Bishop Hiluka
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 7,147
- 14,699
Nami nieleze kwa kifupi kuhusu mijadala inayoendelea humu Jamii Forums kuhusu sakata hili, huku nikiwa nimeandaa nguo zangu chafu kwa kutegemea nitapata mapovu ya kutosha.
Kwanza ieleweke wazi kuwa hiki kinachoendelea sasa kati ya Tanzania na Kenya ni mikakati ya kiuchumi ya kushinda soko baina ya washindani wawili na siyo tahadhari ya virusi vya corona kama inavyosemwa na Wakenya. Kenya siku zote katika Afrika Mashariki inajua kuwa mshindani wake ni Tanzania kwa hiyo wanataka soko lote liwe mikononi mwao.
Sasa nini madhara ya mgogoro huu, nani ataibuka mshindi na nani wataahirika zaidi? Ieleweke kuwa uchumi wa Kenya unategemea kwa kiwango kikubwa sekta ya usafiri wa anga ambayo ndiyo moyo wa sekta ya utalii wa nchi, ikitegemea zaidi safari za ndege za kimataifa. Hapa ngoja niweke sawa: pamoja na kutegemea utalii, Kenya hawana vivutio vingi na vizuri vya utalii kama ilivyo Tanzania na ambacho wamekuwa wakifanya ni kufaidika kupitia mgongo wa vivutio vya Tanzania ikiwemo Mlima Kilimanjaro na Serengeti.
Wamekuwa wakijitangaza kwa kutumia vivutio vya Tanzania na kuwapata watalii, wakitumia KQ kuwapitisha Nairobi ambako hulala katika hoteli zao na kuwaingizia kipato kisha kuwaleta Tanzania katika viwanja vitatu vya KIA, JNIA na Zanzibar. Hata wakati wa kurudi watalii hutumia KQ kutoka Tanzania hadi Nairobi ambako wanalala na baadaye kurudi nyumbani kwao, huku wakiacha fedha nyingi nchini Kenya. Kwa maana hiyo, kama Tanzania itaendelea kuzuia KQ kuingia nchini kuna athari kubwa na ya moja kwa moja katika uchumi wa Kenya kwa sababu watapata hasara kubwa kutokana na matangazo wanayotumia kujitangaza katika vyombo vya habari vya kimataifa.
Tanzania itaathirika kwa kukosa soko la kuuza mazao ya kilimo lakini itafaidika zaidi kiutalii pale ambapo watalii waliokuwa wakitumia KQ kuingia nchini kupitia Nairobi watalazimika kutumia mashirika mengine kuja noja kwa moja Tanzania. Ndiyo maana sishangai kushuhudia mapovu kutoka kwa ndugu zetu wa kaskazini humu JF.