Sakata la Kinyerezi: Hivi ndivyo majirani 8 walivyouwawa kwa kupigwa risasi na askari polisi

Sakata la Kinyerezi: Hivi ndivyo majirani 8 walivyouwawa kwa kupigwa risasi na askari polisi

Mkuu unashangaa huyu shetani anatoboa na bado anagombea tena.MUNGU HUYU HUWA ANAMAKUSUDI YAKE KWA AKILI YA BINADAMU NI VIGUMU KUAMINI
Usipoteze muda wako hata kufikiria tunza kumbukumbu ya ujumbe huu huo muda hafiki
 
Maandamano yanayokuja kila Mzanzibari na biashara zenu mtakuwa targets regardless mnanufaika na mfumo au la, what Samia and her clicks are doing in Tanganyika is too much.
TISS and Police department are part and parcel ya huu unyama unaofanywa kwa Watanganyika na Tanganyika kwa ujumla.

Mkuu, Lets keep the Focus kwa Maadui zetu, Wazanzibar wa kawaida hawana say yeyote kwa serikali yao ni kama vile wewe ambavo huupangii serikali nn inafanya.
 
Wakuu,

Mnakumbuka ile stori iliyokuwa inatrendi siku kadhaa nyuma kuhusu afisa wa polisi mstaafu aliyeuwawa kwa kupigwa risasi huko Tabata.

Sasa mkasa mzima huu hapa. Kilichofanyika ni kitendo cha kinyama sana. Stori nzima iko hapo n=chini

--------------------------

Mpaka sasa kunguru na nzi wamezuka eneo ambapo majirani nane wa mtaa wa Kanga-Kariakoo, Kinyerezi, jijini hapa, walipouwawa. Kabla ya mvua kunyesha Novemba 4, 2025, harufu ya kifo ilikua ndiyo alama ya eneo hilo. Mvua iliweza kusafisha baadhi ya mabaki ya viungo vya binadamu yaliyokuwa yamebaki, ikiwemo damu nzito.

Tukio hili lilitokea usiku wa kuamkia Novemba 3, 2025, majira ya saa tisa. Majirani hao waliuwawa zamu kwa zamu kwa kupigwa risasi. Hii ni baada ya kuambiwa wajilaze nyuso zao zikiangalia ardhi, na kuamrishwa kusali sala ya mwisho.

Majirani hao ambao nyumba zao zimefuatana katika mstari mmoja, walikuwa ni afisa polisi mstaafu, walimu wawili, dereva, wauza duka wawili, afisa wa benki na mfanyabiashara ndogondogo.

“Hapa kulikua hakufai kabla ya hii mvua kunyesha, wao walikuja wakamwagia mchanga, lakini kulikua hakufai, mvua imesafisha safisha, kidogo,” moja ya majirani alitueleza hali baada ya mauaji hayo.

Tukio hili lilianza baada ya duka la jumla lililopo katika mtaa huo kusikika kuwa limevamiwa na vibaka. Polisi mstaafu aliwaongoza majirani wenzake kwenda kuimarisha ulinzi katika eneo hilo, ambapo pia aliamua kupiga simu na kuita polisi.

Polisi wenye silaha walivyofika kwenye eneo hilo waliwaamrisha wote kulala chini. Licha ya kujitetea, hoja zao hazikuweza kufua dafu. Waligawanywa makundi mawili, wakitenganishwa na barabara ambayo imegawanya makazi yao, upande wa kulia na kushoto, wengine wakawekwa karibu na duka hilo la jumla, na wengine wakawekwa upande wa pili, pembeni ya nguzo ya umeme.

Afisa wa benki, ambaye duka la jumla limetazamana na nyumba yake, alikuwa wa mwisho kufika katika eneo hilo. Hii ni baada ya kuona polisi wamefika, akajitokeza kuungana na majirani zake. “Kuna usalama?” aliuliza afisa huyo, ambapo alihakikishiwa na polisi hao kwamba “usalama upo.”

Hata hivyo, tukio hilo liliwabadilikia na kuwa ndiyo safari yao ya mwisho. Mmoja wa marehemu aliyepewa pia jina la utani mtaani kama Ostaadh, ambaye kazi yake ni udereva, akawasihi watu hao kuwa tayari mke wake ameshafariki, na ana mtoto mdogo wa miezi sita, hivyo wasimuue, kilio ambacho hakikusikika.




View attachment 3499643
View attachment 3499642View attachment 3499641


View attachment 3499640

View attachment 3499639
Aisee
 
Hili halijaisha hadi liishe lazima kulipa kisasi. CCM wameiuza Tanganyika utumwani Zanzibar, yaani wametoa kafara ya damu za Watanganyika zaidi ya 10,000 ili Mzanzibari aendelee kuitawala Tanganyika yetu,hili halikubaliki hata kidogo. Tuanze na wanaccm wa huku bara madiwani, wabunge, viongozi wa serikali za mitaa hawa wote ni adui namba moja wa Tanganyika huru.
Mimi nawaambia kama kuna jasiri amguse Kwete panapouma! Mzee amekuwa mpumbavu sana!
 
Siku hizi nikimuona tu askari napata hasira hata sijui zinatoka wapi. Nimetokea kuwachukia sana hawa watu.

Ndio, yawezekana waliofanya yote hayo ni askari kutoka Zanzibar lakini ni upumbavu usiomithilika kukubali kuingiliwa katika majukumu

Ajabu ni kwamba bado kuna watu bila hata aibu wanatetea hiki kilichotokea.

Eee Mungu tuondolee hawa watu duniani, Tanzania hatuwezi kuhimili hivi vishindo
Juzi nimepishana nao wamepakizana kwenye pick up wanasambazwa kwenye lindo nikasikia kidogo kwa mbali kinaniambia wagonge! Jamani magaidi kumbe huwa hayazaliwi yakiwa magaidi, tujisahihishe!
 
Back
Top Bottom