Sakata la kuzuiwa KQ nani mshindi na nani ataathirika?

Bishop Hiluka

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
7,147
Reaction score
14,699
Nami nieleze kwa kifupi kuhusu mijadala inayoendelea humu Jamii Forums kuhusu sakata hili, huku nikiwa nimeandaa nguo zangu chafu kwa kutegemea nitapata mapovu ya kutosha.

Kwanza ieleweke wazi kuwa hiki kinachoendelea sasa kati ya Tanzania na Kenya ni mikakati ya kiuchumi ya kushinda soko baina ya washindani wawili na siyo tahadhari ya virusi vya corona kama inavyosemwa na Wakenya. Kenya siku zote katika Afrika Mashariki inajua kuwa mshindani wake ni Tanzania kwa hiyo wanataka soko lote liwe mikononi mwao.

Sasa nini madhara ya mgogoro huu, nani ataibuka mshindi na nani wataahirika zaidi? Ieleweke kuwa uchumi wa Kenya unategemea kwa kiwango kikubwa sekta ya usafiri wa anga ambayo ndiyo moyo wa sekta ya utalii wa nchi, ikitegemea zaidi safari za ndege za kimataifa. Hapa ngoja niweke sawa: pamoja na kutegemea utalii, Kenya hawana vivutio vingi na vizuri vya utalii kama ilivyo Tanzania na ambacho wamekuwa wakifanya ni kufaidika kupitia mgongo wa vivutio vya Tanzania ikiwemo Mlima Kilimanjaro na Serengeti.

Wamekuwa wakijitangaza kwa kutumia vivutio vya Tanzania na kuwapata watalii, wakitumia KQ kuwapitisha Nairobi ambako hulala katika hoteli zao na kuwaingizia kipato kisha kuwaleta Tanzania katika viwanja vitatu vya KIA, JNIA na Zanzibar. Hata wakati wa kurudi watalii hutumia KQ kutoka Tanzania hadi Nairobi ambako wanalala na baadaye kurudi nyumbani kwao, huku wakiacha fedha nyingi nchini Kenya. Kwa maana hiyo, kama Tanzania itaendelea kuzuia KQ kuingia nchini kuna athari kubwa na ya moja kwa moja katika uchumi wa Kenya kwa sababu watapata hasara kubwa kutokana na matangazo wanayotumia kujitangaza katika vyombo vya habari vya kimataifa.

Tanzania itaathirika kwa kukosa soko la kuuza mazao ya kilimo lakini itafaidika zaidi kiutalii pale ambapo watalii waliokuwa wakitumia KQ kuingia nchini kupitia Nairobi watalazimika kutumia mashirika mengine kuja noja kwa moja Tanzania. Ndiyo maana sishangai kushuhudia mapovu kutoka kwa ndugu zetu wa kaskazini humu JF.
 
Dah! Mataifa yote haya tumezuia ndege zao wangekua wanalialia kama Watanzania sijui tungefanya nini haswa, tumezuia hadi Marekani, Sweden, India n.k, ila cha msingi na muhimu sana kwetu ni usalama wa afya zetu, na kwa vile mumepiga makelele sana hadi mnatia huruma kwa jinsi mnang'ang'ania kuja kwetu, basi mtaruhusiwa kuja ila lazima kila anayekuja na paspoti ya Tanzania apanue mdomo na kutumbukizwa kifaa cha kupima corona, ikigundulika amesheni virusi anageuzwa kwa gharama zake. Lazima tuwapime kama tunavyofanya pale mpakani, pale ambapo mlipiga makelele kama haya ikabidi tuwahurumie.

Watanzania hili la corona mumedhihirisha udhaifu mkubwa sana na imekua mwendo wa tahadhari kutolea na mataifa mengi dhidi yenu licha ya nyie kujiaminisha kwamba hamna corona.
Mnatiwa alama nyekundu kote...

Health Alert: U.S. Embassy Dar es Salaam | U.S. Embassy in Tanzania

 
Hiyo dhana kwamba Kenya inafaidika kwa kutumia vivutio vya Tz ni dhana potovu. Nadhani hizo ni zile hadithi ambazo mlikuwa mnasimuliwa enzi zile za ujamaa. Maanake kwenye enzi hizi za 'info' zinazopatikana virahisi haingii akilini kwamba mtalii ambaye ana nia ya kutalii nchini Tz atajipata yupo Kenya bila kufahamu kwamba safari yake ilikuwa ya kuelekea kwenye nchi nyingine tofauti.

Nyie watz na wengine wengi ukanda huu ndio mnafaidika na uwanja wa JKIA na Nairobi pia, kwasababu jiji la Nai ndio 'hub' ya shughuli nyingi tu Afrika Mashariki na ya Kati. Connection za kimataifa zipo nyingi zaidi jijini Nairobi na sio kwa ndege za abiria tu, hata kwa mizigo pia. Mashirika mengi na kampuni za kimataifa zinaendesha shughuli zao ukanda huu kutoka Nairobi, iwe kwenye 'logistics', utalii, biashara hadi kwenye mission zao ndani ya nchi kama DRC, S.Sudan, Somalia na hata C.A.R. Give credit where it is due, Nairobi ipo 'strategic' hivyo kwasababu ya sera, mikakati mwafaka na kujitangaza sio kibahati bahati.
 
Yani mimi nataka hizi frequency za mara 4 kwa siku za KQ zipunguzwe hadi mara 3 kwa wiki tu. Yani within a year...KQ imefilisika na sisi tunacheka tu.
Yaani mumelia sana kama mbwa alokanyagwa mkia vile hadi munatia huruma, lakini ni kwa nini munang'ang'ania kuingia Kenya kwa udi na uvumba namna hii?
 
Yaani mumelia sana kama mbwa alokanyagwa mkia vile hadi munatia huruma, lakini ni kwa nini munang'ang'ania kuingia Kenya kwa udi na uvumba namna hii?
Nani kakwambia tunataka kwenda kenya? Nyie ndo mnang'ang'ana kuja huku, kila siku mara nne halafu hamtaki sisi tuje kwenu , ati tukae quarantine siku 14. What kind of nonsense is that!? Tukisema kila mtu akae kwake manjifanya majuha!

Sisi si tuna corona! Basi msije kabisa huku. Tuone nani mwanamme.
 
Mimi likua kwenye ofisi ya Korean Air Beijing. Wakati huo ndo wanaanza safari za kwenda Nairobi. Kwenye flyer na banner zao zote eti wameweka mlima Kilimanjaro. Nikawauliza kwa nini mmeweka hii hapa. Kwani nyie hamjui kama huu mlima haupo Kenya. Nikaanzisha ugomvi tu kuwafundisha. Wakaishia kuomba msamaha.

Najua kama hakuna walichofanya baada ya hapo ila meseji sent. Sahivi ni vita tu nyie nyang'au! !!
 
Wakenya mnaandika comment refu kama ndiyo uzi vile... na hakuna hata aya wazee. Maze tutamezea wapi tukiwa tunasoma?

Hata mtu akitaka kuwaqoute anashindwa aanzie wapi.

Tujaribu kufupisha michango na maoni yetu yasomeke vizuri. Na hayana hata aya.
 
Mbona mnalialia nyie si mmefunga kelele za nini, kila mmoja ashinde mechi zake.
 
Kwahiyo wewe MK ng'ombe ni bora kuliko Mtanzania?

Yaani nyie ombeni nisiwe Rais... wakenya wengi wanatabia nisizozipenda na mmenda mbali mmetuharibia watoto walioletwa kusoma huko.

Basi, wakirudi huku ni kujishabadua na vijitabia vya kikenya visivyofahamika ni vya wanaume au wanawake.
 
Hivi kwa nini tusiweke kwamba MTU anayetaka kutumia mlima Kilimanjaro kwenye biashara yake anatakiwa atulipe kwanza ndo tutoe leseni watumie.
 
Jirani, ni hivi, hakuna mtz atapimwa kwa kutupukizwa vijiti na mkenya,pale mpakani watanzania wanapimwa na Sisi watz wenyey. I assure you that,KQ itapndwa na wabongo,na watapimwa joto tu.yaani kwa Hilo,tumeisha wakalisha chini,na Kama huamini,nenda mpakani ndio utaamini
 
You are so mentally consumed by this disease mpaka unasikitisha. Nani ka kwambia huku korona inatutesa?
Kila mkiambiwa hali ni shwari hamsikii.

Leo hii balozi wa Marekani kaenda ikulu with no mask!!

Balozi wa Vietnam pia bila ya mask!

Kila mkiambiwa kama hamuamini njooni mjionee wenyewe. Nyie kazi yenu ni kutuwekea dharau tu.

Sisi watanzania hauwezi dharau. Dunia nzima wanajua, naona ni nyie pekee msioelewa hilo. Sasa mtaona!

Rwandanair wameruhusiwa, tuone nyie sasa!!
 
Hivi kwa nini tusiweke kwamba MTU anayetaka kutumia mlima Kilimanjaro kwenye biashara yake anatakiwa atulipe kwanza ndo tutoe leseni watumie.
Tutawaua kwa njaa hawa.

Vile tukiwatupia taulo kama wadogo zetu wanaleta ujuaji kila wakati.wakati kofi moja tu ICU.
 
Tutawaua kwa njaa hawa.

Vile tukiwatupia taulo kama wadogo zetu wanaleta ujuaji kila wakati.wakati kofi moja tu ICU.
Sawa lakini wao wanaingizia hela kwa hiyo kama inawezekana tungeshea tu au waache kutumia mlima Kilimanjaro kutangaza biashara yao.kumbuka dunia hii ya ubepari Hamna kuhurumiana.
 
Sawa lakini wao wanaingizia hela kwa hiyo kama inawezekana tungeshea tu au waache kutumia mlima Kilimanjaro kutangaza biashara yao.kumbuka dunia hii ya ubepari Hamna kuhurumiana.
Sisi hatuna shida kushare sababu tuna rasilimali nyingi sio moja.
Tatizo ni pale katka share wanapodhani ni sehemu ya haki yao,ndipo tunapowaelekeza njia sahihi ya kupita.hata kwa namna ya maumivu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…