SAKATA LA LUGUMI: Tamko la Ofisi ya Bunge kuhusu mkataba wa LUGUMI

SAKATA LA LUGUMI: Tamko la Ofisi ya Bunge kuhusu mkataba wa LUGUMI

Mwenyekiti wa PAC Aishi anautaka huo mkataba kama nani..Mbona wabunge mishahara yao wanafanya siri..Mkataba ni wa siri

MBONA WEWE HUJAANZA KUWEKA MSHAHARA WAKO HAPA HADHARANI.

WEKA SALARY SLIP YAKO KISHA NDIPO UWATUHUMU WENGINE!!!!!!!!!!!!
 
Tumemsikia mwenyekiti wa PAC akizungumza. Leo lawama zinatupiwa kwa vyombo vya habari
Kwanza, Bunge lilitakiwa likanushe habari za mwenyekiti wa PAC kama upotoshaji halafu ndiyo maelezo yafuate

Hizi habari za kuleta 'maelezo ya kina' ni njia za kutaka kuficha mkataba.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi, usalama na mambo ya nje amenukuliwa akisema mkataba ameshapelekewa.
Bunge likanushe habari hiyo kwanza

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama amekiri kupata mkataba, kama yalikuwa yanahitajika maelezo mkataba ulimfikiaje? Tunajua kila jambo lazima lipitie ofisi ya bunge, sasa wao waliombaje maelezo badala yake ukatolewa mkataba kama alivyosema mwenyekiti wa ulinzi na usalama?

Hizi habari ni kutaka kuficha ukweli, zitaumiza serikali zaidi maana watu wanadadisi kuliko walivyopaswa

Vyombo vya habari vina taarifu tu havina uhusiano na LUGUMI.

Kuna mahusiano ya Serikali, Lugumi na Bunge katika sakata hili kwa maelezo na taarifa zinazokinzana kila uchao

Msitwishe lawama vyombo vya habari kwa kukwepa ukweli





Ni mwendelezo wa watu kutaka kuuficha Ukweli,kwa nini wavilaumu vyombo vya habari? Wamsikilize Haeshi Hirali hapa na si kuanza kuwalisha watu maneno.
 

Attachments

hii habari na ya uongo,kwenye tovuti ya bunge amna hii habari sasa sijui uyu kaitoa wapi.Mods naombeni mchukue hatua.
 
Nilichofaidika nacho ni kujua nani supplier wa hizo machine. Hayo mengine sina shida nayo kabisa. Asanteni
 
Mbona ukanushaji huu umekawia sana? Si bure!
Kiongozi unakubaliana na maelezo ya vyombo vya habari kusingiziwa kupotosha? Tumewaona wenyeviti kwa vinywa vyao wakieleza kuutaka mkataba na kupewa mkataba..hebu chukueni hatua kwa hili tunawaaminia Jamhuri kwa habari za uchunguzi..
 
Mkataba hauwezi kuombwa na kamati ya Bunge? Ni siri ya nani? Kumbe kuna majipu mengi bado?
 
Kwanza naomba uelewe kuwa Aeshi siyo mwenyekiti wa PAC.

Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Mwenyekiti wa PAC na LAAC lazima atoke kambi ya Upinzani. Wapinzani walikataa kushiriki uchaguzi wa PAC na LAAC kwa madai kuwa wajumbe walioteuliwa kutoka kambi ya upinzani hawana uwezo. kwa lugha nyingine, kambi ya upinzani haiwaamini wajumbe wa PAC.

Pili, hakuna sehemu ambayo Rais Magufuli alisema ataweza kutumbua majipu yote lakini vile vile huwezi kutaka Rais Magufuli atumbue pia majipu ambayo hayajaiva na kama akifanya hivyo, kuna wengine watakuja hapa wanadai Rais anakurupuka.
Mkuu hii twist and turn ya ''mkataba'' mpaka ''maelezo ya mkataba'' ina uhusiano gani na Magufuli? Si jana tulishakubaliana tena kuwa hii ngoma bado iko bungeni hivyo huenda Magufuli anasubiri ili asiingilie mhimili mwingine? Tusibiri tu naona ile qualification test ya kama rais wetu Magufuli ni mtumbua majibu asiyeangalia sura imetolewa mapema kabisa ili kumpima.
 
Hili season la kihindi naona stelingi kasha kufa! litaisha kiajabu sana mwisho! Ngoja niende senemax mlimani city nikamalizie hii season ya 4
 
Kwanza hili tamko la bunge limechelewa sana. Kuchelewa huku si bure. Tangu Aeshi alivyizungumza ni wiki inakatika sasa. Huyu msemaji wa bunge mbona hakutoa taarifa?
Hivi hili bunge bado linaendelea kuwa rubber stamp?
 
Kwanza naomba uelewe kuwa Aeshi siyo mwenyekiti wa PAC.

Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Mwenyekiti wa PAC na LAAC lazima atoke kambi ya Upinzani. Wapinzani walikataa kushiriki uchaguzi wa PAC na LAAC kwa madai kuwa wajumbe walioteuliwa kutoka kambi ya upinzani hawana uwezo. kwa lugha nyingine, kambi ya upinzani haiwaamini wajumbe wa PAC.

Pili, hakuna sehemu ambayo Rais Magufuli alisema ataweza kutumbua majipu yote lakini vile vile huwezi kutaka Rais Magufuli atumbue pia majipu ambayo hayajaiva na kama akifanya hivyo, kuna wengine watakuja hapa wanadai Rais anakurupuka.
Kwa mamlaka aliyonayo kwa katiba ya 1977, akipenda anaweza
 
PAC wanajipa madaraka ambayo sio yao...hawana mamlaka ya kukagua mikataba bila idhini ya wahusika
Wewe wacha kujiondoa upeo wa kuelewa mambo sababu ya njaa na kama ni zile nafasi 46 alizo waombea jk tayari zimejazwa
 
Back
Top Bottom