nishati na Madini, lakini hapa nimekupa mfano wa TANESCO na kirefu cha TANESCO na hakuna mtu aliyetafsiri kwamba TANESCO ni kifupi cha hilo nililokupa wewe. Kama ungekuwa hujui ukweli wa Shirika la TANESCO na mtu akakuwekea hivyo, wewe kama Mwanasheria, ungetafsiri hiyo entinty moja au entities mbili?

Johnson Mwanyika: Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo sababu nasema kwamba inategemea, inawezekana mtu aliyeandika kwa kifupi alikosea.

Herbert Mtangi: Mheshimiwa Mwenyekiti, jingine ni kwamba, hii Kamati imeundwa ndani ya Bunge na kwa bahati nzuri siku ile Spika anatamka, wewe kama AG ulikuwapo ndani ya Bunge.

Kwa hiyo, unafahamu kuna mvutano katika mkataba wa Richmond unaozungumziwa hapa. Wewe kama AG, ambaye ndiye msimamizi mkuu katika kitengo kile, katika muda huo mfupi, umewahi kuusoma mkataba huu wa Richmond Development Corporation ambao ndiyo umeundiwa Tume?

Johnson Mwanyika: Mkataba huu niliupitia.

Herbert Mtangi: Kama umeupitia na wewe ni mtaalamu tena wa kubobea wa sheria, nini maoni yako katika mambo mawili; Je, unadhani Richmond ilishindwa kutekeleza mkataba au ilifanya uamuzi tu wa kawaida wa ku-assign kazi zake kwa Dowans?

Johnson Mwanyika: Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati mwingine unapoambiwa toa ushauri wa kisheria, huwa tunaandikiwa na tunaulizwa maswali ambayo tunatakiwa tuyajibu. Kwa hiyo, hili nitakalozungumza hapa, linatokana na ufahamu wangu kuhusu suala hilo.

Ninavyofahamu ni kwamba, kulikuwa na masharti ambayo yalikuwa yamewekwa kwenye ule mkataba. Sharti mojawapo ni kwamba, lazima Serikali ifungune Letter of Credit ili kuwawezesha Richmond kuleta hiyo mitambo.

Hilo lilileta matatizo kidogo, Serikali ilichukua muda kidogo kufungua Letter of Credit, kwa sababu ilishindwa, hilo siwezi kulielewa, watu wa Nishati ndiyo wanaweza kujua zaidi kuliko mimi lakini nadhani mpaka mwisho ile Letter of Credit ilikuwa haijafunguliwa.

Walipochukua watu wa Dowans ndipo Letter of Credit ikafunguliwa na mambo ndiyo yakaanza kuendelea vizuri, hivyo ndivyo ninavyofahamu.

Mohamed Habib Juma Mnyaa: Mheshimiwa Mwenyekiti nashukuru. Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu, kwa vile umesema mkataba umeusoma na kwa kuwa wewe ndiye Mwanasheria Mkuu wa Serikali, mara nyingi sana katika mikataba kunakuwa na kipengele cha definitions na interpretations.

Sasa ikiwa katika Mkataba huu kuna definition ya abbreviation RDECO halafu ikitafsiriwa kwamba, RDEVCO ni Richmond Development Corporation wakati abbreviation hiyo katika definition and interpretation haimo; je, itakubalika kisheria kwamba, hiyo RDEVCO ndiyo Richmond?

Johnson Mwanyika: Labda unipe huo Mkataba niuangalie, nione mahali ambapo una-refer.

Mohamed Habib Juma Mnyaa: Mkataba huu unazungumzia agreement ya emergency between Tanzania Electrical Supply Company na Richmond Development, lakini kwenye definition and interpretations, mimi sijaona hiyo definition au interpretation ya RDEVCO.

Nikija katika minutes, kuna kitu kimetajwa RDEVCO, sasa ikiwa katika interpretation na definition hakuna tafsiri; je, nichukulie hii RDEVCO kuwa ndiyo Richmond Development Company?

Johnson Mwanyika: Mheshimiwa Mwenyekiti, lililokuwa referred kwenye minutes za vikao hivi, karibu watu wote waliohudhuria, mashirika waliyotoka yameandikwa in short form.

Sasa tafsiri iliyotokana kwenye Mkataba ni kwa ajili ya mambo yaliyokuwa kwenye Mkataba wenyewe. Haya mambo yanayozungumzwa kwenye minutes ni minutes za kikao walichokaa hawa watalaamu wa haya mashirika ambayo yamekuwa represented kwenye kikao hiki.

Ukiangalia hata watu wa TANESCO, haikuandikwa Tanzania Electrical Supply Company Limited imeandikwa TANESCO, watu wa CPI wameandikwa CPI, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wameandikwa AG, Benki Kuu wameandikwa Bank of Tanzania hawakuandikwa BoT, lakini hawa wengine ilikuwa ni short form ya makampuni wanayotoka.

Sasa mimi kwa sababu nafahamu kwamba, huyu Gire ni mmoja wa wakurugenzi wa RDEVCO, nina hakika kwamba, iliyoandikwa RDEVCO ilikuwa ni hiyo kampuni inayozungumziwa kwenye mkataba.

Hata ukiangalia kwenye Mkataba kwenye definition section, hakuna ambapo imeandikwa kwamba AG means what. Kwa haya yaliyozungumzwa hapa, mambo ya short form yalikuwa kwenye mikutano iliyofanyika wakati wa ku-negotiate huo mkataba.

Herbert Mtangi: Tukujazie hapo hapo, hebu tusaidie. Umeona Mkataba na minutes: Je, kwa utaalamu wako, kisheria minutes hizo zina form part of the contract?

Johnson Mwanyika: Inategemea watu walivyopatana, walivyoingia Mkataba walipatanaje kwamba hizi minutes ziwe sehemu ya Mkataba au namna gani. Kama walipatana kwamba ziwe sehemu ya Mkataba, inakuwa sehemu ya Mkataba na kama hawakupatana kuwa sehemu ya Mkataba haiwezi kuwa sehemu ya Mkataba.

Maofisa ambao niliwatuma walisema kwamba, wakati wa ku-negotiate walikubaliana hizi minutes ziwe sehemu ya mkataba.

Herbert Mtangi: Je, hilo halikupaswa kuandikwa kwenye ule Mkataba wenyewe kwamba kuna minutes zitakuwa attached na zita-form part of the contract?

Johnson Mwanyika: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninavyofahamu, mara nyingi kuna mikataba mingine ya kuzungumza tu si lazima kila kitu mlichopatana kati yako wewe na mtu mwingine kiandikwe, vile vitu muhimu tu ndiyo vinavyoandikwa. Kama kwenye negotiations walikubaliana kwamba ile itakuwa part ya agreement ni kitu ambacho walipatana, basi.

Lucas Selelii: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwanasheria anaposema kwamba vitu muhimu ndivyo vinavyoandikwa, hivi ndani ya minutes humo kuna vitu muhimu sana kama kumhusisha Pratt and Whitney kwenye Mkataba kati ya Richmond na Pratt and Whitney, lakini ndani ya Mkataba Pratt and Whitney wala hawatajwi kabisa; haoni hicho nacho ni muhimu ingeandikwa kwamba minutes hizi ni part ya Mkataba?

Johnson Mwanyika: Mheshimiwa Mwenyekiti inawezekana labda kulikuwa na upungufu huo, lakini ukweli ni kwamba, yule ofisa ambaye alikuja mbele yenu hapa yeye alisisitiza kwamba, walikubaliana hizi minutes ziwe sehemu ya mkataba na yeye katika utaalamu wake wa kisheria anasema, wakati mwingine ndivyo inavyokuwa si lazima uziandike kwenye mkataba, alivyoeleza yeye.

Stella Manyanya: Unafikiria ni kitu gani pengine kinaweza kikawa kimesababisha huyu mwenzetu wa upande wa pili, kujiita jina ambalo halijaandikishwa popote kisheria lakini wakati huo huo, hata hayo makubaliano unayosema ameingia na huyu Pratt and Whitney amejiita kwa jina lile ambalo ameandikishwa; huoni kama alikuwa anacheza mchezo fulani hivi?

Johnson Mwanyika: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema, mambo yote kuhusiana na huyo mtu kwamba alikuwa ni mtu gani, alitokea wapi, watu wa Nishati ndio wanaelewa vizuri zaidi. Ile timu ambayo ilizungumza na huyu mtu, ndiyo ingepaswa kujua huyu mtu alikosea wapi na ni nani na kwa sababu gani alitumia majina mawili tofauti.

Lucas Selelii: Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niwarudishe nyuma kidogo. Pamoja na kwamba watu wa Nishati na Madini ndio wanajua zaidi, nadhani atakumbuka kwamba, wakati ule wa dharura yeye AG, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, ndio walikuwa watu wa kwanza kupewa hili jukumu; haoni kwamba na yeye anahusika kwa kiwango kikubwa zaidi?

Johnson Mwanyika: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nakumbuka vizuri, katika kikao cha Baraza la Mawaziri cha tarehe 10 Februari, kilichosemwa ni kwamba, watakaosimamia hili zoezi la kutafuta hawa wakandarasi ni Wizara ya Nishati na Madini, ambayo Katibu Mkuu wake atakuwa Mwenyekiti halafu kukawa na wajumbe kutoka Wizara ya Fedha na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, lakini ofisi yangu ilishirikishwa wakati wa ku-negotiate.

Wakati wa kumtafuta huyu mtu, ni maofisa wale wengine kutoka Wizara nyingine ndio waliohusika, Ofisi ya AG ilihusishwa tu wakati wa ku-negotiate huu Mkataba, huo ndio ukweli.

Lucas Selelii: Lakini hapo hapo, taarifa ambazo tunazo, Ofisi ya Mwanasheria haikutajwa zaidi ya AG na Mwenyekiti alikuwa Katibu wa Wizara ya Fedha, ambao baadaye walikuja kuunda hiyo Steering Committee ikaja ikaunda hao unaowasema.

Sasa mimi ninamrejesha hapo mwanzoni, kama Baraza la Mawaziri liliona yeye ni mtu muhimu kuhusika na hili jambo; kwa nini wanajitoa mara kwa mara kwamba hawahusiki?

Johnson Mwanyika: Napenda kurudia kusema kwamba, Baraza la Mawaziri lilisema Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ndiyo imesemwa hivyo si kwa kukosea. Kwa sababu kama nilivyosema, mimi ndiye kiongozi wa ile ofisi lakini wakati wa kutafuta ushauri wa kisheria, si lazima iletwe moja kwa moja kwangu, inapelekwa kwa Law Officers.

Law Officer ni mwanasheria yeyote ambaye ana cheo kinachozidi cha Senior State Attorney. Kwa hiyo, wizara yoyote inaweza kuomba ushauri kutoka kwetu kwa watu wa aina hiyo.

Kama nilivyosema, kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu pia kuna Idara na kuna mtu anayeshughulika na mambo ya Civil and International ni Mkurugenzi wa Civil and International. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, anakutana na hivyo vitu wakati akicheki mafaili ambapo barua zilizoandikwa kwa wiki huwa humo, litapita kwangu nazicheki zote ndiyo najua mambo ambayo yanatendeka kwenye Wizara.

Kiutendaji ni kwamba, wale Law Officers ndio ambao wanatoa ushauri kwa zile wizara, wakiomba kimaandishi kutoka kwenye wizara hizo.

Inawezekana kweli kabisa labda kuna ofisa ambaye alihusishwa mwanzoni kabisa katika zoezi hilo, maana mimi ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kuna Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ndiye Katibu Mkuu, yawezekana kabisa kwamba, kwa sababu ilikuwa ni Makatibu Wakuu ndio walisimamia zoezi hilo, yawezekana kabisa Katibu Mkuu wakati ule ambaye ni Mheshimiwa Limbu, labda alihusishwa kwenye zoezi hili la kwanza kabisa.

Mimi kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, niliteua mtu wakati wa ku-negotiate lakini tender ilikwendaje, watu wa Nishati ndio wanaojua zaidi.

Mohamed Habib Juma Mnyaa: Mheshimiwa Mwenyekiti, itabidi format ya maswali ibadilike kutokana na majibu ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mimi ninalotaka kuuliza, nakuuliza kama Mwanasheria Mkuu; Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu, Richmond ilikuja kwa sababu ya kuzalisha umeme wa dharura kwa kipindi ambacho Tanzania tulikuwa katika janga kubwa la kukosa umeme.

Hivyo, ilitakiwa kuzalisha umeme katika kipindi cha miezi mitano, lakini ilishindwa badala yake imetumia miezi 16 hadi kutimiza zile megawatts 100. je, unaishauri nini Serikali ukizingatia kuwa, umuhimu ule wa dharura haupo tena na gharama Serikali ilizoingia ni mara mbili kwa umeme huu?

Je, tuendelee nao tena kwa kipindi cha miaka miwii kuanzia Oktoba walipokamilisha au vipi? Unaishauri nini Serikali katika kipindi hiki ambapo udharura huo haupo tena?

Johnson Mwanyika: Mheshimiwa Mwenyekiti, tukio hilo linanipa matatizo kidogo kwa sababu hilo ni jambo ambalo linahitaji taaluma ya hao watu ambao wanahusika na mambo hayo. Ninavyofahamu, kuna Mkataba ambao Serikali iliingia na huyo Richmond ambao baadaye ulikuwa assigned kwa Dowans.

Kwa hiyo, kama tulipatana kwamba huyu mtu alete mitambo hiyo akae kwa miaka miwili au mwaka mmoja, tukimwambia aondoke, tutakuwa tunavunja Mkataba ule.

Mohamed Habib Juma Mnyaa: Ikiwa pia tulikubaliana kwamba umeme wa dharura tunauhitaji kwa miezi mitano na hatukuupata kwa miezi mitano hii?

Johnson Mwanyika: Kama nilivyosema ni kwamba, yapo masharti yalikuwapo kwenye mkataba ambayo pia upande wa pili haukutekeleza na ndiyo sababu walishindwa kuleta hizi mashine mapema zaidi.

Dk. Harrison Mwakyembe: Waheshimiwa wabunge, nafikiri tumekaa kiasi cha kutosha na ratiba bado ni ndefu, naomba mniruhusu nichukue fursa hii kumshukuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwa kuitikia wito wetu na kuja ili tuweze kubadilishana mawazo.

Tunakuomba basi huyo Afisa wako Chidowu kama ukipita pale, mtaarifu tu kwamba, tutamuhitaji tena ili tuweze kufanya final touches sehemu ambazo nadhani yeye alitegemea AG ndiye atakuja kuzijazajaza, lakini kumbe ulishampa authority yote na tutakushuru sana ukimtaarifu.
 
Na bado yupo ofisini na alishiriki kutupangia Baraza la Mawaziri!!!

Jamani huyu ndiye tumempa madaraka ya kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali yetu ya Tanzania?? Ina maana au, ndio kusema mimi nimeshindwa kujua mamlaka yake manake hata KATIBA YA JAMHURI imemuongelea huyu mkuu jamani*&%^@$%*!

Lord have mercy.............. Somebody shoot me, NOW!!!
 
There's a natural mystic blowing through the air;
If you listen carefully now you will hear.
This could be the first trumpet, might as well be the last:
Many more will have to suffer,
Many more will have to die - don't ask me why.

Things are not the way they used to be,
I won't tell no lie;
One and all have to face reality now.
'Though I've tried to find the answer to all the questions they ask.
'Though I know it's impossible to go livin' through the past -
Don't tell no lie.

There's a natural mystic blowing through the air -
Can't keep them down -
If you listen carefully now you will hear.

There's a natural mystic blowing through the air.

This could be the first trumpet, might as well be the last:
Many more will have to suffer,
Many more will have to die - don't ask me why.

There's a natural mystic blowing through the air -
I won't tell no lie;
If you listen carefully now you will hear:
There's a natural mystic blowing through the air.
Such a natural mystic blowing through the air;
There's a natural mystic blowing through the air;
Such a natural mystic blowing through the air;
Such a natural mystic blowing through the air;
Such a natural mystic blowing through the air

Not only was it a beautiful song......
 
Na bado yupo ofisini na alishiriki kutupangia Baraza la Mawaziri!!!

Jamani huyu ndiye tumempa madaraka ya kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali yetu ya Tanzania?? Ina maana au, ndio kusema mimi nimeshindwa kujua mamlaka yake manake hata KATIBA YA JAMHURI imemuongelea huyu mkuu jamani*&%^@$%*!

Lord have mercy.............. Somebody shoot me, NOW!!!

Inawezekana ikawa dhambi kusema lakini huyu jamaa hata kwa kumwangalia tu na akiongea mbele za watu anaonekana mtupu sijui ilikuwaje wakampa mambo haya makubwa ila najua ni kazi ya Chenge kufunika yote .
 
Duh kweli hii ndio Afrika....

Mwanasheria Mkuu wa serikali yeye kazi yake ni kupitia barua za wiki kujua kinachotendeka katika Wizara......

Nadhani inatakiwa tupate Job Description ya huyu mtu, kama ni kweli kwa jinsi alivyoeleza basi aendelee kula pension still akiwa ofisini, kama ni otherwise awajibishwe tu...
 
Inawezekana ikawa dhambi kusema lakini huyu jamaa hata kwa kumwangalia tu na akiongea mbele za watu anaonekana mtupu sijui ilikuwaje wakampa mambo haya makubwa ila najua ni kazi ya Chenge kufunika yote .

COME ON ALL AND SING

SASA NIMEAMUA KUIMBA TUU

Na-na-na-na-na-na-na-na-na;
Na-na-na-na-na-na-na-na-na;
Na-na-na-na-na-na-na-na-na;
Na-na-na-na-na-na-na-na-na.

Them belly full but we hungry.
A hungry mob is a angry mob.
A rain a-fall but the dirt it tough;
A pot a-cook but the food no 'nough.
You're gonna dance to JAH music, dance.
We're gonna dance to JAH music, dance.
Forget your troubles and dance.
Forget your sorrow and dance.
Forget your sickness and dance.
Forget your weakness and dance.
Cost of living get so high,
Rich and poor, they start a cry.
Now the weak must get strong.
They say, "Oh, what a tribulation."

Them belly full but we hungry.
A hungry mob is a angry mob.
A rain a-fall but the dirt it tough;
A pot a-cook but the food no 'nough.
We're gonna chuck to JAH music, chuckin'.
We're chuckin' to JAH music, we're chuckin'.

A belly full but them hungry.
A angry mob is a angry mob.
A rain a-fall but the dirt it tough;
A pot a-cook but the food no 'nough.

A angry man is a angry man.
A rain a-fall but the dirt it tough;
A pot a-cook but the food no 'nough.
(Repeat)
A angry mob is a angry mob.
 
Jamani eehh hata mimi sielewii...huyo Mwanyika alikuwa hajawahi kufikiria ipo siku atatoka hapo?anatakiwa ajiandae kwa lolote ..hilo tu ndilo linalomsumbuaa....hana jipya kama kuboronga ameshaboronga atupishe tu hapooo........anatakiwa apewe ushauri..kazi zipo nyingi ushauri wa bure nampa ajiandae kufungua law firm yake....maana alipofika hawezi kupata direct employment...ila atoke ofisini haraka maana akitolewa hatapata hata hao wateja.....maana jina litachafukaa..kabisa...akifukuzwa na JK...naomba kuwakilisha
 
Anasahau kuwa "Responsibility" inakuja na "Accountability" pia.... Nadhani ndio maana mikataba yote imepwaya sababu inaonekana huyu jamaa/ofisi ya AG kweli hawajui wajibu wao.....

TechMaro, hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeandika majukumu yake huyu mkuu lakini yeye mwenyewe, sijui....

Wanasheria ndani ya JamboF mpo lakini?? Hii ni disgrace to the Legal Community (to me!)

Eeee Mola tusaidie............
 
Yaani huyu mwanasheria mkuu anaongea kama mwanasiasa. Hakuna chochote alichojibu hapo. Huyu anastahili kupigwa chini haraka maana anadhalilisha taaluma ya sheria. Raisi kikwete anatakiwa kumwajibisha haraka sana. Akajiunge na wenzake waliotangulia kwenye kilima cha golgota.
 
Yaani huyu mwanasheria mkuu anaongea kama mwanasiasa. Hakuna chochote alichojibu hapo. Huyu anastahili kupigwa chini haraka maana anadhalilisha taaluma ya sheria. Raisi kikwete anatakiwa kumwajibisha haraka sana. Akajiunge na wenzake waliotangulia kwenye kilima cha golgota.

AAAA WAPI..... JAMANI KATAI NCHI INAYOONGOZWA KISANII NSITEGEMEE HUYU MTU KUWAJIBISHWA............
 
Duuuhhh!!!!!...............ANOTHER WEAKEST LINK!!

Mwanyika achia manyanga ndg yangu...............you are EXTREMELY WEAK to hold that position..............no wonder tunakuwa na mikataba ya ajabu ajabu..................kwanza umeonyesha kuwa wewe ni MVIVU kusoma na ni mtu wa kutupia lawama zisizo na msingi wenzako na unakimbia majukumu......tena majukumu ya kiapo chako ulipokuwa unaapishwa.

Binafsi nimeshiriki katika uandaaji wa mikataba mingi sana sana na makampuni makubwa........sijawahi kukutana na AG slack and weak kama huyu wetu


JK pleeeaasse...........hebu tuondolee huyu mtu.........he is weak hawezi kuwa mshauri wako mzuri......wako watu wengi tu ambao ni smart at your disposal Mr President
 
Back
Top Bottom