Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

...........by higher authorities. To record the event the TB minutes of 10th April 2006 read..."at 16:20hours while the discussions were proceeding, a notice was brought to the Tender Board by the Company Secretary that the Board Chairman has directed to suspend the tender process with immediate effect until further notice"


Nasisitiza tu!
 
Alipoandika yule mwandishi wa kenya kuwa Jk anahusika moja kwa moja kwenye hiyo deal ya Richmond wengi si walimuona huyo mwandishi mzushi?.Na waandishi wa kenya walipoandika kuwa waandishi wa TZ wanalamba buti ya JK kwa kusifia hata ujinga wanahabari wa TZ na wananchi wengine walikasirika kwa kuambiwa ukweli.
Ukioa au kuolewa tendo la ndoa haliepukiki hadi mtakapopeana talaka.Sasa wa Tz waliingia mkenge na kufunga ndoa na mafisadi vumilieni hadi siku ya talaka ifike mwaka 2010,itawezekana iwapo watanzania wataamua.
TUJIFUNZE TUSIRUDIE KOSA KUJIUZA KWA KUPEWA T-SHIRT ZA KIJANI,KHANGA,PILAU NA FEDHA KIDUCHU VITU AMBAVYO VITASABABISHA UMASKINI KWAKO HADI VITUKUU
 
GUESS WHAT? MR. LOWASSA HAS A TASTE FOR RAP MUSIC!

I don’t know how many people in this country who do not belong to Generation X (kizazi kipya) can remember a song popularly known as “It wasn’t me!” This song by a Maestro rapper Shaggy or “Mr. Lover’ topped the song charts in the early 2000’s.

Prime Minister (PM) Edward Lowasa is not a man of yesteryears as far as the music is concerned. He is very up to date, so to speak. I was caught between tears and laughter when I read the headline in ThisDay Newspaper of Monday 15th October 2007. The front page headline read as “I wasn’t involved, says PM Lowassa”. With the controversial Richmond deal back on the front pages in the mainstream print media, Mr. Lowassa has once again broken silence over the issue. This time round the PM is coming out with a “it wasn’t me” rap mantra! Who would like bet that Mr. Lowassa doesn’t know one or two things about rap music?

The above story makes a depressing reading when the whole Prime Minister gives out a press release through his press secretary saying “The prime minister was never involved in the Richmond negotiations. All he did was to assume a general, overseeing role in government’s efforts to ensure the power shortage problems afflicting the country at the time were URGENTLY (emphasis is mine) addressed”. Ooh, lala! (to use a French exclamation) Really?

For god’s sake this is exactly what the prime minister’s job description is all about! The role of overseeing government matters. In particular, issues which are urgent in nature require direct overseeing, direction and if need be prudent intervention by the prime minister. Is the prime minister, for example, telling us that it is the first time is learning that TANESCO was pushed aside and short changed during the emergency power supply tendering process? Is the Right Honorable PM announcing to the world that he learnt about this through corridors and the press as a commoner just like me?

Had the Richmond deal come through nicely Mr. Lowassa would have been the first one to go to parliament, chest thumping and with great bravado declaring that this was possible because of his wise leadership and foresightedness. Meanwhile, his speech would be interrupted by “CCM Oyee, Lowassa Juu” from the over excited CCM law makers! But with the Richmond contract gone sour, the PM is pitifully trying to keep a very long distance. Talk of double posturing!

What is so amusing about the prime minister’s response is that the Richmond repudiation has now become a song and dance for the prime minister but the saga has stuck like super glue. The appalling scandal has simply refused to go away just like a bad arm pit odor! Even the best beauticians in town have failed to suppress the stench which has been lingering since 2006. Mr. Lowassa should not grill ThisDay for “reviving” the issue of corruption related to the Richmond transaction. I am certain the PM is well informed about the lecture on corruption by a distinguished former civil servant, Mzee Joseph Butiku. Mr. Butiku intimated to the public on Sunday 14th October 2007 that corruption can not simply go away because it is “unfinished business”. However, the PM seems to think otherwise. But how can Richmond saga die a natural death when up to now the country has never received even an iota of thermo power from a project “generally overseen” by Mr. Lowassa?

To add insult to an injury the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) (a proficient beautician?) was brought into the picture to soothe public anger over the Richmond circus. Quite frankly I do not envy Mr. Edward Hosea in his current plumy job. The PCCB Czar did not know that he was being used as a doormat when he promptly and without any sense of shame cleared the Government of wrongdoing by giving a clean bill of health stating that the Richmond deal was corrupt-free! Eti, (according to PCCB) although the tendering procedures were not followed to the letter, the deal was therefore devoid of graft because the Government did not part with a single coin! How can you envy a man who is being asked to defend the indefensible and cover the un-coverable? In doing so the PCCB chief did not only undermine the credibility of the anti-graft watchdog but also turned himself into a comic.

In theatrical parlance Bwana Hosea was playing the most dubious and awkward part of announcing to the gallery that all those who did not see the emperor’s new and majestic attire were sinners! Where will Mr. Hosea hide is face now that a young mischievous child in the name of Public Procurement Regulatory Authority (PPRA) has embarrassingly come out and pronounced that after all the emperor is naked! This act has now sent the whole prime minister scampering for cover, declaring “it wasn’t him”! Who was it, sir? Mr. Lowossa should do himself a favour by spilling the beans now to save his public standing or else this indignity will haunt him for long while. This will be good fodder for Mr. Lowassa’s foes in 2015.

I am not a lawyer but the little I know about law is that even an intention to commit a crime is illegal under Tanzania laws. Why did a smart lawyer like Edward turn himself into a butt of jokes by turning a blind eye on the most glaring anomalies in the deal that have subsequently been unearthed by PPRA?

Had the Richmond fiasco happened in the mature democracies, Mr. Lowassa would have hanged his prime minister’s gloves long time ago. He would be tendering his cows in Monduli and possibly writing the last chapter of his memoirs. By publicly and implicitly acknowledging that he somehow kept his eye off the ball during the emergency power procurement process, Hon. Lowassa does not merit good grades on the leadership scoreboard. The prime minister has also dismally and abysmally failed to shake off the notion that he was not above board when dealing with the emergency power project. But Tanzania is still a “kindergarten” democracy so Mr. Lowassa is going to stick around for a while.

Mr. Lowassa does not have many options to maneuver on the Richmond deal. As a head of government he should come to terms with the fact that the emergency power project was bungled under his watch. He should take political responsibility, put to task his subordinates who might have “misled” him, swallow his pride and offer public apology so that we can put this scandal behind us. Akubali yaishe in Kiswahili.

If the above prescription proves a bitter pill to swallow, Mr. Lowassa can opt for all night long prayers in the hope that come 2015 the likes of ThisDay Newspaper will not be around to invoke the Richmond ghosts. These ghosts will jog the public’s memory to ensure the Richmond tale is still pending, unfinished business. 2015 will not be the time for the “it wasn’t me” antics.


Byase Luteke is a Socio-Political Critic based in Dar Es Salaam
E-mail: byasel@hotmail.com



Source: THISDAY Suturday 20 October, 2007 page 9
 
Katika uongozi bora hakuna kitu kinaitwa 'it wasnt me' la sivyo Mzee Mwinyi asingeng'atuka kama waziri wa mambo ya ndani wakati wa yale mauaji ya shinyanga.(Na nani aling'atuka kufuatia mauaji ya Bulyankhulu? Watu wako radhi kupigia kelele za Burundi, Congo, Darful...lakini ya kwao ya Bulyankhulu, Mwembe Chai, Zanzibar...hawayaoni.)
Equally subordinates can not be allowed to shelter under superior order. Mambo ya 'nilikuwa natekeleza maagizo/amri kutoka juu ni dhuluma tu. it assumes one is a robot and is incapable of thinking/acting independently. As for Hosea and PCB..I dont envy him either..but does he envy himself? There is only one option and that is Resign Now. John Githong'o in Kenya (yes mwanamume wa shoka!) showed the way! His footprints are still 'loudly visible!.
 
Katika uongozi bora hakuna kitu kinaitwa 'it wasnt me' la sivyo Mzee Mwinyi asingeng'atuka kama waziri wa mambo ya ndani wakati wa yale mauaji ya shinyanga.(Na nani aling'atuka kufuatia mauaji ya Bulyankhulu? Watu wako radhi kupigia kelele za Burundi, Congo, Darful...lakini ya kwao ya Bulyankhulu, Mwembe Chai, Zanzibar...hawayaoni

Ni kweli walifumbia macho ya kwao na ndio maana Chisano amewabwaga
 
Nilipokuwa Dar wiki chache zilizopita nilijifunza mengi sana kuhusu mtazamo wa wananchi wa kawaida juu ya mikataba ya madini. Kuna wananchi wengi sana wana uchungu mkubwa sana kuhusu mikataba hiyo, nadhani ndiyo maana inavuja kama maji ndani ya dema. Namshukuru Invisible kuwa jana niliweza kupata nakala ya mkataba wa Richmond ingawa sijaisoma kwa kina.

Najua kuwa somo la Buzwagi mmekishalifanyia kazi kwa kina sana. Hata hivyo nilitaka kukumbusha tena kuwa mkataba wa Buzwagi ni feki sana hata ukiulinganisha na ule wa Richmond utaona jinsi huu wa Buzwagi unavyopwaya kisheria. Mkataba huu unaweza kupingwa mahakamani kuwa siyo wa serikali ya Tanzania tukaponyesha eneo letu la Buzwagi. Kwa haraka haraka nikilinganisha mikataba huu na ule wa Richmond naona haya yafuatayo:

(1) Buzwagi hauna Seal ya Serikali, wa Richmond unayo.
(2) Buzwagi hauna mashahidi, wa Richmond unao
(3) Pamoja na upungufu huo namba mbili hapo juu, Buzwagi una marekebishyo yaliyofanywa kwa mkono, Richmond hauna marekebisho mengineyo.
(4) Buzwagi una stipulate conditions za kunufaisha kampuni tu, Richmond una vipengele vianavyonufaisha serikali na vile vinavyo vinanufaisha kampuni: japo kwa utata lakini vimeelezwa explicitly.

Sijaelewa kwa nini Karamagi hakushauriwa kuwa mkataba hausainiwi bila kuwepo kwa shahidi.
 
kama kuna ukweli hapo, basi inajibu swali kwanini ameshindwa kumfukuza Msabaha!!! Huwezi kukata tawi la mti uliokalia!!!

mie nina uhakika,Msabaha anahusika na huo mkataba asilimia 100,mie nilikuwapo wakati JK anamuuliza Msabaha,Lini mtamaliza kufunga mitambo yenu?tena Jk alikuwa na hasira sana siku hiyo..na tulikuwa pale Ubungo..
 
Leo wakati kipindi cha maswali na majibu Bungeni kuna mbunge wa CCM kataka kujua kwa nini Richmond sasa wamejiingiza kufanya kazi kama za NHC. Mbunge huyo alimtaka Naibu waziri wa Nyumba Ritha Mlaki kueleza Bunge kama sasa NHC kazi zake zimekoma na kuchukuliwa na Richmond. I was shocked kusikia swali hili na Mlaki alijibu kwa mkato na kusema haijachukuliwa na Richmond wanaweza wakawa ni wakala tu lakini si kuchukua kazi ya NHC.Now kuna mwenye kujua lolote juu ya hili baada ya Ritha kukwepa kujibu maswali ?
 
Leo wakati kipindi cha maswali na majibu Bungeni kuna mbunge wa CCM kataka kujua kwa nini Richmond sasa wamejiingiza kufanya kazi kama za NHC. Mbunge huyo alimtaka Naibu waziri wa Nyumba Ritha Mlaki kueleza Bunge kama sasa NHC kazi zake zimekoma na kuchukuliwa na Richmond. I was shocked kusikia swali hili na Mlaki alijibu kwa mkato na kusema haijachukuliwa na Richmond wanaweza wakawa ni wakala tu lakini si kuchukua kazi ya NHC.Now kuna mwenye kujua lolote juu ya hili baada ya Ritha kukwepa kujibu maswali ?

Wabunge huwa wanakawaida na kuanza Kwakuwa hiki na kile, wewe uliyesikia tuambie alianza na maelezo gani kabla hajauliza!

Na kwa weye mwafrika, unaweza kusikiliza bunge huko uliko kwa kubofya:::: http://www.ijmc.udsm.ac.tz/broadcast.html
 
Kazi ilianza kwa Mbunge kumwambia Waziri aombe msamaha kwa kufuta usemi wake kwaku walikuwa kadanganya Bunge . Then alaka Mbunge mmoja akahojio uhalali wa Richmond kujiingiza kwenye kazi za NHC na ndipo akataka kujua kama Rochmond ndiye mbadala wa NHC . Waziri akasema si mbadala ila huenda ni ma agent tu na akaishia hapo . Nilitegemea waandishi kuunganisha na kuutafuta ukweli zaidi naona kimya nimeamua kumwaga hapa. Niko Dar ila nafanya jitihada za kwenda Dodoma kuchunguza kama mtanipa ridhaa yenu maana msije niita mtu wa udaku bure!!!
 
Leo ni leo Richmond




na Martin Malera



ULE muzimu wa Richmond ulioligharimu taifa sh bilioni 172.9 na kuwahi kulitingisha Bunge siku za nyuma, umeibuka tena.

Kuibuka kwa suala hilo leo, kumeikurupusha usingizini serikali ambayo jana wabunge wake chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu, Edward Lowassa walikutana chini ya mwamvuli wa Kamati ya Wabunge wa CCM kujaribu kuweka sawa mambo wakati hoja hiyo itakapowekwa mezani leo.

Taarifa kutoka serikalini na miongoni mwa wabunge ambazo Tanzania Daima imezipata tangu mwishoni mwa wiki zinaeleza kuwa, kwa siku kadhaa sasa, suala hili ambalo limezua manung'uniko mengi ya chinichini na ya wazi miongoni mwa jamii, limekuwa likiwekewa mikakati ya kulimaliza bila ya kuwapo kwa madhara makubwa kisiasa dhidi ya serikali na viongozi wake.

Kikubwa kinachozua wasiwasi huo ni ukweli kwamba, taarifa ya Kamati ya Bunge ya Uchumi na Uwezeshaji ambayo inasomwa bungeni leo imesheheni hoja nzito zinazoainisha udhaifu mkubwa dhidi ya maamuzi ya serikali katika suala hilo zima.

Ripoti yake hiyo ambayo tayari imesambazwa kwa wabunge na Tanzania Daima kupata fursa ya kuisoma, inalitaka Bunge liunde kamati teule ili kuchunguza undani ya suala hilo kutokana na kuwapo kwa mazingira mengi yenye utata.

Taarifa za uhakika kutoka serikalini na ndani ya CCM zinasema kwamba, kipengele hiki cha kuundwa kwa kamati teule ya Bunge ndicho ambacho kimekuwa kikipingwa kwa nguvu kubwa za chinichini na viongozi wa juu serikalini, kwa sababu ambazo Tanzania Daima haikuweza kuzibaini.

"Tumepata taarifa za uhakika kuwa CCM wanakutana kesho Jumatatu kupewa msimamo wa kukataa hoja ya kuunda kamati teule juu ya Richmond bungeni. Tuna taarifa kutoka kwa wabunge kuwa wanashinikizwa na waziri (anamtaja) waondoe suala hilo kwenye ripoti ya kamati. Tunachosema ni Kabwe Zitto mwingine atatokana na 'skendo' ya Richmond," inasema taarifa ya maandishi kutoka kwa chanzo kimoja cha habari kilichowasiliana na Tanzania Daima juzi Jumapili.

Kwa siku nzima jana, wanasiasa mbalimbali wa CCM na wa upinzani waliwasiliana na chumba hiki cha habari wakifuatilia kwa karibu mwenendo wa sakata hilo huku baadhi yao wakiulizia kuhusu maamuzi ya Kamati ya Wabunge wa CCM kuhusu suala hilo.

Hata hivyo taarifa ambazo gazeti hili lilizipata kutoka Dodoma jana jioni zinaeleza kuwa, wabunge wa CCM walikuwa wameweza kuishinda hoja ya baadhi ya mawaziri waliokuwa wakitaka suala la kuundwa kwa kamati teule liondolewe na hivyo kumfanya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Biashara, Mbunge wa Bumbuli, William Shelukindo (CCM) kuisoma taarifa kamili ya kamati hiyo.

Taarifa za uhakika zinaonyesha kuwa, kamati hiyo ya Bunge katika suala hilo imehoji maswali makuu sita muhimu, yote yakielekeza udhaifu mkubwa katika utoaji wa zabuni hiyo pamoja na uhalali wa Richmond kuiuzia zabuni yake hiyo Kampuni ya Dowans ya Falme za Kiarabu kimyakimya.

Si hilo tu, ripoti hiyo pia inahoji uwezo wa Kampuni hiyo ya Richmond Development Corporation ya Marekani, hasa ikizingatiwa kuwa mwaka 2005 kutokana na uwezo wake mdogo kifedha iliikwamisha serikali katika mradi wa bomba la mafuta la kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza.

"Serikali ilikuwa na taarifa za kutosha kuhusu uwezo duni wa kiutendaji wa Richmond, hasa baada ya kampuni hiyo kushindwa, bila sababu za msingi, kutekeleza mradi wa bomba la mafuta (kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza) mwaka 2005 kinyume cha makubaliano (Memorundum of Understanding) kati ya Serikali na kampuni hiyo. Je, ni sababu zipi za msingi zilizoisukuma Serikali kuufumbia macho," inasema sehemu mojawapo ya ripoti hiyo ambayo Tanzania Daima iliiona.

Aidha, kamati hiyo katika taarifa yake hiyo inaitaka serikali ieleze ni kiasi gani cha fedha imekipokea kutoka kwa Dowans Holdings S.A. kwa kushindwa kukamilisha mradi wa umeme wa dharura katika muda muafaka na hivyo kuifanya ilazimike kulipa dola za Marekani 10,000 kila siku kuanzia Juni mwaka huu.

"Kwa mujibu wa mkataba, Dowans walitakiwa kuilipa TANESCO kiasi cha dola za Marekani 10,000 kwa siku kutokana na ucheleweshaji wa ufungaji wa mitambo ya umeme wa dharura. Kamati ingependa kufahamu ni kiasi gani cha fedha ambacho TANESCO imelipwa mpaka sasa kwa mujibu wa mkataba.

"Utendaji kazi usioridhisha wa Richmond na ushahidi bayana uliojitokeza polepole wa kampuni hiyo kutokuwa na uwezo wa kutosha kifedha na kukosa kabisa uzoefu katika miradi ya umeme, umezua maswali mengi miongoni mwa wananchi kuhusu umakini uliotumika katika kuiteua kampuni hiyo kutekeleza mradi nyeti kitaifa wa aina hiyo na wenye gharama kubwa (sh bilioni 172.9)," inasomeka sehemu ya taarifa hiyo ya kamati.

Kamati hiyo inalitaka Bunge kuhakikisha linalimaliza suala hili tata kwa uwazi na ukweli ili kuweza kutimiza kile inachokielezea kuwa ni kukidhi matakwa ya demokrasia na utawala bora.

Mbali ya hilo, kamati hiyo inaeleza kufarijika na kazi iliyofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya kuchunguza kuwapo kwa mianya ya rushwa katika mchakato wa zabuni hiyo, ingawa ikatamka bayana kwamba taarifa ya taasisi hiyo bado ilikuwa haijitoshelezi katika maeneo mengine kadhaa.

Kamati hiyo katika taarifa yake inasema, Takukuru ililiangalia suala hili katika mtazamo wa kijinai na hivyo kusababisha kuibuka kwa maswali mengine ya msingi yaliyo nje ya sheria ya jinai.

Katika hili kamati hiyo ambayo inaundwa pia na wabunge kadhaa wa upinzani wakiwamo Mohammed Mnyaa, ambaye ni Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, inahoji kuhusu miiko, maadili na taratibu za kazi za Serikali, uadilifu, umakini na uwajibikaji katika utendaji kazi, kama mambo ambayo hayakuangaliwa na ambayo yanapaswa kupatiwa majibu ya uhakika.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, viwingu vya mashaka vilivyotanda juu ya suala hili haviwezi kuondoka kwa kuvifumbia macho au kwa kuvipuuzia bali kwa kuvifanyia kazi kwa uwazi na ukweli ili kukidhi matakwa ya demokrasia na utawala bora.

Kamati hiyo inasema, licha ya kazi iliyofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), bado yako maswali ya msingi yanayohusu miiko, maadili na taratibu za kazi za Serikali, uadilifu, umakini na uwajibikaji katika utendaji kazi, ambayo hayakuangaliwa na yanadai majibu ya uhakika.

Baadhi ya wabunge wa CCM waliozungumza na Tanzania Daima, walisema kuwa wanaunga mkono pendekezo la kutaka kuunda tume kwani ndiyo njia pekee ya kumaliza utata huo.

"Kama rais ameunda tume kuchunguza mikataba ya madini kwenye jambo ambalo tulilipinga kwanini sisi tusiunde kamati kumaliza utata wa hili jambo?" alihoji mmoja wa wabunge wa CCM.

Hata hivyo licha ya ripoti hiyo kukamilika tangu Aprili mwaka huu, ilishindwa kuwasilisha hoja hiyo bungeni kutokana na urasimu uliokuwapo ambao unadaiwa kuchagizwa na mmoja wa vigogo wanaodaiwa kuwa nyuma ya mradi huo.

Mapema mwaka 2006, taifa lilikumbwa na ukame uliosababisha vyanzo vya umeme ambayo ni maji kukauka.

Kutokana na hali hiyo, Serikali ilichukua hatua za dharura ili kuepusha nchi isikumbwe na janga la kukosa nishati ya umeme. Kutokana na hali hiyo Shirika la Umeme nchini (TANESCO) liliingia mikataba na wawekezaji binafsi wa nje kuleta mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura kwa kutumia gesi asilia na dizeli.

Mbali na Richmond, kampuni nyingine iliyoitikia wito wa Serikali kwa haraka ni Aggreko, ambayo ilianza uzalishaji umeme wa dharura bila kuchelewa, hivyo kusaidia mapema kuondoa kero na wasiwasi mkubwa uliozikumba sekta za viwanda, biashara na utoaji huduma nchini.

Kwa mujibu wa taarifa za Kampuni ya DOWANS, ufungaji wa mitambo ya kuzalisha na kuingiza umeme wa megawati 100 kwenye gridi ya taifa ulitegemewa kukamilika Juni, 2007, badala ya mwezi Februari kama iliyosainiwa kwenye mkataba, miezi kadhaa baada ya hali ya dharura kumalizika.
 
Hapa naona PCCB wanavuliwa nguo peupee!!Sijui mafisadi wataweza tena kuizima safari hii
 
Hapa naona PCCB wanavuliwa nguo peupee!!Sijui mafisadi wataweza tena kuizima safari hii

Mfwatiliaji, nadhani unaota! Una matarajio ambayo sidhani kama yatafikiwa! MAkachero wa PCCB waliobobea kwenye upelelezi na wanasheria wao hawakuona kitu; Je, hao Wanasiasa Wabunge watatumia mbinu gani? Kalaga baho!
 
Makachero wa PCCB waliobobea kwenye upelelezi na wanasheria wao hawakuona kitu; Je, hao Wanasiasa Wabunge watatumia mbinu gani? Kalaga baho!

Hawakuona kitu? Are you sure? Inawezekana walisema kuwa hawakuona kitu lakini mazingira yanaonesha kuwa waliona kitu, ila hawakusema. Lakini kweli wewe na akili zako can you trust PCCB?
 
Back
Top Bottom