Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

hata mimi kwa jinsi ndogo niliyomfahamia[not in person]enzi za kamanzima,alivyopewa nafasi nikasema...mkata kuni kapewa shoka jipya...kazi itaboreshwa. lahaula la kwata.....sasa ndio haya.....we acha tu!

hebu kwanza,labda wameshamloga![sio kwa kwenda bagamoyo] maanake kwa stahili hizi mawazo ya kiswahili ndio hushamiri vichwani mwetu!....hivi mungu kaenda likizo nini,kwenye suala hili?


Niliwahi kusema humu kuwa pamoja na makelele yangu humu JF hata mimi leo nikipewa post ya juu na sisiem govt ninaweza kabisa nikawa kitu cha tofauti overnight; hali halisi inalazimu watu wema wapenda nchi wanapopewa nafasi kuwa kama wale aliowakuta. Na pengine wanapopewa hizo post kunakuwa na orientation session fulani ambayo inawamwagia sumu/uchawi.
Huyu Hosea atakuwa alipewa kazi ya kufanya uchunguzi lakini na majibu akawa kashapewa tayari; so the whole exercise was an academic one, to fool those of you who make a lot of noise about richmonduli; sidhani kama Hosea ana guts za kusimama dhidi ya wahusika yeye peke yake, ni dhahiri richmond deal nayo ni kamtandao, kangeweza kumkaba kama ile cobweb fulani iliyowahi kuonyeshwa hapa...yeye naye anapenda kula na kuishi jamani.
Ni wakati muafaka wa kufikiria njia mbadala ya kupambana na maovu TZ
 
Kuna kitu kimoja naweza sema ni Mimi tu siku ya kujaliwa kushika moja ya hizo nafasi,sheria inakuwa sheria na si vinginevyo.Waendelee kuomba hivyo hivyo nisipate wakati na mimi ninaendelea kuomba hivyo hivyo nipate Huku nikiongeza jitihada ya kutafuta.
 
Hivi PCB walipata nafasi ya kumhoji mtoto wa mmoja wa "waliohusika kuunda kamati ya dharura" ambaye ndiye aliyetumia jina la babake kuunganisha mkataba huu? au wanadhani watz hatujui? Jamani wanataka tuwafanyie kazi zote...
 
Kuna neno Mtandao linatumika kwenye Serikali na CCM na nguvu ya mtandao ni kubwa . Hosea he knew kwamba by fighting Sumaye siku zile alikuwa anajiandaa kuwa Mkurugenzi na yeye anajenga Mtandao kikamilifu .Sasa mnategemeas nini ?
 
Najua nini kitafuatia baada ya sakata hili la nishati kati ya Richmond Development Company, Tanesco na Serikali:

a. Serikali/Tanesco itavunja mkataba na RDC
b. Serikali itasema haikuridhishwa na utendaji wa kampuni hiyo.
c. Serikali inafanya juhudi zaidi na makampuni mengine kusaidia kuondoa adha ya kukosa umeme.
d. Waliohusika na mkataba wa RDC na Tanesco, na Wizara wataendelea kutembea vifua mbele bila hatua za kinidhamu dhidi yao kuchukuliwa.
e. Watanzania watapiga makofi, na kumpongeza Kikwete kwa "Kazi nzuri"
f. Watanzania watasahau ya mkataba huu, hadi mwingine utokee tena, na gurudumu la upotovu litaendelea kubingirika!!

Ila kabla ya hayo kutokea sikiliza ukweli kuhusu kampuni hii ni nini?

http://mwanakijiji.podomatic.com

Inasikitisha kuwa mtu wa kijijini kuweza kutabiri kitu dhahiri kama hiki
 
jamboonormal_JK%2BBWM%2BRUKSA.jpg


Kikwete. 'Basi nikamuuliza yule mzungu teni pasenti yangu vipi?
Akanijibu eti mbona Mwinyi na Mkapa walikuwa wanachukua faivu tu?'
Mkapa.'Huyo alikuwa anataka kukuingiza mjini. Anatoa teni na siyo faivu.'
Mwinyi. 'Nini teni? Mimi nilikuwa nawabandua na twenti'
Wote. 'Hahahaha hahahahah ahahahahahahah'

Na huu ni utani ama inaelekeana na ukweli?
Wasanii hao! au mwaonaje?
 
Suala la Richmond lina nafasi ya pekee kwangu. Mwisho wa juma hili lote nimekuwa nikihangaika kufuatilia kampuni hii na kuzungumza na maafisa mbali bali wa jimbo la Texas na wale wa jiji la Houston. Na nilibahatika kutembelea eneo husika kuangalia hii "Richmond Development Company". Niliyoyagundua nikiunganisha na uchunguzi wangu wa mwaka jana yanatisha na ndiyo msingi wa "maswali 10 au zaidi" kwa bwana Hosea na serikali yetu kuhusu suala hili.

Waliodhania kuwa majibu ya "hakuna rushwa" yametufumba macho, wamechelewa...Tuko macho leo hii kuliko huko nyuma. Usikose makala yangu na matangazo yangu KLH News International siku ya Jumatano!!

Kwa ajili ya Nchi,
Na Kwa ajili ya uzao wetu!!

M. M.
 
mzee nyani, mtabiri siyo mtu yule anayefikiri kuwa kitu fulani kitatokea bali yule anayesema kitu fulani kitatokea! Hata hivyo nakubaliana na wewe kuwa "inawezekanaje kutabiri kilicho dhahiri" - how can one predict the obvious..!? the answer is simple.. only with unmatched precision!! Ila don't miss my piece on Wednesday... I'm rising the standard of Tanzanian journalisim... just a notch higher!! hata TD wanaweza wasichapishe....
 
CHADEMA pins down Lowassa on Richmond deal

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

THE opposition party Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) has formally castigated what it describes as the Prevention of Corruption Bureau (PCB)’s poor handling of the Richmond power deal investigation, going so far as to allege Prime Minister Edward Lowassa’s personal involvement in the matter.

In a strongly-worded letter addressed to PCB, CHADEMA questions why a task force appointed by the PM had picked Richmond Development Company as the eventual winner of the power generation contract in complete disregard of the Tanzania Electric Supply Company (TANESCO)’s stated rejection of the US-based company.

The opposition party criticized PCB over its decision to rule out corruption in the whole deal, insisting that the government�s anti-corruption watchdog comes clean on the matter.

The CHADEMA letter is in reaction to a declaration by PCB director general Edward Hosea that ’’there is no evidence to support the allegations of corruption, criminal negligence or payment of secret commissions to government officials in the Richmond deal.’’

The opposition party demands a more detailed explanation from PCB over the statement, which it asserts has not only discredited the anti-corruption watchdog, but also frustrated the campaign against graft.

’’PCB should remain with its noble duty of preventing corruption, rather than turning into an institute of protecting, defending and clearing suspects of corruption charges,’’ says the letter signed by CHADEMA’s acting secretary general John Mnyika.

It queries the rationale behind the decision to award the multi-billion shilling power deal to the ’incompetent’ Richmond, ignoring TANESCO’s proposal for competitive international tendering.

The party faults Hosea’s claim that the Richmond deal occasioned no loss to the government, noting that: ’’Tanzanians went without emergency power for many months�and the president has since admitted that the power blackout lowered the country�s economic growth.’’

According to local economic analysts, last year’s extended nationwide blackout - caused principally by prolonged drought - was the cause of fast-rising inflation and depreciation of the local currency.

The CHADEMA letter called on PCB to make a copy of the full investigative report over the Richmond deal available for public perusal.

It furthermore pressed the anti-corruption watchdog chief to clarify on reports quoting him as saying investigations over corruption charges against members of the parliamentary rights, ethics and privileges committee ceased after the Speaker of the National Assembly closed debate over the issue.

’’To call off an investigation on corruption allegations simply because one leader has declared the debate over the issue closed� it only goes to show how vulnerable to outside influence the bureau is,’’ Mnyika said in the letter also copied to the president, the speaker and the media.

The letter insisted that any infringement of PCB’s independence and autonomy was not healthy for effective anti-corruption campaigning. It noted that PCB did not stop investigating the Richmond deal ’’when the prime minister told Tanzanians to stop discussing the company because the rains have come and power was being supplied.’’

CHADEMA also dug into PCB for its paid-up advertisements in local media early this year, in which it dismissed as unfounded claims by CHADEMA national chairman Freeman Mbowe to the effect that President Kikwete was in possession of a list of corrupt leaders.

’’Unfortunately, just a few weeks after these adverts, the president himself publicly stated that he indeed had such a list. PCB has not tried to refute that statement, or admitted that it previously erred in its denunciation,’’ the letter noted.

It said PCB’s stance meant that nothing substantive was likely to be done against those named in the list.

’’Corruption is a criminal offence�to give corruption suspects too much leeway or decide not to investigate cases of corruption, is tantamount to protecting the criminals. Which in itself is also against the law,’’ the letter charged.
 
Kama nilivyowaahidi nina maswali 10 au zaidi ambayo kama Hosea atayajibu mjadala huu wa Richmond utafikia kilele!!
 
huyu jamaa wa PCb anachojaribu kutueleza watanzania ni kuwa baada ya enzi za kaka Ben, Unyang'au bado utaendelea kuwa sera isiyo rasmi katika jamii yetu. Inaelekea bado hatujafanikiwa kupita ile stage ya crude means of accumulation of capital kujenga tabaka la vibepari uchwara vitakavyoweza kumiliki kasehemu ka uchumi ketu. Unajua tena mambo ya economy growth, wealth making, uwezeshaji, na vimbwanga vingine......

Kazi kwelikweli...

Tanzanianjema
 
Wiki moja iliyopita, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa (TAKURU) Bw. Edward Hosea alitoa maamuzi kuhusu mkataba wa Richmond ambao serikali ya Rais Kikwete iliungia mwaka jana katika jitihada za kutafuta ahueni ya tatizo la nishati lililoikabili nchi yetu. Mkataba huu ulipoingiwa maswali mengi yaliulizwa na shutuma nyingi zilitolewa na mojawapo ya shutuma hizo ni kuwa kuna rushwa ilitumika. Bw. Hosea katika maelezo yake kwa vyombo vya habari alihitimisha mjadala huo kwa kusema kuwa "katika mchakato mzima hakukuwa na rushwa".

Hata hivyo maswali ya msingi ambayo tuliyouliza huko nyuma bado yapo na majibu yake bado yanatakiwa. Nimeandaa maswali kumi yamsingi ambayo Bw. Hosea na timu yake bado wanastahili kuyajibu kwa uwazi na ushahidi wa wazi (siyo maneno matupu).

sikiliza maswali hayo 10 ambayo PCM imekwepa kuyaangalia na kuyatolea majibu. http://www.mwanakijiji.podomatic.com
 
Wajemeni hebu someni makala hii, source ni Tanzania Daima, 16.5.07
M. M. Mwanakijiji



TULIPOKUWA watoto wadogo, wakubwa zetu walikuwa wakitumia mbinu mbalimbali kutuhadaa.

Kitu ambacho hatukujua ni kuwa, tulikuwa tunadhulumiwa kitu fulani kwa kutumia ulaghai wa maneno matamu, na vichekesho visivyo na kichwa wala miguu.

Mojawapo ya janja ya wakubwa hao, ni ile ya kupukuchua mahindi. Katika ulaghai huu, kaka mkubwa au dada mkubwa alikuwa anachukua hindi lililochomwa, ambalo mdogo wake ameshikilia, na anamuahidi "kumtengenezea njia".

Basi, katika kufanya hivyo, atapuchukua mistari michache na kutengeneza njia ya kwenda "Dodoma" na hata ya kwenda "Iringa".

Zile punje za mahindi walizopukuchua, hata hivyo walizibugia mdomoni kwa mbwembwe zote.

Sisi wadogo zao tulifurahia kukabidhiwa mahindi yaliyotengenezwa njia kadhaa!

Ndugu zangu, kile ambacho Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa nchini (Takuru), Edward Hoseah, alichokifanya wiki iliyopita, kinafanana kabisa na hadaa ya kupukuchua mahindi.

Na alichofanya kamanda huyo kinazidi mazingaombwe ya Profesa Ndumba Nangae!

Niwakumbushe kidogo kuhusu mazingaombwe. Katika mazingaombwe yoyote, mwanamazingaombwe mahiri ni yule anayeweza kutumia "vipoteza lengo" ili kuficha vitu kwenye vidole au viganja vyake na hatimaye kufanya viini macho.

Hoseah na wenzake wametumia suala la waheshimiwa Zitto Kabwe na Amina Chifupa kutuletea taarifa muhimu na nyeti, wakijua kwa hakika Watanzania hawana muda wa kufuatilia na kuulizia kwa makini, kwani wamenogewa na utamu wa kachumbari ya masuala ya mapenzi bungeni!

Hata hivyo, kwa mzee wenu hapa kijijini, hakuna jambo ambalo linahusu Tanzania litakaloachwa kupita bila kuangaliwa kwa karibu, kama kupekua kwa kurunzi chini ya uvungu.

Tulilizungumzia suala la Richmond tangu mwanzo wake na tukaweka wazi kuwa hicho kikampuni hakikuwa na uwezo wala ubavu wa kuleta majenereta na kuzalisha umeme!

Tukazua maswali ambayo maelezo ya Hoseah hayakujaribu hata kidogo kujibu.

Ni makusudio yangu kuyazua tena maswali haya ili kila Mtanzania aweze kuelewa ni jinsi gani Hoseah na wenzake wamejaribu ‘kutufunga kamba mbichi mchana kweupe'.

Lengo langu ni kuonyesha kuwa, Takuru ni chombo ambacho hakina ubavu wa kupambana na rushwa kubwa, na hakina uhuru wa kukabiliana na vigogo (na familia zao) katika vita za kutokomeza uovu huu.

Miaka nenda rudi, Takuru imekuwa ikikamata na kuwakaanga dagaa, ikiwachemsha kambare, wakati papa na nyangumi wakiendelea kuogelea bila hofu ya kukamatwa na nyavu hizo za Takuru.

Takuru imebakia kuwa kama simba wa kwenye picha, ambaye ametoa kucha na anaonekana kuunguruma huku meno yake yaliyochongoka yamekenuliwa!

Wote tunajua simba huyo wa karatasi haumi ila anaweza kuwatisha watoto wadogo tu na watu wasio na akili timamu.

Kwa vile Takuru wamesema kuwa kwenye suala la mkataba wa Richmond hakukuwa na vitendo vyovyote vya rushwa, tunaomba basi Hoseah na wenzake wawajibu Watanzania wenzao maswali haya yafuatayo ambayo yamejengengeka tangu mkataba huu kuingiwa.

Kama ushahidi wa majibu yake anao, wauweke hadharani au iundwe tume huru yenye uwezo wa kuita mashahidi na wale wote waliohusika waweze kuitwa hadharani na kuhojiwa kuhusu kuhusika kwao.

Maswali haya yana lengo la kutaka serikali iwe wazi na kutoa hadharani vidhibiti vyote ambavyo vimewafanya wafikie mahali pa kusema katika "mchakato mzima, hakuna rushwa"! Hosea, ya kweli hayo?

Kwanza, ilikuwaje kampuni hiyo ya Richmond Development (RDC) ipewe tenda hii? Majibu aliyoyatoa Hoseah ni ya kitoto na ya shule ya msingi.

Iweje kampuni ya kupiga chapa na kuchapisha vijitabu na vielelezo ipewe tenda ya nishati?

Tangu mwanzo wa suala hili, kampuni hii imejivika majina ya ajabu ajabu na kutangaza uwezo wake.

Kinachoshangaza ni kuwa, hakuna mtu katika serikali yetu aliyethubutu kuangalia kama kampuni hii ya RDC ina rekodi yoyote ya kushughulika na masuala ya nishati, ukiondoa maelezo ya kwenye tovuti yao.

Je, watendaji wetu walipitia ushahidi gani wa kazi za RDC na kuridhishwa nayo, hadi kuamua kuwapa tenda ya mabilioni ya shilingi?

Katika kuwapatia tenda hiyo, sheria ya manunuzi ya serikali ilizingatiwa kwa kiasi gani?

Pili, wakati Balozi Andrew Daraja alipokwenda kutembelea Houston na kukaribishwa na viongozi wa Kampuni ya Richmond Printing, alionyeshwa kitu gani hadi kukubali kuwa, kampuni hiyo ina uwezo wa kushughulikia
masuala ya nishati?

Je, aliona orodha gani ya nchi zilizoridhishwa na utendaji kazi wa RDC hadi kuipigia debe serikalini?

Kama si yeye, ni nani basi aliyesema kampuni hiyo ina uwezo wa kutuletea majenereta?

Tatu, kabla ya Kampuni Richmond kupewa tenda ya nishati, ilipewa tenda nyingine ya kujenga bomba la mafuta toka Mwanza hadi Dar es Salaam, bomba ambalo mradi wake ulibuniwa na Kampuni ya Africommerce.

RDC ilipopewa tenda hiyo kiulaini, watu wa Africommerce walilalamika kupokonywa mradi huo, lakini viongozi wetu hawakujali hilo.

Miezi kumi na nane baadaye, RDC walishindwa kufanya lolote na badala yake mradi huo ukapewa kampuni nyingine toka Uarabuni.

Ilikuwaje kwa kampuni iliyoshindwa kuanza kutekeleza mkataba wa bomba la mafuta kwa miezi 18 kupewa mradi wa kuleta majenereta ndani ya wiki
14?

Jambo moja ni dhahiri. Mtu yule yule aliyeipigia debe kampuni hii hadi ikapewa mradi wa bomba la mafuta, ndiye yule yule aliyeipigia debe na ikapewa mradi wa majenereta.

Hoseah yuko tayari kuwaambia na kuwathibitishia Watanzaina wenzake kuwa, watu wale wale waliohusika na bomba la mafuta sio waliohusika na mradi wa majenereta?

Nne, Kutokana na rekodi zilizoko kwenye ofisi ya Tarafa ya Harris (Harris County) kwenye Jimbo la Texas, nchini Marekani, Kampuni ya RDC imeorodheshwa kuanzia mwaka 2003, ikiwa ni sehemu ya kampuni mama ya Richmond Printing.

Cha kushangaza ni kuwa, chini ya mwaka mmoja baadaye, kampuni hiyo ikapewa tenda ya bomba la mafuta nililotaja kwenye swali la tatu, na hivyo kina Elisante Muro kunyang'anywa mradi wao.

Je, Hoseah na wakubwa wa Wizara ya Nishati na Madini wanaweza kuwaeleza Watanzania ilikuwaje kampuni changa namna hiyo kupewa mradi mkubwa wa nishati wakati haina historia ya biashara ya sekta husika?

Je, tukiwaambia kuwa hiyo ndiyo sababu ya mabenki ya Marekani kuikatalia mkopo wa fedha za awali kampuni hiyo kwa vile hawana historia ya mikopo kama kampuni ya nishati, kina Hoseah watakataa?

Kama Wamarekani wameona kuwa kampuni hiyo haina uwezo wa kustahili mkopo mkubwa wa fedha kiasi hicho, ilikuwaje wasomi wetu na maafisa waliotajwa na Hoseah wakakubali kuipa tenda?

Ni nani huyo aliyeipigia debe kampuni hiyo na mtu huyo ana maslahi gani?

Tano, wakati Rais Kikwete anazungumza na wananchi mapema mwaka huu, alielezea kusita kwake kukubali kampuni hiyo kupewa malipo ya aina yoyote na akawahakikishia wananchi kuwa RDC haikulipwa kwani alikuwa na shaka nayo.

Je, Takuru walimhoji Rais Kikwete awaeleze kwanini alisita na ni nani aliyemshawishi hadi akaacha mkataba huo kuendelea?

Tukiwaambia kuwa yule aliyeipigia debe kampuni hii kwa Rais Kikwete na yule aliyehakikisha kampuni changa namna hii ilipewa tenda kuwa aidha ni mtu mmoja au wana udugu wa damu, Hoseah anaweza kutuonyesha kinyume chake?

Sita, inawezekana ni kweli kuwa hakukuwa na rushwa iliyolipwa moja kwa moja na ikapewa jina "rushwa" kwenye mchakato wa mkataba wa RDC?

Hata hivyo, hatuna budi kumuuliza Hoseah kama alianza kuangalia mchakato huu kabla ya mkataba kuingiwa na umbali gani wa historia ya nyuma alienda.

Sijui kama Hoseah anafahamu uhusiano wa karibu wa Dk. Ibrahim Msabaha (aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati huo) na familia ya kina Gire uliodumu kwa miaka kadhaa sasa (kabla ya mikataba hii).

Inapotokea kuwa rafiki wa familia anapewa mikataba miwili inayohusu sekta moja ambayo rafiki yao ndiye waziri wa wizara hiyo, hatuna budi kuhoji na kuchunguza mikataba hiyo.

Je, Hoseah ameweza kumhoji Msabaha chini ya kiapo na kuhakikishiwa hakupokea yeye (au ndugu zake) kitu chochote ambacho kinakatazwa katika sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2004 na sheria nyingine?

Ni kwa kiasi gani urafiki wa Msabaha na kina Mohamed Gire, Naeem Gire, Zahor Gire, Abdul Gire, Imaduddin Gire, Mumtaz Gire, Adam Gire, Sharrifa Gire na ndugu zao walioko Ulaya na waliopo nyumbani, ulichangia kwa wao kupewa tenda hizo?

Saba, katika maelezo yake kwa wananchi, Hoseah alisema wazi kuwa kutokana na dharura iliyotokea ya nishati, Waziri Mkuu, Edward Lowassa aliingilia kati na kuunda kamati ya watu watatu kuharakisha utatuzi wa tatizo la nishati.

Swali langu kwa Hoseah ni je, ni sheria gani inayompa madaraka Waziri Mkuu kusimamisha sheria ya ununuzi wa serikali ya 2004 na kuweza kuingilia utaratibu wa utoaji tenda?

Waziri Mkuu alipoingilia utaratibu uliowekwa wa kutoa tenda, alifanya hivyo kwa mamlaka gani?

Kusema kuwa ulikuwa ni "wakati wa dharura" ndio mwanzo wa kuleta maamuzi ya kiimla?

Kwa vile Mtanzania mwenzetu ni Waziri Mkuu, isiwe ni kisingizio cha mtu huyo kupinda/kuvunja sheria kwani, ni wakati wa dharura ndipo tunataka kuona viongozi wetu wazisimamie sheria kwa umakini zaidi.

Kama kamati aliyounda Waziri Mkuu haina mamlaka ya kisheria, maamuzi yake basi pia ni batili hata kama yamefanywa kwa nia nzuri!

Kwa maneno mengine, mkataba wa RDC uliingiwa kinyume cha sheria na hivyo hauna nguvu ya kisheria, isipokuwa pale Hoseah na wenzake watakapotuonyesha utaratibu uliotumika kutoa tenda hiyo usiopingana na Sheria ya Manunuzi ya Serikali ya mwaka 2004.

Nane, Mohamed Gire, Afisa Mkuu Mtendaji wa RDC, amekuwa akitoa michango wakati wa kampeni na bila ya shaka ndugu zake nao hufanya hivyo.

Inafahamika kuwa kina Gire waliichangia CCM na kampeni yake ya uchaguzi ya mwaka 2005 (mwaka mmoja baada ya kampuni kuundwa).

Je, Hoseah anaweza kuwaambia Watanzania ni kiasi gani kilipokewa toka kwa kina Gire kusaidia kampeni ya Rais Kikwete, ya Lowassa na ya Msabaha? Tukimwambia kuwa kina Gire walichangia vya kutosha kampeni hizo wakiwa na matarajio ya kupewa mkataba wa bomba la mafuta na kupewa mkataba mwingine wa nishati atatukatalia?

Je, michango ya namna hiyo haiwezi kuonekana kama ni rushwa? Kama CCM watapinga kuwa hawakupokea michango toka kwa kina Gire, wako tayari kutoa orodha ya wachangiaji wao wakubwa wa ndani na nje ya nchi? Hoseah anaweza kutaka orodha hiyo akapewa?

Tisa, katika suala hili zima, jina moja limekuwa likihusishwa na kupatikana kwa mkataba huu na kupewa tenda kwa RDC. Jina hilo ni la Waziri Mkuu, Edward Lowassa (Monduli - CCM). Wakati huo huo kumekuwa na tuhuma kuwa mmojawapo wa watu waliohusika katika kuipigia debe kampuni hii, ni kijana mmoja mwenye mahusiano ya damu na Waziri Mkuu.

Ni kweli kuwa kijana huyo hayupo sasa kwenye orodha ya viongozi wa kampuni hiyo (kama alivyodai mmoja wa viongozi)?

Swali kwa Hoseah, je, wakati wowote katika mchakato wa tenda hii, kuna ndugu wa kiongozi aliyekuwa na nafasi ya uongozi na baadaye akajiondoa/kuondolewa kwa sababu ya kuonekana mgongano wa maslahi?

Mtu huyo ni nani na nafasi yake ni ipi? Je, serikali ilipata nafasi ya kumhoji?

Kumi, tumeambiwa kuwa RDC hawakulipwa na serikali kwa sababu ya kushindwa kutimiza mkataba, hilo linawezekana kuwa ni kweli, lakini ni kweli kuwa fedha za serikali hazikufikia mifuko ya kampuni hiyo?

Ni nani aliuza mkataba wa RDC kwa Dowans? Kama Richmond waliuza mkataba huo kwa kipengele walichoweka kwenye mkataba, na serikali ikailipa Dowans dola milioni zaidi ya mia moja, je, RDC hawakulipwa na Dowans?

Hoseah anaweza kuuhakikishia umma wa Watanzania kuwa hilo la kuuza mkataba halikuwa "janja ya nyani" kwa RDC kulipwa bila ya kufanya kazi?

Naweza kuendelea kuuliza maswali mengi, lakini kwa leo wacha niishie hapa ili niwape muda Takuru kutafuta majibu.

Nafahamu ugumu wa Hoseah na waliohusika kujibu maswali haya kwa undani na kwa ukweli, kwani wameshafikia uamuzi wa kusema "hakukuwa na rushwa".

Kilichotokea ni kile ambacho kilishuhudiwa kwenye fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1986 kule Mexico wakati timu ya Argentina ikiongozwa na mchawi wa soka, Diego Armando Maradona, ilipoweza kuifunga timu ngumu ya Uingereza kwa lile goli ambalo limebakia likijulikana kama "goli la
mkono wa Mungu".

Maradona alifunga goli hilo kwa kunyanyua mkono wake juu ya kichwa chake na mwamuzi alidhania ameona goli la kichwa.

Wakati wachezaji wa Uingereza wanalalamika, mwamuzi alielekeza mkono katikati ya uwanja.

Watanzania tumefungwa goli la Maradona, hakuna pa kulalamika, isipokuwa kuendelea kuuliza maswali.

Hakuna hatua yoyote itakayochukuliwa ili kuionyesha RDC kwa ukweli wake na jinsi mkataba huu ulivyokuwa na maswali mengi.

Mwamuzi (Hoseah) keshahesabu goli, na kapiga kipenga mkono ukielekezwa kwenye mduara wa uwanja, mpira kati! Tushangilie au tulie?

Mwandikie: mwanakijiji@journalist.com
Msikilize: http://mwanakijiji.podomatic.com
 
13 Mei 2007 Ref. No. C/HQ/ADM/SG/25/07


Mkurugenzi Mkuu
Taasisi ya Kuzuia Rushwa(TAKURU)
Dar es Salaam

Ndugu

YAH: TAKURU INALINDA NA KUTETEA RUSHWA?

Tunakuandikia barua kuomba ufafanuzi juu ya taarifa/kauli hizi ambazo wewe mwenyewe ama ofisi yako ilizitoa ambazo zikiachwa ziendelee kama zilivyo kwa maoni yetu zinaidhalilisha TAKURU na hatimaye kukwamisha mapambano dhidi ya Rushwa:

1. TAKURU kuisafisha kampuni ya RICHMOND. "….hakuna ushahidi wowote uliopatikana kuthibitisha vitendo vya rushwa, uzembe na upokeaji wa kamisheni watendaji wa serikali….uchunguzi huo umethibitisha udhaifu wa kawaida katika utendaji na ambao haukuhusisha rushwa au manufaa ya aina yoyote ile kwa upande wa watendaji na hakuna hasara iliyosababishwa na udhaifu huo"(Mwananchi 12/5/2007). "….baada ya kuona hivyo, Richmond ilionekana kufahamu mwenendo wa mambo serikalini…"(Tanzania Daima 12/5/2007). Maswali ya kujiuliza: Ni kwanini Kamati ya Waziri Mkuu iliipa tenda Richmond baada ya Bodi ya Wakurugenzi ya Tanesco kuitaka bodi yake ya sabuni kutangaza upya zabuni hiyo kwa kutimia zabuni za kimataifa? Richmond kuweza kufahamu mwenendo wa mambo ya ndani serikalini sio ishara ya rushwa ya kimadaraka? Ni kweli kama hakuna hasara iliyosababishwa na uamuzi huu wakati ambapo watanzania wamekaa bila umeme kwa miezi mingi bila kupata umeme wa dharura waliotarajia wakati wa dharura, Rais amekiri kwamba umeme ulichangia kushuka kwa kasi ya ukuaji wa uchumi na hata kuongeza mfumuko wa bei na mpaka leo bado megawatts 100 hazijatimizwa na Richmond/Dowans? CHADEMA tunaitaka TAKURU itupatie nakala ya ripoti ya uchunguzi wa TAKURU kuhusu Richmond na iweke wazi ripoti yote kwa umma.

2. Wiki iliyopita umenukuliwa ukitamka kwamba TAKURU haitaliendeleza suala la kuchunguza tuhuma za Wabunge hususani wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kupewa Rushwa kama zilivyotolewa na Mheshimiwa Philemon Ndesamburo, Mbunge wa Moshi Mjini(CHADEMA) eti kwa kuwa spika alishafunga mjadala wa suala hilo bungeni.

3. Kwamba "Mwenyekiti wa Taifa(CHADEMA), Freeman Mbowe alipotosha umma wakati wa ziara yake mwanzoni mwa mwaka 2007 aliposema kwamba Rais ametamka kuwa amepokea orodha ya wala rushwa na kwamba TAKURU inawasafisha wala rushwa". Ofisi yako ilichapa matangazo kwa gharama za walipa kodi kukanusha kwamba Rais hajawahi kupokea orodha ya wala rushwa na kwamba TAKURU haiwasafishi wala rushwa. Miezi michache baada ya tamko lenu, Rais Kikwete amesema tena hadharani kwamba amewahi kuletewa orodha ya wala rushwa. Ofisi yako haijawahi kujitokeza tena mpaka sasa kukanusha kauli ya Rais ama kukiri kwamba palikuwa na makosa katika kauli ya awali ili kurudisha imani.

4. Mara baada ya Mkurugenzi Mkuu mpya kuingia madarakani ulinukuliwa mwishoni mwa mwaka kwamba wala rushwa wajiandae unawapa kipindi cha sikukuu za Noeli(Xmas) na mwaka mpya na mara baada ya hapo wananchi wategemee maamuzi mazito juu yaw ala rushwa. Mpaka sasa ni Mwezi Mei, Ofisi yako haijazikanusha kauli hizi za kuwapa muda wala rushwa wala haijaeleza ni maamuzi/hatua gani kubwa zilizochukuliwa kama ilivyoahidiwa.

Rushwa ni kosa la jinai, rushwa ni adui wa haki. Kauli za kuwapa wala rushwa muda ama kukataa kuchunguza rushwa ni ishara ya kulinda uhalifu ambayo ni kinyume cha sheria kwa raia wa kawaida na hata taasisi za umma. CHADEMA, ikiwa ni chama cha siasa mbadala ni mdau muhimu katika kuchochea uwajibikaji wa serikali na vyombo vya haki na hatimaye kuchochea utawala bora, demokrasia na maendeleo. Ni katika muktadha huu tunakuandikia kutaka ufafanuzi rasmi asili na nia kauli hizi ili ambazo zinaelekea kuidhalilisha taasisi ili tuendelee kuwa na imani na Taasisi ya Kuzuia Rushwa(TAKURU). Kauli ya TAKURU kuacha kuchunguza suala la rushwa kwa sababu tu kiongozi mmoja ametamka kufunga mjadala kuhusu suala hilo ni ishara ya chombo hiki kufanya kazi kwa kuingiliwa na watu ama vyombo vingine na ni kinyume na dhana ya uhuru wa taasisi ya kupambana rushwa ambayo wadau mbalimbali tunaisimamia. Kama uratibu huu wa TAKURU kuacha kuchunguza rushwa kwa sababu tu ya kauli ya kiongozi mmoja basi mapambano dhidi ya rushwa yatakuwa mashakani. Mathalani, Je TAKURU ingeacha kuchunguza tuhuma za rushwa katika mkataba wa RICHMOND/DOWANS kwa sababu tu waziri Mkuu alitamka kwamba watanzania tusiendelee kujadili kampuni hiyo kwa sababu mvua zimenyesha na kwa sasa tunapata umeme ?

TAKURU inapaswa kuendelea kuwa Taasisi ya Kuzuia Rushwa na si Taasisi ya Kulinda, Kusafisha ama Kutetea Rushwa.

Wako katika ujenzi wa Taifa

John Mnyika
Kaimu Katibu Mkuu
Na Mkurugenzi wa Vijana Taifa
0754 694 553
info@chadema.net
www.chadema.net


Nakala: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Spika-Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Vyombo vya Habari
 
hawa jamaa ni manyangau yaliyojipanga kwenda kulindana kwani taarifa za kiuchunguzi kama hizi huwa ni public document kwani huenda wanachotusomea mbele ya wandishi sio kile walichokikuta.
Ndio maana hawa jamaa huwa ukiwahama chama chao wanakukolimba ama wana kumalima. tuu ili usitoe siri .
Si mlimwona 2005 NJELU KASAKA leo karudi na yuko kimya kuliko.
 
Kama inavyofahamika katika jitihada za kutafuta ufumbuzi wa tatizo la umeme lililokuwa limeikumba nchi yetu kutokana na kina cha maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme kupungua sana, serikali iliiingia mkataba wa kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura. Mkataba huo ulisainiwa kati ya serikali kupitia shirika la kuzalisha umeme (TANESCO), na kampuni ya RICHMOND, tarehe 23, June 2006.

Hata hivyo, mchakato mzima wa utoaji zabuni, uingiaji wa mkataba, usimamiaji na utekelezaji wake ulilalamikiwa sna ana wananchi, ikiwa ni pamoja na tuhuma za rushwa, kwamba kampuni hiyo ya Richmond ilijipatia zabuni hiyo, ama kwa upendeleo au kwa njia za rushwa, na kwamba-

(1). Baadhi ya watendaji wakuu wa serikali, kama ofisi ya waziri mkuu, wizara ya nishati na madini, ofisi ya mwanasheria mkuu, hazina na Tanesco walikuwa wamejipataia kamisheni ili kuitoa upendeleo kwa kampuni ya Richmond. Na kwamba baadhi ya watendaji wakuu wa serikali yetu ni wamiliki wa wa hisa katika kampuni hiyo au ni wakurugenzi wake, au watoto wao!

(2). Na kwamba, Kutokana na uzembe na rushwa, kutoka watendaji wa serikali kwenye mkataba huo, serikali yetu ilipata hasara kubwa sana ya pesa za walipa kodi.
 
Kutokana na tuhuma hizi nzito, Taasisi ya kuzuia rushwa nchini iliamua kufanya uchunguzi wa kisheria na kina, kuhusiana na tuhuma hizo nzito, ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo na kisha kuchukua hatua kali za kisheria kwa waliohusika na tuhuma hizo, na kuchukua hatua stahili kwa mujibu wa sheria za nchi!
 
Back
Top Bottom