Sio mkataba ni maelezo ya utekelezaji wa mkataba.... Ina maana hujaona au umeamua kutoona ufafanuzi hapo juuPAC wanajipa madaraka ambayo sio yao...hawana mamlaka ya kukagua mikataba bila idhini ya wahusika
igizo limeingia sehemu ya nne
1.Kamati ya PAC kudai Mkataba
2.Kamati ya Mambo ya nje kupewa jukumu la PAC
3.Said Lugumi kutoweka nchini
4.Bunge kudai kilicho takiwa na PAC si mkataba bali Maelezo
5....
Na yule mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama yeye sio "thirty party" kwa uelewa wako?Wewe ni third part kwenye huo mkataba.
'maelezo ya kina'
Kama wahusika watamruhusu kuona hakuna shida lakini wanaweza kumzuia na asifanye lolote...Na yule mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama yeye sio "thirty party" kwa uelewa wako?
Kuna dhambi gani kwa PAC kuuona huo mkataba? Hivi hili nalo lilihitaji kutolewa press release?
Huyu Lugumi inaonekana ana nguvu kubwa mnoo nyuma yake.
Kwanza naomba uelewe kuwa Aeshi siyo mwenyekiti wa PAC.Mimi naamini maneno ya Aeshi (?) M/kiti wa PAC niliyemsikia kwa masikio yangu na niliyemuona kwa macho yangu akiongea ITV.
Kamwe sitaamini hili tamko lindana la ofisi ya Bunge. Halafu nani alisema Magu anaweza kutumbua kila jipu? !
Kumekuwa na taarifa zinazoendelea kupotosha umma na baadhi ya vyombo vya Habari kuwa Kamati ya Bunge yo Hesabu za Serikali (PAC) ilipokuwa ikitekeleza majukumu yake tarehe 5 April, 2016 ililitaka Jeshi Ia Polisi kuwasilisha Mkataba ulioingiwa Kati ya Jeshi hilo na Kampuni ya Lugumi Enterprises ltd kuhusu mradi wa Utambuzi wa Alama za Vidole AFIS (Automated Fingerprint Identification System). Ofisi ya Bunge inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hili kwamba, taarifa hizo si za kweli na zina lengo Ia kupotosha umma kutokana na kile kilichoamuliwa na kamati hiyo.
Ukweli kuhusu jambo hili ni kwamba tarehe 5 April, 2016, kamati hiyo ilikutana na kujadili Taarifa ya Ukaguzi wa hesabu zilizokaguliwa za fungu 28, Jeshi Ia Polisi kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2014 ambapo kamati pamoja na mambo mengine iliona kuna haja ya kupata maelezo ya kina kwa maandishi katika utekelezaji wa mkataba huo.
Kutokana na haja hiyo, kamati ilimwagiza Afisa Masuhuli ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuwasilisha maelezo ya kina kwa maandishi kuhusu utekelezaji wa mradi huo kwa Ofisi ya Katibu wa Bunge ili kamati iweze kuchambua na kujadili maelezo hayo kabla ya kupendekeza kwa Bunge hatua zaidi za kuchukua. Kufuatia agizo hilo, kamati ilimwandikia pia Katibu wa Bunge taarifa kuhusu agizo hilo tarehe 12 Aprili, 2016 ili kupatiwa maelezo hayo kutoka kwa Afisa Masuhuli.
Ofisi ya Bunge ilimwandikia barua Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo yo Ndani tarehe 12 Aprili 2016 kuwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Kamati Kudumu yo Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyotokana na kikao hicho cha tarehe 5 Aprifi 2016 kabla yo tarehe 18 Aprili, 2016 kama ilivyoshauriwa na kamati. Hivyo ni vyema Umma ukafahamu kuwa kilichoombwa na Kamati ni Maelezo ya utekelezaji wa Mkataba huo na sio Mkataba kama inovyoripotiwa na baadhi yo vyombo vya Habari ambapo Ofisi ya Bunge iliomba maelezo hayo yawasilishwe kabla yo tarehe 18 Aprili, 2016.
lmetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasmano
Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
15 Aprili, 2016.
Kama wahusika watamruhusu kuona hakuna shida lakini wanaweza kumzuia na asifanye lolote...
Kamsikilize tena kama alisema walete mkataba au maelezo ya utekelezaji wa mkataba, binafsi nilisikia maelezo ya utekelezaji wa mkataba.Mimi naamini maneno ya Aeshi (?) M/kiti wa PAC niliyemsikia kwa masikio yangu na niliyemuona kwa macho yangu akiongea ITV.
Kamwe sitaamini hili tamko lindana la ofisi ya Bunge. Halafu nani alisema Magu anaweza kutumbua kila jipu? !
Wanacheza na maneno tu!Hakuwezi kuwa na maelezo ya kina bila ya msingi wa maelezo ya kina. Msingi wenyewe ndio huo mkataba.
Wahusika wote ni watoto wa wenye nchi, lazima majibu yafanane..ccm mble kwa mbele..wenye wivu wajinyonge haya maneno mlala hoi akiimba kakaririshwa tu, wenye mfumo ndio wana maanisha haswa kulingana na matendo yao. Kwa utamu huu kweli ccm haita kaa ikubali kuachia nchi hata kwa mapinduzi,acha vikaratasi bora wampe mzungu tuwe wakoloni.Hii movie haina tofauti na ile ya bumbuli boy.