SAKATA LA LUGUMI: Tamko la Ofisi ya Bunge kuhusu mkataba wa LUGUMI

SAKATA LA LUGUMI: Tamko la Ofisi ya Bunge kuhusu mkataba wa LUGUMI

PAC wanajipa madaraka ambayo sio yao...hawana mamlaka ya kukagua mikataba bila idhini ya wahusika
Sio mkataba ni maelezo ya utekelezaji wa mkataba.... Ina maana hujaona au umeamua kutoona ufafanuzi hapo juu
 
Tumemsikia mwenyekiti wa PAC akizungumza. Leo lawama zinatupiwa kwa vyombo vya habari
Kwanza, Bunge lilitakiwa likanushe habari za mwenyekiti wa PAC kama upotoshaji halafu ndiyo maelezo yafuate

Hizi habari za kuleta 'maelezo ya kina' ni njia za kutaka kuficha mkataba.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi, usalama na mambo ya nje amenukuliwa akisema mkataba ameshapelekewa.
Bunge likanushe habari hiyo kwanza

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama amekiri kupata mkataba, kama yalikuwa yanahitajika maelezo mkataba ulimfikiaje? Tunajua kila jambo lazima lipitie ofisi ya bunge, sasa wao waliombaje maelezo badala yake ukatolewa mkataba kama alivyosema mwenyekiti wa ulinzi na usalama?

Hizi habari ni kutaka kuficha ukweli, zitaumiza serikali zaidi maana watu wanadadisi kuliko walivyopaswa

Vyombo vya habari vina taarifu tu havina uhusiano na LUGUMI.

Kuna mahusiano ya Serikali, Lugumi na Bunge katika sakata hili kwa maelezo na taarifa zinazokinzana kila uchao

Msitwishe lawama vyombo vya habari kwa kukwepa ukweli
 
igizo limeingia sehemu ya nne
1.Kamati ya PAC kudai Mkataba
2.Kamati ya Mambo ya nje kupewa jukumu la PAC
3.Said Lugumi kutoweka nchini
4.Bunge kudai kilicho takiwa na PAC si mkataba bali Maelezo
5....

Chama Cha Majipu kinajikanganya chenyewe, kama wakati wa umeya wa Dar. Uongo, uongo mtupu. Ndio tatizo la kuwa na vilaza bungeni na kumtegemea mtu kama Chenge aokoe jahazi. Na yeye ni kusuka madili tu.

Hapa kunahitajika Uongozi dhabiti wa JPM kuyakemea hayo mapepo.
 
Tulijua tu huu mfupa Magufuli hawezi kuuvunja, haya yaendelezwayo ni uthibitisho kuwa mafisadi wakiguswa nchi itatetemeka....
 
Kuna dhambi gani kwa PAC kuuona huo mkataba? Hivi hili nalo lilihitaji kutolewa press release?

Huyu Lugumi inaonekana ana nguvu kubwa mnoo nyuma yake.



sio lugumi mkuu wanasiasa ndo wenye nguvu kama wanasiasa wakiacha siasa na kutekeleza majukumu yao kwa taifa lugumi ni mweupe kama unga wa ngano!!!
 
Mimi naamini maneno ya Aeshi (?) M/kiti wa PAC niliyemsikia kwa masikio yangu na niliyemuona kwa macho yangu akiongea ITV.

Kamwe sitaamini hili tamko lindana la ofisi ya Bunge. Halafu nani alisema Magu anaweza kutumbua kila jipu? !
Kwanza naomba uelewe kuwa Aeshi siyo mwenyekiti wa PAC.

Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Mwenyekiti wa PAC na LAAC lazima atoke kambi ya Upinzani. Wapinzani walikataa kushiriki uchaguzi wa PAC na LAAC kwa madai kuwa wajumbe walioteuliwa kutoka kambi ya upinzani hawana uwezo. kwa lugha nyingine, kambi ya upinzani haiwaamini wajumbe wa PAC.

Pili, hakuna sehemu ambayo Rais Magufuli alisema ataweza kutumbua majipu yote lakini vile vile huwezi kutaka Rais Magufuli atumbue pia majipu ambayo hayajaiva na kama akifanya hivyo, kuna wengine watakuja hapa wanadai Rais anakurupuka.
 
Mwenyekiti wa PAC Aishi anautaka huo mkataba kama nani..Mbona wabunge mishahara yao wanafanya siri..Mkataba ni wa siri
 
Kumekuwa na taarifa zinazoendelea kupotosha umma na baadhi ya vyombo vya Habari kuwa Kamati ya Bunge yo Hesabu za Serikali (PAC) ilipokuwa ikitekeleza majukumu yake tarehe 5 April, 2016 ililitaka Jeshi Ia Polisi kuwasilisha Mkataba ulioingiwa Kati ya Jeshi hilo na Kampuni ya Lugumi Enterprises ltd kuhusu mradi wa Utambuzi wa Alama za Vidole AFIS (Automated Fingerprint Identification System). Ofisi ya Bunge inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hili kwamba, taarifa hizo si za kweli na zina lengo Ia kupotosha umma kutokana na kile kilichoamuliwa na kamati hiyo.

Ukweli kuhusu jambo hili ni kwamba tarehe 5 April, 2016, kamati hiyo ilikutana na kujadili Taarifa ya Ukaguzi wa hesabu zilizokaguliwa za fungu 28, Jeshi Ia Polisi kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2014 ambapo kamati pamoja na mambo mengine iliona kuna haja ya kupata maelezo ya kina kwa maandishi katika utekelezaji wa mkataba huo.

Kutokana na haja hiyo, kamati ilimwagiza Afisa Masuhuli ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuwasilisha maelezo ya kina kwa maandishi kuhusu utekelezaji wa mradi huo kwa Ofisi ya Katibu wa Bunge ili kamati iweze kuchambua na kujadili maelezo hayo kabla ya kupendekeza kwa Bunge hatua zaidi za kuchukua. Kufuatia agizo hilo, kamati ilimwandikia pia Katibu wa Bunge taarifa kuhusu agizo hilo tarehe 12 Aprili, 2016 ili kupatiwa maelezo hayo kutoka kwa Afisa Masuhuli.

Ofisi ya Bunge ilimwandikia barua Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo yo Ndani tarehe 12 Aprili 2016 kuwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Kamati Kudumu yo Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyotokana na kikao hicho cha tarehe 5 Aprifi 2016 kabla yo tarehe 18 Aprili, 2016 kama ilivyoshauriwa na kamati. Hivyo ni vyema Umma ukafahamu kuwa kilichoombwa na Kamati ni Maelezo ya utekelezaji wa Mkataba huo na sio Mkataba kama inovyoripotiwa na baadhi yo vyombo vya Habari ambapo Ofisi ya Bunge iliomba maelezo hayo yawasilishwe kabla yo tarehe 18 Aprili, 2016.

lmetolewa na:

Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasmano
Ofisi ya Bunge

DAR ES SALAAM

15 Aprili, 2016.

HII TAARIFA HAIJAKAA VIZURI KWANI UNAPOSEMA KITENGO CHA MAWASILIANO PASIPO KUTAJA CHEO, JINA!!!!!!!!!!!!!!

JE, ALIYETOA TAARIFA HII HANA CHEO PAMOJA NA JINA AMEKOSA PIA?????

BADO HAIPO SAWA HII TAARIFA.......... KWANZA HATA HIYO 'MAWASMANO" SIJAJUA INA MAANA GANI.

WATANZANIA TUNAPENDA KUJUA LUGUMI YUPO WAPI KWANI VYOMBO VYA HABARI TUNAELEZWA KUWA AMETOROKA, JE NI SAHIHI MBONA WAHUSIKA HAWAJITOKEZI KUKANA NA HILI PIA?????

JE BUNGE WANAPOTAFUTA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MKATABA NA IKIWA TUNAELEZWA KUWA KATIKA MKATABA NI BIL. 37 LAKINI AKALIPWA BIL 46 JE KAMA KAMATI YA BUNGE WANAELEWA HILI AU WAO WANATAKA UTEKELEZAJI WA MKATABA TU?????

TUWE WAKWELI WAJAMENI!!!!!!!!!!!!!!
 
Kuna
Kama wahusika watamruhusu kuona hakuna shida lakini wanaweza kumzuia na asifanye lolote...

Wahusika hawana choice my friend. Ile kamati ya Bunge ikiutaka mkataba, inauitisha tu na unaletwa. Kwenye mkataba hawaangalii prices tu. Wanaangalia na vitu vingine kama specifications, timelines, methods za malipo etc.
 
Mimi naamini maneno ya Aeshi (?) M/kiti wa PAC niliyemsikia kwa masikio yangu na niliyemuona kwa macho yangu akiongea ITV.

Kamwe sitaamini hili tamko lindana la ofisi ya Bunge. Halafu nani alisema Magu anaweza kutumbua kila jipu? !
Kamsikilize tena kama alisema walete mkataba au maelezo ya utekelezaji wa mkataba, binafsi nilisikia maelezo ya utekelezaji wa mkataba.
 
Hii movie haina tofauti na ile ya bumbuli boy.
Wahusika wote ni watoto wa wenye nchi, lazima majibu yafanane..ccm mble kwa mbele..wenye wivu wajinyonge haya maneno mlala hoi akiimba kakaririshwa tu, wenye mfumo ndio wana maanisha haswa kulingana na matendo yao. Kwa utamu huu kweli ccm haita kaa ikubali kuachia nchi hata kwa mapinduzi,acha vikaratasi bora wampe mzungu tuwe wakoloni.
 
Back
Top Bottom