Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Lile Sakata Liloliingizia Hasara Kubwa Nchi Yetu Na Kumalizwa Bila Wahusika Kuchukuliwa Hatua Zozote Limeingia Katka Sura Mpya Kuna Baadhi Ya Vigogo Kadhaa Hawana Imani ,,na Wengine Presha Juukutokana Na Hofu Za Kutimuliwa Kazi Wakiwemo Walio Katika Tume Ya Kuchunguza Soo Hili!!!

Kwa Mujibu Wa Chanzo Chetu Vigogo Hao Ambao Kwa Namna Moja Au Nyingine Walihusishwa Katika Ripot Ya Mkuu Wa Kazi ....dk Mwakyembe

Jamaa Hivi Sasa Hawana Amani Hata Kidogo Kuna Mmojawapo Ambaye Hivi Sasa Amekuwa Mpole Badala Ya Kuonyesha Ile Haiba Yakeya Uchangamfu ..nadhani Ana Wasiwasi Sana Na Pengine Ataachia Ngzi Kilisema Chanzo,

Chnzo Kingin Kilieleza ..""huyu Jamaa Ni Jamaa Yangu Wakaribu Sana Na Nichoweza Kueleza Amejawa Na Hofu Kweli!!!!!jamaa Alihuzunika Zaidi Baada Ya Mh Pinda Katika Kujumuisha Na Kusema Ameshamaliza Mambo Mengi Yaliohusu Maelekezo Ya Tume Na Anasubiri Nafasi Ya Spika Kumpa Amwage Unga!!!!!babu Kubwa.....hapa Kidogo Pana Utata

Hawa Watu Nahisi Nao Wana Akili..wanajua Soo La Meremeta Lote..kwa Hiyo Kama Huyo Waziri Mkuu Ameshindwa Kutaja Nani Mmiliki Wa Meremeta...hakuna Jipya Wananchi..tusifanywe Wajinga,

"kwako Waziri Mkuu Pinda"

Watanzania Si Wote Mambumbumbu Sa Sahivi Naomba Hili Ulielewe..na Hakuna Anaedanganyika Na Story Kama Wenzako Wlaiopita Walivyokuwa Wakiwadaha Wananchi Ndege Inaruka Ukifanya Mchezo Unaweza Na Wewe Kukisikia Hiko Cheo Kama Lowasa..wale Wanaoukupongeza Wanakujaza Ujinga....eleza

Meremeta Kampuni Ya Nani?????????

Kiwira Imauzwaje?? Na Kwa Sh Ngapi Na Imetolewa Ngapi Bado Ngapi Wacha Longolongo Mzee

Nilisikitika Sana Kumuona Akijibu Kwa Madaa Swaala La Meremeta Ni La Usalama..kama Usalama Wezi Wataje Usalama Ni Watu Na Wamechota Zile Hela Azikuja Na Ndege Waeleze Zikwapi???
Hata Kama Ulipata Mgao Au ?????????

Cha Kusikitika Kingine Ati Jamani Wabunge Wenzangu Kiwira Ilikuwa Hoi Kabisa Alafu Badala Ya Kuelezea Umeifufua Au Umeendelea Kuiua Unadai Hilo Na Mwachia Waziri Mhusika,,

Kwenu Mawaziri
Ukitaka Chukua Ukinuna Acha...kuweni Na Makini Na Huyu Mkuu Wetu Nimemsikiliza Amekuwa Akiwapelekea Vibomu Vingi Mlipuke Na Vyo..kama Anatakiwa Kujibu Mueleze Mzee Pale Kajibu Wewe Msiogope Mjanja Huyu....pamoja Na Hilo

Nakupongeza Kwa Kupitishwa Bajeti Yako Natumaini Hamtokula Ovyo Kama Mwenzako

Edward Lowassa
 
Mzee hii ume cut na ku- paste au ume-edit pia?
Safi sana kama hayo ni mawazo ya wananchi, maana wasiwasi wangu mkubwa ni kwamba wananchi wengi hawaelewi kinachoendelea, bado wako katika zama za "zidumu fikra za mwenyekiti" au bado wana imani kiongozi ni kiongozi hasemi uongo wala hadanganyi.
 
Sasa mtu keshaitwa Pinda unategemea nini majina mengine yanawazuru watu, kama yamenyooka basi atayapindisha na kama yamepinda atayanyoosha, ila naona tulikuwa tumeanza kunyooka au kunyooshana sasa huyu Bwana Pinda athari za jina lake zimeanza kuonekana, hatujui kama yale yaliopinda atayanyoosha.
 
Date::6/29/2008
Mambo ya EPA, Richmond bado kitendawili bungeni

*Wabunge wasema Pinda kaahirisha tatizo
*Wataka kuomba bunge Meremeta ijibiwe

*Wananchi wataka kilichofichwa Richmond

*Chitalilo asema wanaomlaumu ni wahuni

Na Timu ya Mwananchi Jumapili
Mwananchi

SUALA la kashfa ya kampuni iliyopewa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond na wizi wa mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), bado linaendelea kufukuta huku baadhi ya watu wakiona kuwa serikali inaahirisha tatizo badala ya kulipatia ufumbuzi.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini wanaona kwamba hatua ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kushindwa kuweka hadharani nini anachokijua kuhusu wanaohusika na wizi wa EPA na kukataa kuzungumzia Meremeta wakati anahitimisha mjadala wa bajeti ya ofisi yake Ijumaa iliyopita, inaonyesha serikali bado inakigugumizi kuhusu masuala hayo nyeti.

Pia wanasema hatua ya serikali kuahirisha kueleza hatua ya utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati ya Bunge ya Dk Harrison Mwakyembe kuhusu kashfa ya Richmond inaonyesha kuwa bado suala hilo litazidi kuliyumbisha bunge.

Tayari suala la Richmond na EPA limeleta ufa ndani ya Bunge na katika Chama Cha Mapinduzi baadhi wabunge wakijitokeza wazi wazi kuwasafisha watuhumiwa na huku wengine wakitaka wachukuliwe hatua zinazostahili.

Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili ambayo wiki mbili zilizopita ilichapisha habari za ndani za wabunge kujipanga kuibua suala hilo hadi lipate ufumbuzi, unaonyesha kuwa suala hilo bado linafukuta na moto wake unaweza kuwaka wakati wowote endapo serikali itaendelea kupata kigugumizi cha kuchukua hatua.

Kitendo cha baadhi ya wabunge kuanza mbinu za chini chini na za wazi za kuwasafisha wenzao wanaotuhumiwa katika Richmond, EPA na ufisadi wa aina nyingine kimezidi kuongeza ufa unaohitaji ukarabati wa haraka.

Hali hiyo imesababisha Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza zabuni ya Richmond, Dk Harrison Mwakyembe, kusimama bungeni wiki hii kutahadharisha kuwa kuibua hoja hiyo wakati ilishatolewa uamuzi na Bunge ni kukiuka Kanuni za Bunge na hivyo, kulidharau.

Alisema kwamba kamati yake haikumwonea mtu na kwamba kuna mambo mengi ambayo wameyaacha kuyaweka hadharani ili kulinda hadhi ya serikali.

Ingawa hoja hiyo ya Mwakyembe inaonekana kuumiza upande wa pili wa watuhumiwa wa kashfa hizo, imeibua hoja nyingine ya wananchi na wabunge wenzake kumtaka atoe hadharani mambo ambayo anasema kamati yake iliyaacha kuyatoa kwa ajili ya kuilinda serikali.

Baadhi ya watu hao ni Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (Tangayika Law Society-TLS) Erick Ng'mario, ambaye wiki hii alisema katika uchunguzi huwa kuna mambo mengi sawa na mahakamani, hivyo kinachotafutwa ni ushahidi.

Mwingine aliyetoa kauli kama hiyo ni Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party, Augustine Mrema na mmojawapo wa mawaziri aliyejiuzulu kutokana na kashfa ya Richmond, Nazir Karamagi aliyekaririwa wiki hii akisema kuwa Mwakyembe atoe ushahidi aliouacha na iundwe tume huru ya watu kutoka nje ya bunge ichunguze suala hilo.

Hata hivyo, Mwakyembe alipotakiwa jana kutoa ufafanuzi kuhusiana na lawama hizo, alisema hawezi kuzungumzia suala ambalo amekwishalizunguza bungeni.

Hatua za safisha tuhuma za ufisadi zinazofanywa na baadhi ya wabunge zimeanza kuwatokea puani baadhi yao, ambapo Mbunge wa Buchosa, Samwel Chitalilo ameandamwa na wapigakura wake wakimtaka anyamaze kwa kuwa kauli yake ya kumtetea Andrew Chenge na Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa si miongoni mwa mambo waliyomtuma.

Hata hivyo, Chitalilo mwenyewe amelieleza Mwananchi Jumapili jana kuwa, anayachukulia maoni ya watu hao kama ya wahuni.

Alisema watu wenye akili timamu hawawezi kumchafua Rais wa Awamu ya Tatu kwa maneno ya kejeli na kwamba amesisitiza kuwa, Andrew Chenge hakuwa na kosa, wala hajavunja nyumba wala benki, na bado haijathibitika kuwa ana kosa lolote na ni haki yake kama mbunge kumtetea.

Juzi Pinda alitoa maelezo yaliyoonekana kutowaridhisha baadhi ya wabunge ambao walipokea kwa hisia tofauti huku wakionyesha dhahiri ameshindwa kujibu hoja hizo.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alisema serikali inapaswa kuhakikisha masuala haya ya kitaifa yanafikia kikomo kwa kutoa maelezo ya kina kwani kinyume chake ni hatari kwa uchumi wa taifa.

Alisema Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amekosea kuficha ukweli kuhusu Meremeta na kambi ya Upinzani inajiandaa kutumia kanuni za Bunge kumtaka asimame tena bungeni ajibu hoja hiyo.

Alisema sio kweli kwamba Waziri Mkuu amebanwa na sheria kuzungumzia Meremeta kwani ingekuwa hivyo, suala hilo lisingeingia kwenye kamati ya Rais ya kupitia upya mikataba ya madini na kujadiliwa na watu ambao sio watendaji wa serikali.

"Hapa kaandike tu kwamba Zitto kasema haridhiki na majibu ya Waziri Mkuu kuhusu Meremeta kwani kama ingekuwa ni kwa sababu za ulinzi na usalama ilikuwaje suala hilo liliingia kwenye kamati ya madini?" alihoji Zitto.

Kuhusu EPA Zitto alisema ingawa ni busara kusubiri matokeo ya Tume ya Rais, Waziri Mkuu bado alikuwa na nafasi kulieleza Bunge anachojua tofauti na alivyosema kwamba tusubiri matokeo ya tume hiyo.

Naye mbunge wa Masasi, Raymond Mrope alisema ana wasiwasi na utendaji wa viongozi wa serikali katika masuala muhimu ya taifa kwani ameshindwa kuelewa namna ubadhirifu wa mabilioni ya shilingi ulivyofanywa kwenye Richmond.

Mbunge wa Kibakwe (CCM) George Simbachaweni amemsifia Waziri Mkuu kwa majibu ya hoja za wabunge kuhusu Richmond, Mahakama ya Kadhi, Mwafaka, Mgodi wa Kiwira na Meremeta akisema yamemaliza mjadala.
 
Richmond: Vigogo hatarini kudakwa

2008-07-02 17:06:55
Na Mwandishi Wetu, Jijini

Kuna taarifa kuwa lile sakata la mkataba tata baina ya Serikali na kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond limechukua sura mpya baada ya baadhi ya vigogo maarufu kuanza kuliwa mingo ili wadakwe kabla ya kuchukua hatua zozote za kutimkia nje ya nchi.

Taarifa za uhakika toka kwenye chanzo chetu zinadai kuwa hivi sasa, kuna makachero waliojipanga kila kona wanapokuwa vigogo hao ili kuhakikisha hakuna yeyote atakayeweza kutimka nchini kirahisi, ili kukwepa mkondo wa sheria kutokana na `dili` hilo lililozaa kashfa ya malipo ya kifisadi ya zaidi ya Sh. Milioni 180, yanayolipwa na Serikali kila siku.

Taarifa hizo zinadai kuwa kujiandaa kwa makachero wa Jeshi la Polisi na wale wa Usalama wa Taifa katika kuwawinda vigogo husika, zinatokana na taarifa zilizowafikia kuwa kuna mmoja yuko kwenye mipango ya kujiandaa kuikimbia nchi baada ya mambo kuwa mazito.

``Hakuna aliye juu ya sheria...hata huyo uliyemtaja, hawezi kuchomoka kwa namna yoyote...Wana usalama wanazo taarifa zote na wamejiweka tayari kumfuatilia ili akijaribu tu, wamtie mbaroni,`` kimedai chanzo chetu.

``Mimi nakuambia, kwa vyovyote vile, kigogo huyo hawezi kutekeleza mpango wake huo wa kuikimbia nchi kwa sababu Serikali imejipanga vilivyo katika kuzuia jaribio la aina hiyo,`` chanzo chetu kikaongeza.

Kashfa ya mkataba wa Richmond imekuwa gumzo kubwa nchini, hasa baada ya kuanikwa kwa ripoti ya Kamati ya Bunge iliyoongozwa na Mhe. Harisson Mwakyembe kuonyesha kuwa Serikali iliingizwa mkenge kwa kuingia mkataba wa kuzalisha umeme na kampuni hiyo iliyoelezwa kuwa ni ya kitapeli.

Hata hivyo, Richmond waliuhamishia mkataba wao kwa kampuni nyingine ya Dowans, ambayo hadi sasa inadaiwa kuwa inalipwa na Serikali zaidi ya Sh. Milioni 150 kwa siku, huku Tanesco ikitoa tamko kuwa itasitisha kuhusika na kampuni hiyo mwezi ujao.

Katika taarifa hiyo, vigogo kadhaa walitajwa kuhusika kwa namna moja au nyingine na hatua kadhaa zikapendekezwa kuchukuliwa dhidi yao.

Kufuatia mapendekezo ya kamati hiyo ya Dk. Mwakyembe, mbunge wa Kibaha Vijijini ambaye alikuwa Waziri wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha alilazimika kujiuzulu uwaziri wake, kama ilivyokuwa kwa mbunge wa Bukoba Vijijini Mhe. Nazir Karamagi, (pichani ukurasa wa mbele) ambaye aliitema nafasi aliyokuwa nayo ya uwaziri wa Nishati na Madini.

Aidha, Mbunge wa Monduli Bw. Edward Lowassa, naye alilazimika kujiuzulu nafasi ya kuwa Uwaziri Mkuu na kupelekea kuvunjwa kwa baraza zima la mawaziri.

Baadhi ya waliotajwa katika ripoti hiyo ya Dk. Mwakyembe, kwamba wanahusika na Richmond kwa namna mbalimbali ni pamoja na Mbunge wa Igunga (CCM), Mhe. Rostam Aziz, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Johnson Mwanyika na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa , Dk. Edward Hosea.

SOURCE: Alasiri
 
Sakata la Richmond, Dowans: Wabunge walonga

na Mwandishi Wetu, Dodoma
Tanzania Daima

MATUKIO mawili makubwa yenye uhusiano wa karibu, lile la kurejea kwa kasi kwa mjadala wa Richmond bungeni katika siku za hivi karibuni na la kusitishwa kwa mkataba wa kuzalisha umeme wa Dowans yanaonekana kuendelea kuwagawa wabunge.

Mahojiano ya ana kwa ana yaliyofanywa na Tanzania Daima mjini Dodoma na Dar es Salaam jana yanaonyesha kuwa, wabunge wamepokea tukio la juzi la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) la kusitisha mkataba wa Dowans kwa mawazo tofauti.

Akizungumza mjini hapa jana, Mbunge wa Bukoba Vijijini, Nazir Karamagi alisema watu walioingia mkataba na Kampuni ya Dowans ambao umevunjwa rasmi jana, hawapaswi kulaumiwa kutokana na hali ilivyokuwa wakati huo, kwani nchi ilikuwa imebakisha wiki mbili tu iingie gizani.

Karamagi ambaye Februari mwaka huu alilazimika kujiuzulu uwaziri wa Nishati na Madini baada ya jina lake kuhusishwa katika mkataba huo, aliyasema hayo wakati alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu uamuzi huo uliotangazwa juzi na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dk. Idris Rashidi.

Kutokana na hali hiyo, Karamagi aliitahadharisha serikali kuwa, inapaswa kuwa makini na hatua za kujitetea zinazoweza kuchukuliwa na upande ulioathirika kutokana na maamuzi ya kusitishwa kwa mkataba huo.

“Definitely (hakika) aliyeathirika atajitetea aidha, kwa kwenda mahakamani au vinginevyo… kila mkataba una vipengele vya kuuvunja na kujitetea,” alisema Karamagi katika mahojiano yake na Tanzania Daima.

Alisema pia kuwa awali TANESCO ilichelea kuvunja mkataba wake na Richmond ambao ndio walioiuzia mkataba wake Dowans Oktoba 23, mwaka jana kutokana na hofu ya kuchukuliwa kwa hatua za kisheria dhidi yao.

“TANESCO wenyewe waliona kuwa iwapo wangekatisha mkataba wakati ule, Richmond wangetumia vipengele kuzuia uletwaji wa majenereta mengine, hivyo nchi ingeendelea kuteseka,” alisema.

Wakati Karamagi akitoa tahadhari hiyo, wabunge wengine waliohojiwa na Tanzania Daima, walisema kuwa hatua hiyo ya serikali imechelewa sana, hasa ikizingatia kuwa, nchi imelipa fedha nyingi wakati hakukuwa na mkataba halali wa kuifanya ilipe fedha hizo.

“Mnataka niseme nini kuhusu hili? Maoni yangu yako open (wazi). Sisi ndio tuliishauri serikali kuwa hili ni kosa na tukatoa mapendekezo,” alisema Mbunge wa Mkanyageni, Habib Mnyaa (CUF), ambaye alikuwa mmoja wa wajumbe wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mchakato ulioipatia ushindi Kampuni ya Richmond katika kandarasi ya kufua umeme wa dharura.

Hata hivyo, katika mkutano wake na waandishi wa habari juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dk. Idris Rashid, alisema uamuzi wa shirika lake kuvunja mkataba huo, hauna uhusiano na mapendekezo yaliyotolewa na Kamati Teule ya Bunge chini ya Dk. Harrison Mwakyembe, iliyochunguza utata wa zabuni ya Richmond, iliyosababisha mbali ya Karamagi, Waziri Mkuu wakati ule Edward Lowassa na Dk. Ibrahim Msabaha (Nishati na Madini), kujiuzulu nafasi zao.

Kwa upande wake, Mnyaa alisema ripoti ya kamati yao waliyoisoma Februari mwaka huu, ilithibitisha pasipo shaka kwamba, serikali ilikuwa na uwezo wa kuagiza majenereta yaliyoletwa na Richmond kwa nusu ya bei ambayo iliyakodisha.

“Unapeleka maombi yako tu, unayapata majenereta yao mwenyewe, si ya kukodi, hakuna capacity charge,” alisema Mnyaa.

Alipotakiwa kueleza iwapo hatua ya serikali haiwezi kuwa na madhara, alisema hilo linategemea na vipengele vya mkataba, lakini kwa vyovyote vile, katika suala hilo, serikali ina haki.

Hatua hiyo ya serikali ilipongezwa pia na Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini ya Bunge, William Shellukindo ambaye wakati uchunguzi wa utata katika mkataba wa Richmond ukianza mwishoni mwa mwaka jana, alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Biashara na Uwezeshaji, ambayo ndiyo iliyopendekeza kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge.

“Tuliieleza serikali waziwazi kuwa mkataba ni mbovu…tunafurahi kwa sababu sasa serikali inakubaliana na sisi,” alisema Shellukindo.

Shellukindo ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli (CCM), alikwenda mbali zaidi kuwazungumzia watu ambao wamekuwa wakilalamika kuwa walionewa na Kamati Teule ya Bunge, na kubainisha kuwa katika suala la uchunguzi dhidi ya Richmond, hakuna mtu aliyekuwa anafuatwa binafsi.

“Hakuna visa wala kusingiziana, hatukumuonea mtu… mwenye malalamiko afahamu kuwa sasa hivi hatuzungumzii Richmond tena, imemalizika.

“Anayetaka (kuijadili) ajenge hoja ya kulihoji Bunge kwa sababu ripoti ile sasa si ya Mwakyembe, ni maamuzi ya Bunge zima. Hatuna haja ya kupoteza muda kuijadili tena Richmond,” alisema Shellukindo.

Hata hivyo, kwa upande wake, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM) ambaye jina lake lilitajwa mara kadhaa katika ripoti ya Mwakyembe, alipohojiwa kuhusu suala hilo, hakuwa tayari kusema lolote zaidi ya kueleza kusikitishwa kwake na namna mjadala wa Richmond unavyoendelea kinyemela bungeni.

‘‘Mimi ninachoweza kusema ni kwamba, nashangazwa na hatua ya Spika kumruhusu Mwakyembe aendeleze mjadala wa Richmond bungeni hivi sasa, wakati mimi nilinyimwa fursa ya kuzungumzia suala hilo Aprili. Kwa hakika haya yanayotokea bungeni hivi sasa ni sawa na mchezo wa Ze Comedy,” alisema Rostam, huku akikataa kueleza lolote zaidi.

Kwa upande wake, Dk Mwakyembe, alipofuatwa ili kutoa maoni yake kuhusu suala hilo, ikiwa ni pamoja na hatua ya serikali kusitisha mkataba wa Dowans, alikataa kusema lolote.

Naye Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP) alisema anaamini kuwa hapakuwahi kuwapo kwa mkataba halali ilhali taifa likiwa limeingia hasara kubwa kutokana na kuendelea kufanya kazi na Dowans.

“Hakuna walichovunja na tayari tumeshaingia hasara kubwa, serikali iseme itawafanya nini walioingia mkataba huo usiokuwepo,” alisema Cheyo na kubainisha kuwa hatua zilizochukuliwa ni kielelezo kuwa serikali imechukizwa, kama walivyokuwa wamechukizwa wananchi.

Kwa upande wake, akilitolea ufafanuzi suala hilo, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema hatua dhidi ya watu walioingia mkataba huo zipo chini ya dhamana ya Waziri Mkuu, ambaye ndiye aliyeahidi kushughulikia mapendekezo ya Bunge yaliyotokana na kamati teule.

Hata hivyo, Ngeleja alisema kwa upande wao, hiyo ni hatua ya kwanza, na hivi sasa wanatafakari hatua nyingine ya kuchukua kuhusu masuala kadhaa, ikiwamo ukweli kuwa Dowans ilizalisha umeme ambao ulitumiwa na nchi.

“Tutakaa na pande zote, TANESCO na Dowans kuzungumza, lakini baada ya tarehe ya kusitisha mkataba hakuna malipo yatakayofanyika,” alisema Ngeleja. Chini ya mkataba huo, TANESCO ilikuwa ikilipa sh milioni 152 kwa siku kama Capacity Charge.

Akizungumzia msingi wa kusitishwa kwa mkataba huo, Ngeleja alisema baada ya uchunguzi wa kina, serikali imejiridhisha kuwa hakukuwa na kampuni iliyosajiliwa kwa jina la Richmond Development Company LLC, ambayo ndiyo iliyoingia mkataba na serikali.

“Kwa maana hiyo, kwa kuwa hakukuwa na kampuni hiyo, hata mkataba haukupaswa kuwepo kwa sababu hakuna mtu wa kuingia mkataba huo,” alisema.
 
Mgawanyiko lazima uwepo...Kwani kama kawaida kuna CONFLICT OF INTERESTS!

Kama hao wabunge baadhi yao wana share za hayo makampuni yanayolipwa jasho la myonge kila siku basi damu iko mikononi mwao!

Wasijitetee kuwa TAIFA LINGEINGIA GIZANI NA WAKATI LILISHAINGIA GIZANI NA HUKU PESA WAKILIPWA MAFISADI NA MKOLONI WALIYESHIRIKIANA NAYE!

WANANCHI WAWAUNGE WABUNGE WAZALENDO MKONO NA KINA KARAMAGI WALITAKIWA JELA SASA HIVI LAKINI KIKWETE ANAWAACHA NJE ILI WAWAUWE WAZALENDO...EITHER PHISICALLY OR PROPAGANDAWISE!

PROPAGANDAWISE NA WAHAKIKISHIA HAWATASHINDA HAPA JF LABDA SIJUWI WAFANYE NINI!

NA PHYISICALY NIMEMWACHIA MUNGU KWANI NILISHAJITOA MUHANGA!

NA HILO WANALIJUWA KUWA HAKUNA PROPAGANDA ITAKAYORUHUSIWA NA JMUSHI NA WAZALENDO WENGINE HAPA JF!
 
Wakuu,

Hii seketa naona bado ipo tu na sijui kama Pinda atafanye kweli ama anatuzengua.It will be a site to behold unless the recommendations are a 'sliding door screen'


Richmond: Vigogo wahaha upyaa...!

2008-08-15 17:00:45
Na Mwandishi Wetu, Jijini

Kuna habari kuwa baadhi ya vigogo waliotajwa kuhusika katika kuingiwa kwa mkataba tata baina ya Serikali kupitia TANESCO na Kampuni ya Kuzalisha umeme ya Richmond wameanza kuhaha upya baada ya kutolewa taarifa kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda yuko tayari kuanika hatua kadhaa ambazo Serikali imeamua kuzichukua dhidi ya wote waliohusika.

Taarifa ambazo Alasiri imezipata kutoka kwa chanzo kimoja kilicho karibu na vigogo hao, zinasema hofu iliyopo sasa ni kubwa na kwamba wanahaha katika kuhakikisha kuwa wanajua kile kilichokubaliwa na Serikali kuwa kitekelezwe, kati ya mapendekezo 23 yaliyoainishwa na Kamati ya Bunge iliyoibua kwa umahiri mkubwa uozo wote wa mkataba huo, huku ikiongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe.

Kama kuna wakati mgumu zaidi kwa hawa vigogo waliotajwa ni huu... mmoja aliye bosi wangu amekuwa na hofu kubwa kwa sababu hajajua ni uamuzi upi hasa ambao Serikali imekubali kuutekeleza. Anahofia kuwa hatua yoyote dhidi yake inaweza kummaliza, kikasema chanzo chetu hicho.

Hivi akribuni, katika moja ya maelezo yake bungeni, Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye ndiye anayesubiriwa kulieleza Bunge juu ya hatua zilizochukuliwa na Serikiali katika kutekeleza mapendekezo ya Kamati ya Mwakyembe, alisema yeye yuko tayari kutangaza yale yaliyoafikiwa na Serikali wakati wowote ule.

...ninachosubiri sasa ni kupangiwa ratiba na Spika, alisema Mhe. Pinda, wakati akitoa maelezo hayo.

Hata hivyo, sasa zimebaki siku 14 tu kabla ya kuahirishwa kwa Mkutano wa sasa wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano, hivyo hatma ya vigogo hao kuendelea kuwa mikononi mwa Spika Sitta ambaye anasubiriwa kumpangia wasaa muafaka Mheshimiwa Waziri Mkuu ili naye aanike kile ambacho Serikali imeamua kukitekeleza.

Wakati wa kuwasilishwa kwa mapendekezo ya Kamati ya Bunge iliyochunguza Mkataba wa Richmond, Mwenyekiti wa Kamti hiyo Dk. Mwakyembe, alitaja mapendekezo 23, baadhi yake ikiwa ni pamoja na kuondolewa katika nafasi zao baadhi ya watendaji wa Serikali, mapendekezo ambayo yalioungwa mkono na wabunge wote.
 
Last edited by a moderator:
Tumechoka na porojo za viongozi wa serikali ya CCM kila siku hadithi za Pwagu na Pwaguzi. Siye huyu Pinda aliyeahidi kuja na jibu la Mchakato wa kuwawekea wawekezaji wa Canada kinga kwenye kuliibia taifa.

Tutaanza kumuita waziri mkuu wa alinacha.
 
Tumechoka na porojo za viongozi wa serikali ya CCM kila siku hadithi za Pwagu na Pwaguzi. Siye huyu Pinda aliyeahidi kuja na jibu la Mchakato wa kuwawekea wawekezaji wa Canada kinga kwenye kuliibia taifa.

Tutaanza kumuita waziri mkuu wa alinacha.

Nd'o maana niliuliza kama Pinda atafanya kweli ama ni yale ya "ntilie mchuzi
pangu pakavu".

Afu pia CCM needs to delink itself from the Govt.Iko tofauti kubwa uwajibikaji
wa viongozi kwa sababu za serikali au kwa sababu za kichama
 
Tehe tehe wanataka kuja na gelesha kwa ajili ya 2010. Kufukuzwa nyadhifa kitu gani wakati taifa limepata hasara na wao cha juu wamekula.

Tunataka kuona kweli watu ngoma inawatokea puani mpaka wengine wakikumbuka waogope sio kufukuzwa ,kama mtu anaona avuna bilioni katika mchakato fulani na akigundulika ni kwamba anafukuzwa tu hakuna atakaye ogopa kuiba au kufanya deal lolote.
 
Nd'o maana niliuliza kama Pinda atafanya kweli ama ni yale ya "ntilie mchuzi
pangu pakavu".

Afu pia CCM needs to delink itself from the Govt.Iko tofauti kubwa uwajibikaji
wa viongozi kwa sababu za serikali au kwa sababu za kichama

Mkuu, this is a very important point! Yaani mwenyekiti wa chama kuwa Rais kwa mfano ni tatizo kubwa sana. Na ukweli ni kwamba, hata chama chenyewe kinaumia. Lakini Sisiem wanafikiri kuwa it's only to their advantage. The separation of party from government has to happen kwa sababu serikali inawajibika tofauti na chama, kwani serikali inawajibika kwa wananchi wote bila kujali itikadi, while chama inawajibika kwa wanachama wake.

But even if structure haitabadilika lakini mawazo yabadilike basi. Chama kiwe tayari kujikosoa na kuwakosoa viongozi wake. Angalia jinsi Labour party kule UK ilivyopanga kumtimua Gordon Brown maana wanaona anaiangusha chama, sasa utaona wapi kitu kama hicho Bongo?
 
MKuu, this is a very important point! Yaani mwenyekiti wa chama kuwa Rais kwa mfano ni tatizo kubwa sana. Na ukweli ni kwamba, hata chama chenyewe kinaumia. Lakini Sisiem wanafikiri kuwa it's only to their advantage. The separation of party from government has to happen kwa sababu serikali inawajibika tofauti na chama, kwani serikali inawajibika kwa wananchi wote bila kujali itikadi, while chama inawajibika kwa wanachama wake.
But even if structure haitabadilika lakini mawazo yabadilike basi. Chama kiwe tayari kujikosoa na kuwakosoa viongozi wake. Angalia jinsi Labour party kule UK ilivyopanga kumtimua Gordon Brown maana wanaona anaiangusha chama, sasa utaona wapi kitu kama hicho Bongo?

Susuviri,

Very true that point raised.

Nd'o yaliokuwepo Kenya enzi za KANU na Moi ambapo jamaa waliendelea
na sera kama Sisiem not knowing that as time went by it became detrimental for the party.Ukitazama leo, KANU imekufa kabisa na imebaki chama cha Uhuru Kenyatta na wendawazimu wachache wanaoamini KANU itarudi back to power. Kwa hivyo CCM mwelekeo ni huo huo na sijui tuwashtue wanakiharibu
chama ama tuwaache wazame wenywe?..tatizo ni kua katika huu uzamaji
wataiburuza nchi na kutitumbukiza majini.

Simple question:Mbona hadi leo hatujaona mtu hata mmoja akipelekwa
mahakamani kujibu mashtaka ya ufisadi? Tuonacho ni tume baada ya tume na
kamati baada ya kamati.Baadhi ya kamati zinachunguza kamati.Ushawahi kumuona
mbwa akifukuza mkia wake?..nd'o haya basi!

Shukran.
 
Mimi naona hausiki otherwise asingemtosa Edward Lowassa na angezima taarifa ile ya Bunge. Hapa aasingiziwa tu.
 
The way I konw, there is something bigger than we see! Serikali kushindwa kabisa hata kulinyoshea kidole suala kubwa namna hii Maana hata kujiuzuru kwa EL serikali ina iita ni ajali ya kisiasa! Hii inamaanisha kuwa "hatukudhani yangefika huku". Kwa hiyo kunamaslahi ya watu yanalindwa hapa! We not know now, Lakini ipo siku tukuja kujua
 
Mimi naona hausiki otherwise asingmtosa Edward lowasa na angezima taarifa ile ya Bunge. hapa aasingiziwa tu.

Isingekuwa rahisi hivyo kuzima taarifa ya Bunge, EL alijihudhuru kukwepa aibu ya mkulu - hii ngoma na ile ya Kagoda zina ukweli ndani yake - kuna mkono wa jamaa.
 

Attachments

Tatizo kubwa la watanzania miaka ya hivi karibuni ni kuendekeza 'conspiracy theory' na kuacha mantiki.
mtu hafi bali anakolimbwa etc etc. Suala la richmond wote tumesoma na ripoti za waheshimiwa pia. Kosa kubwa ni kutokuwa makini kwa kamati teule iliyoshughulikia suala hilo na PM ilibidi awajibike kama mtendaji mkuu wa serikali.
 
JK lazima anahusika kwenye hili dili. Siku anaongea na wananchi kwenye simu wakimhoji maswali kuhusu richmond akasema namunukuu.

Nadhani hatua zaidi zinahitaji kuchukuliwa kuhusu hili la Richmond. Sasa hiyo imegonga mwamba bungeni mara mbili mpaka wabunge wakanyosha mikono. Wahusika wengine wamekwisha staafu. Sasa hizo hatua zingine zitachukuliwa lini? Na akichukuliwa hatua swahiba wake Lowassa atamweka wapi? Ukaribu aliokuwa nao na Lowassa lazima alimhusisha kwenye hilo kabla ya kutendeka. Nafikiri wana JamiiForums tungetumia hilo kumng'oa huyo msanii wetu kamanda wa mdomoni. Kama kuna anayebishi kuwa si kamanda amtaje mwingine anayemzidi kwa hilo.

Thanks Members.
 
Wana JF... Mjadala huu ulishafungwa na Mhimili wa pili wa Nchi ambao ni Bunge na kwamba kazi za kuwafikisha matuhumiwa mahakamani watakaothibitika na kushiriki kwa ushahidi usio na mashaka tunategemea sheria itachukua mkondo wake. Sidhani kama ni tija kuendelea kujadili suala ambalo mjadala wake umeshafungwa na vyombo husika. Kilichobaki ni kuendelea kuhoji na kufuatilia utekelezaji wa maazimio ya Bunge na mengine yaliyojiri baada ya kufungwa kwa mjadala.

Ikumbukwe kwamba mjadala huu ulikuwa ni mkali, moto na nyeti na wakati mwingine ulitishia mgawanyiko katika nchi.. Kila upande ukiwas na sababu za kuhiji na mwingine kujitetea na bado mambo mengi yamebaki kizani na maswali mengi yanaendelea kuulizwa. Siri nyingi hufichuka kadri muda unavyokwenda na majeraha hugeuka makovu na vidonda vingine haviponi kabisa. Ukomavu wetu wa kisiasa unapaswa kuangalia mambo yajay yenye kuleta maendeleo. Inawezekana nchi imepoteza mchezo kwenye sakata hili..lakini watawala na viongozi wetu wamejifunza mambo fulani mengi
 
Sijakupata, rudia tena. unataka kusema nn?
Nani asijadili? sisi au wao?
 
Back
Top Bottom